





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, hakika Shetani hukimbia kutoka katika nyumba inayosomwa suratul Baqara ndani yake".
Imepokelewa Imamu MuslimAnakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuyatelekeza majumba kwa kutoka swali ndani yake, yakawa kama makaburi yasiyoswaliwa ndani yake. Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Shetani hukimbia nyumba ambayo husomwa suratul Baqara ndani yake.
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara zitamtosheleza".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesoma aya mbili za mwisho katika suratul-Baqara usiku, basi Mwenyezi Mungu atamtosheleza na shari na kila lenye kuchukiza, na imesemwa: Zitamtosheleza na kisimamo cha usiku, na imesemwa: Zita mtosha na nyiradi zote, na imesemwa kuwa: Ni kiwango kidogo kinachoweza kumtosheleza mtu na kusoma Qur'ani katika kisimamo cha usiku, na imesemwa kinyume na hivyo, na huenda yote yaliyotajwa yanakusanywa na tamko hilo.
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allah basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na jema hilo hulipwa mara kumi mfano wake, sisemi (Alif Laam Miim) ni herufi, lakini (Alif) ni herufi, na (Laam) ni herufi, na (Miim) ni herufi".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyAmeeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila muislamu anayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na huzidishiwa malipo hayo mpaka mara kumi mfano wake. Kisha akaliweka wazi hilo kwa kauli yake: (Sisemi "Alif Laam Miim" ni herufi, lakini Alif ni herufi, na Laam ni herufi, na Miim ni herufi): Inakuwa herufi zote tatu zina thawabu thelathini (30).
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akimtaja Allah katika nyakati zake zote.
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa na pupa kubwa ya kumtaja Allah Mtukufu, nakuwa yeye alikuwa akimtaja Allah Mtukufu katika nyakati zote mahala popote na katika hali zote.
Kutoka kwa Saidi Bin Musayyab, kutoka kwa baba yake amesema: Yalipomfika mauti Abuu Twalib, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimjia akamkuta yuko pamoja na Abuu Jahali na Abdallah Bin Umaiyya bin Mughiira, akasema: "Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu) neno ambalo nitakutetea kwalo mbele ya Mwenyezi Mungu", Abuu Jahali akasema: Hivi unataka kuichukia mila ya Abdul Muttwalib (Yaani baba yake) Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akaendelea kumrejelea neno hilo, nao pia wakirudia kumwambia maneno yao, mpaka Abuu Twalib akasema kwa neno lake la mwisho alilowasemesha: Niko katika mila ya Abdul Muttwalib, na akakataa kusema: Laa ilaaha illa llaah, mpokezi anasema: Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Wallahi (Namuapia Allah) nitakuombea msamaha kwa muda wote madam sijakatazwa, Allah akateremsha: "Haifai wala haitakiwi kwa Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina" [Attauba: 113], Na akateremsha kuhusu Abuu Twalib, akasema kumwambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika wewe humuongoi umpendaye, lakini Allah anamuongoa amtakaye" [Al-Qasas:56]
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliingia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa Ami yake Abuu Twalib akiwa katika hali ya kukaribia kufa, akasema kumwambia: Ewe Ami yangu sema "Laa ilaaha illa llaah", neno ambalo nitakutolea ushahidi kwalo mbele ya Allah, Abuu Jahali na Abdallah Bin Abiiy Umaiyya wakasema: "Wewe Abuu Twalib!, unaacha mila ya baba yako Abdul Muttwalib?! ambayo ni kuabudu masanamu, wakaendelea kumwambia hivyo mpaka akasema neno lake la mwisho alilowaambia kuwa: Niko katika mila ya Abdul Muttwalib, mila ya ushirikina na kuabudu masanamu, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nitakuombea msamaha madam sijakatazwa na Mola wangu kuhusu hilo, ikateremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Haipasi kwa Nabii na wale walioamini kuwatakia msamaha washirikina, hata kama watakuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni" [Attauba: 113], Na ikateremka kumuhusu Abuu Twalib kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wewe, humuongoi, unayependa aongoke. Lakini Mwenyezi Mungu, Anamuongoa Anayemtaka. Na Yeye Ndiye Anayemjua zaidi anayefaa kuongoka". Kwani hakika wewe humuongoi umpendaye kumuongoa, bali jukumu lako ni kufikisha, na Allah anamuongoa amtakaye.
Kutoka kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Anayesoma Qur'ani kwa uhodari huwa pamoja na msafara wa Malaika watukufu, na anayesoma Qur'ani huku anasitasita na huku kwake bado ni ngumu huyo anamalipo mara mbili".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba anayesoma Qur'ani, akiwa na hifdhi nzuri na mfanisi, na mahiri na hodari kwa kisomo chake, basi huyu ana thawabu Akhera kiasi cha daraja yake kuwa pamoja na Malaika wema na wakarimu, na kwamba anayesoma Qur'ani na huku akipata tabu ndani yake na anasitasita katika kisomo chake; kwa sababu ya udhaifu wa hifudhi yake, lakini pamoja na hivyo bado anashikamana nayo, na kwake bado ni ngumu na nzito basi ana malipo mara mbili; malipo ya kisomo na malipo ya tabu na kusitasita kwake katika kisomo.
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Soma", Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nikusomee vipi, na hali yakuwa Qur'ani iliteremka juu yako? Akasema: "Ndiyo" Nikasoma suratun Nisaai mpaka nikafika katika aya hii: "Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila Umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa" [An-Nisaai: 41], Akasema: "Inatosha sasa" Nikamgeukia, ghafla nikaona macho yake yakibubujika machozi.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume rehema na amani ziwe juu yake alimuomba Abdallah bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake amsomee chochote katika Qur'ani, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, vipi nikusomee na hali yakuwa Qur'ani iliteremshwa juu yako?! Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi ninapenda kuisikia kutoka kwa mtu mwingine, akamsomea kutoka katika Suratun-Nisaai, alipofikia kauli yake Mtukufu: "Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila Umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa". Yaani: Itakuwa vipi hali yako na hali ya Umma wako pindi tutakapokuleta kama shahidi juu ya Umma wako yakuwa wewe umewafikishia ujumbe wa Mola wako Mlezi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Sasa, simama hapo katika kisomo chako, anasema bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake: Nikamgeukia ghafla nikaona macho yake yakibubujika machozi kwa hofu ya tukio hilo, na kwa kuuhurumia Umma wake.
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Hakika mfano wa mtu wa Qur'ani ni sawa na mfano wa mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa, akimuangalia kila mara atamzuia (kutoroka), na akimuachilia atatoroka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmemfananisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliyesoma Qur'ani na akakizoea kisomo chake sawa iwe kwa kutazama katika msahafu au kuhifadhi kwa moyo, na mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa kwa kamba ambazo hufungiwa wanyama, akimtazama mara kwa mara ataendelea kumshika na kumzuia, na akiacha kumfunga na kumtazama basi ataondoka na kutoroka, akianza kusoma Qur'ani msomaji wa Qur'ani basi huikumbuka, na asipoisoma basi ataisahau; madam kudumu kuisoma kutaendelea basi hifdhi yake itaendelea kubakia.
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: "Pindi Jibrili alipokuwa amekaa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisikia kishindo kutoka juu yake, akanyanyua kichwa chake, akasema: "Huu ni mlango kutoka Mbinguni umefunguliwa leo haukuwahi kufunguliwa kabisa isipokuwa leo, kisha akateremka kutoka kwenye mlango ule Malaika, akasema: "Huyu ni Malaika ameteremka Ardhini hakupata kuteremka kabisa isipokuwa leo, akawasalimia, kisha akasema: "Pokea habari njema ya kupewa Nuru mbili hakupewa Nabii yeyote kabla yako: Ufunguzi wa kitabu (Alfatiha) na Aya za mwisho katika Suratul-baqarah, hautasoma herufi miongoni mwa Sura hizo mbili isipokuwa utapewa (unacho hitaji)"
Imepokelewa Imamu MuslimMalaika Jibril amani iwe juu yake alikuwa amekaa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya mlango unapofunguliwa, Jibril akanyanyua kichwa chake na macho yake mbinguni, kisha akaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mlango huu kutoka mbinguni umefunguliwa leo, na haukuwahi kufunguliwa katu isipokuwa leo, akateremka kutoka humo Malaika kuja Ardhini, hakuwahi kuteremka kabla isipokuwa leo, Malaika akamtolea salamu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akasema kumwambia: Kuwa na habari njema ya kupata Nuru mbili ulizopewa, ambazo hakuwahi kupewa Nabii yeyote kabla yako; nazo ni: Suratul-Fatiha, na Aya mbili za mwisho wa suratul-Baqara. Kisha Malaika akasema: Hatosoma yeyote harufi moja katika hizo isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa yale yaliyomo ndani yake miongoni mwa heri na dua na maombi.