





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Hakika Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka aliteremsha "Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio makafiri" [Maaida: 44] na "basi hao ndio madhalimu" [Maida: 45] na "basi hao ndio waovu" [Maida: 47], akasema: Amesema bin Abbasi: Aliziteremsha Mwenyezi Mungu kwa makundi mawili katika Mayahudi, na moja lilikuwa limelitenza nguvu jingine katika zama za ujinga, mpaka wakaridhiana na wakapatana kuwa kila dhalili aliyeuliwa na mtu mtukufu fidia yake ni Waski hamsini, sawa na (kg 6100), na kila maiti aliyeuliwa na mtu dhalili katika watukufu basi fidia yake ni Waski mia moja (100) sawa na (kg12,200), na walikuwa wakiishi katika maisha hayo mpaka alipokuja Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika mji wa Madina, na makundi yote mawili yakajishusha kwa kufika Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati huo hajajulikana kwa watu, na hakuwa amewalazimisha na kuwatenza nguvu katika hilo, na huo ulikuwa ni wakati wa ule mkataba wa maridhiano (Hudaibia), basi mtu dhalili akamuuwa mtukufu mmoja, basi yule mtukufu akatuma ujumbe kwa ndugu wa yule dhalili kuwa tunataka mtuletee Waski mia moja (kg12,200) yule dhalili akasema: Je ni kweli ndivyo ilivyokuwa katika mitaa yao kwamba dini yao ni moja, na nasaba yao ni moja, na mji wao ni mmoja, kwamba fidia ya baadhi yao ni nusu ya wenzao? Bila shaka hakika sisi tumekupeni kiasi hicho kwa kutudhulumu, na kwakuwa tunawaogopa, ama kwakuwa Muhammadi amekuja hatutokupeni, basi vita ikakaribia kuwaka baina yao, kisha wakaridhiana kuwa wamfanye Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muamuzi wao, kisha yule mtukufu akaanza kueleza na akasema: Wallahi Muhammadi hatokupeni toka kwao zaidi ya kile atakachowapa toka kwenu, na hakika wamesema kweli, hawakutupa isipokuwa kwa dhuluma na kwa kutuogopa sisi, na kuwatenza nguvu, basi tumeni kwa Muhammadi mtu atakayekuleteeni maoni yake: Ikiwa atakupeni mnachotaka basi mfanyeni kuwa hakimu wenu, na asipokupeni basi muepukeni na msimfanye kuwa hakimu, basi wakatuma kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu miongoni mwa wanafiki ili wawaletee habari na maoni ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, walipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, Mwenyezi Mungu alimpa habari Mtume wake ya jambo lao lote na kile walichokitaka, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ewe Mtume! Wasikuhuzunishe wale ambao wanakimbilia kuukanusha unabii wako miongoni mwa wanafiki ambao wameonyesha Uislamu..." [Maida: 41] Mpaka katika kauli yake: "Na yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio mafasiki (waovu)" [Maida: 47] Kisha akasema kuhusu aya hizo, Wallah zimeteremka, na bila shaka wao ndio Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwakusudia.
Imepokelewa na AhmadWalikuwa miongoni mwa Mayahudi wa Madina ni Bani Kuraidha na Bani Nadhiri, na kabila moja lilikuwa limelitenza nguvu na kulishinda kabila jingine katika zama za ujinga, wakaridhiana na wakapatana kuwa kila mtu aliyeuliwa na mtu mtukufu mwenye nguvu katika madhalili waliozidiwa basi fidia yake ni Waski hamsini tu (kg 6,100), na kila maiti mtukufu aliyeuliwa na mtu dhalili basi fidia yake ni mara mbili, Waski mia moja (kg 12,200) na waski moja ni sawa na vibaba sitini. Walikuwa katika utaratibu huo mpaka alipokuja Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kuhama, na makundi yote mawili yakajishusha kwa kufika kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake, naye rehema na amani ziwe juu yake kwa wakati huo alikuwa bado hajapata ushindi dhidi ya maadui zake, na hajawatenza nguvu ili wamtii; kwa sababu hilo lilikuwa mwanzoni mwa kuhama kwake, na ilikuwa kipindi cha mkataba wa maridhiano (Hudaibia). Kabila dhalili mtu mmoja akamuua mmoja katika watu watukufu, kabila tukufu wakatuma ujumbe kwa watu dhalili: Yakuwa tutumieni Waski mia moja kama makubaliano yalivyokuwa tangu awali, kabila dhalili likasema: Je, linawezekanaje hili katika mitaa miwili, dini yao moja, na nasaba yao moja, na mji wao mmoja, halafu fidia ya baadhi yao iwe nusu ya wenzao?!, hakika sisi tulikupeni fidia hii kwa kutudhulumu, na kwa kuwahofu, ama kwakuwa Muhammadi amekuja hatutokupeni fidia hiyo milele. Vita vikakaribia kuwaka baina yao, kisha wakaridhiana kuwa wamfanye Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hakimu kati yao, kisha kabila tukufu likatafakari, wakasema: Wallahi Muhammadi hatokupeni kutoka kwao mara mbili ya kile atakachowapa wao, na hakika wamesema kweli, hawakutupa kiwango hiki isipokuwa kwa dhuluma, na kwa kuwatenza nguvu, tumeni watu kwenda kwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kwa siri watakaokuleteeni mtazamo wake, ikiwa atakupeni mnachokitaka basi mfanyeni kuwa hakimu, na asipokupeni mnachotaka achaneni naye na wala msifanye kuwa hakimu baina yenu. Wakatuma watu kwa siri kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika wanafiki ili wajue mtazamo wake rehema na amani ziwe juu yake, walipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake Mwenyezi Mungu akateremsha wahyi na akamueleza Mtume wake kuhusu swala lao lote na walichokitaka, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika suratul Maida kwanzia kauli yake: "Ewe Mtume, wasikuhuzunishe wale wanaokwenda mbio katika kukupinga, miongoni mwa wale waliosema tumeamini" [Maida: 41]. Mpaka katika kauli yake: "Na asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio mafasiki" [Maida: 47]. Kisha akasema bin Abbas radhi za Allah ziwe juu yao: Kwa makundi hayo mawili Wallahi ndio iliteremka kauli yake Mtukufu: "Na asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio makafiri" [Maida: 44], na "...basi hao ndio madhalimu" [Maida: 45] na "...basi hao ndio mafasiki" [Maida: 47], na hao hakika ndio aliowakusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Funguo za mambo ya ghaibu ni tano, "Hakika kuijua Saa ya Kiyama kuko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ndiye anayeiteremsha mvua. Na anavijua vilivyo ndani ya matumbo ya uzazi. Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho. Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua, Mwenye habari".
Imepokelewa na Al-BukhaariyGhaibu iko kwa Mwenyezi Mungu hakuna aijuaye ila Yeye, na ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa funguo za mambo yaliyofichikana na hazina zake ni tano: Ya kwanza: Hakuna ajuaye ni lini kitasimama Kiyama isipokuwa Mwenyezi Mungu, ikiashiria kuijua Akhera, kwani siku ya Kiyama ndio mwanzo wake, na ikikanushwa elimu ya kilicho karibu basi inashindikana elimu iliyo baada yake. Ya pili: Hakuna ajuaye ni lini inakuja mvua isipokuwa Mwenyezi Mungu, hii ikiashiria mambo ya ulimwengu wa juu, na ameitaja mvua pekee pamoja nakuwa inaweza kuwa na sababu zilizozoeleka zinazoweza kujulisha unyeshaji wake lakini hua hazina uhakika wala yakini. Ya tatu: Yanayokuwa katika mifuko ya uzazi; kama mwanaume au mwanamke, mweusi au mweupe, amekamilika maumbile au amepungua, muovu au mwema na mfano wake, na ametaja uzazi pekee kwa sababu kwa kawaida watu wengi wanaujua, pamoja na hivyo akakanusha yeyote kujua uhalisia wake basi kisichokuwa mfuko kutojulikana ndio bora zaidi. Ya nne: Hakuna ajuaye yaliyoko kesho isipokuwa Mwenyezi Mungu, ikiashiria aina za nyakati na matukio yaliyomo, na ameeleza kwa tamko "kesho" ili uhalisia wake uwe ni wakati wa karibu zaidi, na ikiwa pamoja na ukaribu wake hakuna ajuaye uhalisia wa yatakayotokea ndani yake, pamoja na kuwezekana kupata dalili na alama zake, basi siku baada yake ndio bora zaidi kutojulikana. La tano: Haijui nafsi itafia nchi gani, ikiashiria mambo ya ulimwengu wa chini, pamoja nakuwa kawaida watu wengi hufia katika nchi zao, lakini hilo si uhalisia, bali lau atakufa katika nchi yake pia hajui ni Ardhi gani atazikwa, hata kukiwa na makaburi ya watangulizi wake, "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye habari" ameyazingira yenye kuonekana na yasiyoonekana, na yaliyofichikana na yaliyohifadhiwa, na siri zote, aya ikakusanya aina mbali mbali za ghaibu, na ikaondoa madai yote mabovu.
Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao amesema: Nilikuwa katika Mimbari ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mtu mmoja akasema, si jali ni amali gani nitakayoifanya baada ya Uislamu isipokuwa nitawapa maji mahujaji, na mwingine akasema: Sijali kutofanya amali yoyote baada ya Uislamu isipokuwa nitauimarisha Msikiti mtukufu, na mwingine akasema: Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko yote mliyosema, Omari akawakemea, na akasema: Msinyanyue sauti zenu mbele ya Mimbari ya Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, na hali yakuwa pia ni Ijumaa, lakini nitakaposwali Ijumaa nitaingia na nitamuuliza kuhusu haya mliyotofautiana kwayo, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mnayafanya, enyi watu, yale mnayoyasimamia ya kuwanwyesha mahujaji na kuuimarisha msikiti Mtukufu ni kama Imani ya aliyemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho? [Tauba: 19] Mpaka mwisho wa Aya.
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Nuuman bin Bashiri radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, yakwamba alikuwa amekaa katika Mimbari ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamsikia mtu mmoja akisema: Sijali kutofanya amali yoyote baada ya kusilimu kwangu isipokuwa nitawanywesha maji mahujaji. Na mwingine akasema: Na mimi sijali kutofanya amali yoyote baada ya kusilimu kwangu isipokuwa nitauimarisha Msikiti mtukufu, na akasema mwingine: Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ndio bora zaidi kuliko hayo mliyoyasema. Omari bin Khattwabi akawakemea kwa kunyanyua sauti zao mbele ya Mimbari ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na tukio hilo lilikuwa asubuhi ya siku ya Ijumaaa, lakini nitakaposwali Ijumaa nitaingia na nitamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika haya mliyotofautiana kwayo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha: "Mnayafanya yale mnayoyasimamia ya kuwanwyesha mahujaji na kuuamirisha msikiti mtukufu ni kama imani ya aliyemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Haziwi sawa hali za Waumini na hali za makafiri mbele ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaelekezi watu wanaozidhulumu nafsi zao kwa ukafiri kwenye mambo mema." [At-Tauba: 19].
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake (Hadithi Marfu'u): Katika kauli yake Aliyetakasika na kutukuka: "Na yeyote anayetaka, ndani ya Msikiti Mtukufu, kwenda kombo na haki kwa njia ya udhalimu na akamuasi Mwenyezi Mungu humo ndani, basi tutamuonjesha adhabu kali yenye kuumiza" [Al-Hajji:25] Akasema: "Lau kama mtu atadhamiria ubaya akiwa katika mji wa eden (Yemen) mbali huko, basi Mwenyezi Mungu angemuonjesha adhabu chungu".
Imepokelewa na Ahmad na Al HakimAmeeleza Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake katika kauli yake Aliyetakasika na kutukuka: "Na yeyote anayetaka, ndani ya Msikiti Mtukufu, kwenda kombo na haki kwa njia ya udhalimu na akamuasi Mwenyezi Mungu humo ndani, basi tutamuonjesha adhabu kali yenye kuumiza" [Al-Hajji: 25], akasema: Lau mtu yeyote atawaza ndani ya nafsi yake na akaazimia kufanya jambo baya ndani ya sehemu tukufu ya Makka, likahalalishwa ndani yake aliloliharamisha Mwenyezi Mungu, kama makosa ya ulimi au kuuwa kwa makusudi, basi hiyo ni dhulma, hata kama maazimio atayaweka akiwa katika mji wa Eden huko Yemen, basi huyu atastahiki Mwenyezi Mungu amuonjeshe adhabu chungu kwa sababu ya hilo, hata kama hajalifanya, maazimio yake katika hilo yanatosha.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Ilipoteremka: "Hakika Sisi tumekufungulia wewe, ewe Mtume, ufunguzi ulio waziwazi, ili akusamehe Mwenyezi Mungu" mpaka katika kauli yake: "Ushindi mkubwa" [Fat-hi: 1-5] marejeo ya hili ni katika suluhu ya Hudaibia, na wao wakiwa wamejawa na huzuni na unyonge, na alichinja vichinjwa vyake hapo Hudaibia, akasema: "Hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya ninayoipenda zaidi kuliko dunia nzima".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Anasi bin Maaliki radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba ilipoteremka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kauli yake Mtukufu: "Hakika sisi tumekufungulia ewe Muhammadi ufunguzi wa wazi wazi (1) Ili akusameheme Mwenyezi Mungu yaliyotangulia katika madhambi yako na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika njia iliyonyooka (2) Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu (3) Yeye ndiye aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili wazidi imani juu ya imani yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye ujuzi, mwenye hekima (4) Ili awaingize Waumini wanaume na Waumini wanawake katika Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo, na awafutie makosa yao. Na huko ndiko kufuzu kukubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (5) [Al-Fat-hi: 1-5]. Hili lilikuwa Wakati wa kurejea kwake kutoka Hudaibia, na wakati Maswahaba wakiwa wamegubikwa na huzuni na unyonge, wakiwa wamezuiliwa kutekeleza Umra, kwa sababu ya yale waliyokubaliana katika mkataba, na dhana yao ilikuwa; yote hayo hayana masilahi na Waislamu, na walichinja vichinjwa vyao hapo Hudaibia, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwa hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya inayopendeka zaidi kwangu kuliko dunia nzima, kisha akaisoma.
Kutoka kwa Abuu Dardai radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayehifadhi aya kumi za mwanzo wa suratul Kahf, atakingwa na Dajali". Na katika riwaya nyingine: "Za mwisho wa suratul Kahf".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayehifadhi aya kumi kwa moyo wake za mwanzo wa suratul Kahaf atakingwa na kuepushwa na kuhifadhiwa na fitina za Masihi Dajali atakayetoka zama za mwisho na atadai uungu, na fitina zake ni fitina kubwa itakayotokea katika Ardhi tangu kuumbwa kwa Adam mpaka kusimama kwa Kiyama; kwa yale aliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mambo ya ajabu ambayo atawafitinisha kwayo watakaomfuata, na hii ni kwa sababu mwanzo wa suratul Kahaf kuna maajabu na miujiza mikubwa kuliko fitina na za Dajali kwa watu, atakayezizingatia hatofitinika na Dajali. Na katika riwaya nyingine: Ni aya kumi za mwisho wa sura kuanzia katika kauli yake Mtukufu: "Hivi wanadhani wale waliokufuru kuwa wanaweza kujifanyia..."
Imepokelewa kutoka kwa Uqba bin Aamir -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Zimeteremshwa kwangu aya, hazijawahi kuonekana mfano wake katu, sura mbili za kinga"
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Ukba bin Aamiri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema kumwambia: Usiku huu Mwenyezi Mungu kaniteremshia aya, hazijawahi kuonekana mfano wake katu -yaani katika kuomba kinga- nazo ni sura mbili za kinga: Suratu (Qul Auudhubirabbil falaq), na suratu (Qul Auudhubirabbin naas).
Imepokewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake amesema: Nilikuwa nikihudumia watu vinywaji katika nyumba ya Abuu Twalha, na pombe yao wakati huo ilikuwa ni mchanganyiko, akaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kunadi akanadi: Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa, akasema: Abuu Twalha akasema kuniambia: Toka, nenda kaimwage, nikatoka nikaimwaga, ikatiririka pombe mitaro ya Madina, baadhi ya watu wakasema: Wameuliwa baadhi ya watu na pombe ikiwa tumboni mwao, Mwenyezi Mungu akateremsha: "Hapana ubaya kwa wale walioamini na akafanya matendo mema katika vile walivyokula" [Al-Maaida: 93] Mpaka mwisho wa aya.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Anas bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba alikuwa akitoa huduma ya vinywaji (pombe) kwa wale waliokuwa katika nyumba ya mume wa mama yake Abuu Twalha radhi za Allah za ziwe juu yake, na pombe yao wakati huo ilikuwa ni mchanganyiko, kati ya tende mbivu na tende mbichi, ghafla mnadiji wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akanadi: Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa, akasema: Anasema: Abuu Twalha akasema kuniambia, toka nenda kaimwage na uimimine, nikatoka nikaimwaga na nikaimimina, pombe ikatiririka katika mitaro ya Madina, wakasema baadhi ya watu: Wameuliwa baadhi ya Maswahaba na pombe ikiwa tumboni mwao ikiwa bado haijaharamishwa, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hapana ubaya kwa wale walioamini na wakafanya matendo mema katika yale waliyokula". [Al-Maaida: 93] Mpaka mwisho wa aya. Yaani: Hawana dhambi wale walioamini katika vile walivyokula na kunywa katika pombe kabla ya kuharamishwa kwake.
Imesimuliwa kutoka kwa Abuu Najihi Al-'Irbat bin Sariya, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, ya kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alituaidhi mawaidha makali sana. Nyoyo zikajaa hofu kwa sababu yake, na macho yakamiminika machozi kwa sababu yake, basi tukasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni kama kwamba ni mawaidha ya anayeaga. Basi tuusie." Akasema: "Ninawausia kumcha Mwenyezi Mungu, na kusikia na utii, hata kama atakutawaleni mtumwa. Kwani hakika yeyote kati yenu atakayeishi, ataona tofauti nyingi. Kwa hivyo shikamaneni na Sunna yangu na Sunna ya makhalifa wanyoofu waongofu, zikamateni na kuzing'ata kwa magego. Na jihadharini na mambo ya kuzushwa. Kwani kila jambo jipya (katika dini) ni uzushi, na kila uzushi ni upotofu."
Imepokelewa na Abu Daud na TirmidhiyMtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwapa mawaidha Masahaba, mawaidha makali, nyoyo ziliogopa kwa mawaidha hayo, na macho yalibugujikwa machozi, Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kana kwamba mawaidha haya ni ya mwenye kuaga, kwa sababu waliona ni jinsi gani alivyokuwa na umakini mkubwa katika mawaidha, wakaomba usia, ili washikamane nao baada yake, akasema: Nakuusieni kumcha Allah Mtukufu, nako ni kwa kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho. Na usikivu na utii, yaani: Kwa wenye mamlaka juu yenu, hata kama kiongozi wenu au aliyekutawaleni ni mtumwa, yaani mtu dhalili akawa kiongozi juu yenu, msilibeze hilo, na mtiini, kwa kuchelea kuamsha fitina, bila shaka atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona hitilafu nyingi, Kisha akawabainishia njia ya kutoka katika hitilafu hii, nayo ni kwa kushikamana na sunna yake na sunna za mahalifa wanne waongofu baada yake, Abuubakari Swiddiq, na Omari bin Khattwab, na Othman bin Affan, na Ally bin Abii Twalib, radhi za Allah ziwe juu yao wote, na kuzing'ata kwa magego, yaani meno ya mwisho: Anakusudia kwa kauli hii yaani kufanya bidii katika kubaki katika sunna na kushikamana nazo, Na akawatahadharisha na mambo ya kuzushwa yaliyobuniwa ndani ya Dini, kwani kila uzushi ni upotevu.