





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abuu Umama Al-bahily radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Someni Qur'ani, kwani, itakuja Siku ya Kiyama kama muombezi kwa sahibu wake, Zisomeni Az-Zahraawaini: Al-Baqara na Surat Al-Imran. Kwani, zitakuja Siku ya Kiyama kana kwamba ni mawingu mawili au Ghayayatani (kitu chenye kumpa kivuli mtu kwa juu ya kichwa chake), au kana kwamba ni makundi mawili ya ndege walio katika safu, (sura hizo mbili) zikiwatetea wasomaji wake. Isomeni Surat Al-Baqara. Kwani kuichukua (kuisoma) ni baraka, na kuiacha ni majuto, na wala wachawi hawaiwezi."
Imepokelewa Imamu MuslimAmehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kudumu kuisoma Qur'ani; kwa sababu itawatetea wasomaji wake wenye kuifanyia kazi siku ya Kiyama, kisha akatilia mkazo katika kusoma sura mbili, Baqara na Al-Imrani, ameziita kuwa ni mapambo mawili yenye kung'aa; kwa sababu ya nuru yake na muongozo wake, na kwamba malipo na thawabu za kuzisoma na kuzingatia maana zake, na kuyafanyia kazi yaliyomo, haya yatakuja siku ya Kiyama kama mawingu mawili, au kinginecho, au kama makundi mawili ya ndege waliotandaza mbawa zao walioungana baadhi yao kwa baadhi, zikimkinga msomaji wake na zikimtetea. Kisha akatilia mkazo rehema na amani ziwe juu yake katika kuisoma Suratul-Baqara na kuzingatia maana zake na kuyafanyia kazi yaliyomo, na kwamba hilo lina baraka na manufaa makubwa ndani yake katika dunia na Akhera, na kuliacha hilo kuna masikitiko na majuto siku ya Kiyama, na kwamba miongoni mwa fadhila za sura hii nikuwa wachawi hawawezi kumdhuru mwenye kuisoma.
Imepokelewa kutoka kwa Jundubu bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikuwa pamoja Mtume rehema na amani ziwe juu yake nasi tukiwa vijana karibu na balehe, tukajifunza imani kabla ya kujifunza Qur'ani, kisha tukajifunza Qur'ani, tukaongeza imani kupitia Qur'ani.
Imepokelewa na Ibnu MaajahAmesema Jundubu bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake nasi tukiwa vijana tuliokaribia kubalehe, wenye nguvu na wakali, tukajifunza kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake imani kabla ya kujifunza Qur'ani, kisha tukajifunza Qur'ani; tukazidisha imani kupitia Qur'ani.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Hakuna yeyote katika Manabii isipokuwa alipewa mfano wa yale waliyoyaamini watu, na hakika niliyopewa mimi ni wahyi (ufunuo) wa Mwenyezi Mungu alionifunulia, basi nataraji kuwa na wafuasi wengi kuliko wao siku ya Kiyama".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Manabii wote Mwenyezi Mungu aliwapa nguvu na akawapa alama na miujiza iliyo nje na kawaida ya watu, watakayoitumia kama ushahidi juu ya unabii wao na kumpelekea kuamini atakayeishuhudia kwa kuwasadikisha, na kwamba yeye ameshindwa katika changamoto hiyo, kiasi kwamba hawezi kuizuia yeye mwenyewe binafsi, lakini anaweza kupinga akakaidi. Bali yeye rehema na amani ziwe juu yake alama yake na muujiza wake ni Qur'ani aliyomteremshia Mwenyezi Mungu kwa Wahyi; kwa namna ilivyokusanya miujiza ya wazi tena endelevu kwa wingi wa faida zake na kuenea kwa manufaa yake, kwa kukusanya kwake ujumbe na hoja na habari za yale yatakayotokea, manufaa yake yakamuenea aliyepo na asiyekuwepo na aliyepatikana na atakayepatikana, kisha akasema: Basi ninataraji kuwa na wafuasi wengi zaidi yao siku ya Kiyama.
Kutoka kwa Katada amesema: Aliulizwa Anasi kilikuwa vipi kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake? Akasema: "Kilikuwa ni kuvuta", kisha akasoma: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu" [Al-Faatiha:1] Alikuwa akivuta neno: Bismillaahi, na anavuta Al-Rahmaani, na anavuta neno: Al-Rahiim.
Imepokelewa na Al-BukhaariyAliulizwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake kilikuwa vipi kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Qur'ani? Akasema: Alikuwa akivuta sauti yake kwa kisomo; akivuta herufi Lamu ilioko kabla ya "Haa" katika neno: "Allah", na anavuta herufi "Mim" ilioko kabla ya "Nuun" katika neno "Al-Rahmaan", na anavuta herufi "Haa" katika neno "Al-Rahiim".
Kutoka kwa Abuu Mulaika: Kutoka kwa baadhi ya wake za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: Abuu Aamir, amesema Naafii: Nafikiri ni Hafswa -Yakuwa aliulizwa kuhusu kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Hakika nyinyi hamkiwezi, akasema: Akaambiwa hebu tueleze. Akasema: Akasoma kisomo cha taratibu, akasema Abuu Aamiri: Akasema Naafii: Akatusimulia Abuu Mulaika: "Alhamdulillaah Rabbil-Aalamiin" [Al-Faatiha: 1] Kisha akakata "Al Rahmaanir Rahiim" [Faatiha:3] kisha akakata "Maaliki yaumid diin".
Imepokelewa na AhmadAliulizwa Hafswa mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Kilikuwa vipi kisomo cha Qur'ani cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake? Akasema: Hakika nyinyi hamkiwezi mfano wake, akaambiwa: Tueleze. Amesema Naafii: Akatusomea Abuu Mulaika kisomo alichotulizana ndani yake; ili kielezee na kikaribiane na kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasoma: "Alhamdulillaahi Rabbil Aalamiin" kisha akakata kisomo, "Al Rahmaanir Rahiim", kisha akakata kisomo, "Maaliki yaumid diin".
Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitusomesha Qur'ani katika kila hali madamu hana janaba.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwafundisha Maswahaba zake Qur'ani na akiwasomesha yeye mwenyewe katika hali zote madam hajawa katika hali ya janaba litokanalo na tendo la ndoa kwa wakeze.
Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudri -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kuwa mwanamume mmoja alimsikia mtu akisoma: "Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee." Huku akiirudiarudia. Ilipofika asubuhi, alimjia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake, na akamueleza hilo. Na ni kana kwamba mwanamume huyo aliona jambo hilo ni jambo dogo. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake akasema: “Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika, hiyo ni sawa na theluthi moja ya Qur'ani."
Imepokelewa na Al-BukhaariyAmeeleza Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake kwamba mtu mmoja alimsikia bwana mmoja akisoma suratu: "Qul-huwallaahu Ahad" akiikariri kila usiku na wala hazidishi sura nyingine, palivopambazuka alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamsimulia tukio hilo, ni kana kwamba muulizaji anaiona kuwa ndogo, akatoa kiapo rehema na amani ziwe juu yake kwa maana ya kuonyesha msisitizo, akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake hakika sura hiyo inalingana na theluthi ya Qur'ani.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Ilipoteremka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ni wa Mwenyezi Mungu ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, na chochote mnachokidhihirisha, kati ya viliomo ndani ya nafsi zenu au mnachokificha, Mwenyezi Mungu anakijua, na atawahesabu nacho. Atamsamehe anayemtaka na atampatiliza anayemtaka. Na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu" [Al-Baqara: 284], anasema: Likawa gumu sana hilo kwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha wakashuka chini kwa kupiga magoti, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu tumepewa jukumu la matendo tunayoyaweza, kama Swala, Swaumu, na Jihadi, na Sadaka, na imeteremka juu yako aya hii wala hatuiwezi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Je hivi mnataka kusema kama walivyosema watu wa vitabu viwili kabla yenu, tumesikia na tumeasi? bali semeni: Tumesikia na tumetii tunataraji msamaha toka kwako ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako", wakasema: Tumesikia na tumetii tunataraji msamaha toka kwako ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako, walipoisoma kauli hiyo, zikadhalilika ndimi zao, akateremsha Mwenyezi Mungu punde tu baada ya hapo: "Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na Waislamu, (pia wameamini hivyo) wote wamemwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na vitabu vyake, na Mitume wake hatutofautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na husema tumesikia na tumetii, tunakuomba msamaha Mola wetu na marejeo ni kwako" [Baqara: 285] walipofanya hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akaifuta, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mwenyezi Mungu hailazimishi nafsi yoyote isipokuwa yaliyo sawa na uweza wake. (Faida ya) yale iliyochuma (nafsi hiyo) ni yake na hasara ya yale iliyochuma ni juu yake. (Husema); Mola wetu usitutese kama tukisahau au tukikosa" [Al-Baqara: 286] Akasema: Ndiyo "Mola wetu na usitubebeshe mzigo kama uliowabebesha wale waliokuwa kabla yetu" Akasema: Ndiyo "Mola wetu usitutwike tusiyoyaweza" [Baqara: 286] Akasema: Ndiyo "na utusamehe na utufutie na uturehemu, Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tusaidie juu ya watu makafiri." [Baqara: 286] Akasema: Ndiyo.
Imepokelewa Imamu MuslimAlipoteremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake kauli yake: "Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyoko mbinguni na Ardhini" Kwa kuviumba na kuvimiliki, na maamuzi na kuvipangilia, "Na ikiwa mtadhihirisha" na mkaonyesha wazi na mkatangaza "yaliko ndani ya nafsi zenu" na vifua vyenu "au mkayaficha" mkayasitiri na kuyaficha ndani ya nyoyo zenu "atakuhesabuni Mwenyezi Mungu" siku Kiyama. "basi anamsamehe amtakaye" kwa fadhila zake na rehema zake, "na anamuadhibu amtakaye" kwa uadilifu wake, "na Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni muweza" hakimshindi chochote. Maswahaba walipolisikia hilo liliwapa uzito sana; kwa sababu ndani yake kuna kuadhibiwa mpaka kwa yale yaliyoko moyoni, miongoni mwa fikira. Wakamjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha wakashuka chini kwa kupiga magoti, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumepewa majukumu kabla ya hili miongoni mwa amali za mwili yale tuwezayo kuyafanya; mfano kama swala na swaumu na Jihadi na sadaka, lakini imeteremshwa kwako aya hii na wala hilo hatuliwezi. Akasema kuwaambia rehema na amani ziwe juu yake: Hivi mnataka kusema kama walivyosema Mayahudi na Wakristo: "Tumesikia na tumeasi"? bali semeni: "Tumesikia na tumetii, tunataraji msamaha kutoka kwako Mola wetu, na marejeo ni kwako", Maswahaba kuitika amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wakasema: Tumesikia na tumetii, tunataraji msamaha kutoka kwako Mola wetu, na marejeo ni kwako. Walipolizungumza hilo Waislamu kwa ndimi zao, na nyoyo zao zikatii; Mwenyezi Mungu akateremsha sifa njema kwa Mtume na Umma wake kwa kauli yake: "Ameamini Mtume yale yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake na waumini (pia wameamini hivyo)" na zikanyenyekea ndimi zao na nyoyo zao kwa amri ya Mwenyezi Mungu. "Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake, hatutofautishi yeyote katika Mitume wake". Bali tunawaamini wote "na wakasema tumesikia" kauli yako "na tumetii" amri yako, na tunaomba "maghufira yako Mola wetu" na msamaha wako, "na marejeo ni kwao" na mafikio siku itakaposimama hesabu, walipofanya hivyo, na wakasema walichoamrishwa kusema kama kudhihirisha usikivu na utiifu kwa amri za Mwenyezi Mungu; akaupunguzia Mwenyezi Mungu Umma huu na akaifuta aya hiyo, kwa kauli yake: "Hailazimishi Mwenyezi Mungu Nafsi ila kwa kadiri ya wasaa wake" na uwezo wake na nguvu zake na juhudi zake, "ina" thawabu "za yale iliyoyachuma" na kuyafanya miongoni mwa kheri, "na inabeba" adhabu "za yale iliyoyachuma" kama mzigo wa dhambi, na hamuadhibu Mwenyezi Mungu kwa dhambi la mtu mwingine, wala kwa yale yaliyotiwa wasi wasi na nafsi yake. "Mola wetu, usituadhibu" na ukatutesa "ikiwa tutasahau" tukawa hatukukumbuka, "au tukakosea" tukaiacha haki si kwa makusudi, Mwenyezi Mungu akawajibu kwa hilo akasema: Ndiyo, nimefanya hivyo. "Mola wetu Mlezi usitubebeshe mazito" na mashaka na magumu "kama ulivyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu" katika wana wa Waisraeli na wengineo, Mwenyezi Mungu akapokea na akasema: Ndiyo, nimefanya hivyo. "Mola wetu Mlezi na wala usitubebeshe tusiyoyaweza" miongoni mwa majukumu na mabalaa na mambo ambayo hatuwezi kuyabeba, akasema Mwenyezi Mungu: Ndiyo nimefanya hivyo, "na utusamehe" madhambi yetu na utufutie, "na utughufirie" madhambi yetu na uyasitiri, "na uturehemu" kwa rehema zako pana, "wewe ndiye Mole wetu" na bwana yetu; "tunusuru" kwa kusimamisha hoja na ushindi "kwa watu makafiri" katika kupigana nao na kupambana nao, Mwenyezi Mungu akapokea, akasema kuwaambia: Naam, nimefanya hivyo.
Imepokelewa kutoka kwa Omari bin Khattwab -radhi za Allah ziwe juu yake-: Kuwa mwanume mmoja katika Mayahudi alisema kumwambia: Ewe kiongozi wa waumini, kuna Aya ndani ya kitabu chenu hua mnaisoma, laiti ingelikuwa imeteremka kwetu sisi jamii ya Mayahudi, basi tungeifanya siku hiyo kuwa sikukuu, akasmea: Ni Aya ipi? Akasema: "Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini." [Al-Maaida: 3] Omari akasema: Tunaijua siku hiyo, na mahali ilipoteremka aya hiyo kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa kasimama Arafa siku ya Ijumaa.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuja mtu mmoja katika Mayahudi kwa kiongozi wa waumini Omari radhi za Allah ziwe juu yake akasema kumwambia: Kuna aya ndani ya kitabu chenu cha Qur'ani mnaisoma, lau ingeliteremka kwetu jamii ya Mayahudi katika kitabu chetu cha Taurati basi tungeifanya siku hiyo kuwa sikukuu kwa kuisherehekea; kwa kushukuru neema ya kuteremka aya hii tukufu, Omari radhi za Allah ziwe juu yake akasema kumwambia: Ni Aya ipi?. Akasema: "Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini." Akasema Omari radhi za Allah ziwe juu yake: Tunaijua siku hiyo, na sehemu iliyoteremka aya hii tukufu, aya hiyo imeteremka siku ya Iddi, nayo ni siku ya Ijumaa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye akiwa amesimama Arafa, nazo ni siku mbili tukufu kwa Waislamu.