Hedayat “A fruitful harvest”
from the gardens of “ Verses and Hadiths ”
Inspiring Dawah cards that highlight the profound meanings of Quranic verses and Prophetic Hadiths. Presented in an accessible and engaging style to help Muslims gain a deeper understanding of their faith with ease.
About Hedayat
Hedayat is a platform that combines simplicity of design and ease of use
displaying the benefits derived from Verses and Hadiths in
attractive cards with unique designs.
Unique Designs
Cards with unique and attractive designs that express the content of the text
Reliable Materials
Scientifically reliable benefits reviewed by a group of scholars
Easy Browsing
You can browse the cards easily and display them effortlessly
Different Languages
Cards are available in more than 40 languages for the benefit of all
Hadith Cards
Kutoka kwa Hudhaifa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa kwa Omari radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Ni nani miongoni mwenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akieleza kuhusu fitina? Watu wakasema: Sisi tulimsikia, akasema: Huenda nyinyi mnakusudia fitina ya mtu kwa familia yake na jirani yake? Wakasema: Ndivyo, akasema: Fitina hiyo inafutwa na swala na swaumu na sadaka, lakini ni nani miongoni mwenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akieleza fitina ambayo inapiga kama mawimbi ya Bahari? Akasema Hudhaifa: Akawanyamazisha watu wote kwa hilo, nikasema: Mimi, akasema: Nakuapiza kwa Mwenyezi Mungu, umkose baba yako, ni wewe kweli, Hudhaifa, nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hupitishwa fitina katika nyoyo (kama ufumwavyo mkeka) ukindu (kijiti) kimoja kimoja, moyo wowote utakaozifyonza basi hutiwa ndani yake doa jeusi, na moyo wowote unaozikataa hutiwa doa jeupe, moyo huo mpaka unakuwa katika (hadhi ya) mioyo miwili, katika weupe mfano wa jiwe jeupe, hivyo hakuna fitina yoyote inayoweza kuudhuru milele kwa muda wote mbingu na ardhi zitakapoendelea kubakia kwake, na moyo mwingine ni mweusi ti! kama chungu kilichofunikwa, haukubali jema, wala haukatai ovu, isipokuwa matamanio ulionyweshwa", Hudhaifa akasema: Na nikamsimulia kuwa hakika kati yako wewe na fitina hiyo kuna mlango uliofungwa, na hivi karibuni utavunjwa, Omari akasema: Hivi utavunjwa? umepata hasara ya kumkosa baba, na lau ungelifunguliwa basi huenda ungelirejeshwa tena, nikasema: Hapana, bali utavunjwa, na nikamsimulia kuwa mlango huo ni mtu atauawa au kufa, na ni mazungumzo ya kweli wala si maneno ya kubumba. Akasema Abuu Khalidi, nikasema kumwambia Saa'di: Ewe Abuu Maaliki nini maana ya nyeusi ti!? Akasema: Ni weupe ung'aao katika weusi, anasema, nikasema: Na nini maana ya chungu kilichofunikwa? Akasema: Kilichogeuzwa juu chini.
Imepokelewa Imamu MuslimAlikuwa kiongozi wa waumini Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake katika kikao chake akiwa pamoja na kundi la Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, akasema kuwaambia: Ni nani kati yenu aliyemsikia Mtume rehema na amni ziwe juu yake akieleza kuhusu fitina? Wakasema baadhi yao: Sisi tulimsikia akieleza kuhusu fitina, akasema Omari radhi za Allah ziwe juu yake: Huenda nyinyi mnakusudia fitina na mtihani wa mtu katika mambo yake maalumu; kwa mke wake na mtoto wake, kwa kuchupa mipaka katika kuwapenda, na pupa yake kwao, na kushughulishwa nao sana kuliko mambo ya kheri, au kwa uzembe wake, kwa kutotekeleza mambo ya lazima kwake kuyasimamia katika haki, na kuwaadabisha na kuwasomesha, na vile vile fitina ya mtu kwa jirani yake na mfano wake, huenda nyinyi mnakusudia hiyo? Wakasema: Ndiyo, akasema: Hiyo ni fitina inayopelekea kuihesabu nafsi, ikiwa ni pamoja na madhambi ambayo yanatarajiwa kufutwa kwa mema, kama swala na swaumu na sadaka. Lakini ni nani kati yenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiitaja fitina inayowakumba watu wote kwa sababu ya ukubwa wake na wingi wa kusambaa kwake, inayowavuruga watu kama yanavyovurugika mawimbi ya Bahari? Watu wote wakanyamaza: Akasema Hudhaifa bin Yamani radhi za Allah ziwe juu yake: Mimi nilimsikia, Omari radhi za Allah ziwe juu yake akafurahi, na akasema kumwambia: Umenishangaza kwa haya aliyokuja nayo mtu mfano wako!: Basi hebu sema: Hudhaifa akasema: Amesema rehema na amani ziwe juu yake: Fitina itatokea na itafungamana na mwili na upande wa moyo wa mtu kama godoro linavyonasa udongo katika mbavu za aliyelala hapo, na zitamuathiri katika moyo kwa kushikamana nazo sana, na kutoziacha fitina hizi, na kujirejea rejea kwake fitina baada ya fitina, moyo wowote utakaoingia ndani yake, na ukazipenda, na zikachanganyika nao, kama kuchanganyikana na kinywaji na kuingia ndani yake; basi litapigwa ndani ya moyo wake doa jeusi; na moyo wowote utakaozikataa, basi utapigwa ndani yake doa jeupe, mpaka nyoyo zitakuwa katika aina mbili; katika moyo mweupe kwa sababu ya kushikamana na imani kisawasawa, na kusalimika kwake na mapungufu, na kwamba fitina haijaambatana nao, na wala hazijauathiri mfano wa jiwe gumu jeupe ambalo hakuna kitu kinaweza kunasa hapo, hakuna fitina inayoweza kumdhuru mpaka mtu atakapokutana na Mwenyezi Mungu. Na moyo mwingine ni moyo uliobadilika rangi yake na kuwa mweusi kwa sababu ya fitina, ni kama birika lililolala upande, au lililogeuzwa ambalo hakuna maji yanayoweza kutulizana ndani yake, basi vile vile moyo huu hakuna kheri wala hekima yoyote inayoweza kunasa ndani yake, haukubali jema, na wala haukatai baya, isipokuwa yale aliyoyapenda, na nafsi yake kuegemea kwayo. Na akasema Hudhaifa kumwambia Omari: Hakika fitina hiyo hakuna chochote kitakachotokea katika zama za uhai wako, lakini kati yako wewe na fitina hiyo kuna mlango uliofungwa na unakaribia kuvunjwa, akasema: Yaani utavunjwa kwa nguvu? na lau kama ungelifunguliwa basi ungelirejeshewa ukafungwa tena, akasema Hudhaifa: Hapana, bali utavunjwa, na kwamba mlango huo ni mtu atauawa au atakufa. Na niliyoyaeleza ni habari za kweli na si katika habari za Mayahudi na Wakristo, na wala si jitihada za mtu mwenye mtazamo wa mbali, bali ni katika hadithi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: (Nilimjia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- naye akiwa anapiga mswaki kwa mswaki wa mti mbichi, Akasema: na ncha ya mswaki ikiwa katika ulimi wake, naye akisema: AAGH,AAGH (sauti ya kujigogoa), na mswaki ukiwa mdomoni mwake, kana kwamba anajigogoa).
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAnaeleza Abuu Musa Al Ash'ariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: yakuwa yeye alikuja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- naye akipiga mswaki kwa kutumia mti mbichi kwasababu husafisha kikamilifu na hausambaratiki mdomoni; ukakera, na hakika alikuwa kaweka mswaki juu ya ulimi wake, mpaka akawa kana kwamba anajitapisha.
Kutoka kwa Abuubakri Al-sswiddiq -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Mchungeni(mfuatilieni)Muhammadi -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa watu wa nyumba yake.
Imepokelewa na Al-BukhaariyKatika nukuu ya maneno ya Abuubakari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuna ushahidi wa uelewa wa maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- wa haki za watu wa familia ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Na kuwatukuza kwao na kuwaheshimu kwao, yeyote atakayekuwa ni katika watu wa familia yake na akawa kanyooka katika dini na mwenye kufuata sunna za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- basi huyo ana haki mbili: Haki ya uislamu na haki ya udugu wa karibu na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na nikuwa Abuubakari na maswahaba wengine walikuwa wakiwapenda watu wa nyumba ya Mtume na wakiusia kutendewa mazuri.
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yao- amesema: Uliteremshwa Wahyi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka arobaini, akakaa Makkah miaka kumi na tatu, kisha akaamrishwa kuhama, hivyo akahama kwenda Madina, akakaa Madina miaka kumi, kisha akafariki Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: kuwa Wahyi uliteremshwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na akatumwa akiwa na umri wa miaka arobaini, basi akakaa Makkah miaka kumi na tatu baada ya kuteremshiwa wahyi, kisha akaamrishwa kuhama kwenda Madina na akakaa huko miaka kumi, kisha akafariki -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka sitini na tatu.
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Hamtazami Mwenyezi Mungu mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmetahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuburuza nguo au kikoi chini ya kongo mbili kwa kiburi na kujiona, nakuwa mwenye kufanya hivyo atastahiki ahadi ya adhabu kali yakuwa Mwenyezi Mungu hatomtazama siku ya Kiyama mtazamo wa huruma.
Imepokelewa kutoka kwa Abdillah Bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa muislamu mwenye Uislamu kamili ni yule waliosalimika waislamu kutokana na ulimi wake, hawatukani, na wala hawalaani, wala hawasengenyi, na wala hawazunguki kwa aina yoyote miongoni mwa aina za maudhi kwa ulimi wake, na wamesalimika kutokana na mkono wake, hawatendei ubaya, na wala hachukui mali zao pasina haki, na mfano wa hayo, na mwenye kuhama, ni yule mwenye kuacha yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na kutoka kwa Abuu Musa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Mfano wa yule anayemtaja Mola wake na yule asiyemtaja Mola wake, ni mfano wa aliyehai na aliyekufa", Na tamko la Muslim: "Mfano wa nyumba anayotajwa Mwenyezi Mungu ndani yake, na nyumba asiyotajwa Mwenyezi Mungu ndani yake, ni mfano wa aliyehai na aliyekufa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake tofauti kati ya yule anayemtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu na kati ya yule asiyemtaja, kuwa ni mfano wa tofauti iliyopo kati ya aliyehai na aliyekufa katika manufaa yake na uzuri wa muonekano wake, hivyo mfano wa yule anayemtaja Mola wake ni mfano wa aliyehai ambaye muonekano wake umependeza kwa kuwa na nuru ya uhai, na anamanufaa, na mfano wa yule asiyemtaja Mwenyezi Mungu ni mfano wa maiti ambaye muonekano wake umeharibika, na ndani yake kumebatilika, na hana manufaa ndani yake. Na vile vile nyumba inasifiwa kwa sifa ya kuwa hai endapo wakazi wake wanamtaja Mwenyezi Mungu, na vinginevyo itakuwa nyumba mfu kwa kubweteka wakazi wake na kutomtaja Mwenyezi Mungu; na nyumba ikiitwa hai na maiti wanakusudiwa wakazi wa nyumba hiyo.
Kutoka kwa Hisham bin Hakim bin Hizam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake, ya kwamba yeye alipita kwa watu miongoni mwa Anbat huko Sham, wakiwa wamesimamishwa juani, akasema: Wamekuwaje? Wakasema: Wamefungwa kwa sababu ya jizia (kodi), akasema Hisham: Ninashuhudia kuwa nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu watu duniani"
Imepokelewa Imamu MuslimAlipita Hisham bin Hakim bin Hizam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, kwa wakulima wasiokuwa Waarabu huko Sham, wakiwa wamesimamishwa chini ya joto la Jua, akauliza kuhusu jambo lililowapata? Akaambiwa kuwa wamefanywa hivyo kwa sababu ya kutolipa Jizia (kodi) hali yakuwa wanauwezo wa kulipa. Amesema Hisham radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ninashuhudia kuwa hakika nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu watu duniani kwa dhuluma pasina haki.
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu-Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema: "Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba, kwa paji la uso, na akaashiria kwa mkono wake katika pua yake, na mikono miwili na magoti mawili, na ncha za miguu miwili, na wala tusizikunje nguo na nywele".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu kamuamrisha wakati wa swala asujudu kwa viungo saba katika viungo vya mwili; navyo ni: Cha kwanza: Paji la uso: Nao ni ubapa wa uso ulioko juu ya pua na macho mawili, Na akaashiria -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa mkono wake katika pua yake, akieleza kuwa paji la uso na pua ni kiungo kimoja katika vile saba, na akitia msisitizo kwa mwenye kusujudu kuwa agusishe pua yake katika ardhi. Cha pili: na cha tatu: Ni mikono miwili. Cha nne na cha tano: Ni magoti mawili. Cha sita na cha saba: Ni vidole vya miguu miwili. Na akatuamrisha tusizifunge nywele zetu, au kuzikunja kunja nguo zetu katika ardhi wakati wa kusujudu kwa kuilinda ardhi (Isiguse paji la uso); bali tuziache mpaka zidondoke katika ardhi, ili zisujudu pamoja viungo.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Walikuja watu kutoka kabila la Ukli au Uraina, wakauchukia mjini Madina, kwa sababu hali ya hewa ya Madina haikuwafaa. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaamuru waende katika ngamia wa zaka na wanywe mikojo yake na maziwa yake. Wakaondoka, na baada ya afya yao kurejea, wakamuua mchungaji wa ngamia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wakaiba ngamia hao. Habari zikamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake mapema asubuhi, basi akatuma watu kuwafuatilia, na wakapatikana kabla ya mchana. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaamuru mikono na miguu yao ikatwe, macho yao yakachomwa moto, na wakatupwa kwenye jangwa la mawe (Al-Harra). Wakawa wakiomba maji, lakini hawakupewa. Abu Qilaba anasema: Watu hawa walifanya wizi, wakafanya mauaji, walitoka katika Uislamu baada ya kuwa Waislamu, na walitangaza vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeWalikuja watu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kutoka katika kabila la Ukli na Uraina wakiwa ni Waislamu, wakapatwa na ugonjwa na maradhi mazito kwao, yakavimba matumbo yao, wakachukia kuishi Madina kwa sababu chakula hakikuwapendeza wala hali ya hewa. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaamuru waende katika ngamia za sadaka, na wanywe mikojo na maziwa yake. Wakaenda, na walipopona, na wakanenepa, na rangi zao zikarejea kuwa nzuri, wakamuua mchungaji wa ngamia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na wakachukua ngamia. Habari hiyo ilifika asubuhi na mapema, ndipo Mtume akatuma kikosi cha kuwafuata. Wakawakamata, wakati wa jua kupanda juu wakaletwa wakiwa mateka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Mtume akaamuru mikono yao na miguu yao ikatwe, na macho yao yakatobolewa, kwa sababu walimtendea hivyo mchungaji. Kisha wakatupwa kwenye eneo lenye joto (al-Harra), wakawa wakiwaomba maji lakini hawakupewa mpaka walipokufa. Amesema Abuu Qilaba: Ni kwamba wao waliiba, na wakaua, na wakakufuru baada ya imani yao, na wakampiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake.