





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Baraa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Sijawahi kumuona mwenye nywele ndefu na vazi jekundu zuri kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, nywele zake zinapigapiga mabega yake, na mabega yake yako mbali mbali, si mrefu wala mfupi.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Baraa bin Azibi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba hajawahi kumuona yeyote nywele za kichwa chake ni ndefu zimefika katika mabega yake, na anayevaa kikoi na shuka jeusi na lenye mistari myekundu zuri kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, na kwamba miongoni mwa sifa zake za kimaumbile ni kwamba mabega yake yalikuwa mbali mbali, mwenye kifua kipana, na alikuwa na kimo cha kati na kati, kati mrefu na mfupi.
Kutoka kwa Abubakari Swiddiq radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Niliitazama miguu ya washirikina juu ya vichwa vyetu, na sisi tukiwa pangoni, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau kama mmoja wao angelitazama katika nyayo zake angetuona chini ya nyayo zake, akasema: "Ewe Abubakari, kwani ipi dhana yako kwa wawili ambao Mwenyezi Mungu ndiye wa tatu wao".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlisema kiongozi wa waumini Abubakari Swiddiq radhi za Allah ziwe juu yake wakati wa kuhama: Nilitazama katika nyayo za washirikina nao wakiwa wamesimama juu ya vichwa vyetu juu ya pango na sisi tukiwa ndani yake, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau kama mmoja wao angelitazama katika nyayo zake angetuona chini ya nyayo zake, akasema: Ewe Abubakari, kwani ni ipi dhana yako kwa wawili ambao Mwenyezi Mungu ndiye wa tatu wao kwa kuwanusuru na kuwasaidia, na kuwahifadhi na kuwapa muongozo?!
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake-: Ya kwamba Nabii wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake aliandika ujumbe kwenda kwa Kisra, na Kaisari na kwenda kwa Najashi, na kwa kila jabari, akiwaita wote kuja kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na si kwa Najashi yule aliyemswalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake, ya kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliandika ujumbe kabla ya kifo chake kwa Wafalme wa mataifa waliopembezoni mwake, akiwaita katika Uislamu; akamuandikia Kisra, nalo ni jina la kupachikwa la kila Mfalme Uajemi, na kwenda kwa Kaisari, nalo ni jina la kupachikwa kwa kila mfalme wa Roma, na kwenda kwa Najashi nalo ni jina la kupachikwa la kila mfalme wa uhabeshi. Na akaandika pia kwenda kwa kila mfalme jeuri mwenye kuwakandamiza watu, na mwenye kuwatenza nguvu, na akabainisha Anasi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Najashi aliyetumiwa Ujumbe si Najashi yule aliyesilimu na akafariki na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamswali swala ya maiti asiyekuwepo.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mola wangu, hakika mimi ni mwanadamu, basi yeyote katika Waislamu niliyemtukana au kumlaani au kumpiga kwa mjeledi, basi hilo lifanye kwake kuwa ni utakaso na huruma".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Mola wangu, hakika mimi ni mwanadamu, hivyo basi, muumini yeyote niliyemuudhi au kumtukana au kumshutumu, au kumlaani, na nikamuombea kufukuzwa katika rehema yako, au nilimpiga mjeledi au kipigo chochote, basi lifanye hilo kwake kuwa ni utakaso na ibada na twahara na kafara na rehema utakayomhurumia kwayo.
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Palisemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu waombee dua mbaya washirikina, akasema: "Hakika mimi sikutumwa kuwa mtoa laana, bali nilitumwa kuwa huruma".
Imepokelewa Imamu MuslimAlitakwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake awaombee washirikina dua mbaya kwa Mwenyezi Mungu, akasema: Hakika mimi sikuagizwa na Mwenyezi Mungu na sikutumwa kuwa mtoa laana na kuwaombea watu kuwekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu na niwakatie heri, mimi sikutumwa kwa hayo, bali nilitumwa niwe sababu ya heri na rehema kwa watu wote, na kwa waumini hasa.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Jambo la kwanza alilioanza kupewa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake katika wahyi, ni njozi nzuri (za kweli) usingizini. Akawa haoti njozi isipokuwa itatokea, mfano wa mapambazuko ya asubuhi, kisha akapendezeshwa kujitenga peke yake katika pango la Hira, akawa akitawa huko - ambako ni kuabudu - kwa siku kadhaa, kabla ya kurejea katika familia yake, na alikuwa akichukua chakula cha kutosha kwa ajili ya hilo, kisha alikuwa akirudi kwa Khadija na kumpatia chakula mfano wa hicho, mpaka ukweli ukamjia akiwa ndani ya pango la Hira, Malaika akamjia, akasema: "Soma!" akasema: “Mimi si msomaji.” Akanichukua na akanifunika mpaka nikachoka, kisha akaniacha, akasema: "Soma!" Nikasema: “Mimi sio msomaji". Basi akanichukua na akanifunika mara ya pili mpaka nikapatwa na uchovu, kisha akaniacha, kisha akasema: "Soma!" nikasema: "Mimi si msomaji", basi akanichukua na akanifunika kwa mara ya tatu, kisha akaniacha, na akasema: "Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba Amemuumba mwanadamu kwa pande la damu Soma na Mola wako Mlezi ni Mkarimu" [Al-Alaq: 1-3] Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akarudi huku moyo wake ukitetemeka, akaingia kwa Khadija binti Khuwailidi, Allah amuwiye radhi, na akasema: “Nisaidieni, kuwa pamoja nami, Nisaidieni, kuwa pamoja nami” Basi wakamkumbatia mpaka hofu ikamtoka, basi akamwambia Khadija na kumueleza habari hiyo: “Nilihofia sana nafsi yangu" Khadija akasema: Hapana, Wallahi kamwe Mwenyezi Mungu hatokufedhehesha, hakika wewe utaunga udugu, utamsaidia mnyonge, na utaleta kilichokosekana, na utamkirimu mgeni, na utasaidia wakati wa matatizo ya haki, basi Khadija akaondoka naye mpaka wakafika kwa Waraqa bin Nawfal bin Asad bin Abdil-Uzza, binamu yake Khadija, na alikuwa ni mtu aliyeingia katika Ukristo wakati wa kabla ya Uislamu, na alikuwa akiandika vitabu vya Kiebrania, hivyo aliandika kutoka katika Injili kwa Kiebrania, kiasi alichotaka Mwenyezi Mungu akiandike, alikuwa mzee ambaye amekwisha pofuka, basi Khadija akamwambia: Ewe binamu, sikia kutoka kwa mtoto wa ndugu yako. Waraqa akamuuliza: Ewe mpwa wangu, unaona nini? Basi Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamueleza aliyoyaona. Waraqa akamwambia: Hii ndiyo sheria aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu kwa Musa. Hakika ninatamani ningekuwa hai wakati watu wako, pindi watakapokufukuza watu wako. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Hivi, kwani watanifukuza!?" Akasema: "Ndiyo" Kamwe hakuwahi kuja mtu na kitu kama ulichokuja nacho, isipokuwa alitendewa uadui, na ikiwa siku yako hiyo itanifikia nikiwa hai, basi nitakutetea utetezi wa nguvu. Kisha Waraqa hakuchukua muda mrefu akawa amefariki, na wahyi ukasimama kuteremka kwa muda.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza mama wa Waumini, Aisha, Allah amuwiye radhi, kwamba jambo la kwanza aliloanziwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni njozi za kweli usingizini, akawa haoti kitu katika njozi zake isipokuwa kilitokea wazi mfano wa nuru ya asubuhi, kisha akapendezeshwa kujitenga, na alikuwa akijitenga ndani ya pango la Hiraa akifanya ibada kwa siku kadhaa, kabla ya kurudi katika familia yake, na alikuwa akichukua chakula cha kumtosheleza, kisha anarejea kwa mama wa waumini Khadija radhi za Allah ziwe juu yake, anachukua tena chakula cha kutosha idadi ya siku kama hizo, mpaka ikamjia amri ya kweli, naye akiwa katika pango la Hira. Kisha akamjia Malaika Jibril amani iwe juu yake, akamwambia: Soma, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Mimi si mzuri katika kusoma, anasema: Akanishika akanibana mpaka nikachoka na kuishiwa nguvu, kisha akaniachia na kusema: Soma. Nikasema: Mimi si mzuri katika kusoma, basi akanichukua na kunibana kwa mara ya pili mpaka nikachoka na kuishiwa nguvu, kisha akaniacha, akasema: Soma. Nikasema: Sijui kusoma, basi akanichukua na akanifunika mara ya tatu, kisha akaniacha na akasema: "Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba. Kamuumba mwanadamu kutokana na pande la nyama. Soma na Mola wako Mlezi ni Mkarimu" [Al-Qalaq: 1-3]. Akarejea Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na aya kadhaa, lakini kifua chake kilikuwa kikitetemeka kwa kuhofia kifo, akaingia kwa mkewe mama wa waumini Khadija binti Khuwailidi radhi za Allah ziwe juu yake akasema: Nifunikeni na nguo, nifunikeni na nguo, wakamfunikwa kwa nguo mpaka hofu ikamuondokea, akasema kumwambia Khadija na akampa habari ya kilichotokea, na akasema: Nilihofia kifo juu ya nafsi, Khadija akasema: Si hivyo, Wallahi hawezi kukufedhehesha Mwenyezi Mungu kamwe! Hakika wewe utaunga udugu, na utamsaidia mnyonge ambaye jambo lake halina muelekeo, na utamnyanyua fakiri asiye na kitu; kiasi ambacho utawapa watu yale wasiyoyapata kwa asiyekuwa wewe, na utamkirimu mgeni, na utasaidia kutatua matatizo ya haki. Khadija akamchukua mpaka akamfikisha kwa Waraqa bin Naufali bin Asadi bin Abdil -Uzza, ambaye ni mtoto wa ami yake, na alikuwa ni mtu aliyeachana na mila za kale na akawa mkristo, na alikuwa akiandika kutoka katika Injili kwa lugha ya Kiebrania kiasi alichokitaka Mwenyezi Mungu akiandike, na alikuwa ni mzee mtu mzima aliyepofuka macho yake, Khadija akasema kumwambia: Ewe mtoto wa ammi, hebu msikilize mtoto wa ndugu yako, Waraqa akasema kumwambia: Ewe mtoto wa ndugu yangu, umeona nini? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamueleza habari ya kile alichokiona, Waraqa akasema kumwambia: Huyo ni Malaika Jibrili aliyemteremsha Mwenyezi Mungu kwa Musa amani iwe juu yake, natamani lau ningekuwa wakati huo ni kijana mwenye nguvu, laiti kama nitakuwa hai, wakati wakikufukuza watu wako, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hivi, kwani wao watanifukuza?!. Akasema: Ndiyo, kamwe hajawahi kuja mtu na mfano wa hiki ulichokujanacho isipokuwa aliudhiwa na kutendewa uadui, na ikiwa siku yako hiyo itanikuta nikiwa hai basi nitakutetea utetezi wa nguvu. Kisha hakukaa muda mrefu Waraqa akawa amefariki, na wahyi ukachelewa kuteremka tena kwa muda kidogo.
Kutoka kwa Abuu Salama bin Abdilrahman yakwamba Jabiri bin Abdillah Al-Answari radhi za Allah ziwe juu yao, alisema wakati akizungumzia kipindi cha Wahyi, akasema katika hadithi yake: "Wakati nikiwa natembea ghafla nilisikia sauti kutoka mbinguni, nikanyanyua macho yangu, ghafla yule Malaika aliyenijia nikiwa pango la Hiraa nikamuona amekaa juu ya kiti baina ya mbingu na Ardhi, nikaingiwa hofu kwa ajili yake, nikarudi nikasema: Nifunikeni, Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha: "Ewe uliyejigubika 1 Simama na uonye" [Mudathiri: 2] Mpaka katika kauli yake: "Na yaliyo machafu yahame" [Mudathiri: 5]. Wahyi ukachemka na ukafululiza"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati akielezea kukatika kwa Wahyi na kuzuiwa kushuka kwake mwanzo wa kutumwa kwake: Wakati nikiwa natembea katika mitaa ya Makka ghafla nilisikia sauti kutoka mbinguni, nikanyanyua macho yangu, mara ghafla Malaika Jibril aliyenijia kule pango la Hiraa nikamuona amekaa juu ya kiti baina ya mbingu na Ardhi, nikapata hofu na fadhaa kwa sababu yake, nikarudi kwa familia yangu nikasema: Nifunikeni kwa nguo. Akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ewe uliyejifunika nguo" uliyejigubika kwa nguo zako, "simama" kwa ajili ya kufikisha ujumbe "Uonye" na umtahadharishe asiyeamini utume wako. "na Mola wako Mlezi" Mungu wako muabudiwa "Umtukuze" na umhimidi na umtukuze. "Na nguo zako" na mavazi yako "yasafishe" yaondoshe najisi, "na machafu" kama kuabudu masanamu na mizimu "ihame" iache, Wahyi ukawa na nguvu baada ya hapo na ukakithiri.
Kutoka kwa Abuu Haazim amesema: Nilikaa karibu na Abuu Huraira kwa muda wa miaka hamsini, nikamsikia akihadithia kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akisema: "Walikuwa wana wa Israeli wakiongozwa na Manabii, kila anapokufa nabii anafuatiwa na nabii mwingine, na hakika hakuna nabii baada yangu, na watafuata Makhalifa (viongozi) baada yangu, na watakithiri" Wakasema: Unatuamrisha nini? Akasema: "Timizeni ahadi ya utiifu ya moja baada ya nyingine, wapeni haki zao, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza walikuongozeni vipi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa wana wa Israeli walikuwa wakiongozwa na Manabii, na wakisimamia mambo yao kama wanavyofanya viongozi na watawala kwa raia, kila unapodhihiri ufisadi Mwenyezi Mungu anawatumia Nabii kwa ajili ya kunyoosha mambo yao na kuondoa yale waliyoyabadilisha katika hukumu. Na hakika hakuna Nabii baada yangu ili afanye kama waliyokuwa wakiyafanya wale, na watakuja baada yangu watawala, na watakuwa wengi, na utatokea mzozano na kuhitilafiana baina yao. Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao wakamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Unatuamrisha tufanye nini? Akasema: Atakapochaguliwa kiongozi baada ya kiongozi; uteuzi wa kiongozi wa kwanza ndio uteuzi sahihi na ni wajibu kuutimiza na kuuheshimu, na uteuzi wa pili ni batili na ni haramu kwake kuukataa, na wapeni haki zao, na muwatii na muishi nao kwa usikivu na utii isipokuwa katika maasi, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza na atawahesabu kwa yale wanayokufanyieni.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake-: Ya kwamba kuna kundi miongoni mwa wanafunzi wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- waliwauliza wake za Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu amali zake za siri? (walipojibiwa) wakasema baadhi yao: Mimi sitooa wanawake. Na wakasema baadhi yao: Na mimi sitokula nyama. Na wakasema baadhi yao: Sitolala juu ya godoro. Hilo likamfikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akamshukuru Mwenyezi Mungu na akamsifia, na akasema: "Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi ninaswali na ninalala na ninafunga na ninakula, na ninaoa wanawake; atakayeuchukia muongozo wangu basi hayuko nami".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeLilikuja kundi la Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, katika nyumba za wake za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakiuliza kuhusu ibada zake za siri ndani ya nyumba yake, walipoelezwa wakawa kana kwamba za kwao wameziona ndogo, wakasema: Na tuko wapi sisi na Mtume rehema na amani ziwe juu yake? hali yakuwa amekwisha samehewa yaliyotangulia katika madhambi yake na yajayo, ukilinganisha na ambaye hajajua hata kupatikana kwa msamaha, huyu anahitaji kupitiliza katika kufanya ibada huenda akaupata msamaha huo. Kisha wakasema baadhi yao: Sitooa wanawake. Na wakasema baadhi yao: Sitokula nyama. Na wakasema baadhi yao: Sitolala katika godoro. Hilo likamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akachukia, na akawahutubia watu, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamtukuza, na akasema: Wana nini watu fulani waliosema kadhaa wa kadhaa?! Wallahi mimi ndiye ninayemuhofu sana Mwenyezi Mungu kuliko watu wote na ndiyo mchamungu wenu, lakini ninalala ili nipate nguvu ya kusimama, na ninafungua ili nipate nguvu ya kufunga, na ninaoa wanawake, atakayeipuuza njia yangu, na akaona njia nyingine ndio iliyokamilika, na akachukua njia ya asiyekuwa mimi, huyu hayuko nami.