





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abubakari Swiddiq, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, ya kwamba yeye alisema: Enyi watu! Hakika nyinyi mnasoma aya hii: "Enyi mlioamini lililo lazima juu yenu ni nafsi zenu hatokudhuruni aliyepotoka ikiwa mtaongoka", na hakika mimi nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika watu wakimuona dhalimu na wasimchukulie hatua, basi wako karibu Mwenyezi Mungu kuwaadhibu wote kwa adhabu yake."
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na AhmadAnasimulia Abubakari Swiddiq, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, kuwa watu wanasoma aya hii: "Enyi mlioamini lililo lazima juu yenu ni nafsi zenu hatokudhuruni aliyepotoka ikiwa mtaongoka" [Maaida: 105] Na wanaielewa kuwa mtu anatakiwa ajitume kuirekebisha nafsi yake pekee, na kwamba hatodhurika baada ya hapo kwa upotofu wa wale waliopotea, na kuwa hawajaamrishwa kuamrisha mema na kukataza maovu! Basi akawajulisha kuwa haikuwa hivyo, na kwamba alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Iwapo watu watamuona dhalimu na wasimzuie na dhulma yake, na hali yakuwa wana uwezo wa kumzuia, basi Mwenyezi Mungu yuko karibu kueneza adhabu kutoka kwake kwa wote, anayefanya uovu na anayenyamaza juu yake.
Kutoka kwa Hudhaifa bin Yamani -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye alisema; "Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mtaamrisha mema, na mtakataza mabaya; au hakika atakuwa karibu zaidi Mwenyezi Mungu kukutumieni adhabu toka kwake, kisha mtamuomba na wala hamtojibiwa".
Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na AhmadKauli yake -Rehema na Amani ziwe juu yake-"Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake" Hiki ni kiapo anaapa Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa Mwenyezi Mungu; kwasababu yeye ndiye ambaye nafsi za waja ziko mkononi mwake -Ametakasika na kutukuka-Anaziongoza akitaka, na anazipoteza akitaka, na anazifisha akitaka, na anazibakisha akitaka, hivyo nafsi zote ziko mkononi mwa Mwenyezi Mungu katika uongofu na upotovu, na kuzihuisha na kuzifisha na maamuzi na mipangilio katika kila kitu, kama alivyosema Mtukufu aliyetakasika-: "Na ninaapa kwa nafsi (roho) na aliyeiumba, Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake), Hivyo nafsi ziko mkononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake; na kwasababu hii aliapa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, Na alikuwa mara nyingi akiapa kwa kiapo hiki: (Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake), na wakati mwingine alikuwa akisema: (Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mkononi mwake); kwasababu nafsi ya Muhammad ndio nafsi safi zaidi kuliko zote, akaapa kwa hilo; kwakuwa ni nafsi safi. Kisha akataja alichokiapia, nacho nikuwa tusimamie kuamrisha mema na kukataza maovu; au vinginevyo atufunike Mwenyezi Mungu kwa adhabu itokayo kwake, mpaka ifikie mahali tunamuomba na wala hatukubalii, Na huu ni uwazi juu umuhimu wa kuamrisha mema kama swala na zaka na kutimiza haki, na umuhimu wa kukataza mabaya kama zinaa na riba na maharamisho mengine, na hii inakuwa kwa vitendo kwa yule ambaye ana mamlaka kama baba katika nyumba yake na mgambo wenye jukumu hilo na polisi, au kwa kauli nzuri na hili ni kwa kila mtu, au kuchukia kwa moyo pamoja na kuondoka mahala palipo na uovu, na hii ni kwa yule asiyeweza kukemea kwa vitendo au kwa kauli.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kila kiungo kwa watu kina sadaka, kila siku inayochomozewa jua: Ukafanya uadilifu kati ya watu wawili ni sadaka, na ukimsaidia mtu katika mnyama wake ukambeba kumpandisha au ukamnyanyulia mzigo wake ni sadaka, na neno zuri ni sadaka, na kwa kila hatua unayokwenda kuelekea msikitini ni sadaka, na ukiondoa maudhi njiani ni sadaka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa kila Muislamu ni wajibu kila siku kuhesabu kila kiungo cha mifupa yake kuwa ni sadaka ya hiyari kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa ni njia ya kumshukuru kwa neema ya afya, na kwamba amevifanya viungo vyake kuwa na maungio yanayomuwezesha kukunja na kukunjua, Sadaka hii inafanywa na matendo yote mema na haitegemei kutoa pesa, na miongoni mwake: Uadilifu wako na kusuluhisha kwako kati ya wagomvi wawili ni sadaka, Na katika kumsaidia kwako asiyejiweza kupanda katika mnyama wake, ukambeba, au ukamnyanyulia mzigo, ni sadaka. na neno zuri kuanzia kumtaja Mwenyezi Mungu na dua na salamu na mengineyo, ni sadaka, na kwa kila hatua unayoipiga kwenda katika swala, ni sadaka, na kuondoa kila yanayoudhi katika njia ni sadaka.
Kutoka kwa Wail bin Hadhrami amesema: Salama bin Yazidi Al-Ju'fi radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, hebu tueleze endapo watasimama viongozi wetu wakituomba haki zao, na hali wao wanazuia haki zetu, unatuamrisha nini? Mtume akampuuza, kisha akamuuliza, akampuuza, kisha akamuuliza katika mara ya pili au ya tatu, Ash'athi bin Kaisi akamvuta, na akasema: "Wasikilizeni na muwatii, kwani wao wana yao waliyobebeshwa nanyi mna yenu mliyobebeshwa"
Imepokelewa Imamu MuslimAliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu viongozi wanaotaka haki zao kwa watu ikiwemo kusikilizwa na kutiiwa, na wanazuia haki zilizo juu yao; kama kutenda uadilifu na kuwapa watu ngawira na kurejesha mali za dhulma na kufanya usawa, unatuamrisha tufanye nini tukiwa pamoja nao?. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akampuuza; kana kwamba kalichukia swali hili, lakini muulizaji akarudia mara ya pili na ya tatu, Ash'athi bin Kaisi akamvuta muulizaji ili amnyamazishe. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akajibu na akasema: Sikilizeni kauli zao, na mtii amri zao; kwani wana yao waliyobebeshwa na kulazimishwa kuyafanya ikiwemo uadilifu na raia kuwapa haki zao, na nyinyi mna yenu mliyobebeshwa kama kutii na kutimiza haki na kusubiri juu ya mabalaa.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika dini ni nyepesi, na hatoifanyia mkazo dini yeyote ila itamshinda, basi shikamaneni na mfanye kadiri ya uwezo yanayoweza kukuwekeni karibu, na toeni bishara, na takeni msaada nyakati za asubuhi au mchana au sehemu ya usiku"
Imepokelewa na Al-BukhaariyAlibainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Dini ya Uislamu imeegemezwa katika usahilishaji na wepesi katika mambo yake yote, na usahilishaji unathibitishwa pale panapotokea sababu ya kutokuwa na uwezo na haja, kwa sababu kuzama ndani sana katika matendo ya dini na kuacha upole matokeo yake ni kutoweza na kukoma kufanya amali zote au baadhi yake. Kisha akahimiza rehema na amani ziwe juu yake kuwa kati na kati pasina kupitiliza; Mja asifanye uzembe katika yale aliyoamrishwa, na wala asijibebeshe asiyoyaweza, akishindwa kuifanya amali nzima kamili; basi afanye inayokaribiana na hiyo. Alitoa habari njema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya malipo makubwa ya amali ya kudumu, hata ikiwa ni kidogo, kwa wale ambao hawawezi kufanya amali nzima kikamilifu, kwa sababu ikiwa kushindwa huko hakutokani na yeye mwenyewe, hakutopelekea kupunguzwa kwa malipo yake. Na kwa kuwa ulimwengu huu kwa hakika ni mahala pa kusafiri na mapito ya kuelekea Akhera, ameamrisha rehema na amani ziwe juu yake kutaka msaada katika kudumisha ibada kwa kuiweka nyakati tatu ambazo mtu anakuwa na hamasa: Wakati wa kwanza ni Asubuhi: Kwa kwenda mwanzo wa mchana; kati ya swala ya Alfajiri na kuchomoza jua. Wa pili: Mchana: Kwa kwenda wakati linapopinduka jua. Wa tatu: Giza: kwa mwendo wa usiku mzima au sehemu yake, na kwa sababu amali ya usiku ni ngumu zaidi kuliko amali ya mchana, akaamrisha kufanya baadhi yake, kwa kauli yake: Na baadhi ya usiku.
Imesimuliwa kutoka kwa Ali, Mwenyezi Mungu amridhie, kwamba alisema: Alituma kikosi Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuweka kiongozi bwana mmoja katika Maanswari (watu wa Madina), na akawaamrisha wamtii, akachukia, akasema: Hivi hakukuamrisheni Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mnitii? Wakasema: Ndivyo, akasema: Nikusanyieni kuni, wakakusanya, akasema: Niwashieni moto, wakauwasha, akasema: Ingieni humo, wakataka kuuingia, baadhi yao wakaanza kuwashika wenzao, huku wakisema: Tumeukimbia moto tukaelekea kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, waliendelea katika hali hiyo mpaka moto ukazima, zikatulia hasira zake, habari zikamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Laiti wangeingia wasingelitoka humo mpaka siku ya Kiyama; Utiifu unakuwa katika jambo jema".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlituma Jeshi Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akamfanya bwana mmoja katika Maanswari kuwa kiongozi wao, na akawaamrisha wamtii, yule kiongozi akawakasirikia na akasema kuwaambia: Hivi hakuwaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mnitii? Wakasema: Hasa! akasema: Basi nimekuamrisheni nikusanyieni kuni na muwashe moto kisha muingie humo, wakakusanya kuni na wakawasha moto, walipotaka kuingia humo, wakaanza kutazamana wao kwa wao. Na wakasema: Hakika sisi hatukumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake ila ni kwa sababu ya kuukimbia moto, je, tuuingie? wakiwa bado wako katika hali hiyo muwako wa moto ukazimika, na ikatoweka kwa kiongozi ghadhabu yake. Akaelezwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hilo akasema: Lau wangelimtii na wakaingia katika moto waliouwasha basi wangeliadhibiwa humo na wasingetoka kamwe kwa muda wa kubakia dunia, hakuna kumtii kiumbe katika kumuasi muumba; bali utiifu ni wajibu katika mambo mema na si katika maasi.
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika watakuja viongozi wanaosema uongo na kudhulumu (watu), atakayewasadikisha kwa uongo wao na akawasaidia katika dhulma yao basi huyo si katika mimi, na mi si miongoni mwake, na wala hatokunywa katika Hodhi langu, na ambaye hatowaamini kwa uongo wao na akawa hakuwasaidia katika dhulma yao, basi huyo yuko miongoni mwangu, na mimi ni miongoni mwake, na atakunywa katika Hodhi langu".
Imepokelewa na AhmadAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba watatawala watu baada ya kifo chake viongozi wanaosema uongo katika mazungumzo yao wanasema wasiyoyatenda, na wanadhulumu katika hukumu, atakayeingia kwao na akawasadikisha kwa uongo wao, au akawasaidia kufanya dhulma au kuitamka, kama kutoa majibu kwa lengo la kujipendekeza kwao na kutaraji mazuri waliyonayo; basi mimi niko mbali naye na yeye si miongoni mwangu, wala hatokuja katika Hodhi la mto Kauthari siku ya Kiyama, na ambaye hatoingia kwao na kuwasadikisha kwa uongo wao na kuwasaidia juu ya dhulma yao basi huyo ni miongoni mwangu na mimi ni miongoni mwake, na atakunywa katika Hodhi langu siku ya Kiyama.
Imepokelewa Kutoka kwa Suhaib -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kulikuwa na Mfalme mmoja katika wale waliokuwa kabla yenu, na alikuwa na mchawi wake, alipozeeka, akasema kumwambia Mfalme: Hakika mimi nimezeeka, nitumie kijana nitakayemfundisha uchawi, basi akamtumia kijana ili amfundishe, katika njia aliyokuwa akipita kijana huyo kulikuwa na Kasisi basi, siku moja akakaa naye na akasikiliza mazungumzo yake, yakampendeza sana, basi akawa anapokwenda kwa mchawi anapita kwa Kasisi na anakaa kwake, akifika kwa mchawi mchawi anampiga, basi akamlalamikia hilo Kasisi akasema: Ukimuhofia mchawi, basi mwambie nyumbani walinichelewesha, na ukihofia familia yako basi waambie: mchawi alinichelewesha, basi akaendelea katika maisha hayo, mara ghafla alifika mahali akakuta kuna mnyama mkubwa aliyezuia watu kutoka katika shughuli zao, basi akasema: Leo ndio nitajua je, mchawi ndio bora au yule kasisi ndio bora? Akachukua jiwe na akasema: Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa suala la huyu Kasisi ndio linapendeka zaidi kwako basi muuwe mnyama huyu, ili watu waendelee na shughuli zao, basi akampiga, akawa kamuua, na watu wakaendelea na shughuli zao, akawa kamuendea Kasisi akamueleza tukio hilo, mchamungu akasema kumwambia: Ee mwanangu basi leo wewe umekuwa bora kuliko mimi, kwa hakika jambo lako limefikia pazuri kwa namna ninavyoona, na kwa hakika utapewa majaribu, ukipewa mateso yoyote basi usimuonyeshe yeyote mahala nilipo, na kijana yule alikuwa akiponya vipofu na wenye ukoma na akiwaponya watu kutokana na maradhi mbali mbali, akazisikia habari hizo mmoja kati ya jamaa wa Mfalme alikuwa amekwishapofuka, basi akamuendea akiwa na zawadi, na akamwambia: Yote unayoyaona hapa ni zawadi yako endapo utaniponyesha. Akasema: Hakika mimi simponyeshi yeyote bali anayeponya ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, na endapo utamuamini Mwenyezi Mungu basi nitamuomba Mwenyezi Mungu naye atakuponya, basi yule kipofu akamuamini Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu akamponya, basi bwana huyu akaenda kwa Mfalme na akakaa kama alivyokuwa akikaa awali, basi Mfalme kwa mshangao mkubwa akamuuliza: Ni nani aliyekurejeshea macho yako?!! Akasema: Ni Mola wangu Mlezi. Mfalme akasema: Hivi, kwani una mungu mwingine zaidi yangu? Akasema: Mola wangu Mlezi na Mola wako ni Mwenyezi Mungu, akamkamata, na akaendelea kumpa mateso mpaka akamuelekeza mahali alipo yule kijana, basi yule kijana akakamatwa na akaletwa kwa Mfalme, Mfalme akasema kumwambia: Ee mwanangu hivi uchawi wako umefikia kuponya vipofu na wakoma?, na unafanya mambo kadhaa wa kadhaa?. Akasema: Mimi simponyi yeyote, bali anayeponya ni Mwenyezi Mungu, akamkamata akamtesa, akaendelea kumpa mateso mpaka akamuonyesha mahali alipo Kasisi, basi akaletwa yule mchamungu, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, basi Mfalme akaagiza msumeno, akautia msumeno kati kati ya utosi wake, akamchana mpaka upande mmoja wa kiwiliwili chake ukadondoka, kisha akaletwa yule bwana aliyekuwa akikaa pamoja na Mfalme, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, basi akautia msumeno kati kati ya utosi wake, akamchana mpaka upande mmoja wa kiwiliwili chake ukadondoka, kisha akaletwa yule kijana, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, basi akamkabidhi kwa kundi la watu wake, akasema: Mpelekeni katika mlima fulani, kisha pandeni naye mlimani, mkifika keleleni, endapo atarejea katika dini yake basi muacheni, asiporejea basi mrusheni chini, basi wakaenda naye, na wakapanda naye mlimani, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze dhidi yao kwa chochote ukitakacho, basi mlima ukawatetemesha na wakaanguka wote, na akarudi kwa Mfalme huku akitembea, Mfalme akasema kumuuliza: Wamefanya nini jamaa zako?! Akasema: Mwenyezi Mungu kanitosheleza dhidi yao. Basi Mfalme akamkabidhi kwa kundi jingine katika watu wake, akasema: Nendeni mkambebe katika mtumbwi, muende naye mpaka mfike naye kati kati ya bahari, basi akikubali kurudi katika dini yake maucheni, asipokubali mtumbukizeni, basi wakaenda naye, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze dhidi yao kwa chochote utakacho, basi ule mtumbwi ukawamwaga baharini, na wakaangamia wote, na akarudi kwa Mfalme akiwa anatembea, Mfalme akasema kumuuliza: Wamefanya nini jamaa zako? Akasema: Mwenyezi Mungu kanitosheleza dhidi yao, kisha akasema kumwambia Mfalme: Hakika wewe huwezi kuniua mpaka utekeleze ntakachokuamrisha, akasema: Ni kipi hicho? Akasema: Uwakusanye watu katika uwanja mmoja na unitundike juu ya shina la mti, kisha uchukue mshale mmoja katika ala yangu ya mishale, kisha weka mshale kati kati ya upinde, kisha sema: Bismillaah -Naanza kwa jina la Mwenyezi Mungu- Mola Mlezi wa kijana huyu, kisha nirushie, kwani ukifanya hivyo bila sha utaniua, basi Mfalme akawakusanya watu katika uwanja mmoja, na akamtundika yule kijana juu ya shina la mti, kisha akachukua mshale mmoja kutoka katika ala ya mishale yake, kisha akauweka mshale kati kati ya upinde na akasema: Bismillaah -Naanza kurusha kwa jina la Mwenyezi Mungu- Mola Mlezi wa kijana huyu, kisha akamrushia ukamchoma ule mshale kichwani kwake kati ya jicho na sikio, basi yule kijana akashika kwa mkono wake mahali palipochomwa na mshale akawa amefariki, basi watu wote wakasema kwa sauti moja: Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu!. Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu!. Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu!. Wapambe wakamfuata Mfalme wakamwambia: Unaona ulichokuwa ukikwepa?! Wallahi limetokea ulilokuwa ukilikwepa, tayari watu wote sasa wameamini! Basi Mfalme akaamrisha kuchimbwa Mahandaki, kati kati ya mitaa, basi yakachimbwa, na akakoka moto mkubwa ndani yake, na akasema: Yeyote ambaye hatorejea katika dini yake, basi mchomeni humo, au mwambieni jitose mwenyewe, basi wanajeshi wake wakafanya hivyo, mpaka akaja mwanamke mmoja akiwa na mtoto wake mchanga, basi mama yule akawa mzito sana kujitosa ndani ya moto ule, basi mwanaye yule mchanga akazungumza kumwambia mama yake: Ewe mama yangu kuwa na subira hakika wewe uko katika haki".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kulikuwa na Mfalme mmoja katika umma zilizopita kabla yetu, na alikuwa na mchawi wake, alipozeeka mchawi, akasema kumwambia Mfalme: Bila shaka mimi nimezeeka, nitumie kijana ili nifundishe uchawi. Basi Mfalme akamtumia kijana ili amfundishe, kukawa katika njia ya kijana anapokwenda kwa mchawi kuna mchamungu, siku moja akakaa kwake na akasikiliza mazungumzo yake, yakampendeza, basi akawa kila anapokwenda kwa mchawi anapita kwa mchamungu anakaa kwake, anapofika kwa mchawi mchawi anampiga kwa sababu ya kuchelewa, akamlalamikia mchamungu kitendo hicho, akasema: Ukimhofia mchawi, basi mwambie: Nyumbani walinichelewesha, na ukihofia watu wako basi waambie: Mchawi alinichelewesha, basi wakati akiendelea kuisha katika maisha hayo, ghafla alifika mahali kulikuwa na mnyama mkubwa sana, aliyekuwa kawazuia watu kuendelea na shughuli zao, akasema: Leo ndio nitajua je, mchawi ndio bora au mchamungu ndio bora? Akachukua jiwe, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa suala la mchamungu linapendeka zaidi kwako kuliko jambo la mchawi basi muuwe mnyama huyu, ili watu waendelee na shughuli zao, akamrushia akamuua, na watu wakaendelea na shughuli zao, akamuendea mchamungu akamueleza, mchamungu akasema: Ee mwanangu wewe leo umekuwa bora kuliko mimi, jambo lako limefikia hapa ninapopaona, na kwa hakika utapewa mitihani, ikitokea umepewa mithani basi usimuoneyshe yeyote hapa nilipo, na wakati huo kijana alikuwa akiponya vipofu na wenye mbaranga, na akiwatibu watu kutokana na maradhi yote kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, akasikia taarifa hizi mmoja kati ya jamaa wa Mfalme alikuwa amekwishapofuka, akamuendea akiwa na zawadi nyingi, akasema kumwambia kijana: Zote hizi zilizoko hapa katika zawadi ni kwa ajili yako endapo utaniponya. Akasema: Hakika mimi simponyi yeyote, bali anayeponya ni Mwenyezi Mungu, ikiwa wewe utamuamini Mwenyezi Mungu nitakuombea na atakuponya, basi akamuamini Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu akamponya, akamuendea Mfalme, akakaa karibu naye kama alivyokuwa akikaa awali, Mfalme akasema kumwambia: Ni nani aliyekururejeshea macho yako? Akasema: Ni Mola wangu Mlezi, akasema: Hivi una mola mwingine zaidi yangu? Akasema: Mola wangu Mlezi na Mola wako ni Mwenyezi Mungu. Akamchukua na kumtesa, akaendelea kumpa mateso mpaka akamuelekeza kwa yule kijana, akaletwa yule kijana, Mfalme akasema kumwambia: Ee mwanangu, hivi uchawi wako ndio umefikia kiwango cha kuponya vipofu na wenye mbaranga, na unafanya kadhaa wa kadhaa. Akasema: Hakika mimi simponyi yeyote, bali anayeponya ni Mwenyezi Mungu, basi akamchukua akaanza kumtesa, akaendelea kumpa mateso mpaka akamuelekeza kwa yule mchamungu. Akaletwa yule mchamungu, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, akaagiza uletwe msumeno, akautia msumeno kati kati ya utosi wake, akamchana kwa msumeno huo vipande viwili. Kisha akaletwa yule jamaa wa Mfalme, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, akautia msumeno kati kati ya utosi wake, akamchana kwa msumeno huo vipande viwili. Kisha akaletwa yule kijana, akaambiwa, rudi katika dini yako, akakataa, akamkabidhi kwa wanaume katika jamaa zake, walikuwa kati ya watatu mpaka kumi. Akasema: Nendeni naye mpaka katika mlima kadhaa wa kadhaa, kisha mpandisheni juu ya mlima, mkifikia kileleni, muulizeni, yuko tayari kurudi katika dini yake?, ikiwa atakuwa tayari kurudi basi muacheni, na asipokuwa tayari mtupeni chini, basi wakaenda naye na wakapanda naye juu ya mlima. Akasema yule kijana: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze dhidi yao kwa chochote ukitakacho, basi mlima ukawatetemesha, na ukatikisika mtikisiko mkubwa sana mpaka wakaanguka wote, na akarudi kwa Mfalme akiwa anatembea. Mfalme akasema kumwambia kwa mshangao mkubwa: Jamaa zako wamefanya nini?!! Akasema: Mwenyezi Mungu kanitosheleza dhidi yao. Basi akamkabidhi kwa kundi jingine katika jamaa zake, akasema: Nendeni naye mkambebe katika boti ndogo, kisha nendeni naye mpaka kati kati ya bahari, ikiwa atakuwa tayari kurudi katika dini yake basi muacheni, akikataa basi mtupeni baharini. Basi wakaondoka naye, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze dhidi yao kwa chochote ukitakacho, basi boti ikawapindua wakawa wameangamia wote, na akarudi kwa Mfalme akiwa anatembea. Mfalme akasema: Wamefanya nini jamaa zako?!! Akasema: Mwenyezi Mungu kanitosheleza dhidi yao, kisha akasema kumwambia Mfalme: Hakika wewe huwezi kuniua mpaka ufanye nitakayokuamrisha. Akasema: Ni yapi hayo? Akasema: Uwakusanye watu katika uwanja wa wazi, na unitundike juu ya shina la mti, kisha chukua mshale mmoja kutoka katika ala yangu ya mishale, kisha weka mshale katikati ya upinde, kisha sema: Bismillaah -kwa jina la Mwenyezi Mungu- Mola wa kijana huyu, kisha nirushie, basi ukifanya hivyo bila shaka utaniua, basi akawakusanya watu katika sehemu mmoja, kisha akamtundika juu ya shina la mti, kisha akachukua mshale mmoja katika ala yake, kisha akauweka mshale kati kati ya upinde, kisha akasema: Bismillah -kwa jina la Mwenyezi Mungu- Mola wa kijana huyu, kisha akamrushia, mshale ukamchoma kati ya sikio lake na jicho lake, akaweka mkono wake mahala alipochomwa mshale, na akawa amefariki. Watu wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu, Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu, Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu. Watu wakamfuata Mfalme wakamwambia: Unaona sasa, ulichokuwa ukikihofia? Bila shaka tunamuapa Mwenyezi Mungu kimekutokea ulichokuwa ukikihofia, ambacho ni watu kumfuata kijana huyo, na wote kumuamini Mola wake, akaamrisha Ardhi ipasuliwe mashimo makubwa ya msitatili (pembe nne) kati kati ya njia, na akawasha na kuuchochea moto ndani yake, na akasema: Yeyote ambaye hatorudi katika dini yake basi mtupeni humo, basi wakafanya alichokiamrisha Mfalme, mpaka akaja mwanamke mmoja akiwa na mwanaye mchanga, akasimama, na akabakia hapo na akachukia kuingia katika moto, basi mwanaye akasema kumwambia: Ewe mama yangu vumilia, kwani hakika wewe uko katika haki.
Kutoka kwa Ubai bin Ka'ab radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Kulikuwa na mtu ambaye sifahamu kama kuna mtu alikuwa akiishi mbali kuliko yeye, na swala ilikuwa haimpiti, akaambiwa: Bora ungelinunua Punda ukimpanda nyakati za giza, na unapopita kwenye sehemu ya jangwa. Akasema: "Hainifurahishi nyumba yangu kuwa karibu na Msikiti, mimi ninapenda niandikiwe malipo ya kutembea kwangu, na kurudi kwangu ninaporejea kwa Watu wangu" Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu amekukusanyia malipo yote hayo".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Ubai bin Kaab radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba bwana mmoja katika Maanswari (watu wa Madina) alikuwa ni mtu anayeishi mbali kuliko wote kutoka ulipo Msikiti wa Mtume, na ilikuwa haimpiti swala yoyote; bali anahudhuria swala zote pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akaambiwa: Lau ungenunua punda wa kumpanda katika giza la usiku, na katika joto la Ardhi wakati wa mchana, akasema: Sipendezwi nyumba yangu kuwa karibu na msikiti, hakika mimi ninataka aniandikie Mwenyezi Mungu hatua zangu wakati wa kuja katika swala msikitini, na kurudi kwangu ninaporudi kwa watu wangu, yakafika maneno yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Hakika amekukusanyia Mwenyezi Mungu kwako yote hayo".