





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Barraa bin A'zib -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- "Yakwamba Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa safarini, akaswali swala ya ishaa ya mwisho, akasoma katika moja ya rakaa mbili kwa sura ya wattin wazzaitun, sijawahi kumsikia yeyote mwenye sauti nzuri au kisomo kizuri zaidi yake".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAlisoma Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa sura ya wattin wazzaitun ndani ya rakaa ya kwanza katika swala ya ishaa; kwasababu yeye alikuwa safarini, na safari ni lazima izingatiwe kufanya wepesi (tahfifu) kwasababu ya shida na matatizo yake, na pamoja nakuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa msafiri, lakini hakuyaacha yale yanayochochea kupatikana kwa utulivu na kuhudhurisha moyo wakati wa kusikiliza Qur'ani, nako ni kupendezesha sauti katika kisomo cha swala.
Kutoka kwa Abdallah bin Maliki bin Buhaina radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapo swali anatanua kati ya mikono yake mpaka unaonekana weupe wa kwapa zake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa rehema na amani zimshukie anaposwali, anaikunjua mikono yake wakati wa kusujudu. Alisogeza kila mkono kutoka upande wa karibu yake, kama mbawa mbili, mpaka rangi ya ngozi ya makwapa yake inaonekana; Hii ni katika kupitiliza kuitanua mikono na kuitenganisha na mbavu zake.
Kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: alipozidiwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akawa anagubikwa na matatizo (kilevi cha kifo -sakaratil mauti), akasema Fatma: Nalia kwa matatizo ya baba yangu, akasema: "Hakuna kwa baba yako matatizo baada ya leo". Basi alipofariki Fatma -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- alisema: Ewe baba yangu, kamuitikia Mola aliyemuita! Ewe baba yangu, pepo ya Firdausi ndiyo mafikio yake, Ewe baba yangu, kwa Malaika Jibril ndiko tunako tangaza msiba wake, alipozikwa alisema Fatma -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Hivi zimeridhika nafsi zenu kumwaga udongo juu ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-?!
Imepokelewa na Al-BukhaariyInatupa picha hadithi hii juu ya subira ya Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- juu ya kilevi cha kifo, alipozidiwa katika maradhi ambayo alifariki kwaajili yake, akawa anagubikwa na shida kutokana na ukali wa yale yanayompata; kwasababu yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- yanamzidia maumivu na maradhi, na hii ni kwasababu ya hekima ya hali ya juu: ili ayafikie yale yalioko kwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa daraja za juu kwasababu ya malipo ya subira yake, kila anapofunikwa na shida Fatma -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- anasema: "Nalia kwa misukosuko ya baba yangu" anaumia kwasababu ya matatizo yanaomfika, kwasababu yeye ni mwanamke, na mwanamke huwa hawezi kuvuta subira. Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Hakuna kwa baba yako matatizo baada ya leo"; kwasababu yeye Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alipohama kutoka duniani kahamia kwa rafiki aliyejuu, kama alivyokuwa -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema wakati akikumbwa na shida za kifo- "Ewe Mola wangu kwa rafiki aliyejuu, Ewe Mola wangu kwa rafiki aliyejuu, huku akitazama katika paa la nyumba -Rehema na Amani ziwe juu yake-". Alipofariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akawa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akimlilia kwa huzuni, lakini ilikuwa chinichini (haikuwa kwa makelele), na wala haimaanishi kuchukizwa na maamuzi ya Mwenyezi Mungu na mipango yake. Na kauli yake: "Kamuitikia Mola aliyemuita"; Ni kwasababu Mwenyezi Mungu ndiye ambaye mkononi mwake kuna ufalme wa kila kitu, na ajali za viumbe ziko mkononi mwake. kamuitikia muitaji wa Mwenyezi Mungu, nayo nikuwa yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- atakapokufa atakuwa kama wengineo katika waumini, inapandishwa roho yake mpaka isimamishwe mbele ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka juu ya mbingu ya saba. Na kauli yake: "Ewe baba yangu pepo ya Firdausi ndiyo mafikio yake" -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwasababu yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- ndio kiumbe mwenye nafasi ya juu kuliko wote peponi, kama alivyosema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Niombeeni mimi utetezi; kwani hiyo ni nafasi peponi ambayo haistahiki kwa yeyote ila kwa mja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu, na ninataraji mimi kuwa ndiye mwenye nafasi hiyo", na wala haina shaka kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mafikio yake ni pepo ya Firdausi, na pepo ya Firdausi ndiyo daraja ya juu zaidi katika daraja za pepo, na paa lake lililo juu yake ni Arshi ya Mola Aliyetakasika na kutukuka, na Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- yuko daraja ya juu zaidi kuliko hiyo. Kauli yake: "Ewe baba yangu kwa Jibrili ndiko tunako tangaza msiba wake" Na akasema: Hakika sisi tunatoa habari za kifo chake kwa Jibrili kwasababu Jibrili ndiye aliyekuwa akimuijia akimfundisha kwa wahyi zama za uhai wake, na wahyi umefungamana na uhai wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-. Kisha pindi alipobebwa na akazikwa, alisema -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Hivi nafsi zenu zimeridhika kumwaga udongo juu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-? Yaani hii ni kwasababu ya huzuni yake kubwa juu yake, na huzuni yake na maumivu yake ni kwa kutengana na mzazi wake, na kujua kwake kuwa maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Mwenyezi Mungu alizijaza nyoyo zao mapenzi ya Mtume -Ziwe juu yake Rehema na Amani- aliwauliza swali hili, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye ndiye mwenye maamuzi, na marejeo ni kwake, na kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kitabu chake: (Hakika wewe ni maiti na hakika wao ni maiti).
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Yalikuwa maneno ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni maneno ya wazi anayaelewa kila mwenye kuyasikia.
Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na An-Nasaaiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na AhmadHadithi ya Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba yeye alisema kuwa: Hakika Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yalikuwa wazi maneno, maana yake nikuwa yalikuwa yamepambanuka, hachanganyi herufi baadhi yake kwa baadhi, wala maneno baadhi yake kwa baadhi, yanaeleweka yako wazi kwa kila mwenye kuyasikia hakuna kufungana ndani yake wala kurefusha, hata wangetaka wenye kuhesabu kuyahesabu basi wangeyahesabu, kwasababu ya utaratibu wake mkubwa katika maneno -Rehema na Amani ziwe juu yake-; hii ni kwasababu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kapewa mkusanyiko wa maneno yenye kuweza kumaanisha vitu vingi, na yakawa mafupi sana kwake maneno, na mkusanyiko wa maneno ni kukusanya maana nyingi katika matamshi machache. Na hivi ndivyo inavyotakiwa mtu maneno yake yasiwe ni yenye kuingiliana kiasi kwamba yakafichikana kwa msikilizaji; kwasababu makusudio ya kuzungumza ni kumuelewesha mwenye kuzungumzishwa, kila yanavyozidi kuwa karibu kueleweka ndivyo inavyokuwa bora na vizuri zaidi. Kisha inampasa kila mtu atakapotumia njia hii, yaani atakapofanya maneno yake kuwa vipengele vya wazi, na akayarudia mara tatu kwa yule ambaye hajaelewa, inampasa avute hisia katika hili kuwa yeye anamfuata Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ili aweze kupata kupitia hili thawabu na amfahamishe ndugu yake muislamu. Na hivyo hivyo sunna zote weka akilini mwako kuwa ndani yake unamfuata Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ili kuthibiti kwako kumfuata Mtume na thawabu pia.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Laiti nisingeliogopea uzito kwa waumini -au kwa umma wangu-; ningeliwaamrisha kupiga mswaki kila wakati wa swala".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake lau kama si hofu ya kuwatia tabu waumini katika umma wake basi angeliwawajibishia juu yao kutumia mswaki kwa kila swala.
Kutoka kwa Abdallah bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiitembelea msikiti wa Qubaa kwa kipando na kwa miguu, anaswali ndani yake rakaa mbili. Na katika riwaya nyingine: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akienda msikiti wa Qubaa kila juma mosi akiwa katika kipando na kwa miguu, na alikuwa bin Omar akifanya hivyo.
Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim kwa riwaya zakeEneo la Qubaa ambapo umejengwa hapo msikiti wa kwanza katika uislamu ni kijiji kilichopo karibu na kituo cha Madina tokea pande za kusini mashariki ya mji wa Madina,akawa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anautembelea msikiti wa Qubaa akiwa katika kipando na akiwa kwa miguu, na aliposema kila juma mosi: makusudio nikuwa alikuwa akitenga baadhi ya siku kwaajili ya ziara, na hekima ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake kuja Qubaa siku ya juma mosi katika kila wiki, ilikuwa ni ajili ya kuunga udugu na maanswari na kujua hali zao na hali ya yule aliyechelewa kuipata swala ya ijumaa pamoja naye,na hii ndio siri ya kuichagua ziara katika sikuya juma mosi.
Imepokewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa nikioga mimi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chombo kimoja sisi wote tukiwa na janaba, na alikuwa akiniamrisha najifunga kikoi (kishida), ananigusa na mimi nikiwa katika hedhi, na alikuwa akitoa kichwa chake kwangu, naye akiwa katika itikafu (msikitini), ninamuosha nami nikiwa katika hedhi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu baadhi ya hali zake maalum pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na miongoni mwake: Nikuwa alikuwa akioga kutokana na janaba pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika chombo kimoja wakichota wote kwa pamoja. Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kumwendea akiwa katika hedhi anamuamrisha afunike mwili wake kuanzia kitovuni mpaka magotini, kisha akimshikashika bila ya tendo la ndoa. Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu msikitini anatoa kichwa chake kwa Aisha anamuosha naye akiwa nyumbani kwake na akiwa katika siku zake.
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: (Aliingia Abdur Rahmani bin Abiibakari As swiddiq -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na mimi nikiwa nimemuegemeza kifuani kwangu, na Abdur Rahmani -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akiwa na mswaki mbichi akisukutua nao, akauelekezea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- macho yake-, nikauchukua mswaki nikautafuna, nikausafisha, kisha nikauelekeza kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akautumia kusukutua, sikuwahi kumuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisukutua kusukutua kuzuri kama kule, hakuchukua muda kumaliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: akanyanyua mkono wake na kidole chake, kisha akasema: kwa rafiki aliyejuu -kasema hivyo mara tatu- kisha akafariki, na alikuwa Aisha akisema: Amefariki baina ya tumbo langu na kidevu changu).
Imepokelewa na Al-BukhaariyAnaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kisa kinachotubainishia sisi kiwango cha mapenzi ya mswaki kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na kushikamana kwake na mswaki, na hii nikuwa Abdur Rahman bin Abiibakari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kaka yake na Aisha aliingia kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiwa katika hali ya ulevi wa mauti. naye akiwa na mswaki mbichi, akisugua meno yake, alipouona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki ukiwa kwa Abdur Rahman, hayakumshughulisha yale aliyonayo katika maradhi na ulevi wa kifo, kwasababu ya mapenzi yake juu ya mswaki, akanyanyua macho yake kuutazama, kama mtu mwenye shauku nao, akagundua Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akauchukua mswaki toka kwa ndugu yake, na akakipunguza kichwa cha mswaki kwa meno yake, na akausafisha na kaupendezesha, kisha akampatia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akautumia kusukutua. Aliposafishika na akamaliza kupiga mswaki, alinyanyua kidole chake -akimpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu-, na akichagua kuhamia kwa Mola wake Mtukufu, kisha akafariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-. Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akaweweseka, na ni haki yake kuwa hivyo, kwasababu yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- alifariki na kichwa chake kikiwa juu ya kifua chake.
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakuna yeyote atakayenisalimia isipokuwa Mwenyezi Mungu hunirudishia roho yangu ili nimjibu salam".
Imepokelewa na Abu Daud na AhmadAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hurejeshewa roho yake ili ajibu salam kwa kila aliyemsalimia sawa sawa awe karibu au mbali; na maisha ya Akhera na kaburini ni jambo la ghaibu, hakuna ajuaye uhalisia wake isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee, naye juu ya kila kitu ni muweza.