





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema ndani ya nyumba yangu hii: "Ewe Mola wangu! Yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawatia tabu, basi naye mtie tabu, na yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawahurumia, basi naye mhurumie".
Imepokelewa Imamu MuslimAlimuombea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kila atakayesimamia jambo katika mambo ya waislamu liwe dogo au kubwa, sawa sawa usimamizi huu uwe ni wa umma, au sekta binafsi, na akawaingizia tabu na hakuwahurumia, kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amlipe kutokana na matendo yake, kwa kumtia matatizo na yeye. Nakuwa atakaye wahurumia na wakawafanyia wepesi, na akawarahisishia mambo yao basi Mwenyezi Mungu naye amuhurumie na ampe wepesi katika mambo yake.
Kutoka kwa Ma'akali bin Yasaari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Hakika mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna mja yeyote atakayepewa usimamizi na Mwenyezi Mungu kwa raia, akafa siku atakayokufa hali yakuwa aliwafanyia udanganyifu raia wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia pepo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila mtu ambaye Mwenyezi Mungu atamfanya kuwa ni msimamizi au kiongozi kwa watu, sawa sawa uwe ni uongozi wa umma, kama Raisi au usimamizi wa sekta binafsi kama mtu katika nyumba yake na mwanamke katika nyumba yake, akafanya uzembe kutekeleza haki za raia wake, na akawafanyia udanganyifu na wala hakuwanasihi, akapoteza haki zao za kidini na kidunia, huyu atakuwa kastahiki adhabu hii kali.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayejitoa katika utiifu, na akasambaratisha umoja akafa, atakuwa amekufa kifo cha zama za ujinga, na atakayepigana chini ya bendera kibubusa anachukia kwa sababu ya ndugu zake, au akahamasisha katika (kupendelea kwa sababu ya) udugu, au ana nusuru udugu, akauwawa, basi hicho ni kifo cha zama za ujinga, na atakayejitoa katika umma wangu, akimpiga mwema wake na muovu wake, na wala hajali muumini wake, na wala hamtimizii mwenye ahadi ahadi yake, basi huyo si miongoni mwangu na mimi si miongoni mwake".
Imepokelewa Imamu MuslimAmebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetoka katika kuwatii viongozi, na akaeneza fitina na kuusambaratisha umoja wa Uislamu uliokubaliana juu ya kumtii kiongozi, akafa katika hali hiyo ya faraka na kutomtii kiongozi, atakuwa kafa kifo cha watu wa zama za ujinga, ambao walikuwa hawamtii kiongozi yeyote wala hawajiungi katika kundi moja, bali walikuwa makundi makundi na wabaguzi, wakipigana wao kwa wao. Na akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayepigana chini ya bendera ambayo haiko wazi upande wa haki au batili, anachukia kwa sababu ya ubaguzi wa watu wake au kabila lake, na si kwa kuitetea dini na haki, akapigana kwa ubaguzi pasina kuwa na ujuzi na elimu, akiuawa katika hali hiyo, atakuwa ni sawa na aliye uawa katika zama za ujinga. Nakuwa atakayetoka katika Umma wake -Rehema na amani ziwe juu yake- akimpiga mwema wake, na muovu wake, na wala hajali anayoyafanya na wala haogopi adhabu zake kwa kumuuwa muumini, na wala hawatendei uadilifu makafiri waliochukua ahadi au viongozi, bali anatengua ahadi kwao, jambo hili ni katika madhambi makubwa, atakayelifanya atakuwa amestahiki ahadi hii ya adhabu kali.
Imepokewa kutoka kwa Farja -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Yeyote atakaye kujieni hali yakuwa mmekubaliana kumfanya kiongozi mtu mmoja, akataka kupasua nguvu yenu, Au ausambaratishe umoja wenu, basi muuweni".
Imepokelewa Imamu MuslimAnabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa waislamu watakapokubaliana juu ya kiongozi mmoja, na mshikamano mmoja, kisha akaja anayetaka kumpokonya madaraka, au akataka kuwasambaratisha waislamu kuwafanya kuwa makundi makundi, ni lazima wamzuie na wampige vita, kwa kuzuia shari yake, na kwa kuhifadhi damu za waislamu.
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika katika Jihadi kubwa ni kusema neno la uadilifu kwa kiongozi dhalimu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadAlibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa moja ya aina kubwa ya jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na yenye manufaa makubwa ni neno la uadilifu na ukweli mbele ya mtawala au mfalme dhalimu, kwa sababu ni kuifanyia kazi sheria ya kuamrisha mema na kukataza maovu, iwe kwa maneno au maandishi au vitendo, au kitu chochote kile, ili kuleta manufaa na kuzuia maovu.
Kutoka kwa Abuu Sufiyan Swakhar bin Harbi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: alisema Hiraqli: Hivi anawaamrisha nini? Yaani: Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake, akasema Abuu Sufiyani nikasema: "Muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake msimshirikishe yeye na chochote, na acheni wanayosema baba zenu, na anatuamrisha swala na ukweli, na kujizuia na machafu, na kuunga udugu".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimHaya ni mazungumzo ya Abuu sufiyani Swakhar bin Harbi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- ambayo ni mashuhuri yeye pamoja na Hiraqli, alikuwa Abuu Sufiyani wakati huo ni mshirikina, kiasi kwamba hakusilimu ila kwa kuchelewa, ilikuwa ni kati ya sulhul Hudaibiya (mkataba wa makubaliano wa Hudaibiya) na Fat-hu Makka (kufunguliwa kwa mji wa Makka) alitoka Abuu Sufiyani akiwa pamoja na kundi la makuraishi wakielekea kwa Hiraqli katika mji wa Sham, na Hiraqli alikuwa ni mfalme wa wakristo kwa wakati ule, na alikuwa amesoma katika taurati na Injili na vitabu vilivyotangulia, na alikuwa ni mfalme mwerevu, basi aliposikia ujio wa Abuu Sufiyani na wale walio pamoja naye, nao wakitokea katika miji ya jangwani aliwaita, na akaanza kuwauliza kuhusu hali ya Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- na kuhusu nasaba (ukoo) wake, na kuhusu maswahaba zake, na jinsi gani wanavyomuheshimu, na uaminifu wake Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- basi wanapotaja kitu wanachomueleza anazidi kujua kuwa huyu ndiye Nabii aliyeelezwa katika vitabu vilivyotangulia, lakini yeye -Tunamuomba Allah atuepushe na hilo- ni mtu mwenye uchu na ufalme wake akawa hakusilimu kwa hekima alizozitaka Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ilikuwa miongoni mwa yale aliyomuuliza Abuu Sufiyani ni kumuuliza juu ya yale anayoyaamrisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamueleza kuwa yeye anawaamrisha wao wamuabudu Mwenyezi Mungu na wala wasimshirikishe yeye na chochote, basi wasiabudu zaidi ya Mwenyezi Mungu, si Malaika wala Mtume, na wala si mti wala jiwe, na wala si jua wala mwezi, na wala si kinginecho, ibada zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, na huu ndio ujumbe wa Mtume, akaja Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na yale waliyokuja nayo Mitume kabla yake, kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake asiye na mshirika. Na akisema: "Yaacheni waliyokuwa nayo baba zenu" na hii ni katika kuutangaza ukweli, yale yote yaliyokuwa kwa baba zao katika kuabudu masanamu, aliwaamrisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuyaacha, na ama yale waliyokuwa nayo baba zao katika tabia njema; basi hakuwaamrisha wayaache. Na kauli yake: "Na alikuwa akituamrisha kuswali" swala ni mawasiliano kati ya mja na Mola wake, nayo ni nguzo ya pili yenye mkazo baada ya shahada mbili, na kupitia hii anajulikana muumini na kafiri, hiyo ndiyo ahadi iliyoko kati yetu na washirikina na makafiri, kama alivyosema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Ahadi iliyoko kati yetu sisi na wao ni swala, atakayeiacha atakuwa kakufuru" Na kauli yake: "Na alikua akituamrisha ukweli" Yaani alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiuamrisha umma wake kuwa wakweli, na hii ni kama kauli yake Mtukufu: "Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu na muwe miongoni mwa wakweli", na ukweli ni tabia njema, na unagawanyika sehemu mbili: kuwa mkweli pamoja na Mwenyezi Mungu, na kuwa mkweli pamoja na waja wa Mwenyezi Mungu, na yote mawili ni katika tabia njema. Na kauli yake "Na kujizuia na machafu" Yaani kujizuia na machafu kuna aina mbili: ni kujizuia na matamanio ya tupu, na kujizuia na matamanio ya tumbo. Na ama kujizuia kwa kwanza: nako ni mtu ajizuie na yale aliyoharamishiwa kama zinaa na njia zake na vishawishi vyake. Na ama aina ya pili ya kujizuia: nayo kujizuia kutokana na matamanio ya tumbo, yaani ni kujizuia na vile vilivyoko mikononi mwa watu, na kujizuia kutowaomba, kiasi kwamba mtu hamuombi yeyote chochote; kwasababu kuomba omba ni udhalili, na muombaji mkono wake uko chini, na mtoaji mkono wake uko juu, haifai kumuomba yeyote isipokuwa kwa yale ambayo hayana budi. Ama kauli yake: "kuunga udugu": nako ni mtu kuunga yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu ayaunge katika udugu wa karibu kisha unaofuata, na ndugu wa karibu zaidi ni wazazi wawili, kwani kuwaunga wazazi wawili ni wema na ni kuwaunga, na ndugu wa karibu wana haki ya kuungwa kulingana na ukaribu wao utakavyokuwa, kaka ana haki zaidi kuliko baba mdogo, na baba mdogo ana haki zaidi kuliko baba yake mdogo na baba, na kuunga udugu kunakuwa kulingana na jinsi watu walivyozoea.
Imepokelewa kutoka kwa Bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika utakuja kutokea uchoyo na kujipendelea baada yangu na mambo msiyoyajua (uzushi)" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unatuamrisha nini? Akasema: "Mtekeleze haki ya wajibu kwenu, na mumuombe Allah haki yenu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlieleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake yakuwa waislamu watatawaliwa na viongozi watakaohodhi na kujipendelea mali za waislamu na mambo mengine mengi yasiyokuwa mali, watazitumia kama watakavyo, na watawanyima waislamu haki yao katika mali hizo. Na watakuwa na mambo ndani ya dini mtakayoyakataa kuwa si katika dini. Masahaba Radhi za Allah ziwe juu yao wakauliza: Ni nini watafanya katika hali kama hiyo? Akawaeleza Rehema na amani ziwe juu yake kuwa kusikuzuieni kule kuhodhi kwao mali na kujipendelea kwao, nanyi mkaacha kufanya wajibu wenu kwao, ikiwemo usikivu na utii, bali kuweni na subira na mtii msiwaletee upinzani katika madaraka, na haki yenu iombeni kutoka kwa Allah, na awarekebishe na azuie shari zao na dhulma zao.
Kutoka kwa Nuumaan bin bashiri Radhi za Allah ziwe juu yao, kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina), wakawa baadhi yao wako juu ya safina na wengine wako chini yake, na wakawa wale walioko chini yake wanapohitajia maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, wakasema: Lau kama tungetoboa katika sehemu yetu kitobo wala tusingewaudhi walioko juu yetu, ikiwa watawaacha watekeleze walilolikusudia wataangamia wote, na ikiwa watawashika na kuwazuia wataokoka na wataokoka wote".
Imepokelewa na Al-BukhaariyMtume Rehema na amani ziwe juu yake amepiga mfano wa wale wenye kusimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu, wenye msimamo katika amri ya Mwenyezi Mungu, wenye kuamrisha mema na kukataza maovu, na mfano wa wenye kutumbukia katika mipaka ya Mwenyezi Mungu wenye kuacha mema, na kufanya maovu, na athari ya hilo katika kusalimika jamii, ni sawa na mfano wa watu waliopanda boti, wakagawana nafasi nani akae juu na nani akae chini ya boti, wengine wakapata nafasi ya kukaa juu na wengine wakapata nafasi ya kukaa chini, na wakawa hawa walioko chini wanapotaka kuchota maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, Kisha wale wa chini wakasema: Lau tungeli toboa tundu mahali petu chini ili tusiwaudhi walio juu yetu, basi lau walio juu wangewaacha kufanya hivyo, basi meli ingewazamisha wote, na lau wangeliwakataza na kuwazuia, makundi yote mawili yangeokoka.
Kutoka kwa Ally -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "Waelezeni watu yale wanayoyafahamu, Hivi mnataka akadhibishwe (apingwe) Mwenyezi Mungu na Mtume wake?".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAnaelekeza Kiongozi wa waumini Ally bin Abii Twalib -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa haitakiwa watu wote kuelezwa isipokuwa yale mambo ambayo ni maarufu tena yenye kuwanufaisha watu katika msingi wa dini yake na hukumu yake miongoni mwa tauhidi na kuwabainishia watu halali na haramu, na kuacha yenye kupoteza lengo hilo; katika yale yasiyokuwa na haja ndani yake, au yakawa ni katika mambo ambayo ni sababu ya kupingwa ukweli na kutokubalika kwake katika yale ambayo wanatatizika kuyafahamu, na inakuwa kwao vigumu kuyajua.