





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Sahal bin Sa'di Allah amridhie amesema: Amesema Mtume wa Allah rehema na amani ziwe juu yake: "Tahadharini na madhambi yenye kudharauliwa, kwani mfano wa madhambi yenye kudharauliwa, ni kama watu walioshuka chini ya bonde, akaja huyu na kijiti, na yule na kijiti, na akaja huyu na kijiti, mpaka wakaivisha mkate wao, na bila shaka madhambi yadharauliwayo akihesabiwa mfanyaji wake yanamuangamiza".
Imepokelewa na AhmadAmetahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kupuuza katika kuyafanya madhambi madogo, na kuyakithirisha kwani yanaangamiza yanapokuwa mengi, na akapiga mfano juu ya hilo wa watu walioshuka chini ya bonde, basi akaja kila mmoja wao na kijiti kidogo, mpaka wakaivisha mkate wao kwa mkusanyiko wa vile walivyovikusanya katika vijiti, na hakika madhambi yadharauliwayo pindi anapohesabiwa mfanyaji wake na akawa hajatubia kutokana na madhambi hayo au Mwenyezi Mungu amsamehe, basi humuangamiza.
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kwa hakika nimetumwa ili kutimiliza tabia njema"
Imepokelewa na Al-Bukhari katika Al-Adab Al-Mufrad na Ahmad na Al-BayhaqiAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba, hakika Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka alimtuma yeye ili akamilishe mambo bora na tabia zilizo njema; kiasi kwamba alitumwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili atimize yale waliyokuwa nayo Mitume, na alikuja kukamilisha tabia njema za waarabu, kwani walikuwa wakipenda kutenda kheri na wakichukia shari, walikuwa ni watu wenye utu na ukarimu na utukufu; akatumwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili kukamilishe mapungufu yaliyoko katika tabia zao, kama kujifaharisha kwao kwa nasaba, na kujikweza na kumdharau fakiri na nyinginezo.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ananiudhi mimi mwanadamu, anatukana nyakati na mimi ndiye nyakati, ninaugeuza usiku na mchana".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Hadithil Kudsi: Ananiudhi na ananishusha hadhi mwanadamu anayetukana na kusema vibaya wakati wa kufikwa na matatizo na machukizo; kwa sababu yeye Mtukufu ndiye mpangiliaji peke yake na muendeshaji wa yote yanayotokea; kutukana nyakati ni kumtukana Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na nyakati ni kiumbe na kinaendeshwa, yanatokea matukio ndani yake kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ruqaiyya Tamim Ausi Ad-dari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Dini ni nasaha" Tukasema: Kwa ajili ya nani? Akasema: "Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kitabu chake, na Mtume wake, na kwa viongozi wa waislamu na watu wote."
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa dini imesimama katika msingi wa utakasifu wa nia na ukweli, ili itekelezwe kama alivyowajibisha Mwenyezi Mungu kikamilifu pasina mapungufu au udanganyifu. Pakasemwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Zinakuwa kwa nani nasaha? Akasema: Kwanza: Nasaha ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: Kwa kutakasa matendo kwa ajili yake, na kutomshirikisha, na tuamini ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, na kutukuza amri zake, na kuwaita watu kuja katika kumuamini. Pili: Nasaha kwa ajili ya kitabu chake ambacho ni Qur'ani tukufu: Tuitakidi kuwa ni maneno yake, na ni kitabu chake cha mwisho, na kwamba kimefuta sheria zote zilizokuwa kabla yake, na tunakitukuza na kukisoma haswa ipasavyo, na tunazifanyia kazi aya zake,zilizo wazi na tunazikubali zenye kutatiza na tunapingana na tafsiri mbaya ya wenye kuzipotosha, na tunachukua mazingatio kwa mawaidha yake, na kuisambaza elimu yake, na kuwalingania watu kwayo. Tatu: Nasaha kwa ajili ya Mtume wake Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake: Kwa sisi kuitakidi kuwa yeye ni mwisho wa Mitume, na kumuamini kwa yale aliyokuja nayo, na tutekeleza amri yake, na tuepuke makatazo yake, na tusimuabudu Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa yale aliyokuja nayo, na tunaitukuza na tunaiheshimu, na tunautangaza ujumbe wake, na kuisambaza sheria yake, na kupinga tuhuma zote dhidi yake. Nne: Nasaha kwa viongozi wa Waislamu: Kwa kuwasaidia katika haki, na kutozozana nao katika uongozi, na kuwasikiliza na kuwatii katika kumtii Mwenyezi Mungu. Tano: Nasaha kwa Waislamu: Kwa kuwatendea wema na kuwalingania, na kuacha kuwaudhi, na kuwapendelea heri, na kusaidizana nao katika wema na uchamungu.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kila kiungo kwa mwanadamu kwake ni sadaka, kila siku linalochomoza jua ndani yake ukafanya uadilifu kati ya watu wawili hiyo ni sadaka, na ukamsaidia mtu katika kipando chake ukambeba au ukamnyanyulia mzigo ni sadaka, na neno zuri ni sadaka, na kila hatua unayopiga kwenda msikitini ni sadaka, na ukiondoa udhia barabarani nisadaka".
Imepokelewa na Bukhari na MuslimMtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa kila Muislamu ni wajibu kila siku kuhesabu kila kiungo cha mifupa yake kuwa ni sadaka ya hiyari kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa ni njia ya kumshukuru kwa neema ya afya, na kwamba amevifanya viungo vyake kuwa na maungio yanayomuwezesha kukunja na kukunjua, Sadaka hii inafanywa na matendo yote mema na haitegemei kutoa pesa, na miongoni mwake: Uadilifu wako na kusuluhisha kwako kati ya wagomvi wawili ni sadaka, Na katika kumsaidia kwako asiyejiweza kupanda katika mnyama wake, ukambeba, au ukamnyanyulia mzigo, ni sadaka. na neno zuri kuanzia kumtaja Mwenyezi Mungu na dua na salamu na mengineyo, ni sadaka, na kwa kila hatua unayoipiga kwenda katika swala, ni sadaka, na kuondoa kila yanayoudhi katika njia ni sadaka.
Kutoka kwa Ubaadah bin Swaamit -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulimpa ahadi ya utiifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kusikia na kutii katika uzito na wepesi, na yenye kufurahisha na kuchukiza, na kumthamini kuliko nafsi zetu, na tusiwanyang'anye uongozi wanaostahiki, na tusema ukweli mahala popote tuwapo, tusiogope kwa Mwenyezi Mungu lawama za mwenye kulaumu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alichukua ahadi na mkataba kutoka kwa Masahaba ya utii kwa wenye mamlaka na watawala katika wepesi na ugumu, na katika hali ya utajiri na umasikini, na sawa sawa amri zao ziwe katika yale wanayoyapenda au kuyachukia, hata kama watawala watajipendelea kuliko raia kwa mali ya umma au vyeo au mengineyo, basi ni wajibu kwao kusikiliza na kutii katika wema, na wasitoke dhidi yao, kwa sababu fitina na ufisadi katika kupigana nao ni mambo makubwa na ni mabaya mno kuliko ufisadi unaotokea kwa sababu ya dhulma zao, na katika mambo waliyoyachukulia kiapo ni waseme kweli mahali popote, wakilitakasa hilo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hawamuogopi mwenye kuwalaumu.
Kutoka kwa Ummu Salama mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Watakuja watawala, mtayajua baadhi ya matendo yao kuwa yanakwenda sawa na sheria, na mengine mtayakemea (kwa kuwa yako nje ya sheria) atakayelijua hilo ataepukana na dhima, na atakayekemea atasalimika, lakini atakayeridhia na akawafuata" Wakasema: Kwa nini tusiwapige vita? Akasema: "Hapana, (Msifanye hivyo) madam ni waislamu na wanasimamisha swala".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa tutatawaliwa na viongozi ambao tutayajua baadhi ya matendo yao kuwa yako sawa na yale yanayofahamika ndani ya sheria; na tutayakemea baadhi yake kwa kuwa kwake kinyume na sheria, Atakayechukia moyoni mwake na akawa hakuweza kukemea; basi atakuwa kaondoa dhima ya kupata dhambi na unafiki, Na atakayeweza kukemea kwa mkono au ulimi akawakemea kwa hilo basi atakuwa kasalimika na maasi na kushiriki katika maasi, Lakini atakayeridhia matendo yao na akawafuata ataangamia kama walivyoangamia. Kisha wakamuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kwa nini tusiwapige vita viongozi ambao wanasifa kama hizi? Akawakataza wasifanye hivyo, na akasema: Hapana, msifanye hivyo madama wanasimamisha swala kwenu nyinyi.
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Pindi anapougua mja au akasafiri basi huandikiwa mfano wa yale aliyokuwa akiyafanya akiwa nyumbani tena mwenye afya".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu fadhila za Allah na rehema zake, nakuwa muislamu ikiwa ni katika mazoea yake kufanya matendo mema akiwa katika hali ya afya na yuko nyumbani, kisha apatwa na udhuru akaugua akashindwa kutekeleza ibada hizo, au akashughulishwa na safari, au udhuru wowote; basi huandikiwa malipo kamili, kama ambavyo angefanya wakati wa afya na yuko nyumbani.
Imepokewa Kutoka kwa Tamim Ad-dari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: "Dini ni nasaha" Tukasema: Kwa ajili ya nani? Akasema: "Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kitabu chake, na Mtume wake, na kwa viongozi wa waislamu na watu wote."
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dini imesimama katika misingi ya kutakasa nia (Ikhlas) na ukweli, ili itekelezwe kama alivyowajibisha Mwenyezi Mungu, kikamilifu bila uzembe au udanganyifu. Akaulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nasaha huwa kwa ajili ya nani? Akasema: Kwanza: Nasaha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa kutakasa matendo kwa ajili yake, na kutomshirikisha mwingine pamoja naye, na tuamini ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, na kuzitukuza amri zake, na kulingania watu katika kumuamini. Pili: Nasaha ni kwa ajili ya kitabu cha Mwenyezi Mungu nacho ni Qur'ani Tukufu: Tuitakidi kuwa ni maneno yake, na ni kitabu chake cha mwisho, nakuwa kimefuta sheria zote zilizokuwa kabla yake, na tunakitukuza, na tunakisoma ukweli wa kukisoma, na tunazifanyia kazi aya zake za wazi, na tunazikubali zenye kutatiza, na tunapinga upotoshaji wa wenye kupindisha, na tunayazingatia mawaidha yake, na kuieneza elimu yake, na kuwalingania watu kwayo. Tatu: Nasaha kwa ajili ya Mtume wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: Tuitakidi kuwa yeye ni Mtume wa mwisho, na tumsadikishe katika yale aliyokuja nayo, na tutekeleze amri zake, na tuyaepuke makatazo yake, na tusimuabudu Allah isipokuwa kwa yale aliyokuja nayo, na tuitukuze haki yake, na tumuheshimu, na tuutangaze ujumbe wake, na tuisambaze sheria yake, na tuzikanushe tuhuma dhidi yake. Nne: Nasaha kwa viongozi wa waislamu: Kwa kuwasaidia katika haki, na kutozozana nao katika uongozi, na kuwasikiliza na kuwatii katika mambo ya kumtii Mwenyezi Mungu. Tano: Nasaha kwa waislamu: Kwa kuwafanyia wema na kuwalingania, na kuzuia maudhi dhidi yao, na kuwapendelea kheri, na kusaidizana nao katika wema na uchamungu.