





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote akakifikisha kama alivyo sikia, huenda mfikishiwa akawa mwerevu zaidi kuliko aliye sikia".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadAliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kung'arisha na muonekano na uzuri katika dunia, na amfikishe Mwenyezi Mungu katika mng'ao wa peponi na neema zake na mng'ao wake katika Akhera; kwa yule atakayesikia hadithi yake akaihifadhi ili amfikishie mwingine, huenda aliyenukuliwa hadithi akawa mwerevu na muelewa na akawa na uwezo wa kuchambua hukumu kuliko hata aliyeinukuu hadithi, akawa wa kwanza anahifadhi vizuri, na wa pili akawa anauelewa na uchambuzi mzuri.
Kutoka kwa Abuu Musa radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake, amesema: "Hakika muumini peponi atakuwa na Hema moja la madini ya lulu lililo wazi urefu wake kwenda juu ni maili sitini, muumini humo atakuwa na wake, akiwazungukia na wala baadhi yao hawawaoni wenzao".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya neema za peponi, nakwamba muumini ndani ya pepo atakuwa na hema pana kwa ndani, lilitokana na madini ya lulu yenye kung'aa, upana wake na urefu wake kuelekea juu ni maili sitini, katika kila mahali na kila kona katika kona zake nne kuna wake, na wote hawaonani, muumini atakuwa akiwazungukia.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Amesema Allah Aliyetakasika na kutukuka: Nimewaandalia waja wangu wema, vitu ambavyo jicho halijawahi kuona, wala sikio kusikia, wala haijawahi kupita katika fikira ya moyo wa binadamu yeyote" Akasema Abuu Huraira: Someni mkitaka: "Basi nafsi yoyote haijui yale waliyofichiwa miongoni mwa mambo yenye kutuliza macho" [As-Sajida: 17).
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka amesema: Nimetayarisha na nimeandaa kwa ajili ya kuwatukuza waja wangu wema peponi mambo ambayo uhalisia wake hakuna jicho liliwahi kuona, na wala sikio lolote kusikia wasifu wake, wala kutokea wala kupita ndani ya moyo wa binadamu yeyote uhalisia wake. Akasema Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Someni mkitaka: "Nafsi yoyote haijui yale waliyofichiwa miongoni mwa mambo yenye kutuliza macho" [As-Sajda: 17]
Kutoka kwa Abuu Abdillah Al-Jadali amesema: Nilimuuliza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na maneno machafu wala mwenye kujilazimisha machafu, wala hakuwa na makelele masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya, lakini alikuwa akisamehe na kufuta kosa.
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadAliulizwa mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Haikuwa katika tabia zake uchafu na ubaya wa kauli na vitendo, na wala hakuwa akijilazimisha machafu wala kuyakusudia, wala hakuwa mpiga kelele kwa kunyanyua sauti yake masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya; lakini alikuwa akilipa ubaya kwa wema, na akisamehe ndani ya moyo, na akifuta kosa na kulipuuza katika dhahiri.
Kutoka kwa Haani, mwachwa huru wa Othmani radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Othmani anaposimama juu ya kaburi analia mpaka analowanisha ndevu zake, akaulizwa: Ukikumbuka pepo na Moto wala haulii, na unalia kwa sababu ya hili (kaburi)?! Akasema: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Hakika kaburi ndio kituo cha kwanza katika vituo vya Akhera, ikiwa mtu atasalimika nalo basi yajayo baada yake ni mepesi kuliko hili, na asiposalimika nalo basi yajayo baada yake ni magumu kuliko hili".
Imepokelewa na Tirmidhi na bin MajahAlikuwa kiongozi wa waumini Othmani bin Affani radhi za Allah ziwe juu yake anaposimama juu ya kaburi analia sana, mpaka analowanisha ndevu zake, akaulizwa: Unakumbuka pepo na moto na wala haulii kwa shauku ya pepo wala hofu ya moto! na unalia kwa sababu ya kaburi? Akasema: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alieleza kuwa hakika kaburi ndio kituo cha kwanza katika vituo vya Akhera, mtu akisalimika na akaepukana na mabaya yaliyomo basi vituo vinavyofuata baada yake ni vyepesi mno, na asiposalimika kutokana na adhabu zake; basi adhabu zinazofuata baada yake ni kali kuliko hizo.
Kutoka kwa Bahzi bin Hakim kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfanyie wema zaidi? Akasema: "Mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha anayemfuata kwa ukaribu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu muhimu zaidi kufanyiwa wema kuliko wote, na kumfanyia hisani, na kuamiliana naye vizuri, na kuishi naye vizuri, na kusuhubiana naye na kumuunga: Ni mama, na akasisitiza haki ya mama zaidi kuliko mtu mwingine, kwa kulirudia hilo mara tatu; kwa kubainisha fadhila zake kuliko watu wengine bila kupunguza chochote. Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake anayefuata katika kutendewa wema: Kisha baba, kisha ndugu wa karibu zaidi na wa karibu anayefuata, kila ndugu anavyozidi kuwa karibu basi anakuwa na haki zaidi ya kuungwa udugu kuliko ndugu wa mbali.
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake, yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesema nimeridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na kuwa Uislamu ni dini, na Muhammadi kuwa Mtume, basi atastahiki kwake Papo".
Imepokelewa na Abu DaudAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema: "Nimemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola" na Mungu na Mlezi na Mmiliki, na bwana na Mtengenezaji, "na Uislamu" kwa hukumu zake zote kwanzia amri zake na makatazo yake "kuwa Dini" mila na sheria, itikadi na utii, "na Muhammadi kuwa Mtume" na Nabii; kwa yote aliyotumwa kwayo na akatufikishia, isipokuwa itamstahikia kwake Pepo.
Kutoka kwa Ubada bin Swamiti radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa miongoni mwa walioshuhudia vita vya Badri, naye alikuwa ni mmoja wa vigogo katika usiku wa Aqaba: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema na pembezoni mwake kukiwa na jopo la Maswahaba zake: "Nipeni ahadi ya utiifu ya kuwa msimshirikishe Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na wala msiibe, na wala msizini, na wala msiwauwe watoto wenu, na wala msilete uzushi mtakouzua kwa mikono yenu na miguu yenu, na wala msiasi katika wema, basi atakayeyatimiza hayo miongoni mwenu basi malipo yake yatakuwa juu ya Mwenyezi Mungu, na atakayetenda lolote katika hayo akaadhibiwa katika dunia basi hiyo ndiyo kafara kwake, na atakayetenda lolote katika hayo kisha Mwenyezi Mungu akamsitiri basi hilo litabakia kwa Mwenyezi Mungu akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu" Tukampa ahadi ya utiifu juu ya hayo.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Ubada bin Swamiti radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa ni miongoni mwa walioshuhudia vita vya Bardi kuu, naye akiwa kiongozi wa watu wake waliokuja kutoa mkono wa ahadi ya uaminifu kwa ajili ya kumnusuru Mtume rehema na amani ziwe juu yake usiku wa Aqaba ambayo iko Mina, wakati Mtume akiwa Makka kabla ya kuhama kwake kwenda Madina, ni kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa kakaa na Maswahaba zake akawataka wamuahidi juu ya mambo haya: La kwanza: Wasishirikishe katika ibada za Mwenyezi Mungu kitu chochote hata kikiwa kidogo. La pili: Wasiibe. La tatu: Wasifanye uchafu wa zinaa. La nne: Wasiwauwe watoto wao; wa kiume kwa kuhofia ufakiri na umasikini au watoto wa kike kwa kuhofia fedheha. La tano: Wasilete uongo wataoutengeneza baina ya mikono yao na miguu yao, kwa sababu matendo mengi hutokea kupitia hivi viwili hata kama viungo vingine vitashiriki. La sita: Wasimuasi Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika jambo jema. Atakayethubutu miongoni mwao katika ahadi na akashikamana nayo basi malipo yake yako kwa Mwenyezi Mungu, na atakayefanya lolote miongoni mwa hayo yaliyotajwa -kasoro ushirikina- akaadhibiwa katika dunia kwa kusimamishiwa adhabu juu yake basi hilo ndio kafara yake, na kwa hilo dhambi lake litaondoka, na atakayefanya lolote miongoni mwa hayo kisha Mwenyezi Mungu akamsitiri basi huyu jambo lake liko kwa Mwenyezi Mungu; akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu, wote waliokuwepo wakampa ahadi ya utiifu juu ya hayo.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Ulianza Uislamu ukiwa ni mgeni na utarudi kuwa mgeni kama ulivyo anza, basi shangwe kwa wale wanaoonekana kuwa ni wageni".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Uislamu ulianza ukiwa kwa mtu mmoja mmoja na uchache wa watu wake, na utarejea ukiwa mgeni kwa uchache wa wenye kuutekeleza kama ulivyoanza, twawatamani, na uzuri ulioje kwa wageni, na furaha na kitulizo cha jicho kwao.