Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way






























Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba amefaulu na amebahatika atakayemtii Mola wake akaongozwa na akawezeshwa kuingia katika Uislamu, na akaruzukiwa katika halali kiasi cha mahitaji yake pasina ziada wala mapungufu, na Mwenyezi Mungu akamjaalia kukinai na kuridhika na kile alichompa.
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba atakayeamka miongoni mwenu enyi waislamu akiwa mzima wa afya katika mwili wake akiwa amesalimika na matatizo na magonjwa, akiwa na amani ndani ya nafsi yake na watu wake na familia yake na barabara zake, na akiwa hana hofu, na akiwa na chakula cha halali cha kumtosha kwa siku yake; basi ni kana kwamba kakabidhiwa dunia yote nzima.
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua zenye kukusanya kheri za dunia na Akhera ambazo matamshi yake ni machache na maana yake ni nyingi, na kunakuwa ndani yake na kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu, na malengo mazuri, na anaachana na yasiyokuwa hayo.
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuapa na kukithirisha kiapo hata kama mtu akiwa mkweli katika kuuza na kununua, na akaeleza kuwa ni sababu ya kuondoka bidhaa na mzigo, lakini hilo hupunguza na kubatilisha baraka za faida na chumo, na anaweza kumpelekea Mwenyezi Mungu namna zitakazoharibu mali yake, ima kuibiwa au kuungua kuangamia au kuporwa au kuvamiwa au majanga mengine yatayoharibu mali yake.
Amekataza rehema na amani ziwe juu yake kuutukana au kuulani upepo, kwani umeamrishwa kutoka kwa muumba wake, huja kwa rehema na adhabu, na kuutukana ni kumtukana Mwenyezi Mungu muuba wake, na kuchukia maamuzi yake, kisha akaelekeza rehema na amani ziwe juu yake kurejea kwa Mwenyezi Mungu muumba wake kwa kumuomba kheri zake na kheri zilizo ndani yake, na kheri za yale yaliyotumwa, kama kuleta mvua na kuchevusha mimea na mfano wake, na kuomba kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake na shari zilizo ndani yake, na shari zilizotumwa, kama kuharibu mimea na miti na kuangamiza mifugo na kubomoa majengo, na mfano wake, na katika kumuomba Mwenyezi Mungu hilo kuna kutimiza na kuthibitisha kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuitundika dua na chochote hata ikiwa kwa matashi ya Mwenyezi Mungu; kwa sababu hilo ni jambo linalojulikana na ni la uhakika kuwa hasamehi mpaka atake Mtukufu, na haina maana kuweka sharti la matashi; kwa sababu huwekwa sharti hilo kwa yule ambaye anaweza kufanya pasina kutaka kwa kulazimishwa na vinginevyo ambavyo Mwenyezi Mungu ametakasika navyo Mtukufu, na amelibainisha hilo rehema na amani ziwe juu yake mwisho wa hadithi kwa kauli yake kuwa hakuna wa kumlazimisha, kama Mwenyezi Mungu hakuna kinachokuzwa kwake ila anakitoa na wala hakuna kinachomshinda au kikawa kikubwa kwake chochote mpaka tuseme: Ukitaka, na kuutundika msamaha na matashi ni aina ya kutokuuhitaji msamaha wake, kauli ya mtu kusema: Ukitaka kunipa kadhaa basi nipe, huwa haitumiki kauli hiyo ila pale mtu anapokuwa hana haja au kwa asiyeweza, ama kwa anayeweza na pamoja na uhitaji wake basi anatakiwa kudhamiria kuomba, na aombe maombi ya masikini aliyedhikika mwenye uhitaji, na ajiweke karibu na Mwenyezi Mungu; kwa sababu yeye ndiye tajiri kamili, muweza juu ya kila kitu.
Makundi matatu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliyaombea dua mbaya ya pua zao kugusa mchanga kwa udhalili na unyonge na hasara: Kundi la kwanza: Yule atakayetajwa mbele yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akawa hakumswalia, kwa kusema: Swalla llaahu a'laihi wasallam (Rehema na amani ziwe juu yake) na mfano wake. La pili: Ni yule atakayeupata mwezi wa Ramadhani kisha mwezi ukamalizika kabla hajasamehewa kwa uzembe wake wa kufanya mambo ya kheri. La tatu: Ni mtu atakayewapata wazazi wake wakiwa watu wazima, na hawakuwa sababu ya yeye kuingia peponi kwa sababu ya kuwaasi kwake na uzembe wake katika kutekeleza haki zao.
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa hakuna waislamu wawili watakaokutana njiani na mfano wake wakasalimiana kwa kupeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana kwa viwiliwili au kwa kumaliza kupeana mikono.
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili katika vidole vya Rahmaan kama moyo mmoja; anaugeuza kokote atakako; akitaka anausimamisha katika haki, na akitaka anaupotoa katika haki, na kuzigeuza kwake nyoyo zote ni kama kuugeuza moyo mmoja, hakuna jambo linaloweza kumshughulisha akaacha jambo jingine, kisha akaomba rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Mwenyezi Mungu mwenye kuzigeuza nyoyo, wakati mwingine katika utiifu na wakati mwingine katika maasi, na wakati mwingine katika kukutaja na wakati mwingine katika kughafilika, zigeuze nyoyo zetu zielekee katika utiifu wako.