





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mtazameni aliyeko chini yenu, na wala msimtazame aliyeko juu yenu, kwa kufanya hilo, hilo litakufanyeni msidharau neema za Allah mlizonazo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume rehema na amani ziwe juu yake amemuamrisha muislamu kumtazama katika mambo ya dunia katika nafasi na mali na cheo na mengineyo yule ambaye ana hali ya chini zaidi, na asimtazame katika mambo ya dunia yake yule aliyeko juu yake na bora zaidi kuliko yeye, kwa kumtazama aliyeko chini ni bora na kunastahiki zaidi kumfanya asidharau na kuzidogesha neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yake.
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Hamtazami Mwenyezi Mungu mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmetahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuburuza nguo au kikoi chini ya kongo mbili kwa kiburi na kujiona, nakuwa mwenye kufanya hivyo atastahiki ahadi ya adhabu kali yakuwa Mwenyezi Mungu hatomtazama siku ya Kiyama mtazamo wa huruma.
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Neema mbili wamepoteza thamani yake watu wengi: Afya na wakati".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAlieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu neema mbili kubwa miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kuwa wanapata hasara ndani yake watu wengi, kiasi kwamba wanazitumia mahali pasipostahiki; kwani mwanadamu zikikusanyika kwake neema ya afya na wakati, akazidiwa na uvivu wa kufanya ibada basi kapata hasara; na ndio hali ya watu wengi, na akiutumia muda wake na afya yake katika kumtii Mwenyezi Mungu basi atakuwa kapata faida; hii ni kwa sababu dunia ndio shamba la Akhera, na wakati hufuatiwa na shughuli, na afya hufuatiwa na maradhi, na lau kusingekuwa na chochote zaidi ya uzee basi ungetosha.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema katika sijida yake: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe mimi dhambi zangu ndogo zake na kubwa zake za mwanzo wake na mwisho wake, za wazi zake na za siri zake".
Imepokelewa Imamu MuslimAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiomba katika sijida yake akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe madhambi yangu" Kwa kuyasitiri, na unikinge na madhara yake; uyasamehe na usiyatazame na uyafute, "yote", nakusudia: "Za ndani" ndogo zake, na chache zake, "pana zake" kubwa zake na nyingi zake, "za mwanzo wake" dhambi ya kwanza, "na za mwisho zake", na zilizo kati yake, "za wazi zake na siri zake" miongoni mwa zile asizozijua yeyote ila wewe Uliyetakasika.
Imepokelewa kutoka kwa Abud-dardaa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi siku ya Kiyama".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kukithirisha laana kwa mtu asiyestahiki huyu anastahiki kupata adhabu mbili. Ya kwanza: Hatokuwa shahidi siku ya Kiyama juu ya umma kwa mitume wao kufikisha ujumbe kwao, na wala haukubaliki ushahidi wake duniani; kwa sababu ya uovu wake, na wala hatoruzukiwa shahada, nako ni kufa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Ya pili: Hatopewa nafasi ya kutoa utetezi siku ya Kiyama wakati ambapo waumini wataomba utetezi kwa ndugu zao waliostahiki moto.
Na kutoka kwa Salmani -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye haya Mkarimu, anamuonea haya mja wake atakapo nyanyua mikono yake kumuelekezea kisha amrejeshe patupu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ibn MajahAnahimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kunyanyua mikono wakati wa dua, na akaeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu "huona haya" mwingi wa haya, na haachi kutoa, anamfanyia mja yenye kumfurahisha, na anaacha yenye kumdhuru, "Ni Mkarim" hutoa pasina kuombwa, je hali huwaje baada ya kuombwa! anamuonea haya mja wake muumini kuirejesha patupu mikono yake baada ya kuinyanyua kwa ajili ya dua ikiwa imefeli haina kitu kwa kutojibiwa.
Imenukuliwa kutoka kwa Juwairia mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku moja alitoka kwake asubuhi pindi alipo sali sala ya asubuhi, na yeye akiwa katika sehemu yake ya kusalia, kisha akarudi baada ya kuingia wakati wa dhuha, naye akiwa amekaa, akasema: "Bado upo kwenye hali yako niliyo kuacha nayo?" Akasema: "Ndio", Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika ungesema maneno manne, mara tatu, kama ungeyapima kwa uliyo yasema toka siku ya leo yangeyazidi uzito: Sub-haana llahi Wabihamdihi, Adada khalqihi, Waridhwaa nafsihi, Wazinata Arshihi, Wamidaada kalimaatihi" (Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake, kwa idadi ya viumbe vyake, na ridhaa ya nafsi yake, na uzito wa Arshi yake, na wino wa maneno yake)
Imepokelewa Imamu MuslimAlitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa mkewe mama wa waumini Juwairia radhi za Allah ziwe juu yake mwanzo wa asubuhi aliposwali swala ya Alfajiri, na Juwairia akiwa kakaa mahali aliposwalia, kisha akarejea baada ya mchana kufika kati kati wakati wa dhuha, naye akiwa bado kakaa katika mahali pake, akasema: Hivi bado uko katika hali niliyokuacha nayo? Akasema: Ndio, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika nimesema baada yako maneno manne, na nimeyakiriri mara tatu, lau yangelinganishwa kulingana na malipo na yale uliyoyasema kwa muda wote uliokaa hapa basi yangeliyazidi: "Ametakasika Mwenyezi Mungu" na kutakasika kwake kutokana na mapungufu, "na sifa njema ni zake" kiasi ambacho ana sifa nzuri ambazo amewaongoza kwazo, "idadi kubwa ya viumbe wake" ambazo hakuna awezaye kujua idadi yake isipokuwa Mwenyezi Mungu, "na ridhaa ya nafsi yake" kwa kiasi kinachomridhisha kutoka kwa wale aliowaridhia Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake nalo ni jambo lisiloelezeka, "na uzito wa Arshi yake" ambacho ndicho kiumbe kikubwa na kizito zaidi, "na wino wa maneno yake" na maneno ya Mwenyezi Mungu hayadhibitiki kwa idadi na wala hayamaliziki; na hii inakusanya migawanyiko yote mitatu na inazienea; kwani wino wa maneno yake Mtukufu hauna mwisho wa kiwango chake, wala sifa yake, wala idadi yake, lakini makusudio yake: Ni kupita kipimo katika wingi; kwa sababu yeye ametaja mengi mwanzoni yanayoweza kuhesabika miongoni mwa viumbe, kisha akapanda juu kwa makubwa zaidi katika hayo na akayaelezea kwa neno ridhaa ya nafsi yake, kisha uzito wa kiumbe kikubwa nacho ni Arshi; vya kwanza ni vya kuhesabika na kiwango maalumu, na vya pili ni kwa sifa na namna maalumu, na vya tatu ni kwa ukubwa na uzito.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake, na wala hawakumsalia Nabii wao, isipokuwa itakuwa ni hasara juu yao, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe".
ImepokAbu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu AlkubraaAmetahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu, nakuwa hawatokaa watu katika kikao chochote na wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, na wakawa hawakumsalia Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake isipokuwa kikao hicho kitakuwa ni hasara na majuto juu yao na mapungufu siku ya Kiyama, akitaka atawaadhibu kwa madhambi yao yaliyotangulia na uzembe wao uliofuata, na akitaka atawasamehe ikiwa ni fadhila na rehema kutoka kwake.
Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika katika watu wanaopendeka zaidi kati yenu kwangu mimi, na atakayekaa karibu zaidi kati yenu na mimi siku ya Kiyama ni yule atakayekuwa na tabia njema zaidi kati yenu, na hakika ninaowachukia zaidi kati yenu na watakaokaa mbali zaidi na mimi siku ya Kiyama ni watu wenye maneno mengi, na waropokaji, na wenye kujifakharisha, wakasema: Tushajua maana ya watu wenye maneno mengi na waropokaji, nini maana ya wenye kujifakharisha? Akasema: "Ni wale wenye kiburi".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa miongoni mwa wale wanaowapendeka zaidi kati yenu kwake katika dunia, na wa karibu zaidi katika kikao miongoni mwenu siku ya Kiyama, ni yule mwenye tabia nzuri zaidi yenu, na kuwa anayechukiwa zaidi miongoni mwenu kwake katika dunia, na atakayekuwa mbali zaidi miongoni mwenu katika kikao siku Kiyama ni mwenye tabia mbaya zaidi miongoni mwenu; "Wenye maneno mengi" wenye kukithirisha maneno kwa kukijilazimisha na kwa kutoka katika haki, "na wenye kuzama zaidi" wenye kuzungumza maneno kwa upana kwa kujitia ufasaha na kwa kuyatukuza maneno yao pasina kuchukua tahadhari wala kuchunga, "na wenye kujitia kujua" wakasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwisha wajua wenye maneno mengi na wenye kuzama zaidi, ni wapi wenye kujifanya kujua? Akasema: Ni wenye kiburi wenye kuwakejeli watu, wale wenye kuzungumza kwa upana katika maneno yao, na hufungua vinywa vyao kwa wingi wa maneno.