





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayesema: Sub-haanallaahi wabihamdi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa njema ni zake) ataoteshewa mti wa mtende peponi".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa atakayesema: "Ametakasika Mwenyezi Mungu" ninamtakasa "Mtukufu" kwa dhati yake na sifa zake na vitendo vyake "na sifa njema ni zake" zikiwa zimeambatanishwa na kuegemeza sifa za ukamilifu wake Mtukufu; atasimikiwa na kupandiwa mti wa mtende katika ardhi ya Pepo kwa kila mara atakayosema.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: " Msihusudiane, na wala msipandishiane bei, na wala msichukiane, na wala msitengane, na wala wasiuze baadhi yenu juu ya biashara ya wengine, na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu muislamu ni ndugu wa muislamu, asimdhulumu, na wala asimsaliti, na wala asimdharau, ucha Mungu uko hapa" Na huku akiashiria katika kifua chake mara tatu "Yamtosha mtu kuwa ni shari kwake kwa kumdharau ndugu yake muislamu, kila muislamu kwa muislamu mwenzake ni haramu damu yake, na mali yake, na heshima yake".
Imepokelewa Imamu MuslimAlimuusia Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kwa ndugu yake muislamu kumtendea mazuri, na akabainisha baadhi ya yale yanayomlazimu katika wajibu na adabu kwao; na miongoni mwa hayo: Wasia wa kwanza: Msihusudiane kwa kutamani baadhi yenu neema za wengine ziwaondokee. Wa pili: Wala msipandishiane, kwa kuzidisha katika bidhaa hali yakuwa hana nia ya kununua; isipokuwa anataka kumnufaisha muuzaji, au kumdhuru mnunuzi. Ya tatu: Msichukiane; nako ni kutaka kuleta madhara, kitu ambacho ni kinyume na mapenzi; isipokuwa kuchukiana kutakapokuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; hapo ni wajibu. Ya nne: Msitengane, nako ni kila mmoja miongoni mwenu kumpa mgongo na kisogo ndugu yake, na akampuuza na kumhama. Ya tano: Wasiuze baadhi yenu juu ya biashara ya wengine, kwa mtu kumwambia aliyenunua bidhaa: Nina bidhaa kama hiyo kwa bei nafuu kuliko hiyo, au nina bidhaa bora kuliko hiyo na kwa bei hiyo hiyo. Kisha akausia rehema na amani ziwe juu yake kwa usia wa ujumla, akasema: Na kuweni kama ndugu kwa kuyaacha yaliyotajwa katika makatazo, na kwa kujitolea mapenzi na huruma na upole na kusikilizana na kusaidizana katika mambo ya kheri, ikiwa ni pamoja na kusafisha mioyo na kunasihiana kwa kila hali. Na miongoni mwa mambo yanayojenga udugu huu: Asimdhulumu ndugu yake muislamu na wala asimfanyie uadui. Na wala asiache ndugu yake muislamu akadhulumiwa akamsaliti katika mahali ambapo anaweza kumtetea na akapata haki yake, na akamuondolea dhulma. Na asimdharau na akamuona duni na akamtazama kwa jicho la kumshusha thamani na kumkejeli; na hilo ni matokeo ya kiburi kilichopo ndani ya moyo. Kisha akabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mara tatu kuwa ucha Mungu uko moyoni, na atakayekuwa na ucha Mungu ndani ya moyo wake unaopelekea katika tabia njema, na kumuogopa Mwenyezi Mungu na kumchunga, basi hawezi kumdharau muislamu, na yamtosha kwake kuwa na mambo ya shari na tabia chafu kwa kumdharau ndugu yake muislamu; na hilo ni kwa sababu ya kiburi kilichopo moyoni mwake. Kisha akasisitiza rehema na amani ziwe juu yake hayo yaliyopita kuwa kila muislamu kwa muislamu mwenzake ni haramu: Damu yake: Kwa kumfanyia uadui akamuuwa, au chini ya hapo kama kumjeruhi au kumpiga na mfano wake, na vile vile mali yake: Kwa kuichukuwa pasina haki, na vile vile heshima yake: Kwa kumtukana yeye mwenyewe au ukoo wake.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayemtatulia muumini tatizo moja katika matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atamtatulia yeye tatizo katika matatizo ya siku ya Kiyama, na atakayemfanyia wepesi mwenye ugumu (katika jambo lake) Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi duniani na Akhera, na atakayemsitiri muislamu Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera, na Mwenyezi Mungu humsaidia mja pale mja anapokuwa katika kumsaidia ndugu yake, na atakayeshika njia akitafuta ndani yake elimu, Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kupitia njia hiyo njia ya kuingia peponi, na hawajawahi kukusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu wakisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na wakisomeshana baina yao, isipokuwa huwashukia utulivu na huwagubika rehema na Malaika huwafunika, na Mwenyezi Mungu huwataja (vizuri) kwa wale walioko kwake (Malaika), na yeyote ambaye matendo yake yatamchelewesha kuingia peponi basi ukoo wake hautompeleka mbio (kuingia)".
Imepokelewa Imamu MuslimAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa malipo ya muislamu mbele ya Mwenyezi Mungu ni kulingana na yale anayoyatenda muislamu pamoja na waislamu wenzake; atakayetatua na akafariji na akaondoa, na ampa nafuu muumini ya dhiki na tabu miongoni mwa shida za dunia, basi Mwenyezi Mungu atamlipa kwa kumtatulia tatizo miongoni mwa matatizo ya siku ya Kiyama. Na atakayemfanyia wepesi mwenye hali ngumu na akamrahisishia na akamuondolea ugumu wake, basi naye Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi katika dunia na Akhera. Na atakayemsitiri muislamu, kama akiyaona kwake yale yasiyofaa kudhihirishwa katika mapungufu na kuteleza, basi naye Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anakuwa mwenye kumsaidia mja wake, pale ambapo mja anapokwenda mbio kumsaidia ndugu yake katika masilahi yake ya dunia na Akhera, na msaada unakuwa kwa kumuombea dua, au kwa mwili na mali na mengineyo. Na atakayekwenda kwa ajili kutafuta elimu ya kisheria, akikusudia kupata radhi za Mwenyezi Mugnu Mtukufu; Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kwa elimu hiyo njia ya kuingia pepnoni. Na hawatojikusanya watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu, wakikisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakifundishana baina yao, isipokuwa huwateremkia utulivu na amani, na huwafunika na kuwaenea rehema ya Mwenyezi Mungu, na Malaika huwafunika, na Mwenyezi Mungu huwasifia kwa wale walio karibu kwake, na inatosha kuwa ni fahari kwa mja kutajwa na Mwenyezi Mungu kwa wale walioko juu. Na yatakayekuwa matendo yake ni pungufu, hayatomuunganisha na watu wenye vyeo kwa ajili ya matendo yao, anatakiwa asibweteke kwa utukufu wa nasaba na ubora wa baba zake, na akafanya uzembe katika amali.
Kutoka kwa Agharri radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Enyi watu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninatubia kwa siku mara mia moja".
Imepokelewa Imamu MuslimAnawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu kukithirisha kuomba toba na msamaha, na anajielezea mwenyewe kuwa yeye hutubia kwa Mwneyezi Mungu Mtukufu na kumuomba msamaha kwa siku zaidi ya mara mia moja, na haliyakuwa alikwisha samehewa yaliyotangulia katika madhambi yake na yajayo, na katika hilo kuna ukamilifu wa kujidhalilisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Kikoi cha muislamu kifikie nusu ya muundi, na wala hakuna tabu wala hakuna ubaya kikiwa kati yake na kati ya fundo mbili za miguu, kitakachokuwa chini ya fundo mbili basi hicho ni motoni, na atakayeburuza kikoi chake kwa kiburi hatomtazama Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na AhmadAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanaume muislamu katika kikoi chake, nacho ni kila kinachositiri nusu ya chini kwa wanaume, kwa hali tatu: Ya kwanza: Inayopendeza iwe kati kati ya muundi. Ya pili: Inayojuzu pasina karaha ni ile inayokuwa chini ya kongo mbili; nayo ni mifupa miwili iliyotokeza katika maungio ya muundi na mguu. Ya tatu: Iliyoharamishwa, nayo ni ile inayokuwa chini ya kongo mbili, na inahofiwa kwake kupatwa na adhabu ya moto, na ikiwa ni kwa kiburi na kwa kufurahia na ujeuri, Mwenyezi Mungu hatomtazama.
Kutoka kwa Ma'qal bin Yasari -radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Kufanya ibada katika (nyakati) za vita vurugu na mauaji ni kama kuhama kuja kwangu".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika nyakati za vurugu na fitina na mauaji na kuparaganyika kwa mambo ya watu katika ibada na kushikamana nayo, na kwamba malipo yake ni kama kuhama kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hii ni kwa sababu watu hughafilika nayo, na hawatengi muda ila mtu mmoja mmoja.
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna muislamu yeyote ataomba maombi yasiyokuwa ndani yake na kuomba dhambi wala kukata udugu, isipokuwa Allah atampa kwa maombi hayo moja kati ya mambo matatu: Moja ima amuharakishie maombi yake, au amlimbikizie ili amlipe siku ya Kiyama, au amuondoshee katika mabaya mfano wake" Wakasema: (Maswahaba) kwa hiyo tuzidishe? Akasema: "Allah ni mwenye kuzidisha mara dufu".
Imepokelewa na AhmadAlieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa muislamu atakapomuomba Mwenyezi Mungu na akamuomba maombi ambayo si dhambi, kama kumuomba amrahisishie maasi na dhulma, na wala akawa hakuomba kukata udugu; kama kuwaombea dua mbaya watoto wake au ndugu zake wa karibu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa kwa dua yake hiyo moja kati ya mambo matatu: Ima amharakishie dua yake na ampe alichoomba. Na ima Mwenyezi Mungu amcheleweshee mpaka siku ya Kiyama kwa kumpa daraja za juu zaidi, na rehema na msamaha kutokana na madhambi. Na ima amkinge katika dunia na mabaya mfano wake kwa kiwango cha dua. Maswahaba wakasema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwa hivyo tukithirishe dua; ili tuweza kupata moja kati ya fadhila hizi? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni mengi na ni makubwa kuliko mnavyoviomba, kipawa chake hakimaliziki, na wala hakiishi.
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema wakati wa matatizo: "Laa ilaaha illa llaahul a'dhwiimul haliim, Laa ilaaha illa llaahu Rabbul A'rshil A'dhwiim, Laa ilaaha illa llaahu Rabbu ssamaawaati warabbul A'rshil kariim" Tafsiri: Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mpole, Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola wa A'rshi tukufu, Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola wa mbingu, na Mola wa ardhi, na Mola wa A'rshi takatifu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema wakati wa kuzidi kwa matatizo na huzuni kwake: "Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu" Hakuna wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, "Mtukufu" wa cheo, Mtukufu wa shani, katika dhati yake na sifa zake na majina yake, "Mpole" asiyemharakisha mwenye kuasi kwa kumpa adhabu bali anaichelewesha, na anaweza kumsamehe pamoja nakuwa anauwezo wa kumuadhibu, yeye ndiye muweza Mtukufu juu ya kila kitu ni muweza. "Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa Arshi tukufu" Muumba wa Arshi tukufu, "Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa mbingu na ardhi" na muumba wa mbingu na ardhi, na muumba wa kila kitu ndani yake na mmiliki wake na mrekebishaji wake, na mwenye maamuzi ndani yake kwa namna yoyote aitakayo, "Mola wa Arshi karim" Muumba wa Arshi karim.
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake juu ya kinywa chake, kwani Shetani huingia".
Imepokelewa Imamu MuslimAmemuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kupiga mwayo pale alipofungua kinywa chake kwa sababu ya uvivu au kujaa na mfano wake; kuwa aweke mkono wake juu ya kinywa chake ili akifunge kwa mkono; na hii ni kwa sababu Shetani huingia ndani yake anapokiacha wazi, kuweka mkono kunakuwa ni kizuizi cha kumzuia kuingia.