





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Amri bin Harithi shemeji yake na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kaka yake na mama wa waumini Juwairia binti Harithi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, amesema: Hakuacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kifo chake Dirham moja wala Dinari, wala mtumwa wala kijakazi wala chochote, isipokuwa nyumbu wake mweupe, na silaha yake, na kipande cha Ardhi alichokitoa kama sadaka.
Imepokelewa na Al-BukhaariyAlifariki Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wala hakuacha Dirham ya fedha wala Dinari ya dhahabu, wala mtumwa mmilikiwa wala kijakazi mmilikiwa, wala mbuzi wala ngamia wala chochote katika mali, isipokuwa nyumbu wake mweupe aliyekuwa akimpanda, na silaha yake aliyokuwa akiibeba, na kipande cha Ardhi alichokitoa wakfu kwa ajili ya wasafiri.
Kutoka kwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Hakuwahi kutuhutubia sisi Mtume rehema na amani ziwe juu yake isipokuwa alisema: "Hana imani asiyekuwa na uaminifu, na hana dini asiyekuwa na ahadi (za kweli)".
Imepokelewa na AhmadAnaeleza Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake kuwa ni mara chache sana akihutubia Mtume rehema na amani ziwe juu yake au atoe mawaidha isipokuwa alikuwa akitaja mambo mawili: La kwanza: Hana imani mtu ambaye ndani ya nafsi yake kuna hiyana na mtu katika mali yake au nafsi yake au familia yake. La pili: Hana dini kamili mwenye kufanya hiyana katika ahadi na mikataba na kuivunja.
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisimama kwa watu waliokaa, akasema: "Je, nisikuelezeni mbora wenu na muovu wenu?" Anasema: Wakanyamaza, akalisema hilo mara tatu, mtu mmoja akasema: Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tueleze mbora wetu na muovu wetu, akasema: "Mbora wenu ni yule inayetarajiwa heri yake, na kuaminiwa kutokuwepo kwa shari yake, na muovu wenu ni yule isiyetarajiwa heri yake, na kutoaminiwa shari yake".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyAlisimama Mtume rehema na amani ziwe juu yake mbele za watu waliokaa miongoni mwa Maswahaba zake akawauliza, je nisikuelezeni na nikumbusheni ni nani mbora wenu na ni nani muovu wenu? Wote hawakuzungumza na wala hawakujibu chochote, kwa kuhofia kubainishwa mbora wao na muovu wao na wakahofia fedheha wakanyamaza. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akarudia swali mara tatu, akajibu mtu mmoja miongoni mwao: Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tueleze mbora wetu na muovu wetu. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawabainishia: Kuwa mbora wenu ni yule inayesubiriwa na kutarajiwa heri yake na ihisani yake na wema wake, na kuaminiwa kutowepo shari yake kusiogopwe uadui wake na uonevu wake na dhuluma yake, na kuwa muovu wenu ni yule asiyetarajiwa wala kusubiriwa wala kutamaniwa kupatikana heri yake na ihisani yake na wema wake, na haiaminiwi shari yake, bali unahofiwa uadui wake na uonevu wake na dhuluma yake.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu"
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kwa kawaida hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu kwa wema na mazuri waliyomfanyia, na hii ni kwa sababu mambo haya mawili yote yanaungana, kiasi kwamba katika tabia yake na desturi yake ni kukufuru neema na kuacha kushukuru, pia atakuwa katika kawaida yake ni kukufuru neema za Mwenyezi Mungu na kupuuza katika kushukuru kwa neema hizo.
Kutoka kwa Hassan amesema: Alituhadithi Jundab bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake, ndani ya Msikiti huu, na hatujasahahu tangu alivyotuhadithia, na wala hatuhofii kuwa Jundab alimsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alisema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kulikuwa na mtu katika wale waliokuwa kabla yetu alipatwa na jeraha, akakasirishwa nalo na wala hakuvumilia maumivu, akachukua kisu akaukata mkono wake na akakiharakisha kifo, damu haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, basi nimemharamishia kwake pepo.
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa".
Hadithi hii imepokelewa na Bukhari na Muslim, na matamshi haya ni ya Muslim, na akaipokea Bukhari kwa ufupiIlikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako nimejisalimisha" na nimenyenyekea, "na kwako nimeamini" na nimesadikisha na nimekiri, "Na juu yako nimetegemea" na nimekabidhi na nimetegemea, "na kwako nimetubia" na nimerejea na nimekuja, "na kwako ninapambana" na ninajibizana kwa hoja na maadui zako, "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda kwako" Ninajiegemeza, "kwa utukufu wako" na ngome yako na ushindi wako, "hapana mola wa haki isipokuwa wewe" na wala hakuna muabudiwa wa haki zaidi yako, "unipoteze" kutoka katika uongofu na taufiki ya kupata radhi zako, "Wewe ndiye uliye hai ambaye hafi" na wala hamaliziki, "na majini na watu wote wanakufa".
Kutoka kwa Imran bin Huswaini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Assalaam alaikum, akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kumi" Kisha akaja mwingine akasema: Assalaam alaikum warahmatullaah, akamjibu, akakaa, akasema: "Ishirini" Kisha akaja mtu mwingine akasema: Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh, akamjibu akakaa, akasema: "Thelathini".
Imepokelewa na Abu Daud na Tirmidhiy, Ahmad na Ad-DarimiAlikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Assalaam alaikum" Akamjibu kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ameandikiwa mema kumi, kisha akaja mtu mwingine akasema: "Assalaam alaikum warahmatullaahi" Akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Amepata thawabu ishirini, kisha akaja mwingine akasema: "Assalaam alaikum warahmatullahi wabarakaatuh", akamjibu akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kapata thawabu thelathini; yaani kwa kila tamko ni mema kumi.
Kutoka kwa Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba yeye alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na uchamungu na kujizuia na machafu nakuwa ni mwenye kutosheka".
Imepokelewa Imamu MuslimIlikuwa miongoni mwa dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba uongofu" na njia iliyonyooka katika kuijua haki na kuifanyia kazi, "na uchamungu", kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo, "na kujizuia na machafu" kujizuia na yale yasiyokuwa halali wala si mazuri miongoni mwa kauli au kitendo, "na kutosheka" na viumbe, kiasi ambacho asimuhitaji yeyote zaidi ya Mola wake Mlezi Aliyetakasika na kutukuka.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Inakutosha kwa Safia kadhaa wa kadhaa, (Anasema mmoja wa wapokezi wa hadithi hii: Alikuwa akikusudia ufupi) Akasema: "Hakika umesema neno ambalo lau lingechanganywa na maji ya Bahari basi (lingeyabadili rangi) kwa kuchanganyika nayo" Akasema Aisha: Na nikamsimulia kuhusu mtu fulani, akasema: "Sipendi kuona kuwa kuna mtu nimemsimulia na kwamba mimi nina kadhaa wa kadhaa".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadMama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake alisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Inakutosha kwa Safia (Alikuwa akikusudia mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake) Kuwa miongoni mwa aibu zake za kimaumbile ya kimwili ni mfupi, Mtume akasema: Hakika umesema neno ambalo lau lingechanganywa na maji ya Bahari basi lingeyazidia na kuyabadili na kuyaharibu, Aisha akasema: Na nilichokifanya ni sawa na kitendo cha mtu kumsema mtu ili kumshusha hadhi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Sipendezwi kuzungumza aibu zake, au kusimulia kuhusu yeye au kufanya mfano wa vitendo vyake, au kusema mfano wa kauli zake, kwa sura ya kumdharau hata kama nitapewa kiasi kingi katika mali za dunia kwa hilo.