Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way






























Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
Jariri bin Abdullah Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mwanaume kumwangalia mwanamke wa kando ghafla bila kukusudia? Basi akamuamrisha rehema na amani ziwe juu yake kuwa aelekeze uso wake pembeni upande wa pili mara anapojua hilo, na hatokuwa na dhambi juu yake.
Ameeleza Omari radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisimama baada ya kumpopoa mawe Maaizi bin Malik Al-Aslami radhi za Allah ziwe juu yake, kwa adhabu ya zinaa, akawahutubia watu, na akasema: Jiepusheni na chafu hili na yote yanayotia kinyaa na machafu miongoni mwa maasi aliyoyakataza Mwenyezi Mungu, na atakayeangukia na akafanya chochote basi ni wajibu kwake mambo mawili: La kwanza: Ajifiche katika mahali alipomsitiri Mwenyezi Mungu, na asimueleze yeyote kuhusu maasi yake. La pili: Afanye haraka kutubia kwa Mwenyezi Mungu na wala asiendelee, na yatakayeonekana wazi maasi yake basi tutamsimamishia sheria iliyotajwa ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mwenyezi kwa maasi hayo.
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekaa itikafu katika kuba (hema) ndani ya msikiti wake kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, akasikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake wakidhihirisha kisomo chao cha Qur'ani kwa sauti kubwa inayowaudhi baadhi yao. Akafunua pazia la hema, na akamlaumu aliyefanya hivyo na hakupendezwa, na akasema: Nyinyi wote mnazungumza na Mola wenu kwa kusoma kwenu Qur'ani, basi mmoja wenu asimuudhi mwenzake kwa sauti yake katika kusoma kwake, au ndani ya swala yake.
Anawaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanaume kuvaa nguo zenye rangi nyeupe na kuwavisha maiti pia; kwani ni katika nguo bora.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa safarini katika vita na akiwa pamoja na Maswahaba zake miongoni mwa Muhajirina na Maanswari radhi za Allah ziwe juu yao, mtu mmoja katika Muhajirina akampiga mgongoni mtu mmoja miongoni mwa Maanswari kwa mkono wake. Answari akasema: Nipeni msaada enyi Maanswari, na akasema Muhajiri: Nipeni msaada enyi Muhajirina, akawasikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Nini hiki?. Wakasema: Mtu mmoja katika Muhajirina kampiga mtu katika Maanswari kwa mkono wake, Answari akasema: Nipeni msaada enyi Maanswari, na Muhajiri akasema: Nipeni msaada enyi Muhajirina. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Achaneni na desturi hii ya kijinga, kwani ni mbaya inachukiza na ina udhi; nayo ni kwamba mtu akizidiwa na mgomvi wake anawaita watu wake wanaanza kumsaidia sawa sawa awe kadhulumu au kadhulumiwa, kwa sababu ya ujinga wao, na ubaguzi wao. Amesema Jabiri: Na Maanswari wakati amefika Mtume rehema na amani ziwe juu yake mji wa Madina walikuwa wengi, kisha Muhajirina wakawa wengi baada ya hapo. Akasema kiongozi wa unafiki Abdallah bin Ubai bin Saluli: Jambo limefikia huko?! Wallah tukirejea Madina watukufu (anajikusudia yeye na watu wake) watawatoa katika mji wa Madina madhalili (anakusudia Mtume rehema na amani ziwe juu yake na watu wake). Akasema Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake: Hebu, niache ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nikate shingo ya huyu mnafiki, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Muache, ili watu wasiseme kuwa Muhammadi anauwa wafuasi wake, hata kama ni kwa dhahiri.
Ameeleza Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilala juu ya busati dogo lililoshonwa kutokana na baadhi ya mimea, akasimama ukiwa tayari mkeka umeathiri katika ngozi ya ubavu wake, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau tungelikuandalia godoro laini basi ingelikuwa bora kuliko kujilaza kwako juu ya mkeka mgumu, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Sina mapenzi wala hamu ya dunia mpaka niwe na tamaa nayo, kwani mfano wangu mimi na kubakia katika dunia ni kama msafiri aliyejikinga kivulini kwa muda mfupi kisha akaondoka akakiacha.
Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kwamba watu wa nyumba ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawakuwahi kula milo miwili kwa siku moja isipokuwa mlo mmoja kati ya hiyo utakuwa ni tende.
Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, watu wa nyumba ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawakuwahi kushiba tangu walipoingia Madina kwa chakula cha ngano kwa muda wa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki rehema na amani ziwe juu yake.
Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa godoro alilokuwa akilalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake lilikuwa limetengenezwa kwa ngozi, na limejazwa majani ya mitende, na vile vile mto wake aliokuwa akiegemea.