Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way






























Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu wema na dhambi, akasema: Kubwa kabisa katika wema ni tabia njema pamoja na Allah, kwa kumcha, na pamoja na watu, kwa kuvumilia kero, na kupunguza hasira, na kukunjua uso, na kuwa na maneno mazuri, na kuunga udugu na kutii na kuwa mpole na kutenda wema, na kuishi vizuri na familia, na kusuhubiana na watu vizuri. Na ama dhambi ni kila kitakachokereketa ndani ya nafsi katika mambo yenye kutatiza, na kifua kikakosa utulivu na kutokunjuka, na moyo ukapata shaka, na ukaogoga kwa sababu ni dhambi, na ukawa hukutaka kulidhihirisha kwa mtu au hadharani mbele za watu kwakuwa ni baya, na hii ni kwa sababu nafsi hupenda watu waone yale mazuri yake, ikiwa itachukia watu kuyaona baadhi matendo yake basi hayo ndiyo madhambi wala hayana kheri ndani yake.
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anakubali toba kutoka kwa waja wake, mja akitenda dhambi wakati wa mchana na akatubia usiku Mwenyezi Mungu hukubali toba yake, na akitenda dhambi usiku na akatubia mchana basi Mwenyezi Mungu hukubali toba yake, Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake kwa kuifurahia toba, na kuikubali, na mlango wa toba unabaki wazi mpaka jua lichomoze kutoka magharibi, likiashiria mwisho wa dunia, basi likichomoza mlango wa toba utafungwa.
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika yale yaliyokuja na usia ndani yake kutoka kwa Manabii waliotangulia, na yakaenea kwa watu na watu wakarithishana kutoka kwao karne baada ya karne, mpaka yakamfikia wa mwanzo katika umma huu, ni; tazama unayotaka kuyafanya, ikiwa yatakuwa ni katika mambo ambayo si aibu basi fanya, na ikiwa ni katika mambo ya aibu basi acha; kwa sababu kinachozuia kufanya matendo mabaya ni haya, atakayekosa aibu basi hutumbukia katika kila machafu na maovu.
Ibn Omari Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, ameeleza kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimshika begani - nacho ni kiungo cha juu cha mkono na bega - akamwambia: Kuwa katika dunia hii kana kwamba wewe ni mgeni aliyekuja katika nchi ambapo hakuwa na makazi yake, na hakuna wakazi wa kumkaribisha wala familia tegemezi, wala mahusiano ambayo ni sababu ya hili, kuwa shupavu zaidi kuliko mgeni huyu ambaye ni mpita njia anayepita njiani kuelekea katika nchi yake. Kwa sababu mgeni anaweza kuishi katika nchi ya kigeni na akawa mkazi ndani yake, tofauti na msafiri anayetaka kwenda nchini kwake, haja yake huwa ni kupumzika ili apate wepesi na sio kukaa, na kuwa na hamu ya kuwasili katika nchi yake kama vile msafiri hahitaji zaidi ya yale yatakayomfikisha mwisho wa safari yake, halikadhalika muumini katika ulimwengu huu hahitaji zaidi ya yale yatakayomfikisha mahali pazuri. Akazifanyia kazi bin Omari nasaha hizi na alikuwa akisema: Ukiamka usisubiri jioni, na ukishinda mpaka jioni usisubiri asubuhi, na ihesabu nafsi yako kuwa katika wafu walioko makaburini, na kwakuwa umri haukosi moja katika ya mawili, afya na maradhi; fanya haraka siku za afya yako kwa kufanya ibada kwa ajili ya maradhi yako; na tumia fursa ya matendo mema katika wakati wa afya kabla maradhi hayajakuzuia, na faidika na uhai wako katika dunia, kusanya ndani yake yale yatakayokunufaisha baada ya kifo chako.
Mtu mmoja alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ibada za sunna zimekuwa nyingi kwake mpaka zikamshinda kwa sababu ya udhaifu wake, kisha akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali nyepesi itakayompa thawabu nyingi atakayoshikamana nayo na adumu nayo. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuelekeza kuwa ulimi wake uwe mbichi utikisike kwa kudumu kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kila wakati na kila hali; kama kumsabihi na kumhimidi na kumtaka msamaha na kumuomba na mfano wake.
Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa imani kamili ya Muislamu yeyote haikamiliki mpaka ampendelee nduguye anachokipenda yeye, katika matendo mema, na aina mbalimbali za wema katika dini na dunia, na achukie kwake kinachochukiwa na nafsi yake, na ikiwa ataona kwa ndugu yake Muislamu kuna upungufu katika dini yake, basi ajitahidi kurekebisha, na akiona kuna jambo la kheri basi amtie moyo na amsaidie, na amnasihi katika dini yake au mambo ya dunia yake.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemkataza muislamu kumshutumu na kumtukana ndugu yake muislamu, nakuwa hilo ni katika ufasiki ambao ni kutoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, nakuwa muislamu kukabiliana na ndugu yake muislamu ni katika matendo ya ukafiri, lakini ni ukafiri mdogo.
Anakataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwaanza Mayahudi na Wakristo kwa salam, hata kama watakuwa wamepewa hifadhi katika nchi za kiislamu, achilia mbali makafiri wengineo, na akabainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa tutakapokutana na mmoja wao njiani tumbane mahala pembamba, muumini ndiye atembee katikati ya njia, na anayepisha ni kafiri, na muislamu asiwe dhalili kwa hali yoyote ile.
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama katika kauli na matendo ni tabia njema, na hii ni kwakuwa na uso mkunjufu, na kujizuia na maudhi, na kutenda wema. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anamchukia mtu muovu katika kauli zake na vitendo, mwenye mdomo mchafu katika yale yanayotamkwa na ulimi wake.