





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abuu Dhari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika ardhi yenye mawe katika mji wa Madina, tukaelekea mlima Uhudi, akasema: "Ewe Abuu Dhari" nikasema: Labbaika (nimekuitikia) Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Akasema: "Hainifurahishi mimi kumiliki dhahabu mfano wa mlima huu wa Uhudi, zikapita siku tatu nikawa hata na dinari moja (katika mali hiyo) isipokuwa kiasi ninachokihifadhi kwaajili ya kulipa deni, isipokuwa niseme kwa waja wa Mwenyezi Mungu hivi na vile." akigeuka kuliani kwake na kushotoni kwake, na nyuma yake, kisha akatembea, Akasema: "Hakika wenye vingi ndio wenye vichache siku ya kiyama isipokuwa atakayezungumza kwa mali hivi na vile hivi na vile" akageuka kuliani kwake na kushotoni kwake na nyuma yake, "Na wachache katika wao" kisha akasema kuniambia "Bakia hapo usitoke mpaka nikujie" kisha akaondoka katika giza la usiku mpaka akapotelea, nikasikia sauti imenyanyuka, nikapata hofu isijekuwa kuna mtu kamvamia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- nikataka kumfuata nikakumbuka kauli yake "Bakia hapo usitoke mpaka nikujie" nikabakia mpaka aliponijia, nikasema: Nilisikia sauti nikaingiwa na hofu sana, nikamuelezea akasema: "Hivi uliisikia?" Nikasema: Ndiyo, akasema: "Huyo ni Jibril alinijia akasema: Atakayekufa katika umma wako hamshirikishi Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi" Nikasema: Hata akizini na akaiba? Akasema: "Hata akizini na akaiba".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimMaana ya hadithi: Anaeleza Abuu Dhari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa yeye alikuwa akitembea na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika ardhi yenye mawe katika mji wa Madina, ukawaelekea mlima wa Uhudi ambao unajulikana, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Hainifurahishi mimi: Yaani hainipendezi mimi, kuwa mimi nina miliki dhahabu mfano wa mlima Uhudi na zikapata siku tatu hali yakuwa bado nina chochote katika mali hiyo, hata Dinari moja, isipokuwa kiasi nilichokiweka kwaajili ya kulipa deni, basi lau kama ningekuwa ninamiliki kiasi cha dhahabu halisi mfano wa mlima Uhudi basi ningekitoa chote katika njia ya Mwenyezi Mungu, na nisingebakisha katika mali hiyo isipokuwa kile ninachohitajia kwaajili ya kulipa haki za watu, na kulipa madeni ninayodaiwa, na kisinge zidi chochote juu ya hayo, kwani mimi halinifurahishi kupita siku tatu hali yakuwa bado niko na mali hiyo. Na hii inaonyesha kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni mtu asiyekuwa na tamaa na dunia kuliko watu wote; kwasababu yeye hataki kukusanya mali isipokuwa ile anayoihifadhi kwaajili ya kulipa madeni, na alifariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- hali yakuwa vazi lake la kivita kaliweka rehani kwa Yahudi kwasababu ya ngano aliyochukua kwaajili ya familia yake. Na lau kama dunia ingekuwa inapendeka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi asingemnyima chochote Nabii wake -Rehema na Amani ziwe juu yake-, Dunia imelaaniwa na vimelaaniwa vilivyomo isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na vinavyofuata hilo, na mjuzi au mwenye kujifunza, na yale yote yanayokuwa katika utiifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kisha akasema: "Wenye vingi ndio wenye vichache siku ya kiyama" Yaani wenye kuchuma vingi katika dunia ndio wenye matendo mema machache siku ya kiyama; kwasababu mara nyingi mtu zinapokithiri mali zake huwa anakuwa na hali ya kutosheka na kiburi na kupuuza mambo ya utiifu wa Mwenyezi Mungu; kwasababu dunia inampumbaza, anakua ni mwenye kutaka vingi duniani na kupungukiwa katika akhera. Na kauli yake: "isipokuwa atakayesema kwa mali hivi na vile hivi na vile" Yaani: Akazigawa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha akasema: "Na wachache katika wao" Na maana yake nikuwa wenye kutoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wachache. Kisha akasema: (Atakayekufa hali yakuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote ataingia peponi hata kama atazini na akaiba) Na hii haimaanishi kuwa zinaa na wizi ni mambo mepesi, bali ni mazito, na kwasababu hii aliyachukulia uzito Abuu Dhari na akasema: Hata kama atazini na akaiba? Akasema (Hata kama atazini na akaiba). Na hii ni kwakuwa atakayekufa katika imani na akawa na maasi katika madhambi makubwa; Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu hasemehe kushirikishwa, na anasamehe yasiyokuwa hilo kwa amtakaye" anaweza kumsamehe Mwenyezi Mungu wala asimuadhibu, na anaweza kumuadhibu, lakini hata akimuadhibu mwisho wake mafikio yake ni peponi; kwasababu kila aliyekuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na akawa hakufanya kitu kinachomtoa katika uislamu; basi mafikio yake ni peponi, ama atakayefanya linamuingiza katika ukafiri na akafa katika jambo hilo, huyu akabakishwa milele motoni na matendo yake yameporomoka; kwasababu wanafiki walikuwa wakisema kumwambia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- (Tunashuhudia kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu), na walikuwa wakimtaja Mwenyezi Mungu lakini hawamtaji Mwenyezi Mungu isipokuwa kidogo, na wanaswali lakini (Na wanaposimama katika swala husimama kwa uvivu) lakini pamoja na hiyo wao watakuwa katika tabaka la chini zaidi katika moto. Ikaonyesha juu ya kuipa nyongo (kuipuuza) dunia, nakuwa mwanadamu hatakiwi kuitundika nafsi yake katika dunia, na iwe dunia mkononi mwake na si moyoni mwake, mpaka moyo wake uelekee kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka; kwani huku ndiko kuipa nyongo dunia kikamilifu, Na haimaanishi kuwa usichukue chochote katika dunia; bali chukua katika dunia kilicho halali kwako, na wala usisahau fungu lako katika dunia, lakini iweke mkononi mwako na wala usiiweke moyoni mwako, Na hili ndilo la muhimu.
Na kutoka kwa Abuu Musa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Mfano wa yule anayemtaja Mola wake na yule asiyemtaja Mola wake, ni mfano wa aliyehai na aliyekufa", Na tamko la Muslim: "Mfano wa nyumba anayotajwa Mwenyezi Mungu ndani yake, na nyumba asiyotajwa Mwenyezi Mungu ndani yake, ni mfano wa aliyehai na aliyekufa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake tofauti kati ya yule anayemtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu na kati ya yule asiyemtaja, kuwa ni mfano wa tofauti iliyopo kati ya aliyehai na aliyekufa katika manufaa yake na uzuri wa muonekano wake, hivyo mfano wa yule anayemtaja Mola wake ni mfano wa aliyehai ambaye muonekano wake umependeza kwa kuwa na nuru ya uhai, na anamanufaa, na mfano wa yule asiyemtaja Mwenyezi Mungu ni mfano wa maiti ambaye muonekano wake umeharibika, na ndani yake kumebatilika, na hana manufaa ndani yake. Na vile vile nyumba inasifiwa kwa sifa ya kuwa hai endapo wakazi wake wanamtaja Mwenyezi Mungu, na vinginevyo itakuwa nyumba mfu kwa kubweteka wakazi wake na kutomtaja Mwenyezi Mungu; na nyumba ikiitwa hai na maiti wanakusudiwa wakazi wa nyumba hiyo.
Kutoka kwa Abuu Saidi Al Kudry -radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba siku moja Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikaa juu ya Mimbari na tukakaa pembezoni mwake, akasema: "Hakika mimi ninakuhofieni baada yangu, yale mtakayofunguliwa juu yenu katika maua ya dunia na pambo lake" Mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi kheri inaweza kuleta shari? Akanyamaza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakamwambia: Una nini wewe? Unamsemesha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wala hakusemeshi? Tukamuona akiteremshiwa wahyi, anasema: akafuta jasho, akasema: "Yuko wapi muulizaji?" ni kana kwamba alipendezwa na swali lake, akasema: "Hakika kheri haileti shari, na hakika katika yale yanayooteshwa na masika huua au kudhuru, isipokuwa mifugo wanaokula malisho ya kijani, hula mpaka zinapopanuka mbavu zao hulielekea Jua, hujisaidia haja kubwa na ndogo, na wakapumzika, na hakika mali hii ni kijani kitamu, neema bora ya mtu muislamu ni ile aliyoitoa kumpa masikini na yatima na mpita njia -Au kama alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake- na hakika atakayeichukua pasina haki yake, ni sawa na yule anayekula wala hashibi na atakuwa shahidi juu ya mali hiyo siku ya Kiyama".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikaa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku moja juu Mimbari akiwahadithia Maswahaba zake akasema: Hakika kikubwa ninachokihofia zaidi kwenu nyinyi baada yangu ni yale mtakayofunguliwa katika baraka za Ardhi na maua ya Dunia na pambo lake, na muonekano wake, na yale yaliyomo miongoni mwa aina mbalimbali za starehe na nguo na mazao na mengineyo miongoni mwa yale ambayo watu hujifaharisha kutokana na uzuri wake pamoja nakuwa yanadumu kwa muda mchache. Mtu mmoja akasema: Maua ya Dunia ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, je inaweza kurudi neema hii na kuwa janga na adhabu?! Watu wakamlaumu muulizaji pale walipomuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake kanyamaza, na wakadhania kuwa kamkasirisha. Ikabainika kuwa rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiteremshiwa wahyi, kisha akaanza kufuta jasho katika paji lake la uso, akasema: Yuko wapi muulizaji? Akasema: Mimi. Akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifia, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Kheri ya kweli haiji ila kwa kheri, lakini maua haya si kheri halisi kwa kuwa yanapelekea katika fitina na kushindana na kushughulika nayo na kuwacha kuielekea Akhera kikamilifu, kisha akapigia mfano wa hilo akasema: Hakika mimea ya masika na kijani chake; nayo ni aina za mimea ambazo huwapendeza sana wanyama, na huwaua kwa kuila kwa wingi na kuvimbewa au hukaribia kuwaua, isipokuwa mnyama anayekula mimea ya kijani aliyekula mpaka ikajaa sehemu ya tumbo lake, akaelekea juani na akatoa kinyesi chepesi kutoka tumboni mwake au akakojoa, kisha akayacheua yaliyoko tumboni mwake kisha akayatafuna kisha akayameza, kisha akarudi kula tena. Hivyo mali hii ni kama majani ya kijani matamu, yanaua au yanakaribia kuuwa yanapokithiri; isipokuwa kama atatosheka na kidogo ambacho anahaja nacho na kitakachomtosha kwa njia ya halali, hii haidhuru, na neema bora ya muislamu ni kwa yule atakayetoa na kumpa masikini na yatima na mpitanjia, na yule mwenye kuichukua kwa haki atakabarikiwa katika mali hiyo, na atakayeichukua pasina haki yake mfano wake ni kama mfano wa yule anayekula wala hashibi, na mali hiyo itakuwa shahidi juu yake siku ya Kiyama.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani mwenye haki zaidi ya kumfanyia wema wa karibu? akasema: "mama yako", akasema: kisha nani? akasema: "kisha mama yako" akasema: kisha nani? akasema: "kisha mama yako", akasema: kisha nani? akasema: "kisha baba yako",Hadithi Muttafaqun a'laihi. Na katika riwaya: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani mwenye haki zaidi ya kumfanyia wema wa karibu? akasema: "mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha nayemfuata kwa ukaribu".
Imepokelewa na Imamu Muslim - Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimHadithi inaonyesha kuwa wazazi wote wawili wana haki ya kufanyiwa ukaribu mwema; na kuyajali kikamilifu mambo yao (Na uambatane nao katika dunia kwa wema), lakini haki ya mama iko juu ya haki ya baba kwa daraja nyingi, kwani hakutaja haki ya baba mpaka baada ya kuwa ametaja haki ya mama na akaisisitiza kikamilifu, kwa kutaja kwake mara tatu, bali cheo chake kimekuwa juu ya cheo cha baba pamoja nakuwa wanashrikiana katika kumlea mtoto, huyu kwa mali zake na uangalizi wake, na huyu kwa huduma zake katika kumlisha na kumnywesha na kumvisha na kumlaza, mpaka mwisho. Hii ni kwasababu mama ameumia kwaajili yake kwa mambo ambayo hakuumia nayo baba, kambeba miezi tisa tabu juu ya tabu, na udhaifu juu ya udhaifu; na akamzaa kwa shida; mpaka anakaribia kufa kwasababu ya misukosuko mikubwa anayokumbana nayo, na vile vile kamnyonyesha miaka miwili, anakesha ili yeye apate raha, anafanya kwaajili ya maslahi yake hata kama ataendelea kupata maumivu kwaajili ya hilo, na kwaajili hii wahyi ukatamka: (Na tumemuusia mwanadamu kwa wazazi wawili kuwafanyia wema, kambeba mama yake kwa tabu, na kamzaa kwa tabu, na kumbeba kwake na kumuachisha kwake (kunyonya) miezi thelathini), utaona kausiwa mwanadamu kwa wazazi wake wawili kuwafanyia wema; na hakueleza miongoni mwa sababu zaidi ya zile anazozipata mama ikiwa ni ishara ya ukubwa wa haki yake. Na katika uzuri wa kuishi na wazazi wawili ni kuwapa mahitaji ya chakula na kinywaji na mavazi; na mengineyo katika mahitajio ya kimaisha, ikiwa wanauhitaji, bali ikiwa wakiwa katika maisha ya chini au ya kati, nawe ukawa katika maisha ya neema na mazuri, basi wanyanyue katika daraja yako au zaidi, kwani hilo ni katika kuwafanyia wema na kuwa nao karibu. Na kumbuka alichokifanya Yusuf pamoja na wazazi wake akiwa tayari kapewa ufalme, pindi alipowanyanyua juu ya kiti cha ufalme baada yakuwa kawaleta kutoka kijijini. Na katika kuwafanyia wema, bali ndiyo jumla ya mambo yote, ni yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu katika kauli yake: (Na amehukumu Mola wako kuwa msiabudu ila yeye na wazazi wawili kuwafanyia wema, ikiwa atafikia kwako wewe utuuzima mmoja (kati yao) au wote wawili basi usiwaambie (hata) Aah! na wala usiwakaripie na useme nao kwa kauli nzuri. Na shusha kwao wao mbawa za unyenyekevu kwa huruma, na sema Mola wangu wahurumie kama walivyonilea mimi nikiwa mdogo" Zuia kwao ulimi wa uovu, na uwaepushie aina mbalimbali za maudhi. Na lainisha kwao kauli zako; na shusha kwaajili yao mbawa zako; na uidhalilishe kwaajili ya kuwatii nafsi yako, na uulowanishe ulimi wako kwa dua kwao toka moyoni mwako, na kwakukiri nafsini mwako, na sema: (Mola wangu wahurumie kama walivyonilea nikiwa mdogo), na wala usisahau ziada ya kipaumbele kwa mama, kwa kuifanyia kazi ishara iliyoonyeshwa katika wahyi; na kwa kuendana na kile kilichotamkwa katika hadithi.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- hadithi Marfu'u: "Atakayetoa jinsia (aina) mbili katika njia ya Mwenyezi Mungu huitwa katika milango ya pepo, ewe mja wa Mwenyezi Mungu hii ni kheri, hivyo atakayekuwa miongoni mwa watu wa swala ataitwa katika mlango wa swala, atakayekuwa katika watu wa jihadi ataitwa katika mlango wa jihadi, atakayekuwa miongoni mwa watu wa swaumu ataitwa katika mlango wa Rayyan, atakayekuwa miongoni mwa watu wa sadaka ataitwa katika mlango wa sadaka" Akasema Abuubakari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Namuweka fidia baba yangu na mama yangu kwaajili yako, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! je kama kuna mtu ataitwa katika milango hiyo akawa na dharura, je anaweza kuitwa mtu katika milango hiyo yote? basi akasema: "Ndiyo, na ninataraji wewe utakuwa miongoni mwao".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAtakayetoa sadaka kwa vitu viwili katika vitu vyovyote, mfano kama vyakula au mavazi au kipando au pesa, kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu humuita Malaika katika milango ya pepo wakimkaribisha kuelekea katika milango hiyo, nao wakisema: Hakika umetanguliza kheri nyingi unalipwa kwazo leo malipo makubwa. Wale wenye kukithirisha swala wataitwa katika mlango wa swala, na wataingia hapo, na wenye kukithirisha sadaka wataitwa katika mlango wa sadaka, na wataingia hapo, na wenye kukithirisha kufunga Malaika watawapokea katika mlango wa Rayyan wakiwaita kuingia hapo, na maana ya Rayyan: ni mtu anayekata kiu; kwasababu wafungaji hujizuia na kunywa maji wakapatwa na kiu na hasa hasa katika siku za kiangazi kirefu na chenye joto, hivyo watalipwa kwa kiu yao kwa kukatwa kiu milele katika pepo ambayo wataingia kupitia mlango huo. Aliposikia Abuubakari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe kwake- mazungumzo haya, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, "fidia yako namtoa baba yangu na mama yangu" atakayeingia katika milango hii hatokuwa na mapungufu wala hasara, kisha akasema: "Je inawezekana mtu akaitwa katika milango hiyo yote?" Akasema -Rehema na Amani ziwe juu yake- Ndiyo, na ninataraji wewe kuwa miongoni mwao".
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayeniona mimi ndotoni basi ataniona akiwa macho -au ni kana kwamba kaniona akiwa macho- hajifananishi shetani na mimi".
Imepokelewa na Imamu Muslim - Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimWametofautiana wanachuoni katika kubainisha maana ya hadithi hii, katika mitazamo mingi: Wa kwanza: Nikuwa makusudio yake: ni wale watu wa zama zake, na maana yake nikuwa atakayemuona usingizini na akawa hakuhama, hajawezeshwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhama na kumuona yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiwa macho wazi. Na ya pili: Nikuwa anayeonekana kwake usingizini ndiye Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- halisi, yaani katika ulimwengu wa roho, na kuwa kumuona kwake ni kweli, lakini sharti iwe kwa sifa yake inayojulikana-. Ya tatu: Nikuwa yeye ataona uhakika wa hiyo ndoto akiwa macho akhera; ni kumuona maalumu kwasababu ya kuwa karibu naye na kupata utetezi wake na mfano wa hayo. Kauli yake: "Au ni kana kwamba kaniona akiwa macho" Hii ni riwaya ya Imamu Muslim kaipokea ikiwa na shaka katika mapokezi yake: Je alisema -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Ataniona akiwa macho?" au alisema: "Ni kana kwamba kaniona akiwa macho". Na maana yake: nikuwa atakayemuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika ndoto kwa sifa zake ambazo yeye yuko nazo basi ni kana kwamba kamuona akiwa macho, hii ni kama kauli yake -Rehema na Amani ziwe juu yake-, kama ilivyokuja katika sahihi mbili (yaani kitabu cha sahihi Bukhariy na sahihi Muslim): "Atakayeniona ndotoni, basi atakuwa kaniona" na katika riwaya nyingine ndani ya sahihi mbili pia: "Atakayeniona ndotoni, basi atakuwa kaniona mimi kweli". kauli yake: "Hajifananishi shetani na mimi", na katika tamko jingine: "Atakayeniota mimi usingizini atakuwa kaniona mimi, kwani hakika haimpasi shetani kujifananisha kwa sura yangu". Na maana yake: nikuwa shetani haiwezekani kwake kujifananisha na Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika umbile lake halisia, na vinginevyo anaweza kuja shetani na akasema kuwa yeye ndiye Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na anakuwa katika umbile ambalo si umbile lake -Rehema na Amani ziwe juu yake-, huyu si Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- mtu atakapomuota mtu ndotoni na ikaingia hisia nafsini mwake kuwa huyu ndiye Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake-, basi hebu atafute sifa za huyu aliyemuona, je zinaendana na sifa za Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake au la? Ikiwa zitaendana: Basi atakuwa kamuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Na zisipoendana basi huyo si Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- bali hizi ni dhana toka kwa shetani kaziingiza katika nafsi ya huyu aliyelala kwamba ndiye Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na wala si yeye Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, Na amepokea Imamu Ahmadi na Tirmidhiy katika shamaail: kutoka kwa Yazidi Al faarisiy amesema: Nilimuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ndotoni, nikasema kumwambia bin Abbas: Hakika mimi nimemuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ndotoni, akasema bin Abbasi: hakika Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa akisema: "Hakika shetani hawezi kujifananisha na mimi, basi atakayeniona mimi usingizini hakika atakuwa kaniona mimi", Je unaweza kueleza sifa za huyo bwana uliyemuota? Nikasema: Ndiyo: alipoeleza sifa zake, akasema bin Abbas: lau kama ungemuona ukiwa macho usingeweza kumsifia juu ya hapo" Na maana yake: nikuwa lau kama ungemuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ukiwa macho isingewezekana kumsifia zaidi ya hayo uliyomsifia, na hii maana yake nikuwa yeye alimuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake kweli.
kutoka kwa Nu'man bin Bashiri -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika mtu mwenye adhabu nafuu katika watu wa motoni ni yule atakayekuwa na viatu viwili na soli mbili vitokanavyo na moto, utakuwa ukitokota kwa hivyo ubongo wake kama kinavyotokota chungu, hatoona kuwa kuna yeyote mwenye adhabu kali kuliko yeye, kumbe yeye ndiye ana adhabu nafuu kuliko wote"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu mwenye adhabu nafuu katika watu wa motoni siku ya Kiyama ni yule atayekuwa na viatu viwili na soli mbili, utakuwa ukichemka ubongo wake kutokana na kuchemka kwake, kama linavyochemka sufuria la shaba, na wala hatoona kuwa kuna yeyote mwenye adhabu kali zaidi yake, kumbe yeye ndiye mwenye adhabu nafuu zaidi kuliko wote, na hii ni kwa sababu zitakusanyika kwake adhabu zote mbili, adhabu ya mwili na adhabu ya nafsi.
Kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Yanamfuata maiti mambo matatu: familia yake na mali yake na matendo yake, vinarudi vitu viwili na kinabakia kimoja: wanarudi familia yake na mali yake, na yanabakia matendo yake"
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimMaana ya hadithi: anapokufa mwanadamu wanamfuata wenye kumsindikiza, wanamfuata watu wake wanamsindikiza mpaka kaburini kwake, na zinamfuata mali zake: yaani watumwa wake na wafanyakazi wake na mamluki (anao wamiliki) wake, na yanamfuata pamoja naye matendo yake, vinarudi viwili, na yanabakia matendo yake, ikiwa kama ni ya kheri basi itakuwa kheri na ikiwa ni ya shari pia itakuwa shari.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Amsalimie aliyepanda anayetembea, na anayetembea aliyekaa, na wachache kwa wengi" Na kwa Bukhari: "Mdogo amsalimie mkubwa, na anayepita amsalimie aliyekaa, na wachache kwa wengi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika adabu za kutoleana salamu kati ya waislamu "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh". Mdogo amsalimie mkubwa, na aliyepanda amsalimie anayetembea kwa miguu, na anayetembea kwa mguu amsalimie aliyekaa, na idadi ndogo wawasalimie idadi kubwa.