





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Hussein bin Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakuniswalia"
Imepokelewa na Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na AhmadAmetahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha kumtakia rehema wakati wa kusikia jina lake au wasifu wake, na akasema: Bahili kamili ni yule nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema; na hili ni kwa sababu ya mambo yafuatayo: La kwanza: Nikuwa ni ubahili kwa kitu ambacho mtu hapati hasara sawa iwe ndogo au kubwa, wala hatoi mali, na wala hatumii nguvu wala juhudi. La pili: Ni kuifanyia ubahili nafsi yake kwa sababu anainyima malipo ya kumtakia rehema Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake: kwa sababu anapojizuia kumtakia rehema atakuwa kafanya ubahili na kakataa kutimiza haki ya wajibu kwake kuitekeleza, kwa kutekeleza amri na akapata malipo. La tatu: Kumtakia rehema ndani yake kuna kutimiza haki za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, yeye ndiye aliyetufundisha, na yeye ndiye aliyetuelekeza, na yeye ndiye aliyetuita kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akaja na wahyi huu, na sheria hii, yeye ndiye sababu ya kuongoka kwetu baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, atakayeacha kumtakia rehema basi atakuwa kamfanyia ubahili Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake kwa kutompa haki ndogo kabisa miongoni mwa haki zake
Kutoka kwa Sahal bin Muadhi bin Anas kutoka kwa baba yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayekula chakula, akasema: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki, na akaniruzuku, si kwa ujanja wangu wala kwa nguvu zangu, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadAnamhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kula chakula amshukuru Mwenyezi Mungu, kuwa mimi sina uwezo wa kuleta chakula wala kukila isipokuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na msaada wake, Kisha akatoa habari njema rehema na amani ziwe juu yake kwa yeyote atakayesema hivyo kuwa anastahili msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa dhambi zake ndogo ndogo zilizopita.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala".
Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na NasaaiAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake fadhila za dua baina ya adhana na ikama, nakuwa dua hiyo hairejeshwi na inanafasi kubwa ya kujibiwa, basi muombeni Mwenyezi Mungu ndani ya wakati huu.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu, na unitengenezee dunia yangu ambayo kunapatikana maisha yangu, na unitengenezee Akhera yangu ambako kunapatikana kuishi kwangu milele, na unijalie ziada ya uhai kwenye kila lenye heri, na ujalie kifo ni kitulizo changu kutokana na kila shari"
Imepokelewa Imamu MuslimAliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa dua iliyokusanya ndani yake misingi ya tabia njema alizotumwa kuzitimiliza; nazo ni kutengenezewa dini, na dunia, na Akhera, akachota kutoka katika matamshi haya mafupi kutengemaa kwa mambo makubwa matatu, na akaanza na kutengemaa kwa dini, ambayo ndiyo sababu ya kutengemaa hali ya Dunia na Akhera, akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu" Kwa kuniafikisha kusimamia adabu zake kwa namna iliyokamilika na kutimia zaidi. "Ambayo ndiyo ngome ya jambo langu" Na iwe hifadhi kwa mambo yangu yote, ikiwa dini yangu itaharibika basi yataharibika mambo yangu, na nitapata hasara na kutoka patupu, na kwakuwa hakuwezi kutimia kutengemaa kwa dini inayotakiwa isipokuwa kwa kutengemaa dunia, akasema: "Na unitengenezee dunia yangu" Kwa kunipa afya ya mwili na amani, na riziki, na mke mwema, na kizazi kizuri na yale ninayoyahitaji, na yawe ya halali, na yanisaidie katika kukutii, kisha akataja udhuru katika kuomba kwake kutengemaa kwake; kwa kusema: "Ambayo kuna maisha yangu" Na mahala pa kuishi kwangu na muda wa uhai wangu. "Na unitengenezee Akhera yangu ambayo ndiyo marejeo yangu" Na kurejea kwangu ili kukutana na wewe, na hii ni kwa kutengemaa kwa matendo, na Mwenyezi Mungu kumuwezesha mja katika ibada na ikhlasi, na kuupata mwisho mwema. Na akapangilia rehema na amani ziwe juu yake Akhera baada ya dunia; kwa sababu ya kwanza ndio sababu ya kutengemaa ya pili, atakayekuwa na msimamo katika dini yake kwa namna atakavyo Mwenyezi Mungu, basi Akhera yake itanyooka na atapata furaha ndani yake. "Na uufanye uhai" Yaani: Na kurefushwa kwa umri "Kuwa ni ziada kwangu katika kila kheri" Ili nizidishe amali njema, "Na uyafanye mauti" na kuharakishwa kwake "Raha kwangu kutokana na kila shari" Na fitina na mitihani na majaribu kwa maasi na kughafilika, na ili iwe ni sababu ya kuepukana na matatizo ya Dunia na shida zake, na kupatikana kwa raha.
Kutoka kwa Abuu Mussa radhi za Allah ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba yeye alikuwa akiomba kwa dua hii: "Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu, na yale ya makusudi na ujinga wangu na mzaha wangu, na hayo yote yaliyo kwangu, ewe Mola wangu nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza, wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji, na wewe juu ya kila kitu ni muweza".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeIlikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake zilizokusanya mambo mengi ni kauli yake: "Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe makosa yangu" "na dhambi zangu", na yale yaliyotokea kwangu pasina kujua. "Na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote" na uzembe wangu na kuvuka kwangu mipaka. "Na yale uyajuayo kutoka kwangu" Uliyoyajua ewe Mwenyezi Mungu lakini mimi nimeyasahau. "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe makosa yangu na makusudi yangu" Na yale yaliyotokea kwa makusudi na kwa kujua kwangu kuwa ni dhambi. "Na niliyodhamiria na yale ya mzaha" Na yale yaliyotekea kwa mzaha, na yale yaliyotokea katika hali zote mbili. "Na hayo yote toka kwangu" Kiasi kwamba yote yaliyotajwa yamekusanya madhambi na aibu zote. "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe niliyoyatanguliza" Katika yale yaliyopita, "Na yale niliyoyachelewesha" Katika yale yatakayokuja. "Na yale niliyoyafanya kwa siri" niliyoyaficha "Na niliyoyatangaza" Na kuyaonyesha wazi. "Wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji" Unamtanguliza umtakaye katika viumbe wako katika rehema zako kwa kumpa taufiki katika yale unayoyaridhia, na wewe ndiye unayemchelewesha umtakaye katika hilo, kwa kumnyima uwezo, hakuna wa kuyapeleka mbele uliyoyachelewesha, na wala hakuna kuyachelewesha mambo uliyoyawahisha. "Na wewe juu ya kila kitu ni muweza" Yaani: Unauwezo uliokamilika na maamuzi timamu, mfanyaji pasina kizuizi cha yote uyatakayo.
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha dua hizi, kila anaposhinda jioni na kila anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha na afya katika dini yangu na dunia yangu na familia yangu na mali yangu, ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu -Au aibu zangu- na utie amani yote ninayoyahofia, ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi toka mbele yangu, na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu, na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa tokea chini yangu".
Imepokelewa na Abu Daud, Nasai, Ibn Majah na AhmadHakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha maombi haya pindi anaposhinda jioni na pindi anapoamka. "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba afya" na kusalimika na magonjwa na mabalaa na shida za dunia, na matamanio na fitina za kidunia "Katika dunia na Akhera" kwa au kwa baadae "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha" na kusalimika na aibu, "Katika dini yangu" kutokana na ushirikina na uzushi na maasi, "na dunia yangu" katika majanga na kero na shari, "na familia yangu" mke wangu na wanangu na ndugu zangu, "na mali yangu" na mali zangu na matendo yangu. "Ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu" Yaani: Na yale yaliyokwangu katika aibu na dosari na mapungufu na ufute dhambi zangu, "na utie amani hofu yangu" Mfadhaiko wangu na hofu yangu. "Ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi" Na uzuie kwangu balaa miongoni mwa yale yenye kuudhi na mabalaa, "mbele yangu na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu" Kiasi kwamba aliomuomba Mwenyezi Mungu amuhifadhi kutoka pande zote; kwa sababu mabalaa na maafa humfika mtu na kumuelekea kutoka moja kati ya pande hizi. "Na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa" na nisichukuliwe hatua toka chini yangu ghafla, nikaangamia ghafla "kutoka chini yangu" nikaangamia kwa kudidimizwa.
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimfundisha dua hii: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka na za kuchelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua, na ninajikinga kwako kutokana na shari zote zinazokuja haraka na zinazochelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) miongoni mwa heri alizo kuomba mja wako na nabii wako, na ninajikinga kwako (uniepushe) na shari alizo jikinga kwako mja wako na nabii wako. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba pepo, na yaliyo karibu yake miongoni mwa kauli au matendo, na ninajikinga kwako kutokana na moto na yaliyo karibu na moto miongoni mwa kauli au matendo, na ninakuomba ujaalie kila hukumu utakayo hukumu kwangu iwe ni heri"
Imepokelewa na Ibn Majah na AhmadMtume rehema na amani ziwe juu yake alimfundisha Aisha radhi za Allah ziwe juu yake dua inayokusanya mambo mengi nayo ni maombi manne: La kwanza: Dua inayokusanya kila aina ya kheri: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe kutoka katika kheri zote" kwa ujumla wake, "Za haraka" zilizo karibu kwa wakati wake, na "za baadaye" za mbali, "Nilizozijua" katika zile ulizonifundisha, "na zile nisizozijua" katika zile zinazokuwa katika elimu yako ewe Mtukufu, Na hapa kuna kuyakabidhi mambo yote kwa Mwenyezi Mungu Mjuzi Mwenye habari na Mpole; basi Mwenyezi Mungu humchagulia muislamu kilicho bora kati ya hayo na kizuri, "Na ninajilinda" ninashikamana na ninaomba ulinzi "kwako wewe dhidi ya shari zote, zinazokuja haraka na zinazochelewa, ninazozijua na nisizozijua". Dua ya pili: Nayo ni kinga kwa muislamu ili asichupe mipaka katika dua "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba" na ninakutaka unipe "Katika kheri alizokuomba mja wako na Nabii wako" rehema na amani ziwe juu yake, "na ninajilinda kwako" na ninajiegemeza na kushikamana "kwako kutokana na shari alizojikinga nazo mja wako na Nabii wako" rehema na amani ziwe juu yake, na hii ni dua na ni ombi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ampe muombaji yale aliyomuomba na akayataka Nabii Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili ya nafsi yake, pasina kusema aina ya yale aliyoyaomba rehema na amani ziwe juu yake. Dua ya tatu: Kuomba kuingia peponi na kujiweka mbali na moto, nalo ni ombi la kila muislamu na ndio lengo kuu la matendo yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba pepo" na kufauli kuipata "Na yale yanayotuweka karibu nayo miongoni mwa kauli na matendo" mema yenye kukuridhisha, "na ninajilinda kwako kutokana na moto" kiasi kwamba hakuna kukingwa na matendo machafu ila kwa upole wako, "na yale yenye kutuweka karibu nao miongoni mwa kauli na matendo" katika maasi yanayokukasirisha. Dua ya nne: Kuomba kuridhika na kadari za Mwenyezi Mungu "na ninakuomba uyafanya maamuzi yako uliyoyapitisha yawe ni kheri" na kila jambo alilolihukumu Mwenyezi Mungu kwangu alifanye kuwa ni kheri kwangu, na ni katika dua za kuomba kuridhia hukumu ya Mwenyezi Mungu.
kutoka kwa Abdullahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Ilikuwa miongoni mwa dua za Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako"
Imepokelewa Imamu MuslimMtume rehema na amani ziwe juu yake aliomba kinga ya mambo manne: La kwanza: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na kuondokewa na neema zako" za dini na dunia, na nibakie madhubuti ndani ya Uislamu, na najiweka mbali kutoangukia katika maasi yanayoondosha neema. La pili: "Na kubadilika ghafla neema zako" Kubadilika kwake na kuwa balaa; ninakuomba afya isiyo na kikomo, na kusalimika dhidi ya mabalaa na magonjwa. La tatu: "Na kufikwa ghafla na adhabu zako" kama vile balaa au maasi, gharika na adhabu vinapokuja ghafla, huwa hakuna muda wa kutubia na kurekebisha mabaya, na hapa hufikwa na adhabu kali na kubwa mno. La nne: "na hasira zako zote" na sababu zenye kupelekea kupata hasira zako; kwani yeyote utakayemchukia basi atakuwa kapata hasara. Na alileta Mtume rehema na amani ziwe juu yake tamko la wingi; ili likusanye mpaka sababu za hasira zake Aliyetakasika na kutukuka miongoni mwa kauli na matendo na itikadi.
Kutoka kwa Abdillah bin Amry bin Aaswi radhi za Allah ziwe juu yao wote wawili yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiomba kwa maneno haya: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui"
Imepokelewa na Nasai na AhmadAlijikinga Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na mambo haya: La kwanza: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda" na ninajikabidhi na kujiweka "kwako" si kwa mwingine, "kutokana na kuelemewa na deni" na kunitenza nguvu na misukosuko yake, na ninakuomba msaada wa kulilipa na kulitimiza. La pili: "Na kuzidiwa na adui" na kunitenza nguvu na kunitawala kimabavu, na ninakuomba uzuie adha zake, na unipe ushindi juu yake. La tatu: "Na kutukanwa na maadui" na kufurahi kwao kwa yale yanayowafika waislamu miongoni mwa mabalaa na misiba.