





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alikuwa akisema anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka, na kwako tunashinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutakufa, na kwako tutafufuliwa" Na anaposhinda jioni anasema: "Kwako tumeshinda, na kwako tumeamka, na kwako tunakuwa hai, na kwako tunakufa, na kwako tutafufuliwa" Akasema: Na mara nyingine: "Na kwako ndio marejeo".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn MajahAlikuwa rehema na amani ziwe juu yake anapofikiwa na asubuhi nayo ni mwanzo wa mchana pamoja na kuchomoza Alfajiri anasema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka" tukiwa tumegubikwa na hifadhi yako na kufunikwa na neema zako, tukishughulika na kukutaja, tukitaka msaada kwa jina lako, tukienewa na taufiki yako, tukifanya harakati zenu kwa ujanja wako na nguvu zako, "na kwako tumeshinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tunakufa" yaani; hii ni kama lafudhi iliyotangulia isipokuwa hii imefanywa ya jioni, atasema: Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeshinda, na kwa jina lako Muhuishaji tunakuwa hai, na kwa jina lako Mfishaji tutakufa, "na kwako tutafufuliwa" na kufufuliwa baada ya kifo, na kusambaa baada ya kukusanywa, itaendelea hali yetu namna hii katika nyakati zote, na hali zingine zilizobakia, na wala sitoachana nayo wala sitoihama. Na ikimfikia jioni baada ya Lasiri atasema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeshinda, na kwako tumeamka, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutafuka, na marejeo ni kwako" na marejeo katika dunia, na mafikio katika mwisho, wewe ndiye unayenihuisha na wewe ndiye unayenifisha.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adhabu ya moto".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikithirisha dua kwa dua fupi zenye kukusanya mambo mengi, na miongoni mwake: "Ewe Mwenyezi Mungu! Tupe hapa katika Dunia (mambo) mazuri, na Akhera utupe mazuri na utukinge na adhabu ya moto", Dua hii inakusanya mazuri yote ya Dunia; ikiwemo riziki ya raha na pana na ya halali, na mke mwema, na mtoto kitulizo cha jicho, na starehe, na elimu yenye manufaa, na mfano wa hayo miongoni mwa maombi yanayopendeka na ya halali, na mazuri ya Akhera ni kusalimika na adhabu za kaburi, na kisimamo cha Kiyama na moto, na kupata radhi za Mwenyezi Mungu, na kufaulu kwa kupata neema za kudumu, na kuwekwa karibu na Mola Mlezi Mwingi wa huruma.
Kutoka kwa Shadaad Bin Ausi Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha) Ni kusema: Allaahumma anta Rabbi Laa ilaaha illaa anta, khalaqtani wa anaa abduka wa ana a'laa a'hdika, wawa'dika mastatwa'tu, auudhubika min Sharri maa swana'tu, abuu ulaka bini'matika alaiyya, wa abuu ulaka bidhambi faghfirlii, fa innahuu laa yaghfirudh-dhunuuba illaa anta" Akasema: "Na atakayeisema dua hii mchana akiwa na yakini nayo, akafa katika mchana wake huo kabla hajafika jioni, basi atakuwa miongoni mwa watu wa peponi, na atakayeisema wakati wa usiku akiwa na yakini nayo, akafariki kabla hajafika asubuhi, basi huyo atakuwa miongoni mwa watu peponi".
Imepokelewa na Al-BukhaariyMtume rehema na amani ziwe juu yake anaeleza kuwa Istighfari (Kuomba msamaha) kuna matamshi mengi, nakuwa matamshi bora na makubwa zaidi ni mja kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu wewe ndiye Mola Mlezi hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe, umeniumba na mimi ni mja wako na mimi nipo juu ya ahadi yako na maonyo yako kwa kiasi niwezavyo, ninataka hifadhi kwako kutokana na shari niliyo ifanya, ninakiri kwa neema zako zilizo juu yangu, na ninakiri kwa madhambi yangu, basi nisamehe mimi, kwani hakuna afutae madhambi isipokuwa wewe. Hivyo basi mja anaanza kukiri upweke wa Mwenyezi Mungu, nakuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumba wake na muabudiwa wake hana mshirika wake, na kuwa yeye yuko katika ahadi aliyomuahidi Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, miongoni mwa imani na utiifu kwake, kwa kadiri ya uwezo wake; kwa sababu mja kwa namna yoyote atakavyotekeleza ibada hawezi kutekeleza yote aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu, na wala hawezi kutimiza haki stahiki katika kushukuru neema, nakuwa yeye anajilinda kwa Mwenyezi Mungu, na anajikinga kwake, kwani yeye ndiye mwenye kutakwa ulinzi kutokana na shari zote alizozitengeneza mja, Nakuwa yeye anakiri na kukubali kwa hiari yake neema zake juu yake, na anairudia nafsi yake kwa kukiri na kukubali madhambi yake na maasi yake, Na baada ya kupitia kwa Mwenyezi Mungu, atamuomba Mola wake asitiri makosa yake na amkinge na dhambi zake kwa msamaha wake na fadhila zake na rehema zake, kwani hakuna awezaye kusamehe madhambi ila yeye Mtukufu. Kisha akaeleza rehema na amani ziwe juu yake kuwa dua hii ni katika dhikiri na dua za asubuhi na jioni, nakuwa atakayeisema kwa yakini na kwa kuhudhurisha moyo wake na kwa kuiamini, mwanzo wa siku yake, kwanzia kuchomoza kwa Jua mpaka kupinduka kwake, nao ni wakati wa mchana, akafa, ataingia peponi, Na atakayeisema usiku, nao ni kuanzia kuzama kwa jua mpaka kuchomoza kwa Alfajiri, akafariki kabla hajafika asubuhi, ataingia peponi.
Na kutoka kwa Jaabir Bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Ogopeni dhulma, kwa hakika dhulma ni giza siku ya kiyama. Na ogopeni tamaa, kwa hakika tamaa iliwaangamiza walio kuwepo kabla yenu. Iliwapelekea kumwaga damu zao, na kuhalalisha yaliyo haramu kwao".
Imepokelewa Imamu MuslimAlitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu dhulma, ikiwemo: Kuwadhulumu watu na kujidhulumu mwenyewe na kufanya dhulma katika haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, nayo kuacha kumpa kila mwenye haki haki yake, nakuwa dhulma ni giza kwa wafanyaji dhulma siku ya Kiyama ikiwemo kupata matatizo na misukosuko, Na akakataza tamaa ambayo ni ubahili uliopitiliza pamoja na pupa, na ikiwemo kufanya uzembe katika kutekeleza haki ya mali na tamaa iliyopitiliza ya kuipupia dunia, Na aina hii ya dhulma iliwaangamiza Umma waliokuwa kabla yetu, kiasi ambacho iliwapelekea kuuana wao kwa wao, na kuyahalalisha yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu katika mambo yaliyoharamishwa.
Kutoka kwa Abdallah Bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: Ya kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani zimfikie: Ni Uislamu upi bora? Akasema: "Ni, ulishe chakula, na utoe salamu kwa unayemjua na usiyemjua".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliulizwa Mtume rehema na amani zimfikie: Ni jambo lipi katika Uislamu ni bora? Akataja mambo mawili: La kwanza: Kukirithirisha kuwalisha masikini, na inaingia hapa sadaka na zawadi na kuwakirimu wageni na walima (harusi), na inatiliwa mkazo fadhila ya kulisha masikini katika nyakati za njaa na wakati wa bidhaa kupanda bei. La pili: Kumpa salamu kila muislamu, unayemjua na usiyemjua.
Kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Sema: Ewe Mwenyezi Mungu niongoze na unisimamie, na kumbuka kwa uongofu ni kuongoka kwako njia, na kusimamiwa ni kusimamiwa kupatia (katika kila jambo lako mithili ya) mshale".
Imepokelewa Imamu MuslimMtume rehema na amani ziwe juu yake alimuamrisha Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake amtake Mwenyezi Mungu na amuombe na aseme: "Ewe Mwenyezi Mungu niongoze" na unielekeze na unijulishe "na unisimamie" na uniafikishe, na unifanye kuwa na msimamo katika mambo yangu yote. Uongofu: Ni kuijua haki kwa ujumla na kwa ufafanuzi, na kuwezeshwa kuifuata kwa wazi na kwa siri. Na kusimamiwa: Ni kuwezeshwa na kuwa na msimamo katika mambo yote katika yale ya kweli juu ya haki, nayo ni njia iliyonyooka katika kauli na vitendo na itikadi. Na hii ni kwa sababu jambo lisiloonekana hueleweka wazi kupitia jambo linaloonekana; Hivyo kumbuka unapokuwa unaomba dua hii kuwa: "Uongofu: Ni kuongozwa njia" Hivyo, hudhurisha moyo wako nawe ukiwa unaomba uongofu mfano wa uongofu wa aliyesafarini, kwani huwa hatoki nje ya njia si kulia wala kushoto; na hii ni ili asalimike na kupotea, na kwa hilo anapata usalama, na atafika haraka katika lengo lake. "Na kuafikishwa nakupatia: Ni kupatia kwa mshale" Wewe chunguza wakati wa kulenga kwako mshale katika uharaka wa kufika kwake na kukipata ulichokusudia kukipiga, mrusha mishale anaporusha katika lengo basi huhakikisha ameulenga vizuri mshale katika kile alichokikusudia, hivyo hivyo na wewe unamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa yote unayoyakusudia basi yawe katika mfano wa mshale; utakuwa katika kuomba kwako umeomba kiwango cha juu zaidi cha uongofu, na mwisho wa kusimamiwa. Vuta picha ya maana hii kwa moyo wako ili umuombe usimamizi Mwenyezi Mungu na kupatia katika mambo yako, ili yale unayoyanuia katika hilo yawe katika mfano wa namna unavyofanya mshale.
Imepokelewa kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake-: ِAlikuja Fatma radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akimlalamikia juu ya jiwe la kusagia lililokuwa likichubua mikono yake, na zilimfikia taarifa kuwa Mtume amejiwa na mjakazi, lakini alikuwa hajakutana naye, akalieleza hilo kwa Aisha, alipokuja Aisha akamwambia, anasema Fatma: Akaja kwetu hali yakuwa tumekwisha panda kitandani, basi tukaamka tukasimama, akasema: "Haina haja ya kusimama kaeni tu mahala penu" Akaja akakaa kati yangu na Fatma, mpaka nikahisi ubaridi wa miguu yake tumboni kwangu, Mtume akasema: «Je, nisikujulisheni kitu bora zaidi kuliko hicho mlichoomba? Mtakapokwenda kulala basi msabihini Mwenyezi Mungu; yaani (Sub-haanallaah) mara thelathini na tatu, na mhimidini (Al-hamdulillaah) mara thelathini na tatu, na mtukuzeni (Allahu Akbar) mara thelathini na nne, kufanya hivyo ni bora zaidi kwenu kuliko mfanyakazi.”
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeFatima Mwenyezi Mungu amuwie radhi binti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilalamikia athari za mashine ya kusagia (Jiwe) aliyoipata mkononi mwake, hivyo alipokuja mtumwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuendea na kumuomba ampe mmoja kati ya watumwa hao, ili amsaidia kwa kazi za nyumbani, lakini hakumkuta Mtume nyumbani kwake, ila alimkuta Aisha Mwenyezi Mungu amuwie radhi, hivyo akamwambia kuhusu hilo, Alipofika rehema na amani ziwe juu yake Aisha akamueleza kuwa Fatma alikuja kwake kumuomba mfanyakazi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaja kwa Fatma na Ally Mwenyezi Mungu awawie radhi, ndani ya nyumba yao wakiwa wamelala kitandani wakijiandaa kwa usingizi, akakaa katikati yao mpaka Ally radhi za Allah ziwe juu yake akahisi ubaridi wa miguu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, juu ya tumbo lake, akasema: Hivi nisikufundisheni kilicho bora zaidi kuliko mlichoniomba, kuliko kukupeni mtumishi? Wakasema: Ndio, tufundishe, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Mtakapochukua nafasi zenu za kulala usiku, basi toeni takbira mara thelathini na nne, kwa kusema: Allahu Akbaru, Na toeni tasbihi mara thelathini na tatu, kwa kusema: Sub-haanallaah, Na himidini mara thelathini na tatu, kwa kusema: Al-hamdulillah; Dhikiri hii ni bora sana kwenu nyinyi kuliko kuwa na mtumishi.
Kutoka kwa Abdillah Bin Khubaibi Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye amesema: Tulitoka katika usiku wa mvua kubwa na giza nene, tukimtafuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake; ili atusalishe, anasema: Nikampata, akasema: "Sema" Nikawa sikusema kitu, kisha akasema: "Sema", Nikawa sikusema kitu, akasema: "Sema" Nikasema: Niseme nini? Akasema: "Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu".
Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na NasaaiAnaeleza swahaba mtukufu Abdullah Bin Khubaib radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa wao walitoka katika usiku wenye mvua kubwa, na giza lilikuwa nene, kwa ajili ya kumtafuta Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake; ili awasalishe, wakamkuta, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: "Sema" Yaani: Soma, akawa hakusoma kitu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akarejea kauli yake kwake, Abdullah akasema: Nisome nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Soma suratul Ikhlaswi (Qul-huwallaahu ahadi), na sura mbili za kinga (Qul-Audhubirabbil-falaq), na (Qul-Audhubirabbin-naas), wakati wa jioni, na wakati wa asubuhi, mara tatu tatu, zitakuhifadhi na kila shari, na zitakukinga na kila baya.
Kutoka kwa Abana bin Othman amesema: Nilimsikia Othman bin Affan radhi za Allah ziwe juu yake akisema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Yeyote atakayesema: Bismillaahi lladhi laa yadhurru ma'asmihi shai un fil Ardhwi walaa fis samaai, wahuwas samiiu'l 'aliim, (Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hakuna kinachoweza kudhuru pamoja na jina lake kitu chochote ardhini wala mbinguni, naye ni msikivu na mjuzi) mara tatu, basi halitomfika balaa la ghafla, mpaka atakapoamka, na atakayesema wakati wa asubuhi mara tatu, halitomfika balaa la ghafla mpaka atakapofika jioni" Akasema: Akapatwa na mtihani Abana bin Othman Al-Faaliji, basi yule bwana aliyesikia hadithi akawa anamtazama, akasema kumwambia: Vipi mbona unanitazama? Wallahi sijamsemea uongo Othman, wala Othman hajamsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lakini siku niliyofikwa na balaa, nilichukizwa na jambo fulani nikasahau kuisoma.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na AhmadAmeainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema asubuhi ya kila siku baada ya kuchomoza Alfajiri, na jioni ya kila usiku kabla ya kuzama jua mara tatu: "Bismillaah" Ninataka msaada na ninajilinda dhidi ya kila chenye kuudhi "ambaye hakidhuru" kwa kulitaja "pamoja na jina lake" yaani "chochote" vyovyote vile kitakavyokuwa kikubwa "katika ardhi" na vinavyotoka ndani yake miongoni mwa mabalaa "wala mbinguni" na kinachoshuka kutoka humo miongoni mwa mabalaa "naye ni msikivu" wa kauli zetu "mjuzi" wa hali zetu. Atakayesema wakati wa jioni halitomfika balaa la ghafla mpaka afike asubuhi, na atakayesema wakati wa asubuhi balaa halitomfika la ghafla mpaka afike jioni. Akaipatia riwaya ya hadithi ya Abana bin Othman Al-Falij; Nayo ni kudhoofika kwa baadhi ya upande wa mwili, yule bwana aliyesikia kwake hadithi akamtazama Abana kwa kustaajabu?! Abana akasema kumwambia yule bwana: Mbona wanitazama?! Wallah sijamzulia uongo Othman, wala Othman hajamzulia uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lakini leo yamenifika yale aliyoyakadiria Mwenyezi Mungu kwangu kuyasema, nimepatwa na hasira nikasahau kusema maneno haya yaliyotajwa.