





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomuendea mgonjwa basi anamuombea dua, anasema "Ondosha tatizo, ewe Mola wa watu, na ponya kwani wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomtembelea mgonjwa anamuombea dua kwa kusema: Ewe Mwenyezi Mungu "Ondoa" ondosha "ugumu" na ukali wa maradhi, "Ewe Mola wa watu" na Muumba wao na Mlezi wao, "na ponya" maradhi haya "wewe" Mtukufu "Ndiye mponyaji" na ninaomba kupitia jina lako Mponyaji, "hakuna ponyo" linaloweza kupatikana kwa mgonjwa "isipokuwa ponyo lako" na afya yako, "ponyo" la moja kwa moja "lisiloacha" na kubakisha na kuacha "ugonjwa" na maradhi mengine.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Dinari moja unayoitoa kwenye njia ya Allah, na dinari moja unayoitoa kwa mtumwa, na dinari moja unayoitoa sadaka kwa masikini, na dinari moja unayoitoa kwa familia yako, yenye malipo makubwa kuliko yote ni ile unayoitoa kwa familia yako".
Imepokelewa Imamu MuslimAmetaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya aina za utoaji, akasema: Dinari uliyoitoa katika Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari uliyoitoa katika shingo ya mtumwa, na dinari uliyoitoa sadaka kwa masikini mwenye uhitaji, na dinari uliyoitoa kwa watu wako na familia yako, kisha akaeleza kuwa yenye malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu ni ile uliyoitoa kwa watu wako na familia na wale wanaokulazimu kuwahudumia.
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Amru -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika wewe unafunga milele, na unasimama usiku?", Nikasema: Ndiyo, akasema: "Hakika wewe ukifanya hivyo macho yatadhoofu, na nafsi itanyongeka, Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu ni sawa na kufunga mwaka mzima", Nikasema: Hakika mimi ninaweza zaidi ya hapo, akasema: "Basi funga swaumu Daudi amani iwe juu yake, alikuwa akifunga siku moja na anafungua siku moja, na wala hakimbii anapokutana (na adui)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeIlimfikia habari Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Abdallah bin Amri radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa akiunganisha swaumu na wala hafungui mwaka mzima, na anaswali usiku mzima wala halali, akamkataza hilo na akamwambia: Funga na ufungue, na simama na ulale. Na akamkataza kuunganisha swaumu na kusimama usiku mzima, na akamwambia: Hakika wewe ukifanya hivyo macho yako yatadhoofika na yatabonyea, na itanyong'onyea kwa hilo nafsi yako na itachoka nakuwa na unyonge; hana swaumu atakayefunga mwaka mzima; kiasi ambacho hakupata malipo ya swaumu kwa kwenda kinyume na katazo, na hakufungua kwa sababu aliendelea. Kisha akamuelekeza kufunga siku tatu katika kila mwezi, hizo ni sawa na swaumu ya mwaka mzima; kwa sababu kila siku moja ni sawa na siku kumi, ambayo ndiyo ziada ndogo zaidi ya mema. Akasema Abdullah: Hakika mimi ninaweza zaidi ya hizo. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Basi funga swaumu ya Daudi amani iwe juu yake na ndiyo swaumu bora, alikuwa akifunga siku moja na anafungua siku moja, na alikuwa hakimbii anapokutana na adui; kwa sababu namna ya swaumu yake haikudhoofisha mwili wake.
Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri radhi za Allah ziwe kwao yeye na baba yake: Ya kwamba mama yake bint Rawaha alimuuliza baba yake baadhi ya zawadi katika mali yake anazompa mwanaye, akasitisha kutoa kwa mwaka mzima, kisha akaona amjibu, akasema (Mama Nuuman): Siwezi kuridhika mpaka umfanye Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa shahidi kwa hivyo ulivyomzawadia mwanangu, baba yangu akanishika mkono na mimi wakati huo nikiwa kijana mdogo, akamuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama wa mtoto huyu, binti Rawaha kapenda nikufanye wewe kuwa shahidi kwa zawadi nilizomzawadia mwanaye, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Bashiri una mtoto zaidi ya huyu?" Akasema: Ndiyo. Akasema: Je, wanao wote umewazadia kama huyu?" Akasema: Hapana. Akasema: "Basi usinifanye mimi kuwa shahidi, kwani siwezi kushuhudia dhulma", na kwa Imamu Muslim: "Kamtake ashuhudie mtu mwingine asiyekuwa mimi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim, na ina matamshi mengineAmeeleza Nuuma bin Bashiri radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, ya kwamba mama yake Amra binti Rawaha radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza baba yake baadhi ya zawadi katika mali yake kwa mwanaye, akawa mzito, na akachelewa kumjibu kwa muda wa mwaka mzima, kisha akaona amjibu swali lake, akamhofia mwanaye Nuuman, akasema: Siridhii mpaka umfanye kuwa shahidi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kile ulichomzawadia mwanangu, baba yangu akanishika mkono na mimi wakati huo nikiwa kijana mdogo, akumuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama wa kijana huyu, binti Rawaha kapendezwa nikufanye kuwa shahidi kwa kile nilichomzawadia mwanaye, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ewe Bashiri, je, una mtoto mwingine asiyekuwa huyu? Akasema: Ndiyo. Akasema: Je, wote umewazawadia mfano wa huyu. Akasema: Hapana. Akasema: Basi usinifanye mimi kuwa shahidi, kwani mimi sishuhudii upendeleo na dhulma. Na kwa Muslim alisema kwa kumkemea: Lakini mshuhudishe katika dhulma hii mwingine asiyekuwa mimi.
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema: "Atakayemtembelea mgonjwa ambaye hajafikiwa na mauti, akasema akiwa kwake mara saba: Namuomba Allah Mtukufu, Mola wa Arshi Tukufu, akuponye, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamponya kwa maradhi hayo".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa hakuna muislamu atakayemtembelea muislamu katika maradhi yake, ambaye muda wa mauti yake haujafika, kisha aliyekwenda kumtembelea akamuombea mgonjwa kwa kusema: "Namuomba Allah Mtukufu" katika dhati yake na sifa zake na vitendo vyake, "Mola wa Arshi Tukufu akuponye", na akarudia mbele yake mara saba, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamponya kutokana na maradhi hayo.
Kutoka kwa Ummu Salama mama wa waumini mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayeandaa mnyama kwa ajili ya kuchinja, na ukaandama mwandamo wa mwezi Dhul Hija, basi asipunguze chochote katika nywele zake wala kucha zake mpaka atakapochinja mnyama wake wa Udh-hiya"
Imepokelewa Imamu MuslimAmemuamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayetaka kuchinja Udh-hiya asipunguze chochote katika nywele za kichwa chake au kwapa yake au sharubu zake au zinginezo, wala sehemu ya kucha za mikono yake wala miguu yake utakapoonekana mwandamo wa Dhul-Hija mpaka atakapochinja.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Inapokuja Ramadhani hufunguliwa milango ya pepo na hufungwa milango ya moto, na mashetani hufungwa minyororo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa unapoingia mwezi wa Ramadhani hutokea mambo matatu: La kwanza: Hufunguliwa milango ya pepo na haufungwi mlango wowote katika milango hiyo. La pili: Hufungwa milango ya moto na haufunguliwi mlango wowote katika hiyo. La tatu: Hufungwa minyororo mashetani na majini wakaidi, hawaachwi kuendelea na yale waliyokuwa nayo katika miezi mingine isiyokuwa Ramadhani. Na yote hiyo ni kwa kuutukuza mwezi wa Ramadhani, na kumhamasisha mtendaji kukithirisha ibada, kama swala na sadaka, na dhikiri na kusoma Qur'ani na mengineyo; na kujitenga mbali na madhambi na maasi.
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Lau wangejua watu waliyomo katika Adhana na safu ya kwanza, kisha wasipate nafasi ila kwa kupiga kura ili kuyafikia basi wangelipiga kura, na walau wangelijua yaliyomo katika kuwahi basi wangelishindana, na lau wangelijua yaliyomo katika swala ya usiku na swala ya Asubuhi, basi wangeliziendea hata kwa kutambaa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba laiti watu wangelijua yaliyomo katika Adhana na safu ya kwanza miongoni mwa fadhila na kheri na baraka, kisha wakakosa namna ya kutangulizana na nani awe bora kuliko mwingine ila kwa kupiga kura, basi wangelipiga kura, na lau wangelijua yaliyomo katika kuwahi swala mwanzo wa wakati wake basi wangelishindana kuyaendea, na laiti wangelijua kiwango cha thawabu katika kuiendea swala ya Ishaa na swala ya Alfajiri, basi kungekuwa kwepesi kuziendea hata kwa kutambaa kwa magoti kama anavyotembea mtoto mwanzo wa kukua kwake.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayejirusha kutoka juu ya mlima akajiua basi huyo atakuwa motoni akijirusha humo milele na milele, na atakayemeza sumu akajiua basi sumu yake itakuwa mkononi mwake akiimeza ndani ya Moto wa Jahannamu milele na milele humo, na atakayeiua nafsi yake kwa chuma basi chuma chake kitakuwa mkono mwake akilichomo tumbo lake ndani ya Moto Jahannamu milele na milele humo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmetahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa yeyote atakayekusudia kujiua katika dunia, basi ataadhibiwa siku ya Kiyama ndani ya Moto wa Jahannamu kwa njia hiyo hiyo aliyoifanya yeye mwenyewe katika dunia, hayo yakiwa ni malipo kulingana na alichokifanya, atakayejirusha mwenyewe kutoka juu ya mlima akajiua, basi atakuwa ndani ya Moto wa Jahannam akidondoka humo katika milima ya Jahannamu na katika mabonde yake milele na mile humo, na atakayejipiga mwenyewe kwa chuma tumboni mwake akajiua, basi chuma chake kitakuwa mkononi kwake akichoma kwa chuma hicho tumbo lake ndani ya Moto wa Jahannam milele na milele humo.