





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au akanywa, basi atimize swaumu yake, kwani Mwenyezi Mungu kamlisha na kamnywesha".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekula au kunywa kwa kusahau akiwa kafunga swaumu ya faradhi au sunna basi atimize swaumu yake wala asifungue; kwa sababu hakukusudia kufungua, bali hiyo ni riziki Mwenyezi Mungu kamsogezea na akamlisha na kumnywesha.
Kutoka kwa Abuu Ubaidi, mwachwa huru wa bin Azhari, amesema: Nilishuhudia swala ya Idd pamoja na Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Siku mbili hizi alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufunga ndani yake: Siku ya kufungua kwenu kutoka katika swaumu yenu, na siku nyingine ni ile mnayokula katika vichinjwa vyenu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufunga siku ya Iddil-Fitiri na Iddil-Adh-ha; ama Iddil-Fitiri ni siku ya kufungua kutoka katika swaumu ya mwezi wa Ramadhani, na ama Iddil-Adh-ha ni siku ya kula katika vichinjwa.
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: "Nikuwa Talbiya (kuitika) kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kulikuwa ni: Labbaikallaahumma labbaika -Nimekuitikia ewe Mola nimekutikia, Labbaika laa shariika laka labbaika -Nimekuitikia huna mshirika wako nimekuitikia, Hakika sifa njema na neema zote ni zako pamoja na ufalme, wewe pekee usiye na mshirika.". Amesema: Na alikuwa Abdallah bin Omari akizidisha ndani yake: "Labbaika Labbaika wasa'daika, -Nimekuitikia nimekuitikia na utukufu ni wako, wal khairu biyadaika, -Na heri iko mikono mwako, na hamu zote na matendo mwisho ni kwako".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeZilikuwa talbiya (kuitika katika Hija) kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kuingia katika ibada ya Hija au Umra ni kusema: "Nimekuitikia ewe mola nimekuitikia" Kuitika kwa lazima kwako baada kukuitikia katika yale uliyotuita kwayo miongoni mwa ikhlasi na tauhidi na Hija na mengineyo, "Nimekuitikia, huna mshirika wako, nimekuitikia" wewe peke yako ndiye unayestahiki kuabudiwa huna mshirika wako katika uumbaji wako na uungu wako na majina yako na sifa zako, "hakika sifa njema" na shukurani na sifa "na neema" zinatoka kwako, na wewe ndiye mgawaji wake "ni zako" hugawanywa katika kila hali, "na ufalme" vile vile ni wako, "huna mshirika wako" wote ni wako wewe peke yako. Na alikuwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao akizidisha katika hayo. "Labbaika wasa'daika" Nimekuitikia na utukufu ni wako, nifurahishe kwa furaha moja baada ya nyingine, "na heri iko mikononi mwako" yote, na ni kwa fadhila zako, "Nimekuitikia na shauku zote ziko kwako" na matakwa na maombi ninayaelekeza kwa yule ambaye heri iko mkononi mwake, "na matendo" ni kwa ajili yako, kwani wewe ndiye unayestahiki kuabudiwa.
Na imepokelewa kutoka kwa Aisha -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Utafuteni usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) katika witiri za kumi la mwisho katika Ramadhani".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufanya juhudi kuutafuta usiku wenye cheo kwa kuzidisha amali njema, nao hutarajiwa zaidi kupatikana katika siku za witiri za siku kumi za mwisho wa Ramadhani kila mwaka, nazo ni: Ishirini na moja, na ishirini na tatu, na ishirini na tano, na ishirini na saba, na ishirini na tisa.
Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Yakwamba kuna baadhi ya watu katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, walionyeshwa Lailatul qadri ndotoni katika siku saba za mwisho wa Ramadhani. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Naona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwisho, basi atakayetaka kuitafuta basi na aitafute katika siku saba za mwisho".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeWanaume katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake waliona ndotoni kuwa Lailatul Qadri inakuwa katika siku saba za mwisho wa Ramadhani. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ninaona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwisho wa Ramadhani, atakayeitaka, akiwa na pupa ya kuitafuta, basi ajitahidi kuiwinda na kuitafuta kwa kukithirisha matendo mema kwani inatarajiwa zaidi kuwa katika siku saba za mwisho, nazo zinaanza kwanzia usiku wa tarehe ishirini na nne mwezi wa Ramadhani unapokuwa na siku thelathini, na zinaanza usiku wa tarehe thelathini na tatu mwezi unapokuwa wa siku ishirini na tisa.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba watu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake walisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamechukua malipo mengi wenye utajiri: Wanaswali kama tunavyoswali na wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa sadaka katika mali yao ya akiba. Akasema: Hivi kwani hajakuwekeeni Mwenyezi Mungu mambo mnayoweza kutoa sadaka: Hakika katika kila tasbihi (kauli ya sub-haanallaah) ni sadaka, na kila takbira (Allahu Akbaru) ni sadaka, na kila tahmidi (Alhamdulillah) ni sadaka, na kila tahalili (Laa ilaaha illallaahu) ni sadaka, na kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza maovu ni sadaka, na katika kiungo cha siri cha mmoja wenu kuna sadaka" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi yawezekanaje akidhi mmoja wetu matamanio yake kisha awe na malipo? Akasema: Mnasemaje ikiwa atakiweka katika haramu, je atakuwa na mzigo wa dhambi? basi ndivyo hivyo akikiweka katika halali atakuwa na malipo".
Imepokelewa Imamu MuslimWalilalamikia baadhi ya mafukara wa kiswahaba hali ya umasikini wao kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kutotoa kwao sadaka kwa mali ili wapate malipo mengi kama walivyoyapata ndugu zao wenye mali nyingi na ili na wao wafanye kheri kama wao; kiasi ambacho wao wanaswali kama tunavyoswali, na wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa sadaka kwa mali yao ya ziada na sisi hatutoi! Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaelekeza katika yale wanayoyaweza katika sadaka, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwani hakukujaalieni Mwenyezi Mungu vile mnavyoweza kuvitoa sadaka kwa ajili nafsi zenu?! Kwani kauli yenu: "Sub-haanallaah" Inakuwa kwenu na malipo ya sadaka, na vile vile kauli: "Allaahu Akbar" ni sadaka, na kauli: "Alhamdulillaah" ni sadaka, na kauli: Laa ilaaha illa llaah" ni sadaka, na kuamrisha mema" ni sadaka, na "kukataza maovu" ni sadaka, bali hata katika tendo la ndoa la mmoja wenu kwa mke wake ni sadaka. Wakashangaa, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi akidhi mmoja wenu matamanio yake na awe na malipo katika hilo?! Akasema: Hivi mwaonaje kama akiweka katika haramu kama zinaa au kinginecho, je, atakuwa na madhambi? Hivyo hivyo akiweka katika halali anakuwa na malipo.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: "Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoingia siku kumi (za mwisho wa ramadhani) anauhuisha usiku, na anawaamsha watu wake, na anaongeza juhudi na anakaza kikoi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoingia siku kumi za mwisho wa ramadhani anauhuisha usiku wote kwa aina mbali mbali za ibada, na anawaamsha familia yake kwa ajili ya swala, na anajitahidi katika ibada zaidi ya kawaida yake, na anajitenga kwa ajili yake na anajitenga na wake zake.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Hakuwahi kuswali tena Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala yoyote baada kuteremka kwake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" [An-Naswir:1] Isipokuwa alikuwa akisema ndani yake: "Sub-haanaka Rabbanaa wabihamdika Allaahummagh-firlii, (umetakasika Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako, ewe Mwenyezi Mungu nisamehe)". Na kutoka kwa Aisha amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikithirisha kusema katika rukuu yake na sijida yake: "Sub-haanaka llaahumma Rabbanaa wabihamdika Allaahummagh-firlii" Umetakasika ewe Mwenyezi Mungu, Mola wetu Mlezi, na sifa njema ni zako, ewe Mola wangu Mlezi nisamehe" Akiifasiri Qur'ani.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipoteremshiwa juu yake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" Akaifasiri Qur'ani na akaanza kuitekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli yake: "Basi zitakase sifa za Mola wako Mlezi na umuombe msamaha", akawa akikithirisha kusema katika rukuu zake na sijida zake wakati wa swala: "Umetakasika" Na ni kukutakasa wewe dhidi ya kila mapungufu yale yasiyokufaa, "Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako" Kwa sifa nzuri kwako kwa ukamilifu wa dhati yako na sifa zako na matendo yako, "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe" na zifute kwangu dhambi zangu, na uziachilie mbali.
Kutoka kwa Abuu Umama Iyaasi bin Tha'laba Al-Haarithy radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayejikatia haki ya muislamu kwa mkono wake wa kulia, basi Mwenyezi Mungu atakuwa kamuwajibishia moto, na kamharamishia pepo" Bwana mmoja akamuuliza: Hata kikiwa kitu kidogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hata kikiwa kijiti cha mswaki wa Araki".
Imepokelewa Imamu MuslimAmetahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuapa uongo kwa jina la Mwenyezi Mungu ili kujikatia haki ya muislamu, kwani malipo ya hilo ni kustahiki moto, na kunyimwa pepo, nalo ni katika madhambi makubwa. Bwana mmoja akasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu: Hata kikiwa kilichoapiwa ni kitu kidogo? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hata kikiwa ni kijiti cha mswaki unaochukuliwa kutoka katika mti wa Araki.