





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake: Kiongozi muadilifu, na kijana aliyekulia katika ibada ya Mwenyezi Mungu, na mtu ambaye moyo wake umetundikwa katika misikiti, na watu wawili walipoendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wakakutana kwa ajili yake na wakaachana kwa ajili yake, na mwanaume aliyeitwa na mwanamke mwenye wadhifa na uzuri, akasema: Hakika mimi ninamhofu Allah, na mtu aliyetoa sadaka akaificha mpaka usijue kushoto kwake unachotoa kulia kwake, na mtu aliyemkumbuka Mwenyezi Mungu akiwa faragha, yakabubujika machozi macho yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlitoa habari njema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya aina saba za waumini atakaowapa kivuli Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kivuli cha Arshi yake siku ambayo hakutokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake: Wa kwanza: Imamu muadilifu katika nafsi yake na si muovu, na ni muadilifu kwa raia wake na si dhalimu; naye ni yule mwenye mamlaka ya juu, na anaungana naye kila kiongozi atakayeongoza chochote katika mambo ya waislamu akafanya uadilifu ndani yake. Wa pili: Ni kijana aliyekulia katika ibada ya Mwenyezi Mungu, na akaumaliza ujana wake na uchangamfu wake, mpaka akafishwa katika hali hiyo. Wa tatu: Ni mtu ambaye moyo wake umetundikwa katika msikiti, pindi akitoka mpaka hatulizani mpaka arudi ndani yake kwa sababu ya mapenzi makubwa na wingi wa kushikamana na msikiti na kuendelea kubaki ndani yake kwa moyo, hata kukitokea dharura akiwa msikitini akatoka nje ya msikiti. Wa nne: Ni watu wawili kila mmoja alimpenda mwenzake kweli kweli kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na wakadumu katika mapenzi ya dini na ikawa haikuwakatisha sababu yoyote ya kidunia zaidi kukutana kweli au la sivyo mpaka kifo kikawatenganisha. Wa tano: Na mwanaume aliyetakwa na mwanamke ili kumtumia kufanya machafu, naye ni mwanamke mwenye msingi mzuri na heshima na ukoo mtukufu na cheo na mali na uzuri, akakataa na akasema kumwambia: Hakika mimi ninamuhofu Allah. Wa sita: Ni mtu aliyetoa sadaka ndogo au nyingi, na hakutaka kuonekana ndani yake, bali aliificha mpaka haukujua mkono wa koshoto kwake kilichotolewa na mkono kulia kwake. Wa saba: Ni mtu aliyemtaja Mwenyezi Mungu kwa moyo wake kwa kumkumbuka, au kwa ulimi wake kwa kufanya dhikri, akiwa faragha mbali na watu, yakabubujika machozi kutoka machoni mwake kwa hofu na kwa kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Asiashirie mmoja wenu silaha kwa ndugu yake, kwani hajui, huenda Shetani akaipokonya kutoka mkononi mwake, akatumbukia katika shimo la moto".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmetahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kuashiria juu ya ndugu yake muislamu kwa silaha, kwa aina yoyote ile miongoni mwa aina za silaha, kwa sababu yeye hajui huenda Shetani akamsukuma kuitikisa silaha mkononi mwake, akamuuwa ndugu yake au akamuudhi, akatumbukia katika maasi yanayoweza kumpelekea kuingia katika shimo la moto.
Kutoka kwa Abuu Shuraihi radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini", wakasema: Na ni nani huyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ambaye hapati amani jirani yake kwa kero zake".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAliapa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akasisitiza kiapo chake mara tatu, akasema: Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Maswahaba wakamuuliza: Na ni nani ambaye hawezi kuamini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ambaye jirani anahofia usaliti wake na dhulma zake na shari zake.
Imepokelewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake amesema: Ulikuwa usia mkubwa wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipofikwa na mauti: "(Shikamaneni na) Swala nyinyi na waliomilikiwa na mikono yenu ya kuume, (Shikamaneni na) Swala nyinyi na waliomilikiwa na mikono yenu ya kuume", mpaka akaanza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kushikwa na kwikwi kifuani kwake kwa maneno hayo kwa sababu ya kifo, na maneno hayo yalikaribia kujaa ulimi wake.
Imepokelewa na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn MajahUlikuwa usia mwingi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Umma wake naye akiwa katika ulevi wa kifo: Shikamaneni na swala na mdumu nayo na wala msighafilike nayo, na vile vile timizeni haki za wale wanaomilikiwa na mikono yenu ya kuume miongoni mwa watumwa na wajakazi na wamilikini kwa wema, akaendelea kuukariri, mpaka ukaanza kumkwama katika koo lake, na ulimi wake ukashindwa kuutamka kwa ufasaha.
Kutoka kwa Ubada bin Swaamit -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: "Uuzaji unakuwa ni kuuza Dhahabu kwa dhahabu, na fedha kwa fedha, ngano kwa ngano (ambayo haijakobolewa), na ngano kwa ngano (iliokobolewa), na tende kwa tende, na chumvi kwa chumvi, mfano kwa mfano, sawa kwa sawa, mkono kwa mkono, zikitofautiana aina hizi, basi uzeni mtakavyo, ikiwa mkono kwa mkono".
Imepokelewa Imamu MuslimAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake namna ya biashara sahihi katika aina sita za riba, nazo ni: Dhahabu, fedha, ngano (ambayo haijakobolewa), na ngano (iliyokobolewa), na tende, na chumvi, ikiwa ni katika aina hiyo hiyo, kama kuuza dhahabu kwa dhahabu na fedha kwa fedha....ni lazima kuwe na sharti mbili: Ya kwanza: Kufanana katika uzito ikiwa ni kitu kinachopimika kama dhahabu na fedha, au kufanana katika kipimo ikiwa ni kitu kinachopimika, kama ngano (ambayo haijakobolewa) na ngano (iliyokobolewa) na tende na chumvi. Ya pili: Ni muuzaji kupokea thamani na mnunuzi kupokea bidhaa, na hilo lifanyike katika kikao cha makubaliano ya biashara. Zikitofautiana aina zote hizi kama kuuza dhahabu kwa fedha, na tende kwa ngano kwa mfano, itafaa kuuza kwa sharti moja, nayo ni muuzaji kupokea thamani na mnunuzi kupokea bidhaa katika kikao cha makubaliano, isipofanyika hivyo biashara itakuwa batili, na muuzaji na mnunuzi watakuwa wameingia ndani ya riba katika hilo wote wawili.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kilichoshuka chini ya kongo mbili katika kikoi hicho ni motoni".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAmetahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kushusha chini zaidi ya miguu kila kinachositiri kuanzia chini ya mwili wake kama nguo au suruali au kinginecho, na kinachokuwa zaidi ya kongo mbili katika miguu miongoni mwa kikoi kinachoburuza basi hicho ni motoni ikiwa ni adhabu kwake kwa kitendo hicho.
Kutoka kwa kiongozi wa waumini Abuu Hafsi Omari bin Khattwab radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu Rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilolinuia, atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi (malipo yake yatakuwa) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya dunia ataipata, au kwa ajili ya mwanamke ili amuoe, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa lile alilolihamia".
Imepokelewa na Maimamu wawili wa wanachuoni wa Hadithi, Abu Abdillah Muhammad bin Ismail bin Ibrahim bin al-Mughirah bin Bardizbah al-Bukhari na Abu al-Husayn Muslim bin al-Hajjaj bin Muslim al-Qushayri an-Naysaburi katika Sahih zao mbili, ambavyo ndivyoAnabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yote huzingatiwa nia, na hukumu hii ni ya ujumla katika amali zote, kwanzia ibada na miamala, atakaye kusudia kupata masilahi katika amali yake hatopata zaidi ya masilahi na wala hatopata thawabu, na atakayekusudia katika amali yake kujiweka karibu na Allah Mtukufu, atapata thawabu na malipo kupitia amali yake hata kama litakuwa ni jambo la kawaida, kama kula na kunywa. Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga mfano wa kuweka wazi namna gani nia inaathiri matendo pamoja nakuwa huonekana yote yako sawa katika muonekano wa juu, akaweka wazi kuwa atakayekusudia katika kuhama kwake na kuacha nchi yake ni kutafuta radhi za Mola wake, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kisheria na kunakubalika, atalipwa kwa sababu ya ukweli wa nia yake, na atakayekusudia kwa kuhama kwake ni kupata masilahi ya kidunia, kama mali, au cheo, au mke, basi hatopata kwa kuhama kwake huko zaidi ya manufaa aliyoyakusudia, na wala hatokuwa na fungu la malipo na thawabu.
Kutoka kwa Abdallah bin Nu'man bin Bashiri -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi na kati ya halali na haramu kuna mambo yenye kutatiza, hawayajui mambo hayo wengi miongoni mwa watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza, basi atakuwa kaihifadhi dini yake na heshima yake, na atakayeingia katika mambo yenye kutatiza atakuwa kaingia katika haramu, ni kama mfano wa mchunga mifugo mwenye kuchungia kando kando ya mipaka wanahofiwa (mifugo wake) kuingia humo, tambueni na hakika kila Mfalme ana mipaka yake, na tambueni kuwa mipaka ya Mwenyezi Mungu ni makatazo yake, na tambueni kuwa katika mwili kuna kipande cha nyama, kikitengemaa mwili mzima unatengemaa, na kikiharibika, mwili mzima unaharibika, tambueni kipande hicho ni moyo."
Imepokelewa na Bukhari na MuslimAnaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kanuni kuu katika mambo, nakuwa zinagawanyika sehemu tatu katika sheria: Halali ya wazi, na haramu ya wazi, na mambo yenye kutatiza, hukumu yake haiko wazi upande wa uhalali na uharamu, watu wengi hawajui hukumu yake. Atakayeacha mambo hayo yenye kutatiza kwake, dini yake itasalimika kwa kuwa mbali na kuingia katika haramu, na heshima yake itasalimika kutokana na maneno ya watu, kwa yale wanayoweza kumuaibisha kwa kuyafanya kwake haya yenye kutatiza. Na asiyeyaepuka yenye kutatiza atakuwa kaitumbukiza nafsi yake, ima katika haramu, au watu kumkosea heshima yake. Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kapiga mfano ili abainishe hali ya mwenye kuyafanya mambo yenye kutatiza, nakuwa yeye ni sawa na mchunga mifugo, mwenye kuchunga karibu na ardhi ambayo kaihifadhi mwenye ardhi hiyo, inahofiwa mifugo yake kulisha katika mipaka hii kwa sababu ya ukaribu wake, na hivyo hivyo mwenye kufanya mambo yenye utata ndani yake, basi kwa kufanya hivyo anakuwa karibu na haramu na anahofiwa kutumbukia ndani yake. Na baada yake akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama (Nacho ni moyo) mwili hutengemaa kwa kutengemaa kwake, na huharibika kwa kuharibika kwake.
Kutoka kwa Abuu Hamza Anas bin Maaliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake mtumishi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa imani kamili ya Muislamu yeyote haikamiliki mpaka ampendelee nduguye anachokipenda yeye, katika matendo mema, na aina mbalimbali za wema katika dini na dunia, na achukie kwake kinachochukiwa na nafsi yake, na ikiwa ataona kwa ndugu yake Muislamu kuna upungufu katika dini yake, basi ajitahidi kurekebisha, na akiona kuna jambo la kheri basi amtie moyo na amsaidie, na amnasihi katika dini yake au mambo ya dunia yake.