Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way






























Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dua ndio ibada, la msingi nikuwa yote iwe safi kwa ajili ya Allah, sawa sawa iwe ni kuomba jambo au kutaka jambo, kwa kumuuomba Allah Mtukufu ampe yenye manufaa kwake, na amkinge na yenye kumdhuru duniani na akhera, au dua ikiwa ni ibada, nayo ni kila anayoyapenda Mwenyezi Mungu na kuyaridhia katika kauli na matendo ya wazi na ya siri, ibada za moyo au za mwili au za mali. Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akatoa ushahidi juu ya hilo pale aliposema: Amesema Allah Mtukufu: "..Niombeni mimi nitakujibuni, hakika wale wanaofanya kiburi katika ibada yangu wataingia Jahannam wakiwa madhalili"
Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameamrisha ukweli, na akasema kuwa kushikamana nao kunapelekea katika matendo mema ya kudumu, na mwenye kushikamana na kufanya wema humpeleka mtendaji wake Peponi, na ukweli wake unapoendelea mara kwa mara kwa siri na hadharani, basi hustahiki jina la mkweli; nayo ni sifa ya hali ya juu zaidi ya ukweli. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaonya dhidi ya kusema uongo na kusema maneno ya batili; Kwa sababu inawachochea watu kuacha uadilifu, na kufanya maovu, ufisadi, na dhambi, kisha inawapeleka Motoni, na anapoendelea kukithirisha kusema uongo basi mpaka huandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni miongoni mwa waongo.
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-kuhusu maneno mawili anayoyatamka mwanadamu bila uzito wowote na kwa hali yoyote, nakuwa maneno hayo malipo yake ni makubwa katika mizani, nakuwa Mola wetu Mlezi Mwingi wa rehema -Aliyetakasika na kutukuka- anayapenda: Sub-haanallahil Adhwiim, Sub-haanallahi wabihamdihi; Kwakuwa yamekusanya sifa miongoni mwa sifa za Allah kumsifu kwa Utukufu na ukamilifu, na kumtakasa kutokana na mapungufu -Aliyetakasika na kutukuka-.
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna chochote katika ibada kilicho bora zaidi mbele ya Allah Mtukufu kuliko dua; kwa sababu ndani yake kuna kukiri utajiri wa Allah Mtukufu, na kukiri kushindwa kwa mja na kuhitajia kwake kutoka kwake.
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeitetea heshima ya ndugu yake muislamu akiwa hayupo (katika mazungumzo) kwa kukataza watu kumsema vibaya na kumkosea adabu, basi naye Mwenyezi Mungu ataizuia adhabu kwake siku ya Kiyama.
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayesema kwa siku mara mia moja (100): "Sub-haanallaahi Wabihamdihi"; Yatafutwa makosa yake na yatasamehewa, hata kama yatakuwa mengi mfano wa taka nyeupe (povu) zinazoelea Baharini wakati mawimbi yanapotembea na yanapopiga.
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesema: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul-Mulku walahul hamdu Wahuwa a'laa kulli shai-in qadiir", na maana yake nikuwa: Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah peke yake asiye na mshirika, nakuwa Yeye Mtukufu amepwekeka kwa Ufalme uliotimia, na mwenye kustahiki kutajwa na sifa na mapenzi na kutukuzwa pasina mwingine asiyekuwa Yeye, nakuwa Yeye ni muweza hakuna chochote kinachomshinda. Atakayeirejea rejea dhikiri hii tukufu kwa siku mara kumi (10); Basi atakuwa kapata malipo mfano wa malipo ya atakayeondoa utumwa kwa watumwa wanne katika watoto wa Ismail bin Ibrahim -Amani iwe juu yao-, na ametaja kizazi cha Ismail -Amani iwe juu yake-; kwa sababu wao ndio watukufu zaidi kuliko wengine.
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mwenye kutakiwa kheri na Mwenyezi Mungu basi humruzuku ufahamu katika dini yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mgawaji na msambazaji wa yale aliyopewa na Allah Mtukufu katika riziki na elimu na mengineyo, nakuwa mtoaji halisia ni Allah, na ama asiyekuwa yeye hao ni sababu tu hawawezi kunufaisha ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, nakuwa umma huu utaendelea kusimama katika amri ya Mwenyezi Mungu, hatowadhuru mwenye kuwapinga, mpaka Kiyama kisimame.
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anawapenda baadhi ya waja wake, Na miongoni mwao ni mchamungu: Mwenye kutekeleza amri za Allah, mwenye kuyaepuka makatazo yake. Na anampenda mwenye kutosheka: Aliyetosheka kutowahitajia watu kwa kumuelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu wala hageuki kwa mwingine. Na anampenda mnyenyekevu: Mwenye kujinyenyekeza, mwenye kumuabudu Mola wake Mlezi, mwenye kujishughulisha na yenye kumnufaisha, ambaye hashughuliki na kutaka yeyote amjue au amzungumze kwa sifa au shukurani.