





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Zidisheni sana kukikumbuka kikata ladha" Yaani: Kifo.
Imepokelewa na Tirmidhiy, Nasai na Ibn MajahAmehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kukithirisha kukikumbuka kifo ambacho kukikumbuka kwake mtu anakumbuka Akhera, na kunabomoa mapenzi yake ya kupenda ladha za dunia ndani ya moyo wake, na hasa hasa zile za haramu.
Kutoka kwa Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Tulipita tukiwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Hijiri (miji ya Thamudi), akasema kutuambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msiingie miji ya wale waliozidhulumu nafsi zao, isipokuwa muwe mnalia; kwa kutahadhari msijekupatwa na mfano wa yale yaliyowapata" Kisha akampigia kelele mnyama wake akaongeza mwendo mpaka akapapita.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipopita katika miji ya Thamudi, kutoingia katika miji ya walioadhibiwa, wale waliozidhulumu nafsi zao au kuiendea miji hiyo, isipokuwa anayeingia kama atakuwa analia kwa kuchukua mazingatio kwao; kwa kuhofia asijekufikwa na mfano wa yale yaliyowafika miongoni mwa adhabu, kisha akampigia kelele mnyama wake akaongeza mbio mpaka akaivuka.
Kutoka kwa Hudhaifa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa kwa Omari radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Ni nani miongoni mwenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akieleza kuhusu fitina? Watu wakasema: Sisi tulimsikia, akasema: Huenda nyinyi mnakusudia fitina ya mtu kwa familia yake na jirani yake? Wakasema: Ndivyo, akasema: Fitina hiyo inafutwa na swala na swaumu na sadaka, lakini ni nani miongoni mwenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akieleza fitina ambayo inapiga kama mawimbi ya Bahari? Akasema Hudhaifa: Akawanyamazisha watu wote kwa hilo, nikasema: Mimi, akasema: Nakuapiza kwa Mwenyezi Mungu, umkose baba yako, ni wewe kweli, Hudhaifa, nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hupitishwa fitina katika nyoyo (kama ufumwavyo mkeka) ukindu (kijiti) kimoja kimoja, moyo wowote utakaozifyonza basi hutiwa ndani yake doa jeusi, na moyo wowote unaozikataa hutiwa doa jeupe, moyo huo mpaka unakuwa katika (hadhi ya) mioyo miwili, katika weupe mfano wa jiwe jeupe, hivyo hakuna fitina yoyote inayoweza kuudhuru milele kwa muda wote mbingu na ardhi zitakapoendelea kubakia kwake, na moyo mwingine ni mweusi ti! kama chungu kilichofunikwa, haukubali jema, wala haukatai ovu, isipokuwa matamanio ulionyweshwa", Hudhaifa akasema: Na nikamsimulia kuwa hakika kati yako wewe na fitina hiyo kuna mlango uliofungwa, na hivi karibuni utavunjwa, Omari akasema: Hivi utavunjwa? umepata hasara ya kumkosa baba, na lau ungelifunguliwa basi huenda ungelirejeshwa tena, nikasema: Hapana, bali utavunjwa, na nikamsimulia kuwa mlango huo ni mtu atauawa au kufa, na ni mazungumzo ya kweli wala si maneno ya kubumba. Akasema Abuu Khalidi, nikasema kumwambia Saa'di: Ewe Abuu Maaliki nini maana ya nyeusi ti!? Akasema: Ni weupe ung'aao katika weusi, anasema, nikasema: Na nini maana ya chungu kilichofunikwa? Akasema: Kilichogeuzwa juu chini.
Imepokelewa Imamu MuslimAlikuwa kiongozi wa waumini Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake katika kikao chake akiwa pamoja na kundi la Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, akasema kuwaambia: Ni nani kati yenu aliyemsikia Mtume rehema na amni ziwe juu yake akieleza kuhusu fitina? Wakasema baadhi yao: Sisi tulimsikia akieleza kuhusu fitina, akasema Omari radhi za Allah ziwe juu yake: Huenda nyinyi mnakusudia fitina na mtihani wa mtu katika mambo yake maalumu; kwa mke wake na mtoto wake, kwa kuchupa mipaka katika kuwapenda, na pupa yake kwao, na kushughulishwa nao sana kuliko mambo ya kheri, au kwa uzembe wake, kwa kutotekeleza mambo ya lazima kwake kuyasimamia katika haki, na kuwaadabisha na kuwasomesha, na vile vile fitina ya mtu kwa jirani yake na mfano wake, huenda nyinyi mnakusudia hiyo? Wakasema: Ndiyo, akasema: Hiyo ni fitina inayopelekea kuihesabu nafsi, ikiwa ni pamoja na madhambi ambayo yanatarajiwa kufutwa kwa mema, kama swala na swaumu na sadaka. Lakini ni nani kati yenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiitaja fitina inayowakumba watu wote kwa sababu ya ukubwa wake na wingi wa kusambaa kwake, inayowavuruga watu kama yanavyovurugika mawimbi ya Bahari? Watu wote wakanyamaza: Akasema Hudhaifa bin Yamani radhi za Allah ziwe juu yake: Mimi nilimsikia, Omari radhi za Allah ziwe juu yake akafurahi, na akasema kumwambia: Umenishangaza kwa haya aliyokuja nayo mtu mfano wako!: Basi hebu sema: Hudhaifa akasema: Amesema rehema na amani ziwe juu yake: Fitina itatokea na itafungamana na mwili na upande wa moyo wa mtu kama godoro linavyonasa udongo katika mbavu za aliyelala hapo, na zitamuathiri katika moyo kwa kushikamana nazo sana, na kutoziacha fitina hizi, na kujirejea rejea kwake fitina baada ya fitina, moyo wowote utakaoingia ndani yake, na ukazipenda, na zikachanganyika nao, kama kuchanganyikana na kinywaji na kuingia ndani yake; basi litapigwa ndani ya moyo wake doa jeusi; na moyo wowote utakaozikataa, basi utapigwa ndani yake doa jeupe, mpaka nyoyo zitakuwa katika aina mbili; katika moyo mweupe kwa sababu ya kushikamana na imani kisawasawa, na kusalimika kwake na mapungufu, na kwamba fitina haijaambatana nao, na wala hazijauathiri mfano wa jiwe gumu jeupe ambalo hakuna kitu kinaweza kunasa hapo, hakuna fitina inayoweza kumdhuru mpaka mtu atakapokutana na Mwenyezi Mungu. Na moyo mwingine ni moyo uliobadilika rangi yake na kuwa mweusi kwa sababu ya fitina, ni kama birika lililolala upande, au lililogeuzwa ambalo hakuna maji yanayoweza kutulizana ndani yake, basi vile vile moyo huu hakuna kheri wala hekima yoyote inayoweza kunasa ndani yake, haukubali jema, na wala haukatai baya, isipokuwa yale aliyoyapenda, na nafsi yake kuegemea kwayo. Na akasema Hudhaifa kumwambia Omari: Hakika fitina hiyo hakuna chochote kitakachotokea katika zama za uhai wako, lakini kati yako wewe na fitina hiyo kuna mlango uliofungwa na unakaribia kuvunjwa, akasema: Yaani utavunjwa kwa nguvu? na lau kama ungelifunguliwa basi ungelirejeshewa ukafungwa tena, akasema Hudhaifa: Hapana, bali utavunjwa, na kwamba mlango huo ni mtu atauawa au atakufa. Na niliyoyaeleza ni habari za kweli na si katika habari za Mayahudi na Wakristo, na wala si jitihada za mtu mwenye mtazamo wa mbali, bali ni katika hadithi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alinijia mwanamke mmoja Masikini akiwa amebeba mabinti zake wawili, nikawalisha tende tatu, akawapa kila mmoja wao tende moja, kisha akanyanyua tende moja ili kuitumia , akawalishi mabinti zake kwa kuigawa tende ile vipande viwili, ambayo alihitaji kuila mwenyewe, kikanistaajabisha kitendo chake hicho, nikamueleza Mtume alicho kifanya mwanamke yule, akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu amemuwajibishia pepo kwa kile alichokifanya, au amemuacha huru na moto kwa kile alicho kifanya".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleeza mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba mwanamke moja masikini alimjia akiwa kawabeba watoto wake wa kike wawili, akamuomba chakula, akampatia tende tatu, akampatia kila mmoja miongoni mwa mabinti zake tende moja ili ale, watoto wake wakaihitaji tende ile mmoja aliyotaka kuila, akawakatia tende ile vipande viwili, jambo hilo likamshanga mno Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na akakieleza kitendo alichokifanya mwanamke yule kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakika Mwenyezi Mungu kamuwajibishia Pepo kwa tende hii, au kamuacha huru na Moto.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapofika mmoja wenu katika kikao basi na atoe salamu, na akitaka kunyanyuka pia atoe salamu, kwani ya mwanzo haina haki zaidi kuliko ya mwisho".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na AhmadAlimuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekuja mahali walipokaa watu basi awasalimie, na akitaka kunyanyuka basi awaage jamaa zake pia kwa salamu; kwani salamu ya kwanza wakati wa kuja si bora sana kuliko salamu ya mwisho wakati wa kuondoka.
Kutoka kwa Mus'abu bin Saadi amesema: Alijiona Saadi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ana thamani kuliko aliye chini yake, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakuna msaada na riziki mnayopewa nyinyi isipokuwa ni kupitia kwa watu madhaifu wenu".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAlidhania Saadi bin Abii Waqas radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ana ubora kuliko aliye chini yake katika watu madhaifu, kwa sababu ya ushujaa wake na mfano wa hilo!. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Tambueni kuwa hamnusuriwi wala hampewi riziki isipokuwa kwa watu wenu madhaifu kwa dua zao na swala zao na utakasifu wao wa nia; kwani wao mara nyingi ndio hutakasa dua zaidi, na huwa na unyenyekevu zaidi katika ibada kwa sababu nyoyo zao ziko tupu hazifungamani na mapambo ya dunia.
Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa tunapohudhuria chakula pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake hatuweki mikono yetu mpaka kwanza aanze Mtume rehema na amani ziwe juu yake basi anaweka mkono wake, na hakika sisi kuna wakati tulihudhuria chakula pamoja naye, akaja kijakazi kwa kasi kubwa kana kwamba anasukumwa, akaenda ili aweke mkono wake katika chakula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamshika mkono wake, kisha akaja Bedui kwa kasi kubwa kana kwamba anasukumwa, akamshika mkono wake, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Shetani hukihalalisha chakula kwa kutotajwa jina la Mwenyezi Mungu katika chakula hicho, na bila shaka alikuja na kijakazi huyu ili akihalalishe, nikashika mkono wake, akaja tena na Bedui huyu ili akihalalishe nikamshika mkono, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mkono wake umekamatwa na mkononi wangu pamoja na mkono wake kijakazi".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Hudhaifa radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba wanapohudhuria chakula pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawaweki mikoni yao katika chakula mpaka kwanza aanze Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka mkono wake, na hakika sisi tulihudhuria pamoja naye siku moja katika chakula, akaja kijakazi mmoja, kutokana na kasi yake kana kwamba anasukumwa, akaenda ili aweke mkono wake katika chakula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamshika mkono wake, kisha akaja Bedui kana kwamba anasukubwa, akamshika mkono wake kabla hajagusa chakula, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika Shetani hupata uwezo wa kula chakula, atakapoanza mtu kula chakula pasina kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na alikuja na kijakazi huyu ili ajihalalishie kula, nikamshika mkono wake, kisha akaja na huyu Bedui, ili akihalalishe nikamshika mkono wake, ninamuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mkono wa Shetani ulikuwa mkononi mwangu pamoja na mkono wake, kisha akataja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu na akala.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba maisha ya Dunia kwa muumini ni kama Gereza analoishi kwa amri za kisheria, kama kufanya maamrisho na kuacha makatazo, basi akifa anapumzika na haya na anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwake, katika neema za kudumu, nayo kwa Kafiri ni kama Pepo; kwa sababu anafanya ndani yake kila inachotamani nafsi yake na kuamrishwa na matamanio yake, basi akifa anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama miongoni mwa adhabu za kudumu.
Imepokelewa kutoka kwa Hakiim Bin Hizaam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake akanipa, kisha nikamuomba tena akanipa, kisha akasema kuniambia: "Ewe Hakim, hakika mali hii ni kijani kibichi kitamu, atakayeichukua kwa ukarimu wa nafsi, basi atabarikiwa ndani yake, na atakayeichukua kwa kujikweza hatobarikiwa ndani yake, na atakuwa sawa na yule anayekula wala hashibi, na mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini", Hakim anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ninamuapa yule aliyekutuma kwa haki, sitompunguzia yeyote mali yake baada yako kamwe mpaka ntakapoondoka duniani, akawa Abubakari akimuita Hakim ili ampe chochote, akawa anakataa kupokea chochote kutoka kwake, kisha Omari alimuita ili ampe, akakataa kupokea, akasema: Enyi Waislamu, hakika mimi ninamletea haki yake ambayo Mwenyezi Mungu kamgawia katika ngawira, anakataa kuichukua. Hakim hakumuomba tena mtu yeyote baada ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mpaka alipofariki Mwenyezi Mungu amrehe
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeHakim bin Hizam alimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake mahitaji ya kidunia akampatia, kisha akamuomba mara nyingine akampatia, kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Ewe Hakim, hakika mali hii huvutia na hupendwa sana, atakayeipata bila kuomba na akaichukua pasina kujikweza na pupa, basi atabarikiwa ndani yake, na atakayeichukua kwa pupa na tamaa ya nafsi basi hatobarikiwa ndani yake, na atakuwa kama yule anayekula wala hashibi, na mkono wa juu wenye kutoa ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko mkono wa chini unaoomba, anasema Hakim: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, namuapa yule aliyekutuma kwa haki, sitopunguza mali ya yeyote kwa kumuomba chochote baada yako mpaka niondoke duniani. Basi akawa khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Abubakari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akimuita Hakim ili ampatie sadaka, anakataa kupokea chochote, kisha kiongozi wa Waumini Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alimuita ili ampatie mali, akakataa kuchukua, basi Omari akasema: Enyi Waislamu, hakika mimi nimemletea haki yake aliyomgawia Mwenyezi Mungu kutoka katika mali ya Ngawira waliyoipata Waislamu kutoka kwa Makafiri pasina vita wala mapigano, akakataa kuichukua, Hakim hakupunguza mali ya yeyote kwa kumuomba baada ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mpaka alipofariki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.