





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi Mungu angelimuepusha".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kuna baadhi ya watu wana nywele zilizoshikana tena zilizojaa vumbi, na hawazipaki mafuta wala hajali kuziosha, na wala hawana heshima yoyote mbele za watu, basi watu humsukuma mtu kama huyu katika milango yao, na kumfukuza kwa kumdharau; isipokuwa mtu huyu lau angeapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa litokee jambo basi Mwenyezi Mungu angelitenda jambo hilo kwa sababu ya kumkirimu na kumtukuza kwa kujibu ombi lake, na kumlinda asijekupotoka katika kiapo chake, na hii ni kwa sababu ya ubora wake na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu.
Kutoka kwa Saad bin Abii Waqas radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Tulikuwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Je anashindwa mmoja wenu kuchuma kila siku mema elfu moja?" Akamuuliza muulizaji miongoni mwa waliokuwa naye kwenye kikao: "Vipi anaweza kuchuma mmoja wetu mema elfu moja?" Akasema: "Atasema Sub-haana llahi mara mia moja (100), kisha ataandikiwa mema elfu (1000), au atafutiwa makosa elfu moja (1000)".
Imepokelewa Imamu MuslimMaswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hivi hawezi mmoja wenu kupata katika kila siku mema elfu moja?! Akasema mmoja kati ya waliokaa naye: Ni vipi atapata mtu mema elfu moja kwa siku kwa wepesi? Akasema: Aseme: "Sub-haana llaah" Yaani: Ametakasika Mwenyezi Mungu, mara mia moja; basi hapo ataandikiwa mema elfu moja; kwa sababu jema moja hulipwa mara kumi mfano wake, au yatafutwa kwake makosa elfu moja.
Kutoka kwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakuna maisha bora isipokuwa maisha ya Akhera, basi wasamehe Maanswari (watu wa Madina) na Muhajirina (waliohama kutoka kutoka Makkah)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba hakuna maisha halisi isipokuwa maisha ya Akhera katika radhi za Mwenyezi Mungu na rehema zake na pepo yake; kwa sababu maisha ya Dunia huondoka, na maisha ya Akhera ndio ya kudumu na kubakia, kisha akawaombea msamaha na ukarimu na kutengemaa rehema na amani ziwe juu yake Maanswari wale waliompa makazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake pamoja Muhajirina wale walioacha miji yao na mali zao wakitafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Tambueni kuwa dunia imelaaniwa, na vimelaaniwa vilivyomo, isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na yanayompendeza, na msomi, au mwanafunzi".
Imepokelewa na Tirmidhi na bin MajahAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba dunia na vilivyomo inachukiwa mbele ya Mwenyezi Mungu na haipendezi bali imetengwa mbali, yameachwa yote yaliyomo hayasifiki kwa uzuri; kwakuwa dunia na vilivyomo hushughulisha na kuwatenga mbali watu na Mwenyezi Mungu Mtukufu, isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na kila kinachokaribia hilo na kuwa katika aina hiyo katika yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu, au mwalimu wa elimu ya kisheria anayewafundisha watu, au mwenye kujifunza.
Kutoka kwa Wahshiy bin Harbi radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba wao walisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunakula lakini hatushibi, akasema: "Huenda nyinyi mnakula kila mtu peke yake?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: "Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina la Mwenyezi Mungu, mtabarikiwa katika chakula hicho".
Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na AhmadBaadhi ya Maswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakasema: Hakika sisi tunakula lakini hatushibi. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kuwaambia: Huenda nyinyi kila mtu hukaa peke yake wakati wa kula; akala kila mtu peke yake? Wakasema: Ndiyo. Akasema: Basi kusanyikeni na mle pasina kutengana, na mtaje jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula kwa kusema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mtabarikiwa ndani yake na mtashiba.
Imepokelewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Pindi nilipopandishwa juu mbinguni, nilipita kwa watu wakiwa na kucha za shaba, wakizikwarua kwazo nyuso zao na vifua vyao, nikasema: Ni akina nani hao ewe Jibrili, akasema: Hawa ni wale wanaokula nyama za watu, na wanajitumbukiza katika kuvunja heshima za watu".
Imepokelewa na Abu DaudAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kwamba yeye pindi alipopandishwa juu mbinguni usiku Israa na Miiraji (safari ya usiku na kupandishwa), alipita kwa watu wakiwa na kucha za shaba wakizikwarua na kuzichana kwazo nyuso zao na vifua vyao, akamuuliza rehema na amani ziwe juu yake Jibril amani iwe juu yake: Ni kitu gani walifanya hawa mpaka wanalipwa kwa adhabu hii? Akasema Jibril amani iwe juu yake: Hawa ni wale wanaosengenya watu, na wanazungumza vibaya kuhusu heshima zao pasina haki.
Kutoka kwa Abuu Musa radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake, amesema: "Mfano wa yale aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu miongoni mwa uongofu na elimu ni sawa na mfano wa mvua kubwa iliyonyesha katika ardhi, kukawa na kundi moja zuri lililokubali maji likaotesha malisho na majani mengi, na ilikuwa ni ardhi ni kame iliyomeza maji Mwenyezi Mungu akanufaisha watu kupitia ardhi hiyo wakanywa na wakanywesha na wakalima, na mvua hiyo ikashuka katika sehemu nyingine ya ardhi laini haitulizi maji na wala haioteshi mimea; Huu ndio mfano wa mtu aliyejifunza akaelimika katika dini ya Mwenyezi Mungu na yakamnufaisha aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu akajua na akafundisha, na mfano mwingine ni wa mtu ambaye hakuyatilia maanani na wala hakukubali uongofu wa Mwenyezi Mungu ambao nimetumwa nao".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmefananisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kumstaajabu yule anayenufaika na yale aliyokuja nayo miongoni mwa muongozo na njia inayomfikisha mtu katika lengo, na elimu ya kisheria na Ardhi ambayo inashukiwa na mvua nyingi; ikawa migawanyiko mitatu: Wa kwanza: Ardhi safi nzuri, inayokubali maji ya mvua, ikaotesha mimea mingi mibichi na mikavu, watu wakanufanika nayo. Wa pili: Ardhi inayotunza maji lakini haioteshi mimea, yenyewe inahifadhi maji ili watu wanufaike nayo; wanakunywa na kunywesha mifugo yao na mazao yao. Wa tatu: Ni Ardhi tambarare kavu haitunzi maji na wala haioteshi mazao, yenyewe haikunufaika na maji hayo, na wala watu hawakunufaika nayo. Ndivyo hivyo wenye kusikiliza yale aliyotumwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa elimu na uongofu. Wa kwanza: Ni mwanachuoni mwenye utambuzi katika dini, mwenye kuifanyia kazi elimu yake, mwenye kumfundisha mwingine; huyu yuko katika nafasi ya Ardhi nzuri, iliyokunywa ikanufaika yenyewe na ikaotesha ikamnufaisha mwingine. Wa pili: Ni yule aliyehifadhi elimu lakini hana uelewa na namna ya kuitumia, huyu kakusanya elimu, na amemaliza muda wake wote kwa hilo, isipokuwa yeye hajafanyia kazi sunna zake, na wala hana uelewa wa yale aliyoyakusanya; yeye ni mfano wa chombo kwa wengine, na yeye ni sawa na Ardhi ambayo maji hutuama ndani yake na watu wakanufaika nayo. Wa tatu: Ni yule anayesikia elimu lakini haihifadhi, na wala haifanyii kazi, na wala hainukuu kumpa mwingine; huyu ni kama Ardhi kavu ngumu isiyokuwa na mimea ndani yake, wala haikubali maji au inayomharibia mwingine.
Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Hivi leo hii nyinyi si mnapata chakula na kinywaji mkitakacho? Kwa hakika mimi nilimuona Nabii wenu rehema na amani ziwe juu yake inafika mahala hapati hata tende mbovu ya kutosha kujaza tumbo lake.
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Nuuman bin Bashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, maisha waliyonayo watu miongoni mwa neema, na kwamba wao muda wote wana uhakika wa chakula na kinywaji kwa kiwango watakacho, kisha akaeleza kuhusu hali ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba alikuwa hapati katika tende mbovu kiasi cha kujaza tumbo lake kutokana na njaa.
Kutoka kwa Abul Abbasi Sahli bin Sa'di As-saai'diy radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nijulishe amali ambayo nikiifanya atanipenda Mwenyezi Mungu na watu watanipenda, akasema: "Ipe nyongo dunia Allah atakupenda ,na usivitolee macho vitu vya watu, watu watakupenda".
Imepokelewa na Ibn Majah na wengineo kwa sanadi nzuriMtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali ambayo akiifanya Mwenyezi Mungu atampenda na watu watampenda, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Atakupenda Mwenyezi Mungu utakapoacha yasiyo na msingi katika Dunia, na yale yasiyokunufaisha katika Akhera, na ukaacha yale yanayoweza kuwa na madhara katika dini yako, na watu watakupenda utakapoyapa nyongo yaliyoko mikononi mwao miongoni mwa vitu vya kidunia; kwa sababu wanayapenda kulingana na tabia zao za asili, na atakayebanana nao katika hayo watamchukia, na atakayewaachia watampenda.