





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Mikidadi bin Ma'di Karibi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hajawahi kujaza mwanadamu yeyote chombo chenye shari zaidi kama tumbo, kinamtosha mwanadamu kiasi kidogo cha chakula kinachoweza kumpa nguvu, ikiwa hakuna namna, basi theluthi moja (ya tumbo lake) iwe kwa ajili ya chakula chake, na theluthi moja ya kinywaji chake, na theluthi moja kwa ajili ya pumzi yake".
Imepokelewa na Imamu Ahmad, Tirmidhiy, Nasai na Ibn MajahAnatuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika msingi miongoni mwa misingi ya tiba, nayo ni kinga ambayo mtu analinda kwayo afya yake, ambayo ni kupunguza kula, bali ale kwa kiasi cha kuziba tumbo lake na kupata nguvu ya kufanya kazi zake za lazima, na hakika chombo cha shari zaidi kilichowahi kujazwa ni tumbo, na hii ni kwa sababu ya matokeo ya shibe, kama maradhi mabaya yasiyohesabika yanayokuja haraka au kwa baadaye, ya siri au ya wazi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ikiwa mtu hana namna zaidi ya kushiba, basi afanye kula kuwe kwa kiasi cha theluthi, na theluthi nyingine ya kinywaji, na theluthi nyingine ya pumzi ili asipate dhiki na madhara, na uvivu wa kutekeleza aliyomuwajibishia Mwenyezi Mungu juu yake katika swala la dini yake au dunia yake.
Kutoka kwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Lilimfikia jambo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Maswahaba zake, akawahutubia akasema: "Nilionyeshwa Pepo na Moto, katu sijawahi kuona katika kheri na shari mfano wa siku hiyo, na lau mngejua ninayoyajua basi mngelicheka kidogo na mngelia sana" Akasema: Haikuwahi kutokea kwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ngumu kama hiyo, akasema: Wakafunika nyuso zao huku wakitoa sauti za kugugumia (kwa vilio), anasema: Akasimama Omari akasema: Tumemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na Uislamu kuwa dini, na Muhammadi kuwa Nabii, anasema: akasimama yule bwana akasema: Ni nani baba yangu? Akasema: "Baba yako ni fulani", ikateremka: "Enyi mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni" [Al-Maaida: 101].
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeLilimfikia jambo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Maswahaba zake, nalo ni kwamba wao walimzidishia maswali, akakasirika, na akawahutubia, akasema: Nimeonyeshwa Pepo na Moto; sikuwahi kuona kheri nyingi kuliko nilizoziona siku ya leo Peponi, wala shari kubwa kuliko nilizoziona siku hiyo Motoni, na lau kama mngeliona nilichokiona, na mkajua ninachokijua katika yale niliyoyaona siku ya leo na kabla ya leo, basi mngelihuzunika huzuni kubwa, na kungepungua kucheka kwenu, na kungezidi kulia kwenu. Anasema Anasi radhi za Allah ziwe juu yake: Haikuwahi kutoka kwa Maswahaba wake rehema na amani ziwe juu yake siku ngumu kama hiyo, na wakafunika vichwa vyao huku wakitoa sauti ya kunung'unika inayotoka puani kwa sababu ya kulia sana. Akasimama Omari radhi za Allah ziwe juu yake akasema: Tumemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na Uislamu kuwa dini, na Muhammadi kuwa Nabii. Akasema: Akasimama yule bwana, akasema: Nani baba yangu? Akasema: "Baba yako ni fulani", ikateremka: "Enyi mlioamini! Msiulize kuhusu mambo ambayo yakikudhihirikieni yatakuchukizeni" [Al-Ma’idah: 101].
Kutoka kwa Anas -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu, na hakuna kinachoweza kujaza tumbo la mwanadamu isipokuwa udongo, na Mwenyezi Mungu humsaheme mwenye kuomba msamaha".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba lau kama mwanadamu angelipata bonde moja lililojaa dhahabu, basi angependa kwa sababu ya tamaa yake ambayo ndiyo maumbile yake awe na mabonde mengine mawili, na kwamba mwanadamu haachi kuipupia dunia mpaka anakufa na lijae tumbo lake kwa udongo wa kaburi lake.
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na tabia mbaya na matendo mabaya, na matamanio mabaya"
Imepokelewa Imamu TirmidhiyIlikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga" Yani: Ninaomba ulinzi na ukaribu "kwako" na si kwa asiyekuwa wewe, "kutokana tabia mbovu" alizozikataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake, "katika tabia" kama chuki na husuda na kiburi, "na" mabaya "katika matendo" kama kutukana na kushutumu, "na" yote "matamanio", ambayo nafsi inayatamani hali yakuwa yanakwenda kinyume na sheria.
Kutoka kwa Iyaadh bin Himari ndugu yao na Bani Mujashii radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alisimama kwetu Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake siku moja kwa ajili ya kuhutubia, akasema: Na akaeileza hadithi na ndani yake alisema: "Na hakika Mwenyezi Mungu ameniteremshia wahyi kuwa, kuweni wanyenyevu, mpaka asijikweze yeyote kwa mwingine, na wala asimfanyie uadui yeyote mwenzake"
Imepokelewa Imamu MuslimAlisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Maswahaba zake wakati akihutubia, na ikawa miongoni mwa yale aliyosema ni: Hakika Mwenyezi Mungu amemteremshia wahyi ya kwamba ni wajibu kwa watu wanyenyekeane wao kwa wao, na hii ni kwa kushusha mbawa (kujishusha) kwa viumbe na kuwa wapole, mpaka asijikweze kwa kudai ukubwa na kiburi na utukufu yeyote kwa ukoo wake au mali yake au kinginecho juu ya yeyote, na wala asidhulumu na asifanye uadui yeyote kwa mwenzake.
Kutoka kwa Aisha Mama wa Waumini radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Ewe Aisha, hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole anapenda upole, na hutoa malipo katika upole ambayo hayatoi katika ususuwavu (ukali), na wala hatoi kwa mengineyo".
Imepokelewa Imamu MuslimAlimuhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake juu ya upole, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake anawatakia wepesi na wala hawatakii ugumu, wala hawalazimishi juu ya uwezo wao, ni wajibu kwa mja wake ajipambe kwa ulaini na kuchukua kilicho rahisi; asiwe mkorofi wala mkali, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hutoa malipo kwa sababu ya upole na ulaini katika dunia kama kusifia vizuri, na kutoa mahitaji ya watu na kurahisisha malengo, na Akhera kutoa thawabu nyingi zaidi kuliko jinsi anavyotoa katika ususuwavu na ukali na ukorofi, upole huja na mambo ambayo hayaji katika mambo mengine.
Kutoka kwa Zaidi bin Arqam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Sikwambieni isipokuwa kama alivyokuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kushindwa, na uvivu, na uoga, na ubahili, na ukongwe, na adhabu ya kaburi, Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu uchamungu wake, na uitakase kwani wewe ndiye mbora wa kuitakasa, wewe ndiye msimamizi wa nafsi na mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyo na manufaa, na moyo usiyo nyenyekea, na nafsi isiyo tosheka, na maombi yasiyo jibiwa".
Imepokelewa Imamu MuslimIlikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako" na ninajiegemeza kwako, "Kutokana na kushindwa" kwa kukosa uwezo wa unjanja wenye manufaa, "na uvivu" kwa kushindwa kuendesha mambo, aliyeshindwa hana ujanja, na mvivu hana haja nao, "na uoga" kwa kujizuia kuyaendea yanayopasa kufanywa, "na ubahili" kwa kuzuia yanayopaswa kuyatoa, "na ukongwe" na ukubwa wa umri unaopelekea udhaifu wa mwili, "na adhabu za kaburi" na sababu zinazopelekea katika hayo. "Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu" na uipe na uiwezeshe katika "uchamungu wake" kwa kufanya uchamungu na kuacha maasi, "na uitakase" na uisafishe kutokana na uchafu na tabia mbaya, "wewe ndiye mbora wa kuitakasa" na wala hakuna wa kuitakasa yeyote zaidi yako, "Wewe ndiye msimamizi wake" na mtetezi wake na msimamizi wake, "na Mola wake" Msimamizi wa mambo yake, na Mola wake Mlezi na mwenye kuineemesha. "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyokuwa na manufaa", kama elimu ya nyota na ukuhani na uchawi, au isiyo na manufaa Akhera, au elimu isiyofanyiwa kazi, "na moyo usionyenyekea" kwako, na wala haujishushi, na wala hautulii, wala hautulizani kwa kukutaja, "na nafsi isiyoshiba" wala isiyokinai kwa yale iliyopewa na Mwenyezi Mungu na akairuzuku miongoni mwa halali nzuri, "na kutokana na maombi" yenye kurudishwa "yasiyopokelewa".
Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba mtu mmoja aliyeandikishana kujitoa katika utumwa alimjia akasema: Hakika mimi nimeshindwa kulipa deni tuliloandikishana, basi naomba unisaidie, akasema: Je, nikufundishe maneno ambayo alinifundisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hata kungekuwa juu yako na deni zito mfano wa mlima Swiri Mwenyezi Mungu atakulipia, akasema: "Sema: Allaahumma kfinii bihalaalika an haraamika, wa aghninii bifadhlika amman siwaaka". Tafsiri: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze kwa halali yako dhidi ya haramu yako, na unitajirishe kwa fadhila zako nisimuhitaji yeyote asiyekuwa wewe.
Imepokelewa Imamu TirmidhiyAlimuijia kiongozi wa waumini Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake bwana mmoja mtumwa alikuwa kaandikishana na bwana yake na amekubaliana naye ili aikomboe nafsi yake na aiache huru ili awe huru, na hakuwa na mali, akasema: Hakika mimi nimeshindwa kulipa deni hilo juu yangu, nakuomba unisaidie kulilipa kwa mali, au kwa kunifundisha na kunielekeza, akasema kumwambia kiongozi wa waumini: Je, nikufundishe maneno aliyonifundisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lau kama ungelikuwa na deni mfano wa mlima Swiri wa kabila la Twayyi basi Mwenyezi Mungu angelikulipia kwa mstahiki wake, na angelikuokoa kutoka katika madhila yake, akasema: Sema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze" na uniepushe na uniweke mbali "kwa halali yako" nitosheke nayo "dhidi ya" kutumbukia katika "haramu yako", na unitosheleze "kwa fadhila zako" na ukarimu wako "kutomuhitaji yeyote" katika viumbe.
Na kutoka kwa Salmani Alfaaris -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Watu wa aina tatu hatowasemesha Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama wala hatowatakasa na watakuwa na adhabu chungu, Mzee mzinifu, na masikini jeuri, na mtu aliyemfanya Mwenyezi Mungu kuwa ndio bidhaa, hauzi ila kwa kiapo chake wala hanunui ila kwa kiapo chake".
Imepokelewa TwabraniyAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu aina tatu za watu, wenye kustahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama kwa adhabu tatu, endapo hawatotubia au kusamehewa adhabu: Ya kwanza: Hatowasemesha Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama kwa sababu ya ukali wa ghadhabu yake, bali atawapuuza, au atawasemesha maneno yasiyowafurahisha na yanayoonyesha hasira yake juu yao. Ya pili: Hatowatakasa wala hatowasifia wala hatowasafisha kutokana na madhambi. Ya tatu: Watakuwa na adhabu yenye kuumiza sana Akhera. Na watu wa aina hiyo ni: Aina ya kwanza: Mtu mzima na anajiingiza katika machafu ya zinaa. Ya pili: Fakiri asiyekuwa na mali lakini pamoja na hivyo ana kiburi kwa watu. Ya tatu: Anayekithirisha kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu katika kuuza na kununua, analidhalilisha jina la Mwenyezi Mungu, na analifanya kuwa ndio nyenzo ya kujipatia mali.