





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Nawwaas bin Sam'aan Al-Answaariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kapokea kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Amepigia mfano Mwenyezi Mungu wa njia iliyonyooka ,na pambizoni mwa njia kuna kuta mbili, kuta hizo zina milango ilikuwa wazi, na kwenye milango kuna pazia isiyomuonesha mwenyekupita, na mbele ya kila mlango kuna mwenye kuita akisema: Enyi watu, ingieni nyote moja kwa moja wala msipinde kwenda kwingine, na juu ya huyu muitaji kuna muitaji mwingine akiita juu ya njia, na kila mja anapotaka kufungua kidogo milango hiyo anasema: Ole wako wacha usiufungue mlango huo, ikiwa utaufungua tu hutoweza kujizuia, na njia hapa ni Uislamu, na kuta mbili: Ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, na milango iliyofunguliwa: Ni maharamisho ya Mwenyezi Mungu, na huyo muitaji aliyopo mwanzo wa mlango ni kitabu cha Mwenyezi Mungu, na muitaji aliyepo juu: Ni Mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu katika moyo wa kila Muislamu."
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadAmeweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuwa Mwenyezi Mungu alitolea mfano wa Uislamu na njia iliyonyooka pana isiyokuwa na konakona, na pambizoni mwa njia hii kuna kuta mbili zimeizunguka njia hii katika pande zake mbili, na njia hizo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, katikati ya hizi kuta mbili kuna milango iliyofunguliwa, na hiyo milango ni makatazo ya Mwenyezi Mungu, na katika milango hiyo kuna mapazia ambayo humzuia mwenye kupita kumuona aliye ndani, na mwanzo wa njia kuna mwenye kuita akielekeza watu na kuwaongoza na akiwaambia: Ingieni nyote moja kwa moja wala msipinde kwenda kwingine, na huyu mwenye kuita ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na juu ya njia kuna muitaji mwingine, na huyu muitaji humkemea kila mwenye kutembea katika njia hii ambaye anaelekea kutaka kufunua pazia za milango hiyo humkemea na kumwambia Ole wako usiufungue mlango huo! kwa hakika ukiufungua mlango huo utaingia na wala hutoweza kuizuia nafsi yako isiingie humo, na huyu mwenye kuita ni mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu katika moyo wa kila Muislamu.
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Je anapenda mmoja wenu pindi atakaporudi kwa mke wake apate Ngamia watatu wenye mimba na walio nenepa?" Tukasema: Ndiy. Akasema: "Basi aya tatu anazozisoma mmoja wenu katika sala zake ni bora kwake kuliko Ngamia watatu wenye mimba na walionenepa."
Imepokelewa Imamu MuslimAnaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa malipo ya kusoma Aya tatu katika sala; ni bora kuliko mtu kupata nyumbani kwake Ngamia wakubwa wenye mimba na walio nenepa.
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah Bin Aamir Al-juhaniy-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake: "Mwenye kuisoma Qur'ani kwa sauti ya wazi ni kama mwenye kutoa sadaka hadharani, na mwenye kuisoma Qur'ani kwa siri ni kama mwenye kuficha sadaka."
Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na NasaaiAmeweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kuweka wazi kusoma Qur'ani ni sawa na mwenye kuweka wazi anapotoa sadaka, na mwenye kuficha kisomo cha Qur'ani ni sawa na mwenye kuificha sadaka.
Kutoka kwa Ally amesema: Hakika mimi nilikuwa ni mtu kila nikisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hadithi Mwenyezi Mungu ananinufaisha kwa hadithi hiyo kwa kiasi alichotaka kuninufaisha, na akinihadithia yeyote katika Masahaba zake ninamuapisha, akiniapia ninamuamini, na siku moja alinihadithia Abubakari, na Abubakari akasema ukweli, akasema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna mtu yeyote atakayetenda dhambi, kisha akasimama akajitwaharisha, kisha akaswali, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe", Kisha akasoma aya hii: "Na wale ambao wakifanya machafu au wakizidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakaomba msamaha kutokana na madhambi yao" [Al-Imran: 135].
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na AhmadAmeeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna mja yeyote atakayetenda dhambi, akatawadha vizuri, kisha akasimama na akaswali rakaa mbili kwa nia ya kuomba toba kutokana na dhambi lake hili, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe. Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasoma kauli yake Mtukufu: "Na wale ambao wakitenda dhambi kubwa au wakizidhulumu nafsi zao kwa kutenda dhambi chini ya hizo, wanaikumbuka ahadi ya Mwenyezi Mungu ya malipo mema kwa wanaomtii na malipo mabaya kwa wanaomuasi na wanaelekea kwa Mola wao hali ya kutubia wakawa wanamuomba Awasamehe madhambi yao na wakawa wana yakini kwamba hapana anayesamehe madhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na wao kwa sababu hiyo hawaendelei kwenye maasi, na wao wanajua kwamba wakitubia Mwenyezi Mungu Atawakubalia toba yao". [Surat Al-Imran: 135].
Kutoka kwa Abuu Umama Al-Bahiliy radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akasema: Wasemaje kuhusu mtu aliyepigana vita akitaka malipo kwa Allah na kusemwa vizuri na watu, ana lipi? Akasema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Hana malipo yoyote" Akalirudia hilo mara tatu, akimwambia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Hana malipo yoyote" Kisha akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu hakubali amali yoyote isipokuwa ile itakayokuwa imetakasiwa nia, na ikakusudiwa kupata radhi za Allah (na kwenda kuuona uso wake)".
Imepokelewa na An-nasaiyAlikuja mtu kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kumuuliza na kumuuliza juu ya hukumu ya mtu anayetoka kwa ajili ya vita na jihadi kutafuta malipo kwa Mwenyezi Mungu na kutaka sifa na pongezi kwa watu, je anapokea thawabu? Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, akajibu: Huyo hana malipo yoyote. Alipochanganya kitu kisichokuwa Mwenyezi Mungu katika nia yake, yule bwana akarudia swali lake mara tatu kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake na akamjibu na akathibitisha jibu lile lile kwake kwamba hana malipo, basi Mtume -rehema na amani ziwe juu yake, akampa kanuni ya kukubalika amali kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba Mwenyezi Mungu haikubali amali isipokuwa yote iwe ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu bila ya yeyote kuhusishwa nayo, na iwe ni kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Katika uzuri wa uislamu wa mtu: Ni kuacha kwake yale yasiyomuhusu".
Imepokelewa naTirmidhiy na wengineoAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kuwa miongoni mwa mazuri ya ukamilifu wa Uislamu wa Muislamu na ukamilifu wa imani yake, ni kujiweka kwake mbali na yale yasiyomuhusu na yale yasiyo na faida kwake miongoni mwa kauli na matendo, au katika yale yasiyomuhusu miongoni mwa mambo ya dini na dunia, mtu kushughulika na yale yasiyomuhusu huenda likamshughulisha akaacha yale yanayomuhusu, au likampelekea katika yale yanayomlazimu kuyaepuka; kwani mwanadamu ataulizwa kuhusu matendo yake siku ya Kiyama.
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini si msemaji watu vibaya wala mtoaji wa laana wala muovu wala mwenye kauli chafu"
Imepokelewa Imamu TirmidhiyAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa si katika mambo ya muumini mwenye imani kamili kuwa mtoa aibu za watu katika nasaba zao, wala mwingi wa matusi na laana, wala muovu wa vitendo na kauli ambaye hana haya.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayesema: (Laa ilaaha illa llahu, wah-dahu laa sharika lahu, Lahul mulku, Walahul hamdu, Wahuwa alaa kulli shaini Qadiir) kwa siku mara mia moja, inakuwa kwakwe ni sawa na kuacha huru watu kumi, na anaandikiwa mema mia moja, na anafutiwa makosa mia moja, na inakuwa kwake ni kinga kutokana na Shetani kwa siku yake nzima mpaka afike jioni, na hatokuja yeyote na jambo bora zaidi kuliko atakalokuja nalo, isipokuwa yeyote atakayefanya zaidi ya alivyofanya yeye".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema: "Hapana Mola" na hakuna muabudiwa wa haki "isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika" katika uungu wake na ulezi wake na majina yake na sifa zake, "Ufalme ni wake" na maamuzi na mipangilio yote, "naye juu ya kila kitu ni muweza" pasina wa kumzuia wala wa kumkinga, na asiyoyataka hayawezi kuwa. Atakayesema dhikiri hii kwa siku mara mia moja, ataandikiwa ujira kutoka kwa Mwenyezi Mungu sawa na aliyeacha huru watumwa kumi, na ataandikiwa kwa maneno hayo mema mia moja na daraja Peponi, na yatafutwa kwake makosa mia moja, na yatakuwa ni kinga na kizuizi na ngome dhidi ya Shetani na upotovu wake na usaliti wake katika siku yake hiyo mpaka iingie jioni kwa kuzama jua, na hatoleta yeyote siku ya Kiyama kitu bora kuliko alichokuja nacho, isipokuwa mtu aliyefanya zaidi ya hivyo na akazidisha zaidi ya hapo.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Moyo wa mzee huendelea kuwa kijana katika mambo mawili: Katika kupenda dunia na matumaini ya muda mrefu".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mzee huzeeka na mwili wake kudhoofika, lakini moyo wake huwa kijana kwa kupenda mambo mawili: La kwanza: Kuipenda dunia kwa kuwa na wingi wa mali. La pili: Kuwa na uhai na maisha na umri na matarajio ya muda mrefu.