





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake ghafla akasikia kishindo, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Je, mnajua ni nini hiki?” Akasema: Tukasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi, akasema: «Hili ni jiwe lililotupwa Motoni muda wa (miaka) sabini iliyopita, na sasa linaanguka Motoni mpaka litafika katika kina chake.
Imepokelewa Imamu MuslimMtume rehema na amani ziwe juu yake alisikia sauti ya kushtua kama kuanguka kwa mwili, akawauliza Masahaba aliokuwa nao Mwenyezi Mungu awawie radhi kuhusu sauti hiyo, wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi zaidi. Akawaambia rehema na amani ziwe juu yake: Sauti hii mliyoisikia ni ya jiwe lililorushwa kutoka ukingo wa Jahannam miaka sabini iliyopita lilikuwa likiporomoka na kuanguka humo, hivi sasa mliposikia kishindo ndio limefika katika kina chake.
Kutoka kwa Salama bin Al Ak'wa'i -Radhi za Allah ziwe juu yake. Amesimulia kuwa mtu mmoja alikula chakula kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa mkono wake wa kushoto, akasema: "Kula kwa mkono wako wa kulia", Akasema: Siwezi, akasema: "Kamwe, hutoweza!", Hakuna kilichomzuia ila ni kiburi, akasema: hakuweza tena kuunyanyua kwenda kinywani kwake.
Imepokelewa Imamu MuslimAlimuona Mtume Rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja akila kwa mkono wake wa kushoto, akamuamrisha ale kwa mkono wake wa kulia, Yule bwana akamjibu kwa kiburi na kwa kuongopa kuwa hawezi! Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akamuombea dua mbaya azuiliwe kula kwa mkono wa kulia, Mwenyezi Mungu akajibu dua ya Nabii wake, kwa kupooza mkono wake wa kulia, hakuweza kuunyanyua kwenda kinywani kwake baada ya hapo kwa chakula au kinywaji.
Kutoka kwa Jundabi bin Abdillahi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Alisema mtu mmoja, Wallahi -Namuapa Mwenyezi Mungu- hatomsamehe Mwenyezi Mungu fulani, Akasema Mwenyezi Mungu: Ninani anayejiapiza kwangu kuwa sitomsamehe fulani? Hakika mimi nimemsamehe, na nimeyaporomosha matendo yako". Na katika hadithi ya Abuu Huraira: Nikuwa msemaji hapa alikuwa ni mtu mchamungu, Amesema Abuu Huraira: "Alizungumza neno moja lililoteketeza dunia yake na Akhera yake".
Imepokelewa na Imamu MuslimAnaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa njia ya kutahadharisha juu ya hatari ya ulimi, kuwa mtu mmoja aliapa kuwa Mwenyezi Mungu hatomsamehe mtu mmoja aliyekuwa akitenda madhambi; kana kwamba kamuhukumia Mwenyezi Mungu na kamfungia maamuzi; alipoamini ndani ya nafsi yake kuwa yeye kwa Mwenyezi Mungu ana ubora na thamani na nafasi, na kwa huyu mkosefu ana udhalili, na huku ni kumuelekeza Mwenyezi Mungu na ni utovu wa adabu kwake, akamuwajibishia mtu huyo tabu na hasara Duniani na Akhera.
Kutoka kwa Abdallah bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-Hadithi Marfu'u: "Haitokei kuuliwa nafsi yoyote kwa dhulma isipokuwa hupata binadamu wa mwanzo fungu (la dhambi) kutoka katika damu hiyo, kwasababu yeye ndiye muanzilishi wa kwanza kuua".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimInasimulia hadithi hii sababu ya kubebeshwa mmoja kati ya binadamu damu zinazofuatia ambazo zinazomwagwa baada yake, Inasemekana kuwa ni Qaabil alimuua ndugu yake Haabil kwasababu ya kumuhusudu, wao ndio muuliwa na muuwaji wa mwanzo katika watoto wa adamu; anabeba Qaabil fungu la madhambi ya damu ambazo zinazomwagwa baada yake; kwasababu yeye ndiye aliyeanzilisha kuuwa; kwasababu kila atakayefanya baada yake anaiga kwake.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-yakwamba yeye alimsikia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema:"Hakika mja anaweza kuzungumza neno,asilijali ndani yake akateleza kwa neno hilo na kuingia katika moto ambao umbali wake ni baina ya mashariki na magharibi".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAnatueleza sisi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa kuna baadhi ya watu huwa hawafikirii wanapotaka kuzungumza, je maneno haya nitakayoyazungumza ni ya kheri au la?. na matokeo yanakuwa huyu mzungumzaji anatumbukia kwasababu ya kutofikiria mambo ya haramu, na anaitia nafsi yake katika adhabu ya Mwenyezi Mungu katika moto wa jahanamu, -Mwenyezi Mungu atukinge- na huenda akaporomoka katika moto masafa marefu umbali wa masafa kati ya mashariki na magharibi.
Kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Atakayesema: -Yaani: anapotoka nyumbani kwake-: Bismillaahi tawakkaltu a'la llaahi -kwa jina la Mwenyezi Mungu nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaa- hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, huambiwa: Umeongozwa na umetoshelezwa na umekingwa, na shetani hujitenga mbali naye". Ameongeza Abuudaudi: "Basi husema: -yaani shetani-: kuwaambia mashetani wengine: utaweza vipi kwa mtu aliyeongozwa na akatoshelezwa na akakingwa?".
Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu DaudAmeeleza Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa mtu atakapotoka nyumbani kwake na akasema: Bismillaahi -kwa jina la Mwenyezi Mungu-, Tawakkalu a'lallaahi -Nimemtegemea Mwenyezi Mungu-, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaahi- hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Malaika humuita Ewe mja wa Mwenyezi Mungu umeongozwa katika njia ya haki, na umetoshelezwa mahitajio yako, na umehifadhiwa dhidi ya maadui; basi shetani aliyewakilishwa kwake hujitenga mbali naye, na hapo husema shetani mwingine kumwambia shetani huyu: utawezaje kumpoteza mtu tayari kaongozwa, na katoshelezwa, na amekingwa na mashetani wote? kwasababu yeye amesema maneno haya basi wewe hutomuweza.
Kutoka kwa Abuu Umama radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akihutubu katika Hija ya kuaga akasema: "Mcheni na Allah Mola wenu Mlezi, na salini swala zenu tano, na fungeni mwezi wenu, na tekelezeni zaka zenu, na mtiini mwenye mamlaka kwenu, (Mkiyafanya haya) mtaingia pepo ya Mola wenu".
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadAlihutubia Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya Arafa, katika Hija ya kuaga, mwaka wa kumi hijiria (tangu kuhama kutoka Makka) na Hija hiyo iliitwa hivyo kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwaaga watu ndani yake, Na akawaamrisha watu wote wamuogope Mola wao Mlezi kwa kutekeleza amri zake na kuepuka makatazo yake. Na wasali swala tano alizozifaradhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu usiku na mchana. Na wafunge mwezi wa ramadhani. Na wawape zaka ya mali wastahiki wake na wasizifanyie ubahili. Na wawatii aliowafanya Mwenyezi Mungu kuwa viongozi juu yao, pasipokuwa na kumuasi Mwenyezi Mungu, atakayefanya mambo haya yaliyotajwa basi malipo yake ni kuingia peponi.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapokutana mmoja wenu na ndugu yake basi na amsalimie, ukiwatenganisha kati yao mti, au ukuta, au jiwe, kisha akakutana naye tena basi amsalimie tena"
Imepokelewa na Abu DaudMtume rehema na amani ziwe juu yake anamhimiza muislamu kumsalimia ndugu yake muislamu kila anapokutana naye, hata kama wakiwa wanatembea pamoja na kikawatenganisha chochote, kama mti au ukuta au jiwe kubwa, kisha akakutana naye baada ya hapo basi amsalimie kwa mara nyingine.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo?" wakasema: Ndiyo, ewe Mtume wa Allah, akasema: "Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya kheri."
Imepokelewa Imamu MuslimMtume rehema na amani ziwe juu yake, aliwauliza maswahaba zake iwapo wanataka awaongoze katika matendo yatakayowapelekea kupata msamaha wa madhambi, na kufutwa kwake kutoka katika vitabu vya Malaika wenye kuhifadhi, na kupata daraja za juu Peponi? Maswahaba wakasema: Ndio tunataka hivyo. Akasema: Ya kwanza: Kueneza na kukamilisha udhu kwa shida; kama vile baridi, ukosefu wa maji, na maumivu ya mwili, na maji ya moto. Pili: Kupiga hatua nyingi - ambazo ni kati ya miguu miwili- kwenda misikiti iliyo mbali na nyumbani, na kurudi rudi kila wakati. Tatu: Kungoja wakati wa Swala, na moyo kuambatana nayo, na kujitayarisha kwa ajili yake, na kukaa msikitini kwa ajili yake kungojea jamaa, anaposwali hungojea mahali pake pa kuswali kwa ajili ya swala nyingine. Kisha akaeleza rehema na amani ziwe juu yake kuwa mambo haya ndiyo Jihadi ya kweli; Kwa sababu yanaziba njia za Shetani juu ya nafsi, na yanatenza nguvu matamanio, na yanaizuia isiingiwe na wasi wasi, hivyo kundi la Mwenyezi Mungu likashinda majeshi ya Shetani kupitia hayo; na hii ndiyo Jihadi kubwa zaidi, kwakuwa imekuwa kama kikosi cha jeshi upande wa maadui.