





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abdillahi bin Amri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akasema: Nakupa mkono wa utiifu juu ya kuhama na jihadi nikitaraji malipo toka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akasema: "Je kuna mmoja kati ya wazazi wako wawili yuko hai?" Akasema: Ndiyo, bali wote wawili, akasema: "Je unataka malipo toka kwa Allah?" Akasema: Naam, akasema: "Hebu rudi kwa wazazi wako, na ukaishi nao vizuri" Na katika riwaya nyingine ya kwao: alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamuomba ruhusa ya kwenda jihadi, akasema: "Hivi wako hai wazazi wako?" Akasema: Ndiyo, akasema: "Basi kwao wao pigana jihadi". Kutoka kwa Abdillahi bin Amri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-akasema: Nakupa mkono wa utiifu juu ya kuhama na jihadi nikitaraji malipo toka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akasema: "Je kuna mmoja kati ya wazazi wako wawili yuko hai?" Akasema: Ndiyo, bali wote wawili, akasema: "Je unataka malipo toka kwa Allah?" Akasema: Naam, akasema: "Hebu rudi kwa wazazi wako, na ukaishi nao vizuri" Na katika riwaya nyingine ya kwao: alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamuomba ruhusa ya kwenda jihadi, akasema: "Hivi wako hai wazazi wako?" Akasema: Ndiyo, akasema: "Basi kwao wao pigana jihadi" Kutoka kwa Abdillahi bin Amri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akasema: Nakupa mkono wa utiifu juu ya kuhama na jihadi nikitaraji malipo toka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akasema: "Je kuna mmoja kati ya wazazi wako wawili yuko hai?" Akasema: Ndiyo, bali wote wawili, akasema: "Je unataka malipo toka kwa Allah?" Akasema: Naam, akasema: "Hebu rudi kwa wazazi wako, na ukaishi nao vizuri" Na katika riwaya nyingine ya kwao: alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamuomba ruhusa ya kwenda jihadi, akasema: "Hivi wako hai wazazi wako?" Akasema: Ndiyo, akasema: "Basi kwao wao pigana jihadi".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAlikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akimueleza kuhusu hamu yake na mapenzi yake ya jihadi na kuhama katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na alikuwa huyu bwana kaacha nyuma yake wazazi wake wawili, na imekuja katika riwaya ya Abuudaudi kuwa "Walikuwa wakilia", wakihofia maisha yake, akamuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Je kuna yeyote kati ya wazazi wako wawili yuko hai?" Akasema: Ndiyo, bali wote wawili, akasema: "Na unatafuta malipo toka kwa Allah?" Akasema: Ndiyo, akasema: "Basi rudi kwao ukawachekeshe kama ulivyowaliza". Akamrudisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika lile ambalo ni bora katika haki zake, nalo ni kurudi kwa wazazi wawili na aishi nao vizuri, kwani hilo ni katika kupambana na nafsi katika kusimamia kuwahudumia na kuwaridhisha na kuwatii, kama ilivyokuja katika riwaya ya Bukhariy na Muslim: "Basi kwao wao wawili pigana jihadi". Na aliweka wazi katika hadithi nyingine kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili na kuwatii na kuwafanyia mazuri ni bora zaidi kuliko kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyokuja katika riwaya nyingine ya kutoka kwa bin Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Anasema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamuuliza kuhusu amali bora, akasema: "Ni swala" Akasema: kisha nini?: Akasema: "Jihadi" akasema: Hakika mimi nina wazazi wawili, akasema: "Kuwafanyia kwako wema wazazi wawili ndiyo bora" ameitoa bin Hibbaani, Imeonyesha hadithi hii kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili ndiyo bora kuliko Jihadi, isipokuwa kama itakuwa Jihadi ni faradhi ya lazima, basi hapo itatangulizwa juu ya kuwatii wao; kwasababu ya ulazima wake.
Kutoka kwa Thauban -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Allah- rehema na amani za Allah ziwe juu yake: "Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu" Amesema Abuu Qilaba: Na ameanza na familia, kisha akasema Abuu Qilaba: Na ni mtu gani mwenye malipo bora kuliko yule anayetoa kwa familia yake wakiwa wadogo, akawazuia na machafu au akawanufaisha Mwenyezi Mungu kupitia hicho na akawatosheleza.
Imepokelewa Imamu MuslimAlieleza Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, aina za matumizi, na akazipanga pale panapokuwa na namna nyingi za kutoa matumizi kulingana na kile ambacho ni wajibu zaidi kwako, hivyo alianza na muhimu zaidi na kisha muhimu zaidi. Akaeleza kuwa mali yenye malipo mengi ni ile anayoitoa muislamu kwa wale anaolazimika kuwahudumia; kwanzia mkewe na watoto, kisha kutoa katika kipando kilichoandaliwa kwa ajili vita katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha kuwahudumia jamaa zake na rafiki zake wanapokuwa Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo, amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ndoto hiyo na aisimulie, na akiota ndoto kinyume na hiyo katika yale anayoyachukia, basi ndoto hiyo inatokana na Shetani, basi aombe kinga kutokana na shari yake, na wala asiisimulie kwa yeyote, kwani haitomdhuru".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAmeeleza Mtume rehema amani ziwe juu yake kuwa ndoto njema yenye kufurahisha usingizini hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na akaeleza amshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo, na akiota yanayomchukiza na kumhuzunisha basi hayo yanatokana na Shetani; aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na wala asimsimulie yeyote; kwani ndoto hiyo haitomdhuru, kwani Mwenyezi Mungu ameyafanya hayo yaliyotajwa kuwa ni sababu ya kusalimika na kero zinazoambatana na ndoto.
Kutoka kwa Suhaib -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini, akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake."
Imepokelewa Imamu MuslimAnastaajabu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, jambo na hali za muumini kwa namna ya kufurahishwa; Hii ni kwa sababu hali zake zote ni kheri, na sivyo hivyo kwa yeyote isipokuwa Muumini. Mambo mazuri yakimpata, anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo, analipwa kwa kushukuru. Ukimpata msiba husubiri na hutaraji malipo kwa Mwenyezi Mungu, na hupata malipo ya subira, hivyo anakuwa katika malipo kwa kila hali.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza sauti yake.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadAlikuwa rehema na amani ziwe juu yake anapopiga chafya: Jambo la kwanza: Anaweka mkono wake, au nguo yake juu ya kinywa chake; Kisije kutoka kinywani mwake au puani mwake chochote kitakachomuudhi aliyekaa naye. Jambo la pili: Anashusha sauti yake na wala hainyanyui.
Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Je nisikuelezeni kwa kile ambacho ninakiogopea zaidi kwenu nyinyi kuliko hata masihi dajali? Wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: Ni shirki iliyofichikana, anasimama mtu kuswali anapendezesha swala yake kwakuwa anaona kuna mtu anamtazama".
Imepokelewa na Ibnu MaajahWalikuwa maswahaba wakikumbushana fitina ya masihi dajali na wakiogopeshana juu yake, akawaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa kuna jambo la haramu analowaogopea kuliko hata hofu ya fitina ya masihi dajali, nayo ni shirki katika nia na makusudio ambayo haionekani kwa watu, kisha akalifasiri hilo kwa kuyafanya vizuri matendo ambayo hutafutiwa kwayo radhi za Mwenyezi Mungu kwaajili ya kuwaonyesha watu.
Kutoka kwa Osama bin Zaidi radhi za Allah ziwe juu yake: Aliambiwa: Je, huingii kwa Othman uzungumze naye? Akasema: Hivi mnadhani kuwa mimi siwezi kumsemesha jambo mpaka nanyi msikie? Wallahi nimekwishamsemesha kwa mambo yaliyo kati yangu na yeye, na wala sitaki kufungua jambo ambalo sihitaji kuwa wa mwanzo kulifungua, na wala sitaki kumueleza yeyote awe kiongozi kwangu: Hakika yeye ni kiongozi baada yakuwa nimemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Ataletwa mtu siku ya Kiyama, kisha atupwe motoni, ujiviringishe utumbo na vyote vilivyomo tumboni mwake, atazunguka nao (motoni) kama punda anavyozunguka na jiwe la kusagia nafaka, watamkusanyikia watu wa motoni, watamuuliza: We fulani umepatwa na nini? Hivi si ni wewe ulikuwa ukituamrisha mema na kutukataza maovu? Atasema: Ndiyo ni mimi, ila nilikuwa nikiamrisha mema wala siyafanyi, na nikikataza maovu ninayafanya".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliambiwa Osama bin Zaid Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili: Hivi huendi kwa Othman bin Affan, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, ukamwambia kuhusu fitina zilizotokea baina ya watu na kutafuta kuzizima. Basi akawaeleza kuwa alizungumza naye kwa siri ili kutafuta maslahi, si kuchochea kwa fitina, na lengo lake lilikuwa kwamba hataki kuwashutumu viongozi hadharani, ikawa ni sababu ya kurefusha mzozo kwa kiongozi, na ni mlango wa fitina na uovu, na siwezi kuwa wa kwanza kuufungua. Kisha Osama Mwenyezi Mungu awawie radhi, akasema kuwa: Anawanasihi viongozi kwa siri na wala hambembelezi yeyote kwa kumsifu, hata akiwa kiongozi, na wala hawabembelezi kwa kuwasifu kwa uongo, na hiyo ni baada ya yeye kuwa alisikia kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ataletwa mtu Siku ya Kiyama na kutupwa Motoni, na utumbo wake utatoka nje ya tumbo lake kutokana na ukali wa adhabu, na atasokota utumbo wake katika hali hii Motoni kama punda anayezunguka jiwe lake la kusagia nafaka, watu wa Motoni watamzunguka kwa duara kisha watamuuliza: Ewe fulani, je si wewe aliyekuwa ukiamrisha mema na kukataza maovu?! Atasema: Mimi nilikuwa nikiamrisha mema na wala siyafanyi, na ninakataza maovu na ninayafanya.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Atakaye walea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya Kiyama mimi na yeye (Namna hii)" Na akaviunganisha vidole vyake viwili.
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayeruzukiwa mabinti wawili au dada wawili, akawasimamia katika mahitaji na malezi na kuwaelekeza katika kheri na kuwatahadharisha na shari na mfano wa hayo mpaka wakakua na kubalehe; atakuja siku ya Kiyama akiwa yeye na Mtume rehema na amani ziwe juu yake mfano wa hivi viwili, akaunganisha vidole vyake viwili, kidole cha shahada na cha kati.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -sala na amani ziwe juu yake-: "Hamtoingia peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, je nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? toleaneni salamu kwa wingi kati yenu".
Imepokelewa Imamu MuslimAmebainisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake yakuwa hatoingia peponi ila muumini, na wala haikamiliki imani na wala haitengemai hali ya jamii ya kiislamu mpaka wapendane baina yao. Kisha akaelekeza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake katika jambo muhimu zaidi ambalo litaleta mapenzi kwa wote, nalo ni waislamu kutoleana salam baina yao, aliyoifanya Mwenyezi Mungu kuwa ni salam kwa waja wake.