





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Je, nisiwaambieni matendo bora zaidi kwenu, na masafi zaidi mbele ya Mfalme wenu, na yatakayo kunyanyueni juu zaidi katika daraja zenu, na bora kwenu kuliko kutoa dhahabu na pesa, na bora kwenu kuliko hata kukutana na adui yenu na mkapiga shingo zao na wakapiga shingo zenu?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: “Ni kumtaja Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadMaswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hivi je mnata nikuelezeni na nikufundisheni amali bora zaidi kuliko zote katika amali zenu, na yenye utukufu kuliko zote na yenye kukua zaidi na safi zaidi na takatifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu Mfalme Aliyetukuka? na yenye nafasi ya juu zaidi katika nafasi zenu za peponi? na ambayo ni bora zaidi kwenu kuliko kutoa sadaka ya Dhahabu na fedha? na bora kwenu kuliko hata kukutana na makafiri vitani, mkapiga shingo zao, na wakapiga shingo zenu? Maswahaba wakasema: Ndio tunalitaka hilo. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ni kumtaja Mwenyezi Mungu katika nyakati zote na katika mikao yote na hali zote.
Kutoka kwa Salmaani bin Swurad -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa nimekaa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kukawa na watu wawili wakitukanana, mmoja wao uso wake ulikuwa mwekundu (kwa hasira) na ikavimba mishipa yake ya shingo, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata" Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani", akasema: Hivi mimi ninawendawazimu?
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeWalitukanana na kushutumiana watu wawili mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na ukawa mwekundu uso wa mmoja wao na ikavimba mishipa inayozunguka shingo yake. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi ninajua neno ambalo lau angelisema huyu aliyekasirika basi hasira zingemuondokea, lau angesema: Audhubillaahi mina sh-shaitwanir rajiim - Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa. Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jilinde kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani. Akasema: Hivi mimi ni mwendawazimu?! Alidhania kuwa hajilindi na Shetani isipokuwa mwenye wazimu.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Katada -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Ndoto njema hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ndoto mbaya hutoka kwa Shetani, atakapoota mmoja wenu ndoto mbaya anayoiogopa basi na ateme kushotoni kwake, na aombe ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari zake, kwani ndoto hiyo haitomdhuru".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ndoto nzuri yenye kufurahisha usingizini hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mtu kuota anayoyachukia na kumhuzunisha hutoka kwa Shetani. Atakayeota yanayomchukiza basi ateme kushotoni kwake, na aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake; kwani haitomdhuru, kiasi ambacho Mwenyezi Mungu amefanya hayo yaliyotajwa kuwa ni sababu ya kusalimika na hayo yenye kuchukiza yanayoambatana na ndoto.
Kutoka kwa Ukba bin Aamir Al-Juhaniy -radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kunusurika? Akasema: "Shika ulimi wako, na ikutoshe nyumba yako, na lia kwa ajili ya makosa yako".
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadUkba bin Aamiri alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu sababu za muumini kuokoka katika dunia na Akhera? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Shikamana na mambo matatu: La kwanza: Hifadhi ulimi wako katika yale yasiyokuwa na kheri ndani yake, na kuzungumza kila shari, na usitamke ila la kheri. La pili: Baki nyumbani kwako ili umuabudu Mwenyezi Mungu katika nyakati za faragha, na ujishughulishe na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ibada, na jitenge nyumbani kwako na fitina. La tatu: Lia na ujute na utubie kwa yale uliyoyatenda katika madhambi.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba mtu wa kijijini alimjia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema: Nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia peponi. Akasema: "Umuabudu Mwenyezi Mungu na wala usimshirikishe na chochote, na usimamishe swala na utoe zaka ya wajibu, na ufunge mwezi wa ramadhani" Akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, sitozidisha zaidi ya hapo, basi alipoondoka, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayependezwa na kumtazama mtu miongoni mwa watu wa peponi basi na amtazame huyu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuja mtu mmoja miongoni mwa watu wa vijijini kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili amjulishe kuhusu amali itakayomuingiza peponi, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamjibu kuwa kuingia peponi na kuokoka na moto yote haya yanasimama katika nguzo za Uislamu, kuanzia kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na usimshirikishe na kitu chochote katika ibada. Na usimamishe swala tano alizoziwajibisha Mwenyezi Mungu kwa waja wake katika kila usiku na mchana. Na utoe zaka ya mali aliyoiwajibisha Mwenyezi Mungu juu yako, na uitoe kuwapa wastahiki wake. Na uhifadhi na kudumu nayo swaumu ya ramadhani katika wakati wake. Yule bwana akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, sitozidisha chochote zaidi ya amali hizo za faradhi nilizozisikia toka kwako katika ibada, na wala sitopunza chochote katika hizo. Alipoondoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Yeyote atakayependezwa na kumuangalia mtu miongoni mwa watu wa peponi basi na amtazame bedui (Mtu wa kijijini) huyu.
Kutoka kwa Sahli bin Sa'di Assaaidiy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yake mbele ya Allah mtukufu basi kafiri asingekunywa fundo moja la maji".
Imepokelewa na Imamu TirmidhiyKatika hadithi kumebainishwa udhalili wa Dunia kwa Mwenyezi Mungu -Mtukufu- nakuwa haina thamani, na lau ingekuwa hata na thamani ndogo zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi asingemnywesha kafiri hata funda moja ya maji, achilia mbali kule kuneemeka kwake nayo na kustareheka na mambo yake mazuri, Hivyo ikawa dunia ni dhalili mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, tofauti na Akhera, kwani hiyo ni nyumba ya neema za kudumu kwa watu wenye imani na ni maalumu kwaajili yao kinyume na makafiri, hivyo inawapasa watu wenye imani wajue uhalisia wa hii dunia na wasiiegemee, kwani ni nyumba ya kupita na si nyumba ya kudumu, wachukue ndani yake yale yatakayowasidia Akhera ambayo ndiyo nyumba ya kudumu. Amesema Mtukufu: "Na hakuna chochote mlichopewa basi hicho ni starehe ya dunia na pambo lake, na yaliyo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo bora na ni yenye kubakia, hivi hamzingatii, hivi kwani tuliyemuahidi ahadi nzuri naye atakutana nayo anaweza kuwa sawa na tuliyemstarehesha starehe za maisha ya dunia kisha yeye siku ya kiyama atakuwa ni miongoni mwa wenye kuhudhurishwa".
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), atakayewakuta wazazi wake wawili wakati wa utuuzima, mmoja wao au wote wawili, na akawa hakuingia peponi".
Imepokelewa Imamu MuslimMtume rehema na amani ziwe juu yake aliomba dua ya udhalili na fedheha mpaka akahisi kana kwamba mtu ametia pua yake kwenye mchanga – akarudia mara tatu – akaulizwa: Ni nani huyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, uliyemuombea dua mbaya? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Atakayewakuta wazazi wake wawili, mmoja wao au wote wawili, wakati wa utuuzima, wakawa si sababu ya yeye kuingia Peponi; na hii ni kutokana na kukosa kuwatendea wema na kutowatii.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akitembea katika njia ya kuelekea Makka, akapita karibu na mlima Jumdan, akasema: “Tembeeni huu ni mlima Jumdan, Wamepata ushindi wenye kujitenga” Wakasema: Ni akina nani hao wenye kujitenga ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Ni wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi katika Wanaume, na wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi katika wanawake.”
Imepokelewa Imamu MuslimMtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza nafasi ya wale wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na kwamba wao ni wa kipekee na wametangulia wengine katika kufikia daraja za juu katika Bustani za neema, na akawafananisha na mlima Jumdan ambao ni wa kipekee ukilinganisha na milima mingine.
Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Macho ya aina mbili hautoyagusa moto: Jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, na jicho lililokesha likilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa na Imamu TirmidhiyMaana ya hadithi: Nikuwa moto hautogusa jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo pindi anapokumbuka mtu ukubwa wa Mwenyezi Mungu na uwezo wake juu ya waja wake na uzembe wake katika haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu; akalia kwa kutaraji rehema zake na kuogopa adhabu zake na hasira zake, basi huyu kaahidiwa kusalimika na moto. Na jicho jingine ambalo moto hautoligusa, nalo ni: Yule atakayelala akilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu katika mipaka au sehemu ya mapigano kwa kuhifadhi roho za waislamu. Na kauli yake: "Hautoyagusa moto" Hii ni katika sehemu ya kutaja sehemu ya kitu na makusudio yake ni chote: nakuwa atakayelia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu na atakayelala akilinda katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anaiharamisha miili yao katika moto.