





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kusema kwangu: Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allaahu Akbaru, kunapendeka sana kwangu kuliko vitu vyote vilizochomozewa na jua".
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kumtaja Allah Mtukufu kwa maneno haya matukufu ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na utajo huo ni kusema: "Sub-haana llaah": Ni kumtakasa Mwenyezi Mungu kutokana na mapungufu. "Alhamdulillaah": Ni kumsifia kwa sifa za ukamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza. "Laa ilaaha illa llaah": Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. "Allaahu Akbaru: Mkubwa na Mtukufu kuliko kila kitu.
Imepokewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Tulikuwa kwa Omari akasema: "Tumekatazwa kujilazimisha".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAnaeleza Omari -Radhi za Allaha ziwe juu yake- kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwakataza kuyafanya mambo yenye uzito bila kuwa na haja nayo, sawa sawa iwe ni kauli au kitendo.
Kutoka kwa Omari bin Abii Salama -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa kijana mdogo ndani ya nyumba ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na mkono wangu ulikuwa ukizunguka huku na kule katika sahani (ya chakula), akasema kuniambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: " Ewe kijana, mtaje Mwenyezi Mungu, na kula kwa mkono wako wa kulia, na kula kile kinachokuelekea" Ulibakia kuwa ndio ulaji wangu huo hata baada yake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Omari bin Abii Salama -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-, huyu ni mtoto wa mke wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Ummu Salama -Radhi za Allah ziwe juu yake-, na alikuwa chini ya malezi yake na usimamizi wake, kwamba yeye alikuwa wakati wa kula akihamisha mkono wake katika pande zote za chombo ili achukue chakula, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamfundisha adabu tatu miongoni mwa adabu za kula. Adabu ya kwanza: Kusema: "Bismillah" Mwanzo wa kula. Ya pili: Kula kwa mkono wa kulia. Ya tatu: Kula upande ulio karibu naye katika chakula.
Na imepokewa kutoka kwa bin Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake - amesema: "Atakapo kula mmoja wenu basi na ale kwa mkono wake wa kulia, na atakapo kunywa basi na anywe kwa mkono wake wa kulia, kwani Shetani anakula kwa mkono wake wa kushoto, na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto".
Imepokelewa Imamu MuslimAnamuamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- muislamu ale na anywe kwa mkono wake wa kulia, na anakataza kula na kunywa kwa mkono wa kushoto; na hii ni kwa sababu Shetani anakula na anakunywa kwa kushoto.
Kutoka kwa Al-Abbasi bin Abdil Muttwalib radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nifundishe kitu nitakachomuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu. Akasema: "Muombe Allah afya", nikakaa siku kadhaa kisha nikarudi, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nifundishe kitu ambacho nitamuomba Mwenyezi Mungu. Akasema kuniambia: "Ewe Abbasi, ewe ami yake na Mjume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya katika Dunia na Akhera".
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadAmi yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake Al-Abbas bin Abdul Muttalib Allah amuwie radhi alimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amfundishe dua ya kumuomba Mwenyezi Mungu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamfundisha amuombe Mwenyezi Mungu afya njema na salama kutokana na balaa na kasoro za Dini, Dunia na Akhera, akasema: Baada ya siku chache nikarejea kwake rehema na amani ziwe juu yake kwa mara nyingine tena nikimuomba anifundishe dua nimuombe Mwenyezi Mungu, akasema rehema na amani ziwe juu yake akimwambia kwa mapenzi na upole: Ewe Abbas, ewe ami wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya aondoe madhara yote na alete kheri na manufaa katika Dunia na Akhera.
Imesimuliwa kutoka kwa Abdul-Rahman bin Abi Laila, kuwa, siku moja walikuwa kwa Hudhaifa, akaomba maji, Mmajusi mmoja akampa kitu cha kunywa, alipokiweka kikombe mkononi mwake, akakitupa, na akasema: Kwani si nilishamkataza zaidi ya mara moja au mbili - kana kwamba anasema: Sikufanya hivi kwa matashi yangu - bali nilimsikia Mtume, rehema na amani ziwe juu yake akisema: “Msivae hariri wala dibaji (Sufi) wala msinywe katika vyombo vya dhahabu au vya fedha, wala msile katika vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu na fedha, kwani ni vyao (Makafiri) katika dunia na sisi ni vyetu Akhera."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume, Rehema na Amani zimshukie, amekataza wanaume kuvaa hariri za kila aina. Aliwakataza wanaume na wanawake kula na kunywa katika vyombo vya dhahabu na fedha. Akasema kuwa ni kwa ajili ya waumini tu Siku ya Kiyama; Kwa sababu waliviepuka katika ulimwengu huu kwa kumtii Mwenyezi Mungu, Ama makafiri wao si vyao huko akhera. Kwa sababu waliharakisha vizuri vyao katika maisha yao ya dunia kwa kuvitumia, na kuasi kwao amri ya Mwenyezi Mungu.
Imepokelewa kutoka kwa Omari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanaume yeyote atakayevaa hariri duniani hatovaa Akhera endapo hatotubia, na hii ni adhabu kwake.
Kutoka kwa Abuu Said Al-Khudri amesema: Muawia alitoka kwenda msikitini akakuta kundi, akasema: Nini kimewakalisha hapa? Wakasema: Tumekaa tukimkumbuka Mwenyezi Mungu. Akasema: Mnamuapa Mwenyezi Mungu kuwa hakuna lililowakalisha isipokuwa hilo? Wakasema: Wallahi hakuna lililotukalisha isipokuwa hilo. Akasema: Basi tambueni kuwa sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu kwa lolote, na hakuna aliyekuwa katika nafasi yangu kwakuwa na mazungumzo machache zaidi kuliko mimi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: Na hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, siku moja alitoka kwenda katika kundi la Maswahaba zake na kusema: “Mbona mmekaa pamoja?” Wakasema: Tumekaa tukimkumbuka Mwenyezi Mungu na kumhimidi kwa kuwa ametuongoza kwenye Uislamu, na kwa kutujaalia. Akasema: “Mnamuapa Mwenyezi Mungu kuwa hakuna lililokukalisheni isipokuwa hilo?" Wakasema: "Wallahi hatukukaa kwa lolote ila hilo.” Akasema: «Ama mimi sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu, lakini Jibril alinijia na kuniambia kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anajifaharisha kupitia nyinyi, huko kwa Malaika.!"
Imepokelewa Imamu MuslimAlitoka Muawia bin Abi Sufian, Mwenyezi Mungu awawie radhi, kwenda katika kundi moja msikitini na akawauliza wamekusanyika kwa jambo gani, Wakasema: Tunamtaja Mwenyezi Mungu, basi akawaapisha, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kwamba hawakutaka katika kikao chao na mkusanyiko wao isipokuwa ni kumtaja Mwenyezi Mungu, wakaapa kwa hilo, kisha akawaambia: Sikukuapisheni kwa tuhuma yoyote juu yenu au kuwa na shaka juu ya ukweli wenu, kisha akaeleza kuhusu hali yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba hakuna aliyekuwa karibu naye kuliko yeye. Kwa sababu Ummu Habiba alikuwa ni dada yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwa sababu alikuwa ni miongoni mwa waandishi wa wahyi, lakini ilikuwa ni nadra sana kusimulia hadithi, Basi akawaambia kuwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, siku moja alitoka nyumbani kwake na akawakuta wamekaa msikitini wakimdhukuru Mwenyezi Mungu na kumhimidi kwa yale aliyowaongoza katika Uislamu na kuwakirimia. Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, akawauliza na kuwaapisha sawa na alivyofanya Muawia kwa jamaa zake, Mwenyezi Mungu amuwie radhi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaambia kuhusu sababu ya kuwauliza kwake na kuapa kwao: kwamba Malaika Jibril, amani iwe juu yake, alimjia na kumwambia kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anajifakhirisha kupitia nyinyi kwa Malaika, na anawadhihirishia ubora wenu na anawaonyesha uzuri wa amali yenu, na anakusifieni mbele yao.
Kutoka kwa Abdillahi bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Yakwamba Omar bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Je anaweza kulala mmoja wetu akiwa na janaba? Akasema: "Ndiyo, atakapotawadha mmoja wenu basi na alale"
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAlimuuliza Omar bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ikiwa mmoja wao atapatwa na janaba mwanzoni mwa usiku, kwa kumuingilia mke wake hata kama hakumwaga au akajiotea, Je alale nayeye akiwa na janaba? Akawaruhusu -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa hilo, kwa kupunguza hadathi (uchafu) huu mkubwa kwa udhu wa kisheria; na hapo haina tatizo mtu kulala na janaba.