





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Anas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake hadithi Marfu'u: "Yeyote atakayetoka katika kutafuta elimu basi huyo yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka atakaporejea".
Imepokelewa na Imamu TirmidhiyMaana ya hadithi: Nikuwa atakayetoka nyumbani kwake au katika mji wake; kwaajili ya kutafuta elimu ya kisheria,huyo anakuwa katika hukumu ya aliyetoka kwaajili ya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu,mpaka atakaporudi kwa watu wake; kwasababu anakuwa ni kama mpiganaji katika kuihuisha kwake dini na kumdhalilisha shetani na kuitaabisha nafsi.
Kutoka kwa Abuu Dharri, Jundubi bin Junada, na Abuu Abdulrahman, Muadhi bin Jabali radhi za Allah ziwe juu yao kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Mche Mwenyezi Mungu popote ulipo, na ovu lifuatishe jema litalifuta, na ishi na watu kwa tabia njema"
Imepokelewa Imamu TirmidhiyAmeamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo matatu: La kwanza: Kumuogopa Mwenyezi Mungu na hii inakuwa kwa kutekeleza wajibu, na kuacha maharamisho, katika kila mahali na nyakati na hali, katika siri na wazi, na wakati wa afya na balaa na mengineyo. La pili: Ukiangukia katika ovu, basi fanya baada yake jambo jema kama swala na sadaka na wema na kuunga udugu na toba na mengineyo, kwani hayo hufuta madhambi. La tatu: Ishi na watu kwa tabia njema, kama kutabasamu katika nyuso zao, na upole na ulaini na kutenda wema na kuacha maudhi.
Imepokewa Kutoka kwa Abii Bakra -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji na muuliwaji wote motoni" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu huyu muuaji anaeleweka, na vipi kuhusu muuliwaji? Akasema: "Hata yeye alikuwa na pupa ya kumuuwa mwenzake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, akiwa na dhamira kila mmoja wao ya kummaliza mwenzake; Basi muuaji motoni kwa sababu ya kutekeleza mauaji ya kumuua mwenzake, Kuhusu muuliwaji, hilo likamtatiza Swahaba: Ni vipi anakuwa motoni? Akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hata yeye pia anakuwa motoni kwa sababu ya pupa yake ya kumuua mwenzake, na hakikumzuia kuuwa zaidi ya muuaji kumuwahi na kummaliza.
Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia, atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, (basi malipo yake yatakuwa) ni kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya kuipata dunia, au kwa ajili ya mwanamke atakaemuoa, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kile alichokiendea." Na lafudhi ya Bukhari: ""Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yote huzingatiwa nia, na hukumu hii ni ya ujumla katika amali zote, kwanzia ibada na miamala, atakaye kusudia kupata masilahi katika amali yake hatopata zaidi ya masilahi na wala hatopata thawabu, na atakayekusudia katika amali yake kujiweka karibu na Allah Mtukufu, atapata thawabu na malipo kupitia amali yake hata kama litakuwa ni jambo la kawaida, kama kula na kunywa. Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga mfano wa kuweka wazi namna gani nia inaathiri matendo pamoja nakuwa huonekana yote yako sawa katika muonekano wa juu, akaweka wazi kuwa atakayekusudia katika kuhama kwake na kuacha nchi yake ni kutafuta radhi za Mola wake, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kisheria na kunakubalika, atalipwa kwa sababu ya ukweli wa nia yake, na atakayekusudia kwa kuhama kwake ni kupata masilahi ya kidunia, kama mali, au cheo, au mke, basi hatopata kwa kuhama kwake huko zaidi ya manufaa aliyoyakusudia, na wala hatokuwa na fungu la malipo na thawabu.
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba mtu mmoja alisema kumwambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Niusie, akasema: " Usikasirike" Akarudia mara kadhaa, akasema: "Usikasirike".
Imepokelewa na Al-BukhaariyMmoja kati ya Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- alimuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amjulishe katika jambo litakalomnufaisha, akamuamrisha asikasirike, na maana ya hapa nikuwa aziepuke sababu zinazoweza kumpelekea katika kukasirika, na aidhibiti nafsi yake na hasira zinapompata, asiendelee na hasira zake mpaka kufikia kuuwa au kupiga au kutoa matusi na mfano wa hayo. Na yule bwana akarejea tena kuomba usia mara kadhaa, hakumzidishia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika usia zaidi ya "Usikasirike"
imepokewa Kutoka kwa Omari bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Hakika yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyomruzuku ndege, anatoka asubuhi akiwa na njaa anarudi mchana akiwa kashiba".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadAnatuhimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuleta manufaa na kuzuia madhara katika mambo ya Dunia na Akhera, kwani hakuna yeyote mwenye kutoa wala kunyima wala kudhuru wala kunufaisha isipokuwa Yeye Aliyetakasika na Kutukuka, Na tufanye sababu zinazoleta manufaa na kuzuia madhara, pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa dhati, wakati wowote tutakapofanya hivyo, Mwenyezi Mungu ataturuzuku kama anavyowaruzuku ndege wanaotoka asubuhi wakiwa na njaa, kisha wanarudi jioni matumbo yakiwa yamejaa, na kitendo hiki kwa ndege ni aina ya kufanya sababu za kutafuta riziki, bila kubweteka wala uvivu.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, katika yale anayoyasimulia kutoka kwa Mola wake Mtukufu, amesema: "Mja alifanya dhambi akasema: Ee Mola wangu nisamehe dhambi yangu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, na humsitiri kwa ndambi hiyo au humuadhibu kwa kutenda dhambi, kisha akarudi tena akatenda dhambi, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe dhambi yangu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, na ana adhibu kwa kutenda dhambi, fanya utakavyo nimekusamehe".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnasimulia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mola wake Mlezi ya kwamba mja anapofanya dhambi kisha akasema: Ewe Mola wangu nisamehe dhambi yangu, Mwenyezi Mungu husema: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, akamsitiri na akamsamehe, au akamuadhibu, basi hakika nimemsamehe. Kisha mja akarudi akafanya dhambi, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe dhambi yangu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, akamsitiri na akamsamehe, au akamuadhibu, basi kwa hilo nimemsamehe mja wangu. Kisha mja akarudi akafanya dhambi, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe dhambi langu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, akamsitiri na akamsamehe, au akamuadhibu, basi kwa hilo nimemsamehe mja wangu, afanye atakavyo madamu kila anapofanya dhambi analiacha na anajuta na anaazimia kutolirudia dhambi hilo mara nyingine, madamu ataendelea kufanya hivi, anatenda dhambi na anatubia nitaendelea kumsamehe, kwani toba hubomoa yaliyo kabla yake.
Imepokewa kutoka kwa Abdullahi bin Amry -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika waadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika mimbari za nuru, kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake yote miwili ni kulia , wale wanaofanya uadilifu katika hukumu zao na familia zao, na vile wanavyovitawala"
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wanaohukumu kwa uadilifu na haki baina ya watu walio chini ya utawala wao na hukumu zao, na familia zao, nikuwa watakaa katika makao ya juu zaidi yaliyoumbwa kwa nuru, ikiwa ni takrima kwao siku ya Kiyama. Na mimbari hizi ziko kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake miwili Mtukufu yote ni kulia.
Imepokelewa kutoka kwa Othman -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mwenye kunyimwa upole basi kanyimwa kheri yote"
Imepokelewa Imamu MuslimAnatueleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kunyimwa upole akawa hakuafikishwa katika mambo ya dini na dunia, na katika mambo yake mwenyewe, na yale anayoyafanya na wengine, basi atakuwa kanyimwa kheri yote.