





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abuu Dardai -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu na swala na sadaka?" Wakasema: Tueleze, akasema: "Kusuluhisha kati ya watu, kwani kuharibika kwa mahusiano baina ya watu hilo hunyoa".
Imepokelewa na Abu Daud na TirmidhiyAliwauliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake: Je, nikuelezeni lililo bora kuliko kuzidisha ibada za sunna kama swaumu na swala na sadaka? Wakasema: Ndio. Akasema: Ni kuwapatanisha waliogombana kwani ugomvi huleta mfarakano na kujitenga na kuchukiana na kupeana migongo kati ya watu, kwani yanayoambatana na kuharibika kwa mahusiano baina ya watu miongoni mwa chuki ndio jambo ambalo katika tabia zake huangamiza na kuing'oa dini na dunia kama wembe unavyong'oa nywele.
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema: "Gaweni mirathi kwa wastahiki wake, itakayobakia basi mwenye kustahiki zaidi upande wa mwanaume ni wa kiume".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wenye kusimamia ugawaji wa mirathi wazigawe kwa wastahiki wake kwa mgao wa uadilifu wa kisheria kama alivyotaka Mwenyezi Mungu Mtukufu, ataanza kwa kuwapa wale wenye fungu lililokadiriwa tayari kisheria, kulingana na mafungu yao katika kitabu cha Mwenyezi Mungu, nayo ni: Theluthi mbili, na theluthi moja, na sudusu (moja ya sita) na nusu, na robo, thumunu (moja ya nane), mali itakayobakia baada ya hapo, hiyo atapewa ndugu wa karibu na maiti katika wanaume, na ndugu hao huitwa aswaba (warithi wasio na mipaka).
Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwizi unakatwa mkono wake kwa kuiba robo Dinari ya dhahabu, na zaidi ya hapo, na kiwango chake kinalingana na kiasi cha Gramu 1.06 ya dhahabu.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hapigwi mtu zaidi ya viboko kumi isipokuwa kama itakuwa katika kutelekeza sheria miongoni mwa sharia za Mwenyezi Mungu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kupigwa mtu yeyote zaidi ya viboko kumi isipokuwa katika maasi, na pia hakuna maelekezo yoyote yaliyokuja katika sheria kueleza idadi maalumu ya viboko au kipigo au adhabu maalumu, na makusudio yake haizidishwi katika kipigo cha kuadabisha zaidi ya viboko kumi, kama kumpiga mke au mtoto.
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayefuga mbwa isipokuwa mbwa wa mawindo au wa mifugo, basi yatapungua katika matendo yake kila siku kiratu (shehena) mbili", Amesema Salim: Na alikuwa Abuu Huraira akisema: "Au mbwa wa shamba", Naye akawa na shamba.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmetahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufuga mbwa, isipokuwa kwa haja ya kuwinda, au kulinda mifugo na mazao, na atakayemfuga pasina haja hizo zitapungua katika thawabu za matendo yake kila siku shehena mbili; ambazo ujazo wake unajulikana mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia msikitini kisha akaingia mtu mmoja, akaswali, kisha akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akajibu salamu, na akasema: "Rudi kaswali, kwani wewe hujaswali", akarudia kuswali kama alivyoswali mwanzo, kisha akaja, akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Rudi kaswali kwani wewe hujaswali" (akafanya hivyo) Mara tatu, akasema: "Namuapa yule aliyekutuma kwa haki, siwezi kuswali vizuri zaidi ya hivyo, basi naomba nifundishe, akasema: "Utakaposimama katika swala basi toa takbira (sema: Allaahu Akbaru), kisha soma kiasi chepesi ulichonacho katika Qur'ani, kisha rukuu mpaka utulizane ukiwa umerukuu, kisha nyanyuka mpaka ulingane wima, kisha sujudu mpaka utulizane ukiwa umesujudu, kisha nyanyuka mpaka utulizane ukiwa umekaa, na ufanye hivyo katika swala yako yote".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake msikitini, akaingia baada yake mtu mmoja akaswali rakaa mbili haraka haraka, na hakutulizana katika kisimamo chake na rukuu yake na sijida yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akimfuatilia katika swala yake, akaja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa kakaa pembezoni mwa msikiti, akamsalimia, akamjibu salamu, na akasema kumwabia: Nenda karudie swala; kwani wewe hujaswali. Akarudi na akaswali haraka kama alivyoswali mwanzo, kisha akaja akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema kuwambia: Rudi kaswali; kwani wewe hujaswali, alifanya hivyo mara tatu. Yule bwana akasema: Namuapa yule aliyekutuma kwa haki, siwezi kufanya vizuri zaidi ya hivyo, basi nifundishe, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Utakaposimama katika swala basi toa takbira ya kuhirimia swala, kisha soma mama wa Qur'ani (Suratul-Faatiha) na kile atakachotaka Mwenyezi Mungu ukisome, kisha rukuu mpaka utulizane ukiwa umerukuu kwa kuweka viganja vyako juu ya magoti yako na unyooshe mgongo wako na umakinike katika rukuu yako, kisha nyanyuka na unyooshe mgongo wako mpaka mifupa irudi katika viungo vyake na ulingane sawa ukiwa wima, kisha sujudu mpaka utulizane ukiwa umesujudu kwa kuliweka sawa paji la uso na pua, na mikono miwili na magoti mawili na ncha za vidole vya miguu miwili juu ya ardhi, kisha nyanyuka mpaka utulizane ukiwa umekaa kati ya sijida mbili, kisha fanya hivyo katika kila rakaa ndani ya swala yako.
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Pindi mja muislamu au muumini atakapotawadha akaosha uso wake, madhambi yake yote yanayotokana na kuangalia yanaondoka na tone la maji au tone la mwisho usoni mwake, akiosha mikono yake yanaondoka madhambi yote yatokanayo na mikono pamoja na tone la mwisho, akiosha miguu yake madhambi yote yatokanayo na kutembea yanaondoka na tone la mwisho, mpaka muislamu anabaki msafi hana madhambi".
Imepokelewa Imamu MuslimAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakapotawadha muislamu au muumini akaosha uso wake wakati wa udhu, yanatoka katika uso wake makosa yote madogo madogo aliyoyatazama kwa macho yake pamoja na maji ya yanayodondoka baada ya kuosha, au pamoja na tone la mwisho la maji, akiosha mikono yake yanatoka katika mikono yake makosa yote madogo madogo iliyoyachuma mikono yake au pamoja na tone la mwisho la maji, na akiosha miguu yake yanatoka makosa yake yote madogo madogo iliyotembea kuyafuata miguu yake, mpaka atoke akiwa kasafishika na madhambi madogo madogo kwa kumalizika kwa udhu.
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao (yeye na baba yake), amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitufundisha kutaka uchaguzi (kwa Mwenyezi Mungu) katika mambo yetu yote kama anavyotufundisha sura katika Qur'ani, Akisema: "Atakapo dhamiria mmoja wenu kufanya jambo, basi na aswali rakaa mbili zisizokuwa za faradhi, kisha aseme: 'Allahumma Inniy As-takhiiruka bi ilmika, wa astaq-diruka biqud-ratika wa as-aluka min fadhw-lika al-adhwiim, fa innaka taqdiru walaa aq-diru wata'alamu walaa a'alamu wa anta allaamul ghuyuub, Allahumma inkunta ta'alamu anna haadhal amru- na atataja jambo lenyewe -Khairun lii fii diiniy wadun-yaaya wamaashii wa aaqibatu amriy (Ajiluhuu wa Aajiluhu) Faq-dirhu lii wayassirhuu lii thumma baarik liiy fiihi, wa in kunta ta'alamu anna haadhal amru sharrun lii fii diiniy wa dun yaaya wa maashiy wa Aaqibatu Amriy Fas-rif-huu anniy was-rifniiy anhu waqdir liyal khaira haithu kaana thummar-dhinii bihi" Tafsiri: "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakutaka uchaguzi kupitia elimu yako, na ninakuomba uwezo kupitia uwezo wako, na ninakuomba unipe kutoka katika fadhila zako tukufu, kwani wewe unaweza na mimi siwezi, na unajua na mimi sijui na wewe ni mjuzi wa yaliyofichikana, Ewe Mola wangu ikiwa unajua kuwa jambo hili (Anataja shida yake) ni kheri kwangu katika dini yangu na dunia yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (iwe kwa haraka au kwa kuchelewa) basi nakuomba niwezeshe na unifanyie wepesi kwangu kisha unibariki mimi ndani ya jambo hili, Na ikiwa unajua kuwa jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu na dunia yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu, basi liepushe nami na uniepushe nalo, kisha nipangie heri mahala popote itakapokuwa kisha niridhishe nayo".
Imepokelewa na Al-BukhaariyMuislamu akitaka kufanya jambo katika mambo ambayo hayajulikani upande ulio sawa ndani yake, basi ni sheria kwake aswali swala ya Istikhaara (ya kuomba uamuzi) kiasi kwamba alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwafundisha Maswahaba zake radhi za Allah ziwe juu yao swala hii kama anavyowafundisha sura ndani ya Qur'ani, anaswali rakaa mbili zisizokuwa za faradhi kisha anamuomba Mwenyezi Mungu kwa kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba uchaguzi" Kwa kuomba uniongoze katika jambo lenye kheri zaidi baina ya mambo mawili, na ninakuomba "Kupitia elimu yako", pana iliyozingira kila kitu, "na ninakutaka kupitia uwezo wako", wenye kutekelezeka kwani wewe hakikushindi chochote, "na ninakuomba katika fadhila zako" na wema wako "mtukufu" mpana; kwani kipawa chako ni fadhila kutoka kwako, na hakuna yeyote mwenye haki yake juu ya neema; "kwani wewe unaweza" juu ya kila kitu, na mimi ni dhaifu nisiyejiweza "na wala siwezi" jambo lolote isipokuwa kwa msaada kutoka kwako, "na" wewe "unajua" kwa elimu iliyokusanya na kuvizingira vyote vyenye kuonekana na visivyoonekana, na kwa kheri na shari, "na" mimi "sijui" chochote isipokuwa kwa taufiki yako na uongofu wako, "na wewe ni Mjuzi wa mambo ya ghaibu" wewe unaelimu isiyokuwa na mipaka, na uwezo wenye kutendeka, na hakuna kwa lolote katika hayo kwa yeyote asiyekuwa wewe awezaye kufanya hayo, ila yale uliyoyapanga kwake na ukamuwezesha. Kisha muislamu atamuomba Mola wake Mlezi, na atataja haja yake, kwa kusema: " Ewe Mola wangu" hakika mimi nimekabidhi jambo kangu kwako, basi "ikiwa unajua" katika elimu yako kuwa jambo hili "hapa atalitaja" kwa mfano kama kununua nyumba, au kununua kwangu gari hili, au kumuoa kwangu mwanamke huyu au mengineyo.... Ikiwa jambo hili lilikwishatangulia katika elimu yako yakuwa ndani yake kuna "kheri kwangu katika dini yangu" ambayo ndiyo ngome ya jambo langu, "na maisha yangu" katika dunia yangu "na mwisho wa jambo langu" na hatima ya jambo langu, au alisema: "haraka ya jambo langu na kuchelewa kwake" katika dunia na Akhera; "liwezeshe" na uliandae na ulitimize "kwangu", na ulirahisishe "na ulifanye kuwa jepesi kwangu" "kisha libariki" na ukithirishe kheri "ndani yake kwangu", "na ikiwa unajua" ewe Allah "kuwa jambo hili" nililokuamba uamuzi kwalo "ni shari kwangu katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu -au alisema katika haraka ya jambo langu na kuchelewa kwake, basi liepusha nami na uniepushe nalo, na unikadirie kheri mahala popote itakapokuwa, kisha niridhishe nayo" na kwa hukumu zako zote ninazozipenda na ninazozichukia.
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake amesema-: "Ewe baba Saidi, yeyote atakayeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola, na Uislamu kuwa ndiyo dini, na Muhammadi kuwa ni Nabii, basi atakuwa kastahiki Pepo", Abuu Saidi likamshangaza sana hilo, akasema: Naomba uyarudie tena maneno hayo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akarudia, kisha akasema: "Na la mwisho mja ananyanyuliwa kwalo daraja katika Pepo, umbali ulio kati ya daraja mbili hizo ni kama baina ya mbingu na ardhi", Akasema: Ni lipi hilo ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa Imamu MuslimAlimueleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake kwamba yeyote atakayemuamini Mwenyezi Mungu na akamridhia kuwa Mola na Mungu na mmiliki na mtukufu na muamrishaji, na Uislamu kuwa ni dini, kwa kutii na kujisalimisha katika amri zake zote na makatazo yake yote, na Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kuwa ni Nabii, kwa yote aliyotumwa kwayo na akayafikisha; itamthibitikia kwake Pepo, Abuu Saidi akastaajabu radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Yarudie tena ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akafanya hivyo, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Na nina jambo jingine ambalo Mwenyezi Mungu Mtukufu humnyanyua mja daraja mia moja Peponi kwalo, masafa yaliyoko kati ya daraja mbili hizo ni kama umbali ulioko baina ya mbingu na ardhi, akasema Abuu Saidi: Na nilipi hilo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.