





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akifungua swala kwa takbira (Allaahu Akbaru) na kisomo kwa kuanza na Alhamdulillaahi Rabbil a'alamiin, na alikuwa anaporukuu hanyanyui wala hainamishi kichwa chake, lakini kati na kati, na alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu hasujudu mpaka alingane wima, na alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida hasujudu mpaka alingane sawa kwa kukaa, na alikuwa akisoma tahiyatu kila baada ya raka mbili, na alikuwa akiutandika mguu wake wa kushoto na kuusimamisha mguu wake wa kulia, na alikuwa akikataza mkao wa Shetani, na akikataza mtu kulaza mikono yake kama wanyama wakali, na alikuwa akihitimisha swala kwa salamu
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake sehemu ya swala ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba alikuwa akifungua swala yake kwa takbira ya kufungua swala, akisema: "Allaahu Akbaru", na akifungua kisomo kwa suratul Faatiha. "Alhamdulillaah Rabbil A''alamiin..." Na alikuwa anaporukuu baada ya kisimamo, hainui kichwa chake na wala hakishushi wakati wa rukuu, bali anakifanya kilingane sawa kikiwa kimenyooka, na akinyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu ananyooka wima kabla hajasujudu, na akinyanyua kichwa chake kutoka katika sijida ya kwanza, hasujudu sijida ya pili mpaka atuliazane akiwa amekaa. Na alikuwa akikaa baada ya kila rakaa mbili kwa ajili ya tahiyatu, na anasema: "Attahiyyatu lillaahi was swalawaatu wat twayyibaatu...", na alikuwa anapokaa baina ya sijida mbili au kwa ajili ya tahiyatu analaza mguu wake wa kushoto na kuukalia, na anasimamisha mguu wake wa kulia. Na anamkataza mwenye kuswali kukaa ndani ya swala yake kama mkao wa Shetani, nao ni kulaza miguu yake yote miwili katika Ardhi, na kukaa kwa pande zake mbili za nyuma, au kuambatanisha makalio yake na Ardhi na akasimamisha miguu yake na kuweka mikono yake katika Ardhi kama anavyoitandaza mbwa, au akalaza mwenye kuswali mikono yake kwa kuinyoosha katika sijida kama anavyoilaza mnyama mkali. Na alikuwa akihitimisha swala yake kwa salamu: "Assalaam alaikum warahmatullah" upande wa kulia mara moja na mara nyingine upande wa kushoto.
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake-: Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani za Allah ziwe juu yake akiwa juu ya mimbari, waonaje kuhusu swala za usiku, akasema: "Ni rakaa mbili mbili, atapochelea Alfajiri aswali rakaa moja, iwe ni witri kwa aliyo swali" na yeye alikuwa akisema: "Fanyeni swala yenu ya mwisho iwe ni witri", kwa hakika Mtume rehema na amani za Allah zimshukie kaamrisha hivyo.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye akiwa anahutubia juu ya Mimbari: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nifundishe ni namna gani nitaswali usiku?. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Utaswali na kutoa salamu katika kila rakaa mbili, ukihofia kuchomoza kwa Afajiri basi swali rakaa moja itakufanyia kuwa witiri rakaa zingine ulizoswali, na hakika yeye rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiusia kuifanya swala ya mwisho ya usiku kuwa ni witiri.
Kutoka kwa Ikrima: Ya kwamba Ally radhi za Allah ziwe juu yake aliwachoma watu fulani, zikamfikia taarifa Bin Abbas akasema: Lau ningelikuwa mimi nisingewachoma, kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Msiadhibu kwa adhabu ya Mwenyezi Mungu", na ningewaua tu kama alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayebadili dini yake basi muuweni".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAlijitahidi Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake akawachoma watu fulani kwa moto, miongoni mwa mazandiki walioritadi kutoka katika Uislamu, zikamfikia taarifa Abdallah bin Abbas radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, akamuunga mkono kwa kuwauwa kwake; lakini akakemea kuwachoma kwa moto. Na akasema: Lau ningelikuwa katika nafasi yake nisingeliwachoma kwa moto; kwa sababu yeye rehema na amani ziwe juu yake alibainisha kuwa haadhibu kwa moto isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa moto, lakini inatosha tu kuwauwa, kwani alisema rehema na amani ziwe juu yake: Atakayeritadi kutoka katika Uislamu na akabadili dini yake kwa dini nyingine basi muuweni.
Kutoka kwa Muadhi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi alipomuelekeza kwenda Yemen alimuamrisha achukue miongoni mwa ng'ombe katika kila thelathini ndama alianza kufuatana na ng'ombe wengine, wa kiume au kike, na katika kila arobaini mwenye miaka miwili, na kutoka kwa kila anayeishi humo asiye muislamu Dinari au kitu chenye thamani sawa na Dinari kama Maafiri, nazo ni nguo hutengenezwa Yemen.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadMtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma Muadhi bin Jabali radhi za Allah ziwe juu yake kwenda Yemen kwa ajili ya kuwafundisha watu na kuwafikishia ujumbe, na miongoni mwa yale aliyomuamrisha achukue kutoka kwa Waislamu zaka za ng'ombe zao katika kila ng'ombe thelathini achukue dume moja au ng'ombe aliyeanza kufuatana na wengine machungani; naye ni yule aliyetimiza mwaka moja, na katika kila ng'ombe arobaini achukue ng'ombe mkamilifu; naye ni yule aliyetimiza miaka miwili. Na achukue jizia (kodi) kutoka kwa watu wa kitabu, Mayahudi na Wakristo, kwa kila mwanaume aliyebalehe, Dinari, au kinacholingana na Dinari katika nguo za Yemen ziitwazo: Maafari.
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake -: Alikataza kula kila chenye meno ya chonge katika wanyama wanaoshambulia, na kila chenye mdomo wa chonge katika ndege.
Imepokelewa Imamu MuslimAlikataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kula kila chenye kuwinda katika wanyama wenye kushambulia, kinachowinda kwa meno ya mbele, na akakataza kula kila ndege anayekata na kukamata kwa mdomo wake.
Imepokelewa kutoka kwa Uqba bin Aamir -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kafara ya nadhiri ndio kafara ya kiapo".
Imepokelewa Imamu MuslimAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kafara ya kiapo cha jumla kisipoambatanishwa na kile anachokitaka au kukitaja: Ni kama kafara ya kiapo.
Kutoka kwa Safina radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kikimuosha kibaba cha maji kutokana na janaba, na ukimtia udhu ujazo wa kiganja.
Imepokelewa Imamu MuslimAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akioga kutokana na janaba kwa kiasi cha kibaba, na akitawadha kwa ujazo wa kiganja, na kibaba: Ni ujazo wa viganja vinne, na kiganja: Ni kiasi cha ujazo wa viganja viwili vya mtu wa maumbile ya kati na kati.
Kutoka kwa Ibrahim Nakhai kutoka kwa Hammamu bin Harithi amesema: Alikwenda haja ndogo Jariri kisha akatia udhu, na kafuta juu ya khufu zake, wakasema: Kwa nini unafanya hivi? Akasema: Ndio, Nilimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikidhi haja ndogo, kisha akatia udhu na kafuta juu ya khufu zake. Amesema A'mashi: Amesema Ibrahimu: Ilikuwa ikiwashangaza sana hadithi hii; kwa sababu kusilimu kwa Jariri kulikuwa baada ya kuteremka Suratul-Maaida.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikidhi haja ndogo Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake kisha akatawadha, na akatosheka na kufuta juu ya khofu zake na hakuosha miguu yake, wakasema kumwambia walioko nao: Mbona unafanya hivi?! Akasema: Ndio, nilimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikidhi haja ndogo, kisha akatawadha na akafuta juu ya khofu zake. Na Jariri alisilimu kwa kuchelewa baada ya kuteremka kwa suratul-Maaida ambayo ndani yake ina aya ya udhu, akiashiria kuwa kufuta juu ya khufu hakukufutwa kwa aya hiyo.
Kutoka kwa Jabiri bin Samura radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza vizuri, na akasema: Alikuwa hanyanyuki kutoka katika mswala wake alioswalia hapo Alfajiri au asubuhi, mpaka linapochomoza Jua, basi linapochomoza Jua anasimama, na walikuwa wakizungumza wanajikuta wameingia katika mazungumzo ya zama za ujinga, wanacheka na yeye anatabasamu.
Imepokelewa Imamu MuslimNa miongoni mwa sunna za Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza kwa kunyanyuka, na alikuwa hasimami kutoka katika mswala wake aliouswalia Alfajiri, mpaka Jua lichomoze. Jua linapochomoza anasimama, na walikuwa wakizungumza wanachukua katika baadhi ya mambo yao ya kabla ya Uislamu na huku yeye kanyamaza, wanacheka, na huenda yeye akatabasamu pamoja nao.