





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Busru bin Saidi, ya kwamba Zaidi bin Khalidi Al-Juhani, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimtuma kwenda kwa Abuu Juhaim radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amuulize alisikia nini kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mtu anayepita mbele ya anayeswali? Akasema Abuu Juhaim: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Lau angejua mwenye kupita mbele ya mwenye kuswali nini anachokipata, basi kusimama arobaini ni bora kwake kuliko kupita mbele yake" Amesema Abuu Nasri: Sijui alisema: Siku arobaini au miezi au miaka?
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kupita mbele ya mwenye kuswali swala ya faradhi au sunna, na kwamba lau angelijua mwenye kufanya hivyo kwa makusudi yale anayoyapata katika madhambi; basi angechagua kusimama arobaini; hilo ni bora zaidi kwake kuliko kupita mbele yake. Amesema Abuu Nasri mpokezi wa hadithi: Sijui alisema: Siku arobaini, au miezi au miaka.
Kutoka kwa Lakitwu bin Swabira -radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Nilikuwa na msafara wa bani Muntafiq -au katika msafara wa bani Muntafiq- kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, anasema: Tulipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hatukumkuta nyumbani kwake, na tukakutana na Aisha Mama wa Waumini, anasema: Akaamrisha tupikiwe mkate, basi tukapikiwa, anasema: Na tukaletewa Kinai -na kinai ni bakuli lenye tende- kisha akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Je, mmepata chochote? Au mmeagiziwa chochote?" Anasema: Tukasema: Ndiyo, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, anasema: Wakati tukiendelea kukaa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mara tukaona mchungaji akiwaswaga mbuzi wake kuingia zizini, akiwa na kitoto cha mbuzi kikilia, akasema: "Imezaa kitoto gani ewe fulani?" Akasema: Cha kike, akasema: "Basi tuchinjie badala yake mbuzi mwingine" Kisha akasema: "Usidhanie kuwa, sisi tumemchinja mbuzi huyo kwa ajili yako, sisi tuna mbuzi mia moja hatutaki zizidi hapo, akizalisha mchungaji kitoto cha mbuzi basi tunachinja badala yake mbuzi mwingine" Anasema: Nikasema: Ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu hakika mimi nina mwanamke katika ulimi wake kuna kitu -yaani ana maneno machafu- akasema: "Basi mpe talaka" Anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika ana ujamaa na mimi na nimezaa naye watoto. Akasema: "Muamrishe" Anasema: Mpe nasaha. "Endapo atakuwa na chembe ya kheri basi atatekeleza unachomwambia, na wala usimpige mkeo kama unavyopiga mtumwa wako" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nieleze kuhusu Udhu? Akasema: "Eneza maji ya udhu, na uachanishe kati ya vidole, na pandisha maji yafike puani, isipokuwa utakapokuwa umefunga".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai na Ibn MajahAmeeleza Laqitwu bin Swabira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba yeye alifika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa pamoja na watu wengine kutoka katika jamii yake ya Bani Muntafiq, anasema: Hatukumkuta nyumbani kwake, na tukamkuta Mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akaamrisha tuandaliwe mkate wa ngano na samli, na tukaletewa bakuli la tende. Kisha akaja rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Je, mmeletewa chochote katika chakula? Tukasema: Ndiyo, anasema Laqitwu: Wakati tukiwa bado tumekaa naye rehema na amani ziwe juu yake, ghafla akaja mchungaji wa mbuzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwaswaga kwenda katika zizi lake, huku akiwa kabeba kitoto cha mbuzi kikipiga kelele, akasema: Umezalisha nini? Akasema: Jike. Akasema: Basi tuchinjie badala yake mbuzi mwingine mkubwa, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Usidhanie kuwa sisi kwa ajili yenu tumejikalifisha na tukamchinja, bali sisi tuna mbuzi idadi yake ni mia moja, na wala hatutaki wazidi katika idadi hii, akizaliwa mbuzi mpya tunachinja badala yake mbuzi mwingine, akasema Laqitwu: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mke wangu ulimi wake ni mrefu na ana maneno machafu, nifanye nini kwake? Akasema: Basi mpe talaka. Anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika nimeishi naye muda mrefu sana, na nimezaa naye. Akasema: Basi mpe nasaha, ikiwa ndani ya moyo wake kutakuwa na kheri atazifanyia kazi nasaha zako, na ikiwa hatobadilika, basi mpige kipigo kisichojeruhi, na wala usimpige kama unavyompiga mtumwa wako. Kisha akasema Laqitwu: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nieleze kuhusu Udhu. Akasema: Fikisha maji ya Udhu mahala pake, na ukipe kila kiungo haki yake, na wala usiache kitu katika faradhi zake na sunna zake, na achanisha vidole vya mikono yako na miguu yako wakati wa kuviosha, na upitilize katika kuyavuta maji ndani ya pua yako wakati wa udhu na kuyatoa kwake, isipokuwa ikiwa ulitia nia ya swaumu ili maji yasiingie tumboni mwako.
Kutoka kwa bin Masoud radhi za Allahi ziwe juu yake amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaondoka kwa ajili ya haja yake, tukaona ndege akiwa na makinda mawili, tukawachukua makinda wake, akaja yule ndege akaanza kupepesa mbawa zake, basi akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Ni nani aliyemuhuzunisha ndege huyu kwa mwanaye? Mrejesheeni mwanaye", na akaona kijiji cha wadudu chungu tulichokichoma kwa moto, akasema: "Hakika hastahiki kuadhibu kwa Moto isipokuwa Mola Mlezi wa Moto".
Imepokelewa na Abu DaudAmeeleza Abdallah bin Masudi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba wao walikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaondoka rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili kukidhi haja yake, Maswahaba zake wakapata ndege aina ya Hummara akiwa na makinda mawili, wakayachukua, yule ndege akaanza kupeperusha mbawa zake na kuzipepesa kwa huzuni kwa kuwakosa makinda wake, akaja rehema na amani ziwe juu yake na akasema: Ni nani aliyemuhuzunisha na akamuhofisha kwa kuchukua vitoto vyake? Kisha akaamrisha virejeshwe kwake. Kisha akaona kijiji cha wadudu chungu kilichochomwa kwa moto, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ni nani aliyekiunguza hiki? Wakasema baadhi ya Maswahaba: Sisi. Akasema kuwaambia: Hakika haifai kwa yeyote kuadhibu kiumbe hai kwa moto; isipokuwa Mwenyezi Mungu muumba wake.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Siku moja sisi tukiwa Msikitini pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake ghafla akaja bedui, akasimama akaanza kukojoa Msikitini, wakasema Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Koma, koma!, anasema: Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Msimkatishe, muacheni" Wakamuacha mpaka akamaliza kukojoa, kisha baada ya hapo Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuita, akasema kumuambia: "Hakika Misikiti hii haifai kuwekwa chochote katika mikojo hii, wala uchafu wowote, bali hii ni kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuswali, na kusoma Qur'ani" Au kama alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake, anasema; akumuamrisha mtu mmoja miongoni mwao akaja na ndoo ya maji akapamwagia.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake msikitini kwake akiwa pamoja na Maswahaba zake, akaja bedui mmoja kutoka kijijini, akaanza kukojoa katika kona ya msikiti. Maswahaba wakamkaripia na wakasema: Koma, na wacha unachokifanya. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Muacheni, na wala msimkatishe mkojo wake, wakamuacha mpaka akamaliza. Kisha rehema na amani ziwe juu yake akamuita na akamwambia: Hakika misikiti haifai kwa chochote miongoni mwa mikojo hii, wala aina yoyote ya uchafu, bali ni kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na swala, na kusoma Qur'ani na mfano wa hayo. Kisha akamuamrisha rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja katika Maswahaba akaja na ndoo iliyojaa maji akayamwaga katika mkojo wake.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekataza kustanji kwa kinyesi cha wanyama au mfupa, na akasema: "Vitu hivyo havisafishi sawa sawa".
Imepokelewa na Addar- AlqutniAmemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekidhi haja yake sawa iwe haja ndogo au kubwa, kustanji kwa mfupa wa mnyama au kinyesi chake na mabaki yake yaliyokauka; na akasema: Hivyo haviondoshi najisi, na wala havisafishi vizuri.
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotoka kukidhi haja anasema: "Ghufraanaka" Msamaha unatoka kwako.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotoka kukidhi haja yake msalani anasema: " Ninakuomba (Msamaha) Ewe Mwenyezi Mungu.
Kutoka kwa Salman radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Washirikina walisema kutuambia: Hakika mimi ninamuona jamaa yenu anakufundisheni kila kitu, mpaka anakufundisheni kukidhi haja, akasema: Ndiyo, hakika yeye ametukataza kustanji mmoja wetu kwa mkono wake wa kulia, au kuelekea kibla, na akakataza kinyesi cha wanyama na mifupa, na akasema: "Asistanji mmoja wenu kwa chini ya mawe matatu".
Imepokelewa Imamu MuslimAmesema Salman Al-Faarisi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Washirikina walisema kwa kutukejeli: Hakika Nabii wenu anakufundisheni kila kitu, mpaka anakufundisheni namna gani mtakidhi haja zenu kama haja ndogo au kubwa! Akasema Salmaan: Ndiyo, ametufundisha adabu za kukidhi haja; na miongoni mwake ni kwamba alitukataza rehema na amani ziwe juu yake kustanjia baada ya kukidhi haja kwa mkono wa kulia, kwa kuulinda na najisi na kwa kuupa heshima, au kuelekea kibla wakati wa haja ndogo au kubwa, na akakataza kustanji kwa kinyesi cha wanyama na mabaki yake na mifupa yake, na asitosheke aliyekidhi haja katika kustanji kwa chini ya mawe matatu.
Imepokelewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake amesema: Katika sunna atakaposema muadhini katika adhana ya Alfajiri: Hayya Alal-fala'h, aseme: Aswalatu khairu mmina nnaum. Yaani: Swala ni bora kuliko usingizi.
Imepokelewa na Ibnu Khuzaymah, Addar- Alqutni na AlbayhaqyAmeeleza Anasi bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuwa miongoni mwa mambo aliyoyakubali Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika sunna zake, ni Muadhini kusema katika Adhana Alfajiri pekee, baada ya kauli yake: "Hayya a'lal falaah" asema: "Asswalaatu khairuni minan nauum" Yaani swala ni bora kuliko usingizi.
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- Ya kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakitosimama Kiyama mpaka watu wajifaharishe katika Misikiti".
Imepoekelewa na Abu Daud, Nasai na Ibn MajahAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa miongoni mwa dalili za kukaribia kwa Kiyama na kumalizika kwa Dunia, ni watu kujifaharisha kwa kuipamba Misikiti yao, au kujifaharisha kwa dunia yao ndani ya misikiti ambayo haikujengwa ila kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu.