





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muhammadi Abdallahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hatokuwa na imani mmoja wenu mpaka yawe matamanio yake ni yenye kufuata yale niliyokujua nayo".
Imepokelewa na katika kitabu cha Al-Hujjah kwa msururu sahihi wa wasimuliziAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanadam hawezi kuwa muumini mwenye imani kamili ya wajibu mpaka mapenzi yake yafuate yale aliyokuja nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa amri na makatazo na mengineyo, ayapende aliyoamrishwa, na ayachukie aliyokatazwa.
Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Amry -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mambo manne yatakayekuwa kwake basi atakuwa mnafiki, ana akiwa na jambo moja miongoni mwa hayo basi atakuwa na tabia ya unafiki mpaka aiache: Yule anayesimulia akasema uongo, na akiahidi hatimizi, na akigombana hupita mipaka, na akiingia makubaliano hufanya hiyana".
Imepokelewa na Bukhari na MuslimTabia nne amezitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zitakapokusanyika kwa muislamu atakuwa na mfanano mkubwa na wanafiki kwa sababu ya tabia hizi, na hili linakuwa kwa yule ambaye sifa hizi ndio tabia yake mara kwa mara, ama atakayezifanya mara chache huyu haingii katika sifa hizi, nazo ni: Ya kwanza: Akizungumza husema uongo kwa makusudi na kutokuwa mkweli katika maneno yake. Ya pili: Akitoa ahadi katika makubaliano haitimizi, na humfanyia hiyana aliyeahidiana naye. Ya tatu: Akiahidi ahadi yoyote haitimizi na huenda kinyume. Ya nne: Akizozana na akagombana na yeyote ugomvi wake huwa mkali sana, na hupotoka katika haki, na hufanya hila ya kuipinga na kuibatilisha, na husema maneno ya batili na uongo. Unafiki ni mtu kudhihirisha tofauti na yale anayoyaficha, na maana hii ipo kwa mtu mwenye sifa hizi, na unafiki wake unamuhusu yule anayezungumza naye, na akamuahidi, na akamwamini, na akagombana naye, na akamuahidi mtu, si kwamba atakuwa mnafiki katika Uislamu anaudhihirisha na kuficha ukafiri, hapana, na atakayekuwa na sifa moja katika sifa hizi; basi atakuwa na sifa ya unafiki ndani yake hadi atakapoiacha.
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -sala na amani ziwe juu yake- amesema: "Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni".
Imepokelewa Imamu MuslimAnaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna atayemsikia katika umma huu, Myahudi au Mkristo au mwingine yeyote utakayemfikia ujumbe wa Mtume -sala na amani ziwe juu yake- kisha akafa na hakumuamini isipokuwa atakuwa miongoni mwa watu wa motoni ataishi humo milele daima.
Kutoka kwa Aisha na Abdillah bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yao wamesema: Yalipomfika Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mauti akawa anaweka nguo yake juu ya uso wake, anapozidiwa kupumua anaifunua kutoka usoni kwake, na anasema naye akiwa katika hali hiyo: "Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mayahudi na Maswara, waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa ni Misikiti" Akitahadharisha waliyoyafanya.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Aisha na bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yao- yakuwa kilimpofika kifo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alianza kuweka kipande cha kitambaa juu ya uso wake, akibanwa na pumzi kwa sababu ya kilevi cha kifo anakitoa usoni kwake, akasema akiwa katika hali hiyo mbaya: Mwenyezi Mungu amewalaani Mayahudi na Manaswara, na akawafukuza kutoka katika rehema yake; na hii ni kwa sababu wao walijenga Misikiti juu ya makaburi ya Manabii wao, laiti kama jambo hili lisingekuwa na hatari basi asingelieleza katika sehemu kama hii, kwa sababu hii ameukataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake kufanana na kitendo hicho; kwa sababu ni katika vitendo vya Mayahudi na Manaswara, na ni kwa sababu ni njia inayopelekea katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu, Allah amewalaani watu walioyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa misikiti".
Imepokelewa na AhmadAlimuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mola wake asilifanye kaburi lake kuwa mithili ya sanamu lenye kuabudiwa na watu kwa kulitukuza, na kulielekea wakati wa kusujudu; kisha akaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi mungu yuko mbali na amemumfukuza na kumtowa kwenye rehema zake yeyote atakaye fanya makaburi ya manabii kuwa ni misikiti,kwani kulifanya kuwa msikiti ni njia ya kuelekea kuliabudu na kuliitakidi hivyo.
Kutoka kwa Anas bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie, yakuwa yeye Amesema: "Hakika ukubwa wa malipo huendana sawa pamoja na ukubwa wa matatizo, na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapowapenda watu huwapa mtihani; atakayeridhia atapata radhi, na atakayechukia atapata hasira (za Mwenyezi Mungu)."
Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu TirmidhiyAnatueleza Mtume rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi kuwa muumini linaweza kutokea kwake jambo lolote katika matatizo, katika nafsi yake au mali yake au kinginecho, nakuwa Mwenyezi Mungu atamlipa juu ya matatizo hayo ikiwa kama yeye atavumilia, nakuwa kila majanga yanavyozidi kuwa makubwa na hatari yake kuwa kubwa ndivyo malipo yake yanavyokuwa makubwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha anabainisha rehema na Amani zimfikie kuwa mitihani ni katika alama za kuwapenda Mwenyezi Mungu waumini, nakuwa hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake ni lazima yafanyike hakuna namna, lakini atakayesubiri na akaridhia, basi Mwenyezi Mungu atamlipa kwa hilo kwa kumridhia na zinamtosha zaidi thawabu zake, nakuwa atakayechukia na akakerwa na hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake, basi Mwenyezi Mungu atamchukia na zinamtosha zaidi adhabu zake.
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Amesema Allah aliyetakasika na kutukuka: Mimi nimetosheka (sihitaji) washirika kushirikishwa nao, yeyote mwenye kufanya jambo akashirikisha ndani yake mwingine pamoja nami, nitamuacha na ushirika wake".
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka amesema kuwa: Yeye amejitosheleza na uhitaji wa washirika wa kushirikishwa naye, Yeye ni tajiri wa kila kitu, na kuwa mwanadamu atakapofanya jambo katika ibada na akalifanya kuwa ni la Mwenyezi Mungu na mwingine asiyekuwa yeye, basi Allah humuacha na halikubali jambo hilo, na hulirejesha kwa mwenye nalo. Ni lazima kutakasa amali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani Yeye Mtukufu hakubali isipokuwa yale yatakayokuwa yametakaswa kwa kutaka radhi zake Yeye Mkarimu.
Imepokelewa Kutoka kwa Jundub -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kabla ya kufariki kwake kwa siku tano naye akisema: "Hakika mimi ninajivua dhima kwa Mwenyezi Mungu, kwa mimi kuwa na mwandani (Mtu mwenye mapenzi ya dhati zaidi) miongoni mwenu, hakika Allah Mtukufu kanifanya mimi kuwa mwandani wake, kama alivyomfanya Ibrahim kuwa mwandani, na lau kama ningelijifanyia mwandani katika umma wangu basi ningemfanya Abubakari kuwa mwandani, tambueni kuwa; Hakika wale waliokuwa kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Manabii wao na wema wao kuwa misikiti, tambueni vyema (kuweni makini)! yakuwa Msijelifanya kaburi langu kuwa msikiti, hakika nakukatazeni msifanye hilo".
Imepokelewa Imamu MuslimAlinieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa nafasi yake imefikia kiwango cha juu kabisa cha mapenzi, kama alichopata Ibrahim -Amani iwe juu yake-, na kwa ajili hiyo alikanusha kuwa na mwandani zaidi ya Allah; Kwa sababu moyo wake umejaa mapenzi ya Allah Mtukufu na kumtukuza kwake na kumtambua kwake, hivyo hauwezi kupata nafasi kwa yeyote zaidi ya Allah, Na lau kama angelijifanyia mwandani katika viumbe basi angelikuwa ni Abubakari. Kisha akatahadharisha kwa kuchupa mipaka inayofaa katika mapenzi kama walivyofanya Mayahudi na Wakristo katika makaburi ya Manabii wao na wema wao mpaka wakayageuza kuwa miungu ya kishirikina inayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na wakajenga juu ya makaburi yao misikiti na mahekalu, na akaukataza -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake wasijekufanya mfano vitendo vyao.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -sala na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu hupata wivu, na hakika muumini hupata wivu, na wivu wa Mwenyezi Mungu ni pale muumini anapoyafanya yale aliyomharamishia juu yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu hupata wivu na huchukia na hukarahika, kama ambavyo muumini hupata wivu na huchukia na kukarahika, nakuwa sababu ya wivu wa Mwenyezi Mungu ni pale muumini anapoyafanya yale aliyomharamishia Mwenyezi Mungu juu yake miongoni mwa machafu kama zinaa liwati (Ushoga na ubasha) wizi na kunywa pombe na mengineyo katika machafu.