





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Miji inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake, na miji inayochukiwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa sehemu zinazopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake; kwa sababu ni nyumba za ibada, na zimeasisiwa kwa uchamungu, na miji inayochukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake; kwa sababu masoko mara nyingi ndio kitovu cha ghushi na udanganyifu na riba na viapo vya uongo, na kwenda kinyume na ahadi, na kupuuza kumtaja Mwenyezi Mungu.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayekuwa na dhuluma yoyote ya ndugu yake kama heshima au chochote, basi na wamalizane leo hii, kabla ya wakati ambao hapatakuwa na Dinar wala Dirham, ikiwa atakuwa na amali njema basi zitachukuliwa kwake kwa kiasi cha dhuluma yake, na akiwa hana mema basi yatachukuliwa maovu ya mwenye haki na atabebeshwa yeye".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAmemuamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kutumbukia katika dhuluma ya ndugu yake Muislamu katika heshima, au mali, au damu, basi amuombe aliyemdhulumu amsamehe madamu bado yuko Duniani, kabla haijafika siku ya Kiyama, kiasi ambacho Dinar ya dhahabu wala Dirham ya fedha haitofaa kitu kwa kumlipa aliyemdhulumu ili aikomboe nafsi yake; kwani kisasi siku hiyo kitakuwa kwa matendo mema na mabaya; kiasi kwamba aliyedhulumiwa atachukua kutoka katika mema ya aliyemdhulumu kwa kiwango cha dhuluma yake alichodhulumiwa, ikiwa dhalimu hatokuwa na mema basi yatapunguzwa maovu ya aliyedhulumiwa na kubebeshwa dhalimu kwa kiwango cha dhuluma yake.
Kutoka kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Watafufuliwa watu siku ya Kiyama wakiwa peku, uchi, hawajatahiriwa" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wanawake na wanaume wote pamoja, kila mmoja anamtazama mwenzake? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Aisha, jambo litakuwa kubwa mno, kuliko hata mtu kushughulika kumtazama mwenzake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmesimulia Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya yale yatakayokuwa siku ya Kiyama, na kwamba watakusanywa watu baada ya kufufuliwa kutoka makaburini mwao kwa ajili ya hesabu, na hali yao ni kwamba watakuwa miguu peku bila viatu, miili yao ikiwa uchi bila nguo wala kizuizi, na wakiwa hawajatahiriwa kama siku waliyozaliwa na mama zao, aliposikia mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akasema kwa kustaajabu: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wanawake na wanaume wote pamoja kila mmoja akimtazama mwenzake?! Mtume rehema na amani ziwe juu yake akambainishia: Kwa jambo la kisimamo na kukusanywa baada ya kufufuliwa kutoka katika kifo lina misukosuko kiasi kwamba watu macho yao hayatojali kutazama utupu.
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kumwambia Ashajji Abdil-Kaisi: "Hakika kwako wewe kuna mambo mawili anayapenda sana Mwenyezi Mungu: Upole, na utaratibu".
Imepokelewa Imamu MuslimAlisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kumwambia Mundhiri bin Aidhi, Ashajji ni kabila la Abdil-Kaisi na yeye ndiye alikuwa mtemi wao radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Hakika kwako kuna sifa mbili anazipenda mno Mwenyezi Mungu, nazo ni: Akili, kuhakiki mambo, na utulivu, na kutokuwa na pupa.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu anapompenda mja humuita Jibril na husema: Hakika mimi ninampenda fulani basi mpende, anasema: Jibril humpenda, kisha anaita huko mbinguni na kusema: Hakika Mwenyezi Mungu anampenda fulani basi mpendeni, wanampenda wakazi wa mbinguni, anasema kisha anapewa kukubalika katika Ardhi, na anapomchukia mja humuita Jibril na kusema: Hakika mimi ninamchukia fulani basi mchukie, anasema; Basi Jibril humchukia, kisha ananadi kwa wakazi wa mbinguni; hakika Mwenyezi Mungu anamchukia fulani basi mchukieni, anasema: basi wanamchukia, kisha anawekewa kuchukiwa katika Ardhi".
Swahiih MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu anapompenda mja muumini; mwenye kutii amri zake mwenye kujiepusha na makatazo yake humuita Jibril: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anampenda fulani basi mpende. Basi bwana wa Malaika, Jibril amani iwe juu yake humpenda, basi Jibril hunadi kwa Malaika walioko mbinguni. Hakika Mola wenu anampenda fulani basi nanyi mpendeni, basi humpenda wakazi wa mbinguni, kisha anapewa kukubalika katika nyoyo za waumini kwa kumpenda na kuvutiwa naye na kumridhia. Na anapomchukia Mwenyezi Mungu mja humuita Jibril: Hakika mimi ninamchukia fulani basi mchukie; Basi Jibril humchukia, kisha ananadi Jibril kwa wakazi wa mbinguni: Hakika Mola wenu Mlezi anamchukia fulani basi mchukieni; wanamchukia, kisha anawekewa kuchukiwa na kutofurahiwa ndani ya nyoyo za waumini.
Imepokewa Kutoka kwa Omar bin Khattwab -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Walikuja mateka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mara kukawa na mwanamke miongoni mwa mateka akikamua maziwa yake na kunyonyesha, akipata mtoto katika mateka anamchukua, anamkumbatia na kumuweka tumboni kwake na kumnyonyesha, basi Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kutuambia: "Hivi mnadhani mwanamke huyu anaweza kumtupa mwanaye motoni?" Tukasema: Hapana, hawezi kumtupa, akasema: "Basi Mwenyezi Mungu ana huruma zaidi kwa waja wake kuliko mwanamke huyu kwa mtoto wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeWaliletwa mateka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka katika kabila la Hawazini, mara kukawa na mwanamke miongoni mwao akimtafuta mwanaye, kila akipata mtoto anamnyonyesha kwa sababu ya kudhurika kwake kwa wingi wa maziwa katika matiti yake, mara, akampata mwanaye katika mateka akamchukua, akamkumbatia tumboni kwake na akamnyonyesha, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwaambia Maswahaba zake: Hivi mnadhani mwanamke huyu anaweza kumtupa mwanaye motoni? Tukasema: Kamwe, hawezi kumtuka kwa hiyari yake milele. Akasema: Basi Mwenyezi Mungu ana huruma zaidi kwa waja wake Waislamu kuliko mwanamke huyu kwa mtoto wake.
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Waadhini wote watakuwa na shingo ndefu zaidi kuliko watu wote siku ya Kiyama".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba waadhini wote ambao huwaita watu kuja katika swala ndio watakuwa watu wenye shingo ndefu zaidi siku ya Kiyama kwa sababu ya utukufu wa amali yao, na wingi wa kheri zao, na ukubwa wa malipo yao.
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- anasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayekutana na Mwenyezi Mungu hali yakuwa hamshirikishi na chochote halitomdhuru dhambi lolote kwa hilo, na atakayekufa na hali yakuwa anamshirikisha, basi hakuna jema litakalomnufaisha".
Imepokelewa na AhmadAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekufa na akakutana na Mwenyezi Mungu akiwa na tauhidi hamshirikishi na chochote basi huyo ni katika watu wa Peponi, hata kama akiadhibiwa kwa dhambi motoni, na atakayekufa huku akimshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote hakuna jema lolote litakalomnufaisha; na Pepo kwake ni haramu.
Kutoka kwa Abuu Mussa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alisimama kwetu Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa maneno matano, akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mtukufu, halali, na wala haimstahikii kulala, hushusha mizani ya uadilifu na huinyanyua, yanapandishwa kwake matendo ya usiku kabla ya matendo ya mchana, na matendo ya mchana kabla ya matendo ya usiku, pazia lake ni nuru, -na katika riwaya nyingine-: Lau kama angeliondoa, basi utukufu wa uso wake ungeunguza viumbe vyake mpaka pale ambapo macho yake yanafikia."
Imepokelewa Imamu MuslimAlisimama Mtume rehema na amani ziwe juu yake akihutubia kwa Maswahaba zake kwa sentensi tano kamilifu, nazo ni: Ya kwanza: Kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka halali. Ya pili: Haiwezekani katika haki yake kulala; kulingana na ukamilifu wa usimamizi wake na uhai wake. Ya tatu: Ya kwamba Yeye Mtukufu anashusha mizani na kuinyanyua kulingana na vile vinavyopimwa miongoni mwa matendo ya waja yanayopanda kwake juu, na zinapimwa riziki zao zinazoshuka katika Ardhi, riziki ambayo ndiyo sehemu na fungu la kila kiumbe huishusha Yeye Mtukufu na kumfanya awe masikini, na huipandisha na kumfanya awe tajiri. Ya nne: Hupandishwa kwake waliyoyafanya waja usiku kabla ya mchana unaofuata baada yake, na amali zao za mchana kabla ya amali za usiku unaofuata baada yake; Malaika wanaohifadhi matendo ya waja hupanda na matendo ya usiku baada ya kumalizika kwake katika mwanzo wa mchana, na wanapanda na amali za mchana baada ya kumalizika kwake katika mwanzo wa usiku. Ya tano: Pazia lake Mtukufu linalozuia kumuona ni nuru au moto, laiti angelifunua basi mwangaza wa uso wake ungeunguza kila kitu mpaka pale linapoishia jicho lake katika viumbe vyake; mwangaza wa uso wake ni nuru yake na utukufu wake na mng'ao wake. Na makadirio: Nikuwa, lau angeliondoa na kukifunua kinachozuia kumuona ambacho ni pazia, na akajitokeza wazi nuru ya uso wake ingeliunguza kila kitu mpaka linapoishia jicho lake katika viumbe vyake; navyo ni viumbe vyote; kwa sababu jicho lake Aliyetakasika na kutukuka limezingira viumbe vyote.