





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Anasema Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: Mimi nipo katika dhana ya mja wangu kwangu, na Mimi nipo naye wakati anaponitaja, atakaponitaja ndani ya nafsi yake nami nitamtaja ndani ya nafsi yangu, na akinitaja katika umati nami nitamtaja katika umati bora kuliko huo, na akisogea kwangu shibri (futi) moja na mimi ninasogea karibu naye kwa mita nzima, na akisogea kwangu kwa mita moja mimi ninasogea kwake kwa zaidi ya mita moja (Baa'a) na akinijia kwa kutembea basi mimi nitamjia kwa mchakamchaka"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Mimi nipo katika dhana ya mja wangu kwangu, nitampeleka mja wangu kulingana na dhana yake kwangu na hii ni kwa kutaraji mazuri na kutaraji msamaha, na nitamfanyia yote anayoyataraji kutoka kwangu katika mambo ya kheri au mengineyo; na mimi niko pamoja naye kwa kumhurumia na kumuwezesha na kumuongoza na kumlea na kumuunga mkono pindi anaponitaja. Akinitaja ndani ya nafsi yake akiwa peke yake amejitenga kwa kunisabihi na kunitukuza au kwa kinginecho; basi nami nitamtaja ndani ya nafsi yangu. Na akinitaja katika kundi la watu; basi nami nitamtaja katika kundi kubwa na zuri kuliko hilo. Na atakayesogea kwa Mwenyezi Mungu kwa kiwango cha shibri (futi) moja basi Mwenyezi Mungu humzidishia na kuzidi kujiweka karibu zaidi kwa kiasi cha dhiraa (mita). Na akijiweka karibu naye kwa kiasi cha dhiraa (mita) anajiweka naye kwa kiasi cha zaidi ya mita moja (Baa'a). Na akija kwa Mwenyezi Mungu akiwa anatembea Yeye anamjia kwa mchakamchaka. Mja atakapojiweka karibu na Mola wake Mlezi kwa kumtii na kuelekea kwake, basi Mola Mlezi Mtukufu humzidishia ukaribu ikiwa ni malipo kulingana na amali yake. Kila unapozidi kukamilika uja (utumwa) wa muumini kwa Mola wake Mlezi Mwenyezi Mungu Mtukufu hujiweka karibu naye, hivyo, kipawa cha Mwenyezi Mungu na thawabu zake ni nyingi kuliko amali za mja na tabu zake, na uhalisia nikuwa thawabu za Mwenyezi Mungu ni nyingi kuliko amali kwa kutazama namna na wingi wake. Muumini huwa na dhana nzuri, na kutenda mema, na kwenda mbio na kuzidisha mpaka atakapokutana na Mwenyezi Mungu.
Kutoka kwa Twalha bin Ubeidi LLah -Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoka maeneo ya Najid, kichwa chake kikiwa kimetimka, tunasikia mvumo wa sauti yake, na wala hatuelewi anasema nini, mpaka akasogea karibu na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ghafla akaanza kuuliza kuhusu Uislamu, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Swala tano mchana na usiku" Akasema: Je kuna la wajibu juu yangu zaidi ya hayo? Akasema: "Hapana ila kama utajitolea" Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Na kufunga mwezi wa ramadhani" Akasema: Je kuna la wajibu juu yangu zaidi ya hilo? Akasema: "Hapana ila kama utajitolea" Akasema na akamtajia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- zaka, akasema: Je kuna la wajibu juu yangu zaidi ya hilo? Akasema: "Hapana ila kama utajitolea" Akageuka na kuondoka yule bwana huku akisema: Wallahi sitozidisha juu ya hayo wala sitopunguza, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Kafaulu ikiwa atakuwa mkweli".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtu mmoja miongoni mwa watu wa Najdi alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na nywele zake zikiwa zimetimkatimka na sauti yake ikiwa juu, wala haeleweki anasema nini, mpaka alipomkaribia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akauliza kuhusu faradhi za Uislamu? Basi Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, akaanza na swala, na akamwambia kuwa Mwenyezi Mungu amemfaradhishia kuswali swala tano katika kila mchana na usiku. Akasema: Je, ninalazimika kuswali swala zingine zaidi ya hizi tano? Akasema: Hapana, labda kama utajitolea kuswali swala za sunna. Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Na miongoni mwa ibada alizokuwajibishia Mwenyezi Mungu juu yako ni kufunga mwezi wa Ramadhani. Yule bwana akasema: Je, ninalazimika kufunga funga zingine zaidi ya swaumu ya Ramadhani? Akasema: Hapana, ila kama utajitolea kufunga. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamtajia Zaka Yule bwana akasema: Je, ninalazimika chochote katika sadaka baada ya zaka ya faradhi? Akasema: Hapana, ila kama utajitolea. Baada ya mtu huyo kusikia faradhi hizo kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aligeuka na kuapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa atashikamana nazo bila ya kuongeza wala kupunguza, akasema rehema na amani zimshukie baada ya kauli yake hiyo: Ikiwa bwana huyu atakuwa mkweli kwa alichoapia, basi atakuwa miongoni mwa waliofaulu.
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: “Siku bora zaidi iliyochomozewa jua ni siku ya Ijumaa, ndani yake aliumbwa Adam, na ndani yake aliingizwa Peponi, na ndani ya siku hii akatolewa humo, na hakitosimama Kiyama ila siku ya Ijumaa".
Imepokelewa Imamu MuslimMtume rehema na amani ziwe juu yake anatueleza kuwa siku bora kabisa iliyochomozewa na jua ni Ijumaa, Miongoni mwa sifa zake: Mwenyezi Mungu alimuumba Adam, amani imshukie, na ndani yake akamuingiza Peponi, na ndani yake akamtoa na akamteremsha duniani, na Kiyama hakitosimama ila siku ya Ijumaa.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Hakika atakuja mtu mnene tena mkubwa siku ya kiyama akiwa halingani mbele ya Mwenyezi Mungu hata na uzito wa bawa la mbu".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimHakika mtu mkubwa ni yule mwenye nia kubwa mwenye kujikweza kwa waja wa Mwenyezi Mungu duniani mwenye kujipa ujabari mwenye kujifaharisha kwa matendo yake na kauli zake, basi huyo siku ya kiyama hatolingana mbele ya Mwenyezi Mungu hata na uzito wa bawa la mbu, na wala hatokuwa na thamani wala nafasi.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hatomsitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsitiri siku ya kiyama"
Imepokelewa Imamu MuslimAnabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu hatomsitiri ndugu yake katika jambo miongoni mwa mambo, isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atamsitiri siku ya Kiyama; kwani malipo huendana na matendo, na stara ya Mwenyezi Mungu kwake inakuwa kwa kuzisitiri aibu zake na maasi yake kwa kutoyatangaza mbele ya umati wa siku ya Kiyama, na huenda inawezakuwa kwa kutoyahesabu na kutomkumbusha.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muslim Al-Khaulani, amesema: Alinihadithia kipenzi mwaminifu, ama yeye kiukweli ni kipenzi changu, na ama kiukweli kwangu ni mwaminifu, Auf Bin Maliki Al-Ashjai radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikuwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake,inakaribia kama watu tisa au nane au saba hivi, akasema: "Hivi hamumpi ahadi ya utiifu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?" Na tulikuwa bado wageni katika hilo, tukasema: Tumekwisha kupa ahadi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kisha akasema: "Hivi hamumpi ahadi ya utiifu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?" Tukasema: tumekwisha kupa ahadi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kisha akasema: "Hivi hamumpi ahadi ya utiifu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?" Akasema: Tukanyoosha mikono yetu na tukasema: Tukasema: tumekwisha kupa ahadi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu,........
Imepokelewa Imamu MuslimAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kundi la Masahaba, akawataka mara tatu mfululizo wampe ahadi ya utiifu na wampe ahadi ya kushikamana na mambo haya: La kwanza: Kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake kwa kutekeleza amri zake na kujiepusha na makatazo yake, na wasimshirikishe na kitu kingine. La pili: Kusimamisha swala tano za faradhi, katika usiku na mchana. La tatu: Kusikia na kutii katika mambo mema kwa yule atakayesimamia majukumu ya waislamu. La nne: Kushusha haja zao zote kwa Mwenyezi Mungu na wasiwaombe watu chochote katika haja hizo, na katika hilo Mtume rehema na amani ziwe juu yake akashusha sauti yake. Na hakika Masahaba radhi za Allah ziwe juu yao waliyafanyia kazi yale waliyoyatolea ahadi, mpaka akasema mpokezi wa hadithi: Hakika niliwaona baadhi yao hao Masahaba unadondoka mjeledi wa mmoja wao, na hamuombi yeyote amuokotee, bali anashuka na anauchukua yeye mwenyewe.
Kutoka kwa bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayepatwa na umasikini akaushusha kwa watu hautozibwa umasikini wake, na atakayeushusha kwa Mwenyezi Mungu, basi ni karibu zaidi Mwenyezi Mungu kumpa riziki ya haraka au ya baadaye".
Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na AhmadAmeeleza bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayepatwa na umasikini" Yaani: shida kubwa, na yamekithiri matumizi ya neno hili katika umasikini na maisha magumu. "Akauteremsha kwa watu" Yaani: Aliweka wazi kwao, na akaidhihirisha kwa njia ya malalamiko kwao, na akataka kuondolewa kwa umasikini wake toka kwao. Hivyo matokeo ni: "Hautozibwa umasikini wake" Yaani: haitokidhiwa haja yake, na hautoondoka umasikini wake, kila inapotatuliwa shida yake inampata shida nyingine zaidi ya hiyo. Na ama "atakayeishusha kwa Mwenyezi Mungu" akategemea kwa Mola wake basi "anakuwa karibu mno Mwenyezi Mungu" Kumpa haraka "kwake riziki ya haraka, yuko karibu kumpa mali na amfanye kuwa tajiri "Au ya baadaye" katika Akhera.
kutoka kwa Albaraa bin Aazib Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Muislamu atakapoulizwa kaburini anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu", Hiyo ndiyo kauli yake Mtukufu: "Huwapa umakinifu Mwenyezi Mungu wale walioamani kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika akhera" [Ibrahim: 27].
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMuumini ataulizwa kaburini, watamuuliza Malaika wawili waliopangiwa kufanya hivyo, nao ni Munkari na Nakiri, kama walivyotajwa katika Hadithi kadhaa, atashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hii ndio kauli thabiti aliyoisema Mwenyezi Mungu: "Huwapa umakinifu Mwenyezi Mungu wale walioamani kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika akhera" [Surat Ibrahim: 27].
Na imepokewa kutoka kwa bin Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake - amesema: "Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na wasimamishe swala, na watoe zaka, pindi watakapofanya hivyo watakuwa wamezikinga kutokana nami damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki ya uislamu na hesabu yao itakuwa juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu alimuamrisha kupigana na washirikina mpaka washuhudie kuwa hapana muabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake asiye na mshirika, na wamshuhudilie Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake utume, na kuyafanyia kazi makusudio ya shahada hii, ikiwemo kuhifadhi swala tano usiku na mchana, na wawape zaka za faradhi wastahiki wake. Wakifanya mambo haya basi Uislamu utakinga damu zao na mali zao, haitokuwa halali kuwaua isipokuwa watakapofanya uhalifu au kosa la jinai watakalostahiki kwalo kuuawa kwa mujibu wa hukumu za Uislamu, kisha siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atasimamia hesabu yao kwani yeye ndiye ajuaye siri zao.