





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Imani ni zaidi ya vitengo sabini au zaidi ya sitini, bora yake ni kauli ya Laa ilaaha illa llaah, na ya chini yake ni kuondoa udhia barabarani, na haya ni sehemu katika imani".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa imani ina sehemu moja pamoja na mambo mengi, yanakusanya matendo itikadi na kauli. Nakuwa jambo la juu zaidi katika mambo ya imani ni kauli ya: Laa ilaaha illa llaah", kwa kujua maana yake, na kufanyia kazi matakwa yake, yakuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola Mlezi Mmoja wa pekee mwenye kustahaki kuabudiwa peke yake pasina mwingine zaidi yake. Nakuwa tendo dogo kabisa katika matendo ya imani ni kila chenye kuwaudhi watu katika njia zao. Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa haya ni katika mambo ya imani, nayo ni tabia inayomsukuma mtu kufanya mazuri na kuacha mabaya.
Kutoka kwa Abuu Bashiri Radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba yeye alikuwa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya safari zake, anasema: Akatuma mjumbe Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na watu wakiwa mahali pao pa kulala: "Kusibaki katika shingo la mnyama bangili za shaba au kengele isipokuwa (ahakikishe) zimekatwa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya safari zake, na watu wakiwa mahali pao pa kulala wanapopumzikia katika vipandwa vyao na mahema yao, akamtuma mtu kwenda kwa watu akawaamrishe wakate vikamba vinavyotundikwa kwa wanyama sawa sawa ziwe zimetokana na kamba ya upinde -kamba ya upinde, au kinginecho kama kengele au kiatu, na hii ni kwa sababu walikuwa wakitundika kwa kuogopa kijicho, wakaamrishwa kuvikata; kwa sababu havizuii kwao chochote, nakuwa manufaa na madhara yako mkononi mwa Allah peke yake asiye na mshirika.
Kutoka kwa Abdillah bin Hakim- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho".
Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na AhmadAtakayegeuka kwa moyo wake au vitendo vyake au kwa vyote viwili katika kitu ambacho anataraji manufaa au kuzuia madhara, Mwenyezi Mungu humuwakilisha katika kitu hicho ambacho amekielekea, atakayemuelekea Mwenyezi Mungu humtosheleza na humfanyia wepesi kila zito, na mwenye kumuelekea asiyekuwa yeye Mwenyezi Mungu humfungamanisha katika kitu hicho na humfedhehesha.
Kutoka kwa Twariki bin Ashiyam Al-Ashjai Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayesema: Laa ilaah illa llaah, na akayapinga yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu itakuwa haramu mali yake na damu yake, na hesabu yake itakuwa juu ya Allah".
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesema na akashuhudia kwa ulimi wake yakuwa "Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu", Yaani: Hakuna muabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na akayakanusha yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na akajitenga na dini zote isipokuwa Uislamu, itakuwa haramu mali yake na damu yake kwa muislamu, hatumiliki isipokuwa dhahiri katika matendo yake, hapokonywi mali yake na wala haimwagwi damu yake, isipokuwa atakapofanya uhalifu au jinai linalopelekea hivyo kwa mujibu wa hukumu za Uislamu. Na Allah atasimamia hesabu yake siku ya Kiyama, akiwa ni mkweli atamlipa, na akiwa mnafiki atamuadhibu.
Imepokewa Kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Wenye huruma huwahurumia Ar-Rahmani -Mwingi wa huruma-, wahurumieni walioko ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni."
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadAnabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wale wenye kuwahurumia wenzao huwahurumia Rahman -Mwingi wa rehema- kwa huruma yake iliyokienea kila kitu; Yakiwa ni malipo sawa na matendo yao. Kisha akaamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake-kuwahurumia wote walioko ardhini kwanzia binadamu au wanyama au ndege, au wengineo katika aina ya viumbe mbali mbali, na malipo ya hilo; mtahurumiwa na Mwenyezi Mungu kutoka juu ya mbingu yake ya saba.
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye adhabu nafuu zaidi siku ya Kiyama: Je, mngekuwa na kitu chochote katika ardhi mngejikomboa nacho? Basi watasema: Ndio, atasema: Nilikutakeni jambo jepesi zaidi kuliko hili, nanyi mkiwa katika mgongo wa Adam: yakuwa msinishirikishe na chochote, mkakataa isipokuwa kunishirikisha na chochote".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu ambao watateswa kidogo na Moto wa Jahannam baada ya kuingia humo: Lau mngekuwa na dunia na vyote vilivyomo ndani yake, mngeweza kujikomboa kutokana na mateso haya? Watasema: Ndio, Basi Mwenyezi Mungu atasema: Nilikutaka na nikakuamrisheni jambo jepesi kuliko hilo, ilipo chukuliwa ahadi kwenu mkiwa katika mgongo wa Adam, ya kwamba msinishirikishe na chochote. Nilipowatoa katika dunia hii mlikataa kufanya chochote isipokuwa ushirikina.
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Kuna watu walimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu makuhani, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hawana lolote" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika wao husimulia jambo baadhi ya nyakati na likawa kweli, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Neno hilo huwa limetoka katika ukweli, Jini hulikwapua na kulinong'oneza katika sikio la kipenzi chake mfano wa kuku anavyotetea, hulichanganya na uongo zaidi ya mia moja (100)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu wale wanaoeleza mambo yajayo yaliyofichikana, akasema: Msiwajali, na wala msiyachukue maneno yao, na wala msiyajali mambo yao. Wakasema: Hakika kauli yao huendana na uhalisia katika baadhi ya nyakati, kama ambavyo huelezea kutokea kwa jambo la gahibu ndani ya mwezi fulani siku fulani, na likatokea sambamba na kauli yao. Akasema -Rehema na amani ziwe juu yake-: Hakika Majini huiba yale wanayoyasikia katika habari za mbinguni, wakashuka kuja kwa watu wao miongoni mwa makuhani wakawaeleza waliyoyasikia, kisha kuhani anaongeza katika yale aliyoyasikia kutoka mbinguni uongo mia moja (100).
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na Muadhi akiwa nyuma yake alisema: "Ewe Muadhi bin Jabali", Akasema: Labaika Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema hivyo mara tatu: " Hakuna mtu yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa ukweli toka moyoni mwake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia moto", akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, je, niwaeleze watu ili wapate habari njema? Akasema: "Ukifanya hivyo, watabweteka". Na alieleza Muadhi jambo hili wakati wa kifo chake kwa kuogopa kupata dhambi za kuficha elimu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Muadhi bin Jabali -Radhi za Allah ziwe juu yake- amepanda nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya mnyama wake, akamuita: Ewe Muadhi? Akarudia wito mara tatu; Kwa kusisitiza umuhimu wa yale atakayomueleza. Na mara zote hizo Muadhi -Radhi za Allah ziwe juu yake- akimjibu kwa kusema: "Labaika kwa heshima yako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu", Yaani: Nimekujibu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu jibu moja moja, na ninataka utukufu kwa kukujibu wewe. Akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa hakuna yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuaubudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yaani: Hakuna muabudiwa wa haki isopokuwa Allah, na kuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa ukweli toka moyoni mwake, si muongo, ikiwa atakufa katika hali hii basi Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni. Muadhi -Radhi za Allah ziwe juu yake- akamuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- awaeleze watu ili wafurahi na wajipe bishara njema? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akachelea watu kubweteka katika hilo, na wapunguze kufanya matendo. Muadhi hakumsimulia hilo yeyote ila kabla ya kifo chake; kwa kuhofia kuingia katika dhambi za kuficha elimu.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anateremka Mola wetu Mlezi -Aliyetakasika na kutukuka- katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku, husema: "Ni nani anayeniomba nimjibu? Ni nani anayenitaka shida yake nimpe? Ni nani anayeniomba msamaha nimsamehe?".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka huteremka kila usiku katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku, na anawahamasisha waja wake wamuombe, kwani yeye anamjibu mwenye kumuomba, na anawahimiza wamtake haja zao, kwani yeye humpa anayemuomba, na anawaita wamuombe msamaha kutokana na madhambi yao kwani yeye huwasamehe waja wake waumini.