





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Abdillahi bin Omari- radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema: Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msiape kwa masanamu, wala kwa baba zenu"
Imepokelewa Imamu MuslimMtume rehema na amani ziwe juu yake amekataza kuapa kwa mashetani, yaani wingi wa shetani, nayo ni masanamu waliyokuwa wakiyaabudu washirikina badala ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo yalikuwa sababu ya ujeuri wao na ukafiri wao. Anakataza rehema na amani ziwe juu yake kuapa kwa baba za mtu; Ilikuwa ni desturi ya Waarabu katika zama za kabla ya Uislamu kuapa kwa baba zao kwa kujifaharisha na kwa kuwatukuza.
Kutoka kwa Buraida -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Atakayeiapia amana basi huyo si miongoni mwetu".
Imepokelewa na Abu Daud na AhmadAmekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akatahadharisha kuapia amana, nakuwa atakayefanya hivyo si miongoni mwetu.
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Tulikuwa tumekaa pembezoni mwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa pamoja nasi Abubakari na Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao katika kundi, akasimama Mtume rehema na amani ziwe juu yake mbele yetu, akaondoka na akachelewa, tukahofia asije kudhuriwa mbele yetu, tukapatwa na hofu tukasimama, mimi nilikuwa wa kwanza kufadhaika, nikatoka nikimtafuta Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake mpaka nikafika katika ukuta wa Answari (watu wa Madina) katika ukoo wa bani Najjar, nikauzunguka ili nipate mahala mlango ulipo, sikuupata! Ghafla nikaona kimviringo kidogo kinachoingia ndani ya ukuta kutokea nje kilipo kisima, nikakifukua, nikaingia kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Akasema kwa mshangao "Nani we, Abuu Huraira?!" Nikasema: Ndiyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: "Nini kimekuleta?" Nikasema: Ulikuwa umekaa pamoja nasi ukasimama ukaondoka na ukachelewa kurudi, tukahofia usije kudhurika mbele yetu, tukapatwa na mfadhaiko, mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kufadhaika, nikaja katika ukuta huu, nikafukua kama anavyofukua Mbweha, na hawa watu wako nyuma yangu. Akasema: "Ewe Abuu Huraira" Na akanipa viatu vyake, Akasema: "Nenda na viatu vyangu hivi viwili, yeyote utakayekutana naye mbele ya ukuta huu na hali yakuwa anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo ukiwa na yakini kabisa na hilo, basi mpe habari njema kuwa yeye ni katika watu wa peponi", akawa mtu wa kwanza kukutana naye ni Omari. Akasema: "Ni vya nini viatu hivi viwili ewe Abuu Huraira?" Nikasema viatu hivi ni vya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, kaniagiza navyo kuwa yeyote nitakayekutana naye na hali yakuwa anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo ukiwa na yakini kabisa na hilo, basi nimpe habari njema kuwa yeye ni katika watu wa peponi, Omari akanipiga kibao kwa mkono wake kifuani kwangu kati ya maziwa mawili nikaangukia kisogo changu, akasema: Rudi ewe Abuu Huraira!, nikarudi kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikataka kuangua kilio, akanifuatilia Omari naye akiwa nyuma yangu, nilipofika, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake "Umekuwaje ewe Abuu Huraira?" Nikasema: Nimekutana na Omari nikamueleza ulichoniagiza, akanipiga kibao kifuani kati ya maziwa yangu mawili, nikaangukia kisogo, akasema: "Rudi!" Basi akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Omari, ni nini kimekupelekea kufanya ulichokifanya?" Omari akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nakuthamini na niko radhi fidia yako kumtoa baba yangu na mama yangu, hivi ni kweli umemtuma Abuu Huraira akiwa na viatu vyako, kuwa atakayekutana naye hali yakuwa anashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo ukiwa na yakini kabisa na hilo, basi ampe habari njema kuwa yeye ni katika watu wa peponi? Akasema: "Ndiyo nimemtuma", Omari akasema: Ni bora usifanye hivyo, hakika mimi nahofia watu watabweteka na hilo, acha watende, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Basi Abuu Huraira waache".
Imepokelewa Imamu MuslimAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kakaa katika kundi la Maswahaba zake, akiwa miongoni mwao Abubakari na Omari, akasimama rehema na amani ziwe juu yake akaondoka, kisha akachelewa, wakahofia asijekupatwa na kero kutoka kwa adui; ima kwa kutekwa au kinginecho. Wakasimama Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao wakiwa na mfadhaiko, akawa wa mwanzo kufadhaika ni Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake, akaondoka mpaka akafika katika Bustani ya Bani Najjari, akaanza kuizunguka huenda anaweza kupata mlango ulio wazi akawa hakuupata, lakini alipata upenyo mdogo katika ukuta yanapoingilia maji, akaukunja mwili wake mpaka akaingia akamkuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema kumwambia? Akasema: Ndiyo. Akasema: Umepatwa na nini?. Abuu Huraira akasema: Ulikuwa pamoja nasi, ukasimama ukaondoka na ukachelewa, tukahofia usijekudhurika mbele yetu, nikawa mimi ndio wa mwanzo kufadhaika, nikaja katika ukuta huu, nikapenya kama anavyopenya mbweha, na hawa watu wakiwa nyuma yangu. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akampa viatu vyake kama nembo na alama kuwa yeye ni mkweli, na akasema kumwambia: Nenda na viatu vyangu hivi, utakayekutana naye nyuma ya ukuta huu, akiwa anashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na wala hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, moyo wake ukiwa na yakini nalo; atakayekuwa na sifa hii basi huyo ni katika watu wa peponi. Akawa wa kwanza kukutana naye ni Omari, akasema kumwambia: Ni vya nini viatu hivi ewe Abuu Huraira? Akasema: Hivi ni viatu vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amenituma kwavyo kwa yeyote nitakayekutana naye akishuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu moyo wake ukiwa na yakini na hilo, basi nimbashirie Pepo. Omari akapiga kifua cha Abuu Huraira kwa mkono wake akaanguka kwa nyuma, akasema: Rudi ewe Abuu Huraira, nikarudi kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikiwa na mfadhaiko na uso wangu ukiwa umebadilika nikiwa nataka kulia, na Omari akanifuata na akawa anatembea nyuma yangu. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Umekuwaje ewe Abuu Huraira? Nikasema: Nimekutana na Omari, nikamueleza ulichonituma, akanipiga kipigo kikali, nikaanguka kwa nyuma, na akasema: Rudi. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ewe Omari, nini kimekupelekea kufanya hivyo? Akasema Omari: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimtoe fidia kwa ajili yako baba yangu na mama yangu, hivi ni kweli ulimtuma Abuu Huraira akiwa na viatu vyako, kwamba atakayekutana na Mwenyezi Mungu huku akishuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo wake ukiwa na yakini na hilo ampe habari nje ya pepo?. Akasema: Ndiyo. Akasema: Usifanye hivyo, kwani mimi ninahofia watu watabweteka kwa kauli hiyo pekee pasina kufanya matendo, acha wafanye. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Basi waache.
Imepokelewa kutoka kwa Abdillah Bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa muislamu mwenye Uislamu kamili ni yule waliosalimika waislamu kutokana na ulimi wake, hawatukani, na wala hawalaani, wala hawasengenyi, na wala hawazunguki kwa aina yoyote miongoni mwa aina za maudhi kwa ulimi wake, na wamesalimika kutokana na mkono wake, hawatendei ubaya, na wala hachukui mali zao pasina haki, na mfano wa hayo, na mwenye kuhama, ni yule mwenye kuacha yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesema wakati anasikia adhana: Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mahmuudanil ladhii wa a'ttah, (Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa wito huu uliotimia, na swala iliyosimama, mpe Muhammad utetezi na fadhila, na umfufue mahali pakusifiwa ulipomuahidi) basi utakuwa halali kwake utetezi wangu siku ya Kiyama".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAnabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema wakati amemsikia muadhini baada ya kumaliza adhana: "Ewe Mwenyezi Mungu Mola wa wito huu" nayo ni matamshi ambayo hutumika kuita katika ibada ya Mwenyezi Mungu na swala, "Uliotimia" uliokamilika, wito wa tauhidi na ujumbe, "na swala iliyosimama" yenye kudumu ambayo itasimamishwa hivi punde, "mpe" mgawie, "Muhammadi utetezi" na cheo cha juu peponi ambacho hakimstahiki mwingine ila yeye rehema na amani ziwe juu yake, "na fadhila" cheo cha juu zaidi ya vyeo vya viumbe, "na umfufue" na umpe "nafasi yenye kusifiwa" anayosifiwa mwenye kuwanayo; nao ni utetezi mkuu wa siku ya Kiyama, "uliyomuahidi" kwa kauli yako "Huenda akakufufua Mola wako katika nafasi yenye kusifiwa" ili iwe yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Atakayeomba dua hii atastahiki kuupata utetezi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya Kiyama.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwatukane Maswahaba wangu, kwa sababu, lau kama yeyote kati yenu atatoa dhahabu sawa na (mlima) Uhud (katika njia ya Mwenyezi Mungu), basi haiwezi kuwa sawa na theluthi mbili ya kilo ya mmoja wao wala nusu yake."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwatukana Maswahabah hasa wa mwanzo katika Muhajirina na Ansari; na akaeleza kuwa lau mmoja miongoni mwa watu angetoa dhahabu nyingi kama mlima Uhudi, zisingefikia thawabu zake kwa hilo malipo ya kibaba cha Swahaba mmoja au nusu yake - na kibaba ni kujaza viganja viwili vya mtu wa wastani-; Na hii ni kwa sababu ya ikhilas yao kuwa zaidi, na ukweli wa nia zao, na kuwahi kwao kutoa na kupigana kwao katika njia ya Mwenyezi Mungu kabla ya ufunguzi wa mji wa Makka, ambapo uhitaji wake ulikuwa mkubwa.
Kutoka kwa Jaabir radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Hatoingia motoni mtu aliyeshuhudia vita vya Badri na Hudaibia".
Imepokelewa na Ahmad na asili yake ipo katika Sahih MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba hatoingia motoni aliyehudhuria vita vya Badri vilivyotokea katika mwaka wa pili wa Hijiria (kalenda ya kiislamu) akipigana pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wala aliyehudhuria suluhu ya Hudaibia, na ndani yake kukiwa na uungaji mkono wa ridhaa (Baiatu ridhiwani) uliotokea katika mwaka wa sita wa Hijiria.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alisema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Abubakari na Omari: "Hawa wawili ni mabosi wa watu wazima wa peponi kwanzia watu wa mwanzo na wa mwisho, isipokuwa Manabii na Mitume".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyAlieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Abubakari Swiddiq na Omari Al-farouq radhi za Allah ziwe juu yao ndio viumbe bora baada ya Manabii, na ndio watu bora katika watu walioingia peponi baada ya Manabii na Mitume.
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi".
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadAlieleza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kuwa wajukuu zake Hassan na Hussein watoto wa Ally bin Abii Twalib na Fatma binti wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake na Allah amridhie, wao ni mabosi katika fadhila wa kila aliyekufa akiwa kijana na akaingia peponi, au wao ni mabosi wa vijana wa watu wa peponi, kasoro Manabii na Mahalifa (viongozi) waongofu.