





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Yahya Bin Umaara Al-Maaziniy amesema: Nilimshuhudia Amri Bin Abii Hasan akimuuliza Abdallah Bin Zaidi, kuhusu udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akaagiza bakuli la maji, akatawadha mbele yao udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akamimina katika mikono yake kutoka katika bakuli, akaosha viganja vyake mara tatu, kisha akaingiza mkono wake ndani ya bakuli, akasukutua na akapandisha maji puani na akapenga, kwa michoto mitatu, kisha akaingiza mkono wake akaosha uso wake mara tatu, kisha akaosha mikono yake mara mbili mpaka katika viwiko viwili, kisha akaingiza mkono wake akafuta kichwa chake, akaanza upande wa mbele na akapeleka mpaka nyuma ya kichwa, mara moja, kisha akaosha miguu yake mpaka katika kongo mbili.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmebainisha Abdallah Bin Zaidi radhi za Allah ziwe juu yake namna ya udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kwa vitendo, akaomba chombo kidogo chenye maji, kwanza kabisa akaanza kuosha viganja vyake, kisha akainamisha chombo na akamimina maji akaiosha mara tatu nje ya chombo, Kisha akaingiza mikono yake ndani ya chombo, akachota michoto mitatu, katika kila mchoto anasukutua na anapandisha maji puani na anapenga, Kisha akachota kutoka ndani ya chombo akaosha uso wake mara tatu, kisha akachota kutoka ndani ya chombo akaosha mikono yake mpaka katika viwiko viwili mara mbili mbili, kisha akaingiza mikono yake ndani ya chombo akafuta kichwa chake kwa mikono yake akaanza na mbele ya kichwa chake mpaka akafika katika kisogo chake juu ya shingo, kisha akairejesha mpaka akafika mahali alipoanzia, kisha akaosha miguu yake pamoja na kongo mbili.
Kutoka kwa bin Shammasa Al Mihriy Amesema:Tulifika kwa Amru bin Aaswi naye akiwa katika safari ya kifo, akalia kwa muda mrefu, na akageuza uso wake kuelekea ukutani, mwanaye akaanza kusema, Ewe baba yangu, kwani hakukubashiria Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake kwa jambo kadhaa (yaani pepo)? kwani hakukubashiria Mtume-Rehema na Amani ziwe juu yake kwa jambo kadhaa? akageuka kwa uso wake, kisha akasema: Hakika jambo bora katika yale tunayoyaandaa ni kushuhudia kuwa Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hakika mimi nilikuwa katika hali za aina tatu: Nilijikuta mimi kuwa hakuna anayemchukia kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuliko mimi, Na hakuna kitu nilichotamani zaidi kama kumtia mikononi ili nimuue, basi lau ningekufa katika hali hiyo ningekuwa ni katika watu wa motoni, Basi Mwenyezi Mungu alipouweka Uislamu moyoni mwangu, nilimuendea Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- Kisha nikasema: Nyoosha mkono wako wa kulia ili nikupe utiifu wangu kwako, basi akanyoosha mkono wake wa kulia nikakunja mkono wangu, akasema: "Umekuwaje wewe Amru?" Nikasema: Nilitaka niweke sharti kwanza, akasema: "Unaweka sharti la kitu gani?" Nikasema: Nisamehewe, akasema: "Hivi hukujua kuwa uislamu hufuta makosa yaliyokuwa kabla yake, na kuwa kuhama kunafuta makosa yaliyokuwa kabla yake, nakuwa Hija hufuta makosa yaliyokuwa kabla yake?" Kuanzia hapo hapakuwa tena na yeyote niliyempenda zaidi kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- wala niliyemuheshimu zaidi machoni mwangu kuliko yeye, Na sikuwa naweza kumtazama kwa macho yangu; kwasababu ya kumuheshimu, na hata kama ningeombwa nimsifie nisingeweza; kwasababu mimi sikuwa naweza kumtazama kwa macho yangu, na lau ningekufa katika hali hiyo ningetaraji kuwa miongoni mwa watu wa peponi, Kisha tukatawala mambo ambayo mpaka sasa sijui hali yangu ndani yake? Basi ikiwa nitakufa nisifuatwe na maombolezo wala moto, na mkinizika, basi nimwagieni udongo kidogo kidogo, kisha bakini kaburini kwangu kwa kiasi cha muda wa kuweza kumchinja ngamia na kumchuna, na kugawanywa nyama yake, ili nijiliwaze kwenu, na nisubiri nini nitawajibu wajumbe wa Mola wangu.
Imepokelewa na Imamu MuslimImekusanya hadithi ya Amru bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- maudhui za habari njema na pongezi za kheri ndani ya kisa, na muhtasari wa kisa hiki kitukufu: Nikuwa yeye walimfikia baadhi ya jamaa zake naye akiwa katika safari ya kifo, akalia kilio kikubwa, na akageuza uso wake upande wa ukutani -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, naye akiwa katika safari ya kifo ataachana na dunia, mwanaye akasema kumwambia: Unalilia nini na haliyakuwa tayari alishakubashiria pepo Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-? Akasema: Ewe mwanangu, hakika mimi nilikuwa katika hali tatu, kisha akazitaja hali hizi tatu: Yakuwa yeye alikuwa akimchukia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- chuki ya hali ya juu, nakuwa duniani hapakuwa na mtu anayemchukia zaidi kama yeye, mpaka Mwenyezi Mungu akauingiza Uislamu ndani ya moyo wake akaja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, akasema: Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu: Nyoosha mkono wako ili nikupe utiifu wangu juu ya uislamu, na alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni mwenye tabia nzuri kuliko watu wote akanyoosha mkono wake, lakini Amri bin Aaswi akakunja mkono wake, si kwasababu ya kiburi, lakini ni kwasababu ya kuyathibitisha yale atakayoyaeleza, akasema kumwambia: "Umekuaje?" Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika mimi ninaweka sharti -yaani juu ya kusilimu- Akasema: "Ni kitu gani unaweka sharti?" Akasema: Ninaweka sharti kuwa anisamehe Mwenyezi Mungu mimi yaliyopita katika ukafiri miongoni mwa madhambi. Hii ndio ilikuwa hamu yake kubwa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Anaweka sharti kuwa Mwenyezi Mungu amsamehe, alidhani kuwa Mwenyezi Mungu hatomsamehe katika yale aliyokuwa nayo nyuma, Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akasema kumwambia-: "Hivi hukujua kuwa uislamu unabomoa(unafuta) yaliyokuwa kabla yake, na kuwa kuhama kunabomoa yaliyokuwa kabla yake, nakuwa Hija inabomoa yaliyokuwa kabla yake?". Mambo matatu. Ama Uislamu unabomoa yaliyokuwa kabla yake kwa ushahidi wa kitabu kitukufu: Amesema Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka: "Waambie wale waliokufuru: "kama wataacha (yale mabaya waliyokuwa nayo) watasamehewa yaliyopita, na wakiyarudia (tutawatesa kama tulivyo watesa wao mara zilizopita) Imekwisha kuwapitia wao mifano (ya mambo yaliyowapata) watu wa zamani". Na kuhama: atakapohama mtu kutoka katika mji wake ambao anaishi ndani yake, na katika mji wa kikafiri hilo linafuta yaliyokuwa kabla yake. Na hija: inabomoa yaliyokuwa kabla yake; kwa kauli ya Mtume- Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayehiji akawa hakufanya mabaya na akawa hakufanya machafu atarudi kama siku alivyozaliwa na mama yake". Hapo akampa utiifu -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akampenda Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- mapenzi makubwa mpaka akawa ni mtu anayependeka zaidi kwake, na mpaka akawa hawezi kumkazia jicho; kwa kumuheshimu yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- Ametakasika mwenye kuzigeuza nyoyo! jana alikuwa akimchukia chuki kubwa mpaka anatamani apate nafasi ili amuuwe, na sasa hivi hawezi hata kunyanyua jicho lake kumtazama; kwasababu ya kumuheshimu, na wala hawezi hata kumuelezea kwasababu hawezi kumtazama akamaliza, kiasi ambacho hakuweza kumjua vizuri; kwasababu ya mapenzi yake kwake -Rehema na Amani ziwe juu yake- Anasema -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-. Laiti angelikufa katika hali ya kwanza; basi angelikuwa ni katika watu wa motoni: Anasema: Na lau ningelikufa katika hali ile yaani hali ya pili; ningetaraji kuwa miongoni mwa watu wa peponi, hebu tazama alivyojipa uwezekano, amejihakikishia kuwa laiti angelikufa katika hali ya kwanza; angelikuwa miongoni mwa watu wa motoni, Ama hali ya pili kutokana na hofu yake kubwa amesema: Laiti ningelikufa katika hali hii basi ningetaraji kuwa miongoni mwa watu wa peponi, na hakusema: Ningekuwa ni miongoni mwa watu wa pepo; kwasababu ushuhuda wa kuingia peponi ni jambo gumu. Kisha yeye baada ya hapo akasimamia mambo -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, alisimamia madaraka na uongozi, na yakatokea yaliyotokea katika kisa cha vita vya Muawiya na wengineo, na Amru bin Aaswi alikuwa anafahamika kwa waarabu kuwa ni katika waarabu wajanja na werevu mno, basi anasema: ninahofia kwa haya yaliyotokea kwangu baada ya ile hali ya katikati huenda yakawa yameyazingira matendo yangu. Kisha akatoa usia -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa yeye atakapokufa asifuatwe na maombolezo, na muombolezaji: Ni mwanamke anayemuomboleza maiti, na analia kilio kinachofanana na mlio wa punda, na akaamrisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- watakapomzika wabakie katika kaburi lake kiasi cha kuchinja ngamia mmoja, na kugawika nyama yake, mpaka awajibu wajumbe wa Mola wake nao ni Malaika wale wanaomjia maiti anapozikwa, Maiti anapozikwa humjia Malaika wawili na wanamkalisha ndani ya kaburi lake, na wanamuuliza maswali matatu: wanasema: Nani Mola wako? Na ni ipi dini yako? Na ni nani Nabii wako?. Akaamrisha Amru bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- watu wake wasimame juu yake kiasi cha kuchinjwa ngamia na kugawanywa nyama yake; ili ajiliwaze kupitia wao, Na hii inaonyesha kuwa maiti huwa anawahisi watu wake, na imethibiti kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa maiti husikia nyayo za viatu vyao, wanapoondoka baada ya kumzika, nyayo za viatu za kimya kimya anazisikia maiti wanapoondoka baada ya kumzika. Na imethibiti kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi ambayo daraja yake ni (Hasan) kuwa yeye alikuwa anapomzika maiti anasimama juu yake, na Anasema: "Muombeeni msamaha ndugu yenu, na muombeeni kuthubutu; kwani yeye wakati huu anaulizwa", Hivyo ni sunna na inapendeza anapozikwa maiti mtu asimame juu ya kaburi lake na aseme: Ewe Mwenyezi Mungu mpe uthubutu (umakinifu), Ewe Mwenyezi Mungu mpe uthubutu (umakinifu), Ewe Mwenyezi Mungu mpe uthubutu (umakinifu), Ewe Mwenyezi Mungu msamehe; kwasababu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa anapotoa salamu basi anatoa salamu mara tatu, na anapoomba anaomba mara tatu. Kilichopo nikuwa mtoto wa Amru bin Aaswi alisema kumwambia: Alikupa habari njema wewe Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ya kuingia peponi, na hii ni sehemu ya kujipa bishara njema na kujipongeza kwayo.
Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: (Nilimjia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- naye akiwa anapiga mswaki kwa mswaki wa mti mbichi, Akasema: na ncha ya mswaki ikiwa katika ulimi wake, naye akisema: AAGH,AAGH (sauti ya kujigogoa), na mswaki ukiwa mdomoni mwake, kana kwamba anajigogoa).
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAnaeleza Abuu Musa Al Ash'ariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: yakuwa yeye alikuja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- naye akipiga mswaki kwa kutumia mti mbichi kwasababu husafisha kikamilifu na hausambaratiki mdomoni; ukakera, na hakika alikuwa kaweka mswaki juu ya ulimi wake, mpaka akawa kana kwamba anajitapisha.
Kutoka kwa Ammari Bin Yasiri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliniagiza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika haja fulani, nikapatwa na janaba, nikawa sikupata maji, nikajigaragaza katika udongo kama anavyojigaragaza mnyama, kisha nikamuendea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Nikamsimulia hilo, akasema: "Hakika ilikuwa inakutosheleza kupiga kwa mikono yako hivi" Kisha akapiga kwa mikono yake miwili chini ya ardhi mpigo mmoja, kisha ukapaka mkono wa kushoto juu ya mkono wa kulia, na juu ya viganja vyake na uso wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlimtuma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Ammari Bin Yasiri radhi za Allah ziwe juu yake katika moja ya safari kwa baadhi ya haja zake, akapatwa na janaba kwa tendo la ndoa au kushukwa na manii kwa matamanio, na hakupata maji ili aoge, Na alikuwa hajui hukumu ya tayamam kwa ajili ya janaba, bali alikuwa anajua hukumu yake kwa hadathi ndogo, akajitahidi na akadhani kuwa kama ambavyo hufuta kwa udongo baadhi ya viungo vya udhu kwa kuondoa hadathi ndogo, akaona kuwa kutayamam kwa kuondoa janaba ni lazima aeneze udongo mwili mzima; kwa kuchukulia kipimo katika maji, akajigeuzageuza katika udogo mpaka akaueneza mwili mzima na akaswali, alipokuja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akamueleza kuhusu hilo; ili aone je yeye amepatia au amekosea? Akambainishia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- namna ya kujitwaharisha kutokana na hadathi mbili, ndogo kama haja ndogo, na hadathi kubwa kama janaba: Nako ni mtu kupiga kwa mikono yake miwili juu ya udongo mpigo mmoja, kisha afute kwa mkono wa kushoto juu ya mkono wa kulia, na juu ya viganja vyake na uso wake.
Kutoka kwa Twariq bin Shihabi Al bajaliy Al Ahmashiy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na mguu wake ukiwa tayari umeuweka kwenye kipandwa (yaani yuko tayari kwa safari): Ni jihadi ipi bora? Akasema: "Ni neno la haki kwa kiongozi muovu".
Imepokelewa na An-Nasaaiy - Imepokelewa na AhmadMtu mmoja alimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake akiwa tayari kajiandaa kwaajili ya safari: Ni jihadi ipi yenye thawabu nyingi? Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamueleza kuwa jihadi bora, ni yeye kumuamrisha mema kiongozi dhalimu, au amkataze maovu, jihadi haishii pekee kupigana na makafiri, bali ina daraja, na iliyotajwa ndiyo ina malipo mengi zaidi; kwasababu inahofiwa mtu kuuawa au kukamatwa kwasababu ya ujeuri na kiburi cha kiongozi na kwasababu ya uchache wa wenye kujitosa katika hilo.
Imepokelewa kutoka kwa Jariri Bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimpa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kusikia na kutii, na nasaha kwa kila muislamu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza swahaba Jariiri Bin Abdallah radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye alishikamana na maamrisho na akampa ahadi Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kutekeleza swala tano za faradhi usiku na mchana, kwa kutimiza sharti zake na nguzo zake na wajibu zake na sunna zake, na kutelekeza zaka ya wajibu, nayo ni ibada ya mali ya lazima, huchukuliwa toka kwa matajiri na kupewa wanaostahiki katika mafakiri na wengineo, na kuwatii viongozi, na kumpa nasaha kila muislamu, na hii ni kwa kuchunga masilahi yake, na kumfikishia kheri, na kumkinga na shari kwa kauli na vitendo.
Kutoka kwa Muadhi bin Jabali -radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimshika mkono wake, na akasema: "Ewe Muadhi, Wallahi hakika mimi ninakupenda", Akasema: "Ninakuusia ewe Muadhi usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni ibaadatika" Ewe Mwenyezi Mungu nisadie katika kukutaja na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako".
Imepokelewa na Abu Daud, Nasai na AhmadMtume rehema na amani ziwe juu yake alishika mkono wa Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake, na akasema kumwambia: Wallahi hakika mimi ninakupenda, na ninakuusia ewe Muadhi usijekuacha kusema mwisho wa kila swala: Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie kukutaja, katika kila kauli na kitendo kinachoniweka karibu na utiifu, "na kukushukuru" kwa kutimia neema na kuzuia mabaya, "na kuzifanya vizuri ibada zako" kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa kumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Kutoka kwa Abuu Huraira na Abdillahi bin Amri na Aisha- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye amesema: (Adhabu kali ya moto itazipata nyayo za miguu).
Imepokelewa na Imamu Muslim - Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim kwa riwaya zakeAnatahadharisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- juu ya kufanya uzembe katika swala la udhu, na kutotekeleza udhu vilivyo, na anahimiza juu ya kuzingatia kuukamilisha, na kwakuwa mwisho wa miguu mara nyingi ndio huwa hayafiki maji ya udhu, basi mapungufu yanakuwa katika twahara na swala kwasababu hiyo, na akaeleza kuwa adhabu itamiminika juu ya hilo na kwa mfanyaji wake anayefanya uzembe katika twahara yake ya kisheria.
Kutoka kwa Abdillahi bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: "Alichelewesha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swala ya Ishaa, akatoka Omar, akasema: Swala Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamelala wanawake na watoto, akatoka na kichwa chake kikitona maji akisema: Lau kama nisingehofia kuwapa tabu umma wangu basi ningewaamrisha swala hii waiswali wakati huu".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAlichelewa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika swala ya ishaa, mpaka usiku ukawa mkubwa,na wakalala wanawake na watoto, miongoni mwa wale wasiokuwa na uwezo wa kuvumilia kusubiri kwa muda mrefu, akaenda kwake Omar bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akasema: Swala, hakika wamelala wanawake na watoto. Akaja-Rehema na Amani ziwe juu yake- kutoka nyumbani kwake akielekea msikitini na kichwa chake kikitona maji kwasababu ya kuoga na akazungumza kwa kulibainisha hilo kuwa kilichobora katika swala ya ishaa ni kuichelewesha, lau kama si tabu wanazozipata wale wenye kuisubiri swala: Lau kama nisingehofia tabu kwa umma wangu basi ningewaamrisha swala hii katika wakati huu wakuchelewa.